Mkanda wa jeshi (Herpes zoster/ shingles) fahamu kuhusu dalili na tiba yake

Mkanda wa jeshi (Herpes zoster/ shingles) fahamu kuhusu dalili na tiba yake

Nakumbuka Sister wangu aliugua ugonjwa huu akiwa na umri wa 13 au 14 miaka,lakini mpaka leo Ana 36 age yuko poa,sio wote wenye mkanda wa jeshi wanangoma,

Uncle wangu aliugua mkanda wa jeshi akiwa karibia na 50 yrs ni kweli alikuja kufarikia baadae na HIV akiwa na umri wa 56 yrs,
 
800px-Italian_garlic_PDO.JPG



kitunguu Saumu kinaweza kutibu mkanda wa jeshi, chukua Kitunguu Saum usage juice, kisha pasha moto iwe vuguvugu. halafu osha sehemu yenye


ugonjwa. kisha chukua nyingine kidogo weka katika Asali safi ya nyuki halafu baada ya kuosha upake dawa hiyo. baada ya siku 11 hadi 21 utakua umepona. Chanzo. MziziMkavu


HAYA TENA WENYE MKANDA WA JESHI TUMIE KITUNGUU SAUMU KISHA MUJE MUNIPE FEEDBACK.
 
NA PIA WAWEZA KUKILA KITUNGUU SAUMU KWA HAYO MARADHI YA MKANDA

WA JESHI KWA KUTUMIA NJIA HII HAPA CHINI NA UKAPONA PIA UKAWA

UNAKILA NA KUJIPAKA JARIBUNI KISHA MULETE FEEDBACK. FANYA HIVI:


Nunua kitunguu swaumu.Menya chote kama vile uandaavyo kwa ajili ya kupikia.Twanga ama

saga,vikishasagika changanya na maji ya uvuguvugu kidogo kipimo cha kijiko cha chai ili

vilainike.Chota msagiko wote wa vitunguu na uvimeze.



Tahadhari,jitahidi uwe na mfuko ama sehemu ya maliwatoni maana kama hauna tumbo zuri

unaweza tapika.(Mara chache sana hutokea kutapika)


Ukishakaa kama dk 15 hali yako itarudi kawaida ya kuto tapika.Baada ya SIKU 7 Utaona

matokeo yake hakuna tena hayo maradhi.

Pia kama una Presha ya kushuka usitumie hii dawa maana huwa inashusha sana

Presha,labda

Unywe na kahawa baada ya kuinywa dawa hii ili kuipandisha tena presha!




MATUMIZI YA KITUNGUU SAUMU?

Kitunguu saumu unakila kwa muda wa siku 7 Mfululizo kila siku asubuhi unakila kabla ya kula kitu au kunywa


kitu. Ukitaka kupona kabisa Mkanda wa jeshi tumia hicho kitunguu saumu kwa muda wa siku 21 kila siku asubuhi utakuwa umepona

kabisa tumia kisha uje unipe feedback
Msisite kuja kutoa ushuhuda wenu hapa wakuu.
 
Ndugu wanaJF (wataalamu wa tiba). Napenda kufahamu endapo kuna ukweli kwamba mtu akiugua ugonjwa uitwao mkanda wa jeshi anakuwa tayari ameshapata UKIMWI? Na endapo ana ugojwa huo afanyeje ili apone kwa urahisi? Kwa upande wa vyakula atumie vyakula gani ili kurahisisha uponaji? Nawasilisha.
 
Ndugu wanaJF (wataalamu wa tiba). Napenda kufahamu endapo vyakula atumie vyakula gani ili kurahisisha uponaji? Nawasilisha.
zitafakari njia zako maaana!!!!
 
Magonjwa / conditions tofauti na UKIMWI zinaweza kusababisha mkanda wa jeshi. Rejea kifo cha Mwalimu Nyerere, ambaye tumeambiwa alifariki kwa kansa ya damu (Leukemia) naye alikuwa na mkanda wa jeshi.
 
Kwa ufahamu wangu ugonjwa wa Mkanda wa jeshi ni dalili kwa kinga ya mwili imepungua. Sasa kinga ya mwili inaweza kupungua kwa sababu kuu mbili (I stand to be corrected). Kwanza ni maambukizi ya VVU na pili ni umri mkubwa wa mtu hasa kuanzia miaka 60 na kuendelea, na ndo maana kadiri mtu anavyozidi kuzeeka husumbuliwa na magonjwa kadha wa kadha.
 
