Mkanda wa jeshi (Herpes zoster/ shingles) fahamu kuhusu dalili na tiba yake

Mkanda wa jeshi (Herpes zoster/ shingles) fahamu kuhusu dalili na tiba yake

Onana tena na daktari kwa ushauri zaidi na kama itakuwa ngumu kwa tiba za hospitali kutokana na hali ya ujauzito wake zipo baadhi ya tiba huwa hazidhuriani na hali yake 0715689004
 
Pole sana mkuu,
ila nina swali, kwani mkanda wa jeshi una sababishwa na nini...?
Mkuu unasababishwa na reactivation ya virus ajulikanae Kama Varicella Zoster ambaye analeta tetekuwanga utotoni.

Pole sana mdau wangu mkubwa wa riwaya. I pray for you and your family. Lkn ni bora pia ukafika hospital sio dispensary kwa vipimo vikubwa na tiba

Asante mkuu, pia ngoja niwasubiri madokta hapa.

Onana tena na daktari kwa ushauri zaidi na kama itakuwa ngumu kwa tiba za hospitali kutokana na hali ya ujauzito wake zipo baadhi ya tiba huwa hazidhuriani na hali yake 0715689004

Nashukuru mkuu ila Kama hiyo namba ni ya Mshana Jr basi tena.
 
hapana ni namba yangu ninatamani tushauriane
 
mkanda wa jeshi huashiria kinga ya mwili iko chini.

Pambana mkuu, Fika hospitali angalau za ngazi ya wilaya kwa vipimo na matibabu.
Usimwache mkeo kwenda peke yake "mediko"

Sasa Erithromycin naijua kwa ubora wake wa kushambulia bacteria ila sijui Kama inaongeza kinga ya mwili. Au kulitakiwa kuwe na dawa ingineyo?
 
Sasa Erithromycin naijua kwa ubora wake wa kushambulia bacteria ila sijui Kama inaongeza kinga ya mwili. Au kulitakiwa kuwe na dawa ingineyo?

siko vizuri kwenye taaluma ya dawa mkuu.
 
mkanda wa jeshi huashiria kinga ya mwili iko chini.

Pambana mkuu, Fika hospitali angalau za ngazi ya wilaya kwa vipimo na matibabu.
Usimwache mkeo kwenda peke yake "mediko"

Ni kweli mkuu sio vibaya pia kucheck HIV status
 
Kapimeni damu kwanza mm navyo jua mkanda wa jeshi unawapata sana sana waathirika wa HIV nenda na mkeo hospital mkapime kwanza!!! Itakuwa ulioa kabla hamjaenda kupima ww unajiamin huna Ila mkeo atakuwa anakuficha MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
Nenda hospitali na sio Zahanati, huko ndio una chance ya kukutana na daktari. Aliyemuona mkeo ni tabibu sio daktari.
 
Kapimeni damu kwanza mm navyo jua mkanda wa jeshi unawapata sana sana waathirika wa HIV nenda na mkeo hospital mkapime kwanza!!! Itakuwa ulioa kabla hamjaenda kupima ww unajiamin huna Ila mkeo atakuwa anakuficha MziziMkavu
Mkuu tuna mtoto wa kwanza mwenye afya njema na miaka miwili kasoro. Hawezi kuwa alinidanganya maana cliniki nilihudhuria naye.
Nenda hospitali na sio Zahanati, huko ndio una chance ya kukutana na daktari. Aliyemuona mkeo ni tabibu sio daktari.

Hii Hospitali ya Levolosi Arusha si ya kubeza mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Kirchhoff,

MKANDA WA JESHI (HERPES ZOSTER/SHINGLES)

Kwa takriKwa bani miongo mitatu sasa, tumeshuhudia ongezeko kubwa la mlipuko wa ugonjwa wa mkanda wa jeshi linaloendana na ongezeko la hususani ugonjwa wa UKIMWI. Hali hii imefanya baadhi ya watu kuamini kuwa, ugonjwa huu ni dalili ya wazi kabisa ya mtu kuwa na VVU, imani

ambayo kwa kiasi kikubwa ina ukweli ndani yake ingawa si kwa wote wanaopatwa nao.Mkanda wa jeshi au shingles au herpes zoster kwa majina ya

kitabibu ni ugonjwa unaosababishwa na virus wa aina ya Varicella-zoster ambao pia husababisha ugonjwa wa tetekuwanga au chickenpox. Ugonjwa huu huathiri ngozi ambapo huambatana na vipele na michubuko kama ya kuungua yenye kuambatana na maumivu makali .