Mkanda wa Jeshi(Herpes Zoster au kwa jina lingine Shingles) ni Ugonjwa unaompata mtu ambaye hapo zamani aliwahi kuugua Tetekuwanga(Chicken Pox au kwa jina lingine Varicella Zoster).

Ili mtu apate Mkanda wa jeshi mara nyingi ni wakati Kinga za Mwili zimepungua.
Kinga za Mwili zinaweza kupungua kutokana na:

1/Magonjwa(Kwa mfano Ukimwi, Kansa, Kisukari, TB nk)
2/Umri(Uzee, Utoto nchanga)
3/Lishe Duni.
4/Ujauzito.
5/Matibabu(Mionzi, Madawa makali(Steroid, Broad spectrum Antibiotics, Chemotherapy), Kupandikiza(Transplantation))

*Toka kuja na kuenea kwa Ukimwi duniani idadi ya wanaogua Ugonjwa wa Mkanda wa jeshi imeongezeka sana kwa sababu Ukimwi ni chanzo kikuu cha Kupunguza kinga mwilini. Please nenda kapime ili ujue nini chanzo cha kupata Mkanda wa Jeshi.

NOTE:
Maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi duniani yanatambuliwa rasmi(Diagnosed) kwa kutumia vipimo vya Maabara pekee na sio kwa kukisia kupitia dalili za ugonjwa(Clinical Suspecious).

Please go and test, it is Easy, Simple, Cheap and Rapid to know your HIV sero status.
 
Ndugu wanaJF (wataalamu wa tiba). Napenda kufahamu endapo kuna ukweli kwamba mtu akiugua ugonjwa uitwao mkanda wa jeshi anakuwa tayari ameshapata UKIMWI? Na endapo ana ugojwa huo afanyeje ili apone kwa urahisi? Kwa upande wa vyakula atumie vyakula gani ili kurahisisha uponaji? Nawasilisha.
DAWA YA KUTIBU MKANDA WA JESHI FANYA HIVI:

Dawa ya Tiba Mbadala jaribu hii Nunua kitunguu swaumu Kimoja kizima.Menya

chote kama vile uandaavyo kwa ajili ya kupikia.Twanga ama saga,vikisha sagika changanya na maji ya uvuguvugu kidogo

kipimo cha kijiko cha chai ili vilainike.Chota msagiko wote wa vitunguu na uvimeze.


Tahadhari,jitahidi uwe na mfuko ama sehemu ya maliwatoni maana kama hauna tumbo zuri unaweza tapika.
(Mara chache

sana hutokea kutapika)
Ukishakaa kama dk 15 hali yako kutotapika itarudi kawaida. Jaribu kutumia kila siku Asubuhi kabla ya kula

kitu tumia hii dawa mpaka hapo utakapo pona maradhi yako kisha uje hapa unipe

Feedback. Chanzo.MziziMkavu
 
Mtoa mada fahamu UKIMWI (Ukosefu wa kinga mwilini) unasababishwa na vitu vingi mfano virus vya ukimwi (vvu), ukosefu wa lishe, magonjwa ya muda mrefu, matumizi ya dawa muda mrefu, uzee nk, ni kweli mkanda wa jeshi husababishwa na UKIMWI kwa sababu virusi vinavuosababisha mkanda wa jeshi huweza kumshambulia mtu ambaye kinga yake imeshuka (opportunistic infections), si lazima UKIMWI huo usababishwe na VVU. Sio kila mwenye mkanda wa jeshi ana VVU
 
Ndugu wanaJF (wataalamu wa tiba). Napenda kufahamu endapo kuna ukweli kwamba mtu akiugua ugonjwa uitwao mkanda wa jeshi anakuwa tayari ameshapata UKIMWI? Na endapo ana ugojwa huo afanyeje ili apone kwa urahisi? Kwa upande wa vyakula atumie vyakula gani ili kurahisisha uponaji? Nawasilisha.

Kuwa na mkanda wa jeshi si kuwa na UKIMWI ila ni ishara kuwa kinga yako imeshuka, mkanda wa jeshi unatibika kama unavyotibika UKIMWI. Vyakula vya kuepuka ni vile vinavyoharibu kinga ya mwili ambavyo bilashaka wavijuwa. Kama una swali uliza.
 
Naomba uniorodheshee baadhi ya vyakula vinavyoharibu kinga ya mwili
 
Back
Top Bottom