Visababishi
Kama tulivyokwisha tangulia kueleza hapo juu, ugonjwa huu husababishwa na virus aina ya Varicella-zoster ambao pia husababisha ugonjwa wa tetekuwanga. Baada ya mtu kupatwa na tetekuwanga, virus hawa hubaki katika hali ya kupooza/kutokuwa na madhara (dormant) katika neva fulani za mwili. Baada ya miaka kadhaa, iwapo itatokea kinga ya mwili ikashuka kwa sababu yoyote ile, virus hawa hupata tena nguvu/kuwa na madhara (active), kuibuka na kusababisha ugonjwa wa mkanda wa jeshi.Kwa kawaida shambulio la mkanda wa jeshi hutokea mara moja maishani ingawa laweza kujirudia.

Vihatarishi
Mkanda wa jeshi unaweza kumpata mtu wa umri wowote ule ingawa watu walio katika makundi haya wapo katika hatari kubwa zaidi:
Wenye umri wa zaidi ya miaka 60
Mtu aliyewahi kuugua ugonjwa wa tetekuwanga kabla ya umri wa mwaka mmoja
Watu ambao kinga yao ya mwili imepungua kwa sababu mbalimbali kama vile matumizi ya aina fulan za dawa, magonjwa kama vile maambukizi ya VVU (HIV/AIDS), saratani na utapiamlo.

Je mkanda wa jeshi huambukizwa?
Hapana ugonjwa huu hauambukizwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine! Lakini iwapo itatokea mtoto au mtu mzima ambaye hajawahi kupatwa na ugonjwa wa tetekuwanga maishani mwake na ambaye pia hajawahi kupata chanjo dhidi ya ugonjwa huo akakutana na mtu mwenye ugonjwa wa mkanda wa jeshi, mtoto au mtu huyo atapatwa na ugonjwa tetekuwanga na siyo mkanda wa jeshi.

Dalili
Dalili ya awali kabisa ya mkanda wa jeshi ni maumivu makali sehemu fulani/ upande mmoja wa mwili yakiambatana na hali ya ganzi na hisia za kuungua kwenye ngozi. Maumivu pamoja na hisia za kuungua huwa makali sana na hutokea kabla ya vipele/michubuko kutokea kwenye ngozi.
Kawaida, vipele au michubuko huusisha eneo fulani la mwili kuanzia kwenye uti wa mgongo kuzunguka kuelekea eneo la tumbo au kifua. Michubuko pia inaweza kutokea kwenye maeneo yanayozunguka uso, macho, mdomo au masikio.Dalili nyingine ni pamoja na :
Maumivu ya tumbo
Homa
Maumivu ya mwili mzima
Vidonda sehemu za siri
Maumivu ya kichwa
Maumivu ya viungo
Kuvimba kwa mitoki/ matezi
Iwapo neva za maeneo ya uso zitaathiriwa, mgonjwa anaweza kupatwa na matatizo ya kuona, kuonja, au kusikia.

Vipimo
Ni nadra sana kufanya Vipimo maalum kwa ajili ya utambuzi wa ugonjwa huu, isipokuwa kwa nchi zilizoendelea. Kwa ujumla utambuzi wa ugonjwa huu hufanyika kwa kuchukua historia ya mgonjwa na kuchunguza sehemu ya ngozi iliyoathiriwa.
Vipimo vya damu yaani FBP huonesha ongezeko la chembe nyeupe za damu na antibodies dhidi ya virus wa tetekuwanga.

Matibabu
Matibabu ya mkanda wa jeshi hujumuisha matumizi ya dawa kama vile Acyclovir, Famciclovir na Valacyclovir kwa ajili ya kuua virus wanaosababisha ugonwja huu. Dawa hizi husaidia kupunguza maumivu, kuzuia madhara zaidi ya ugonjwa huu na kupunguza muda wa ugonjwa.
Dawa hizi hutolewa angalau saa 72 baada ya mgonjwa kuanza kuhisi maumivu na hali ya kuungua. Ni vema dawa zianze kutumika kabla ya vipele/michubuko kujitokeza.
Jamii ya dawa za corticosteroids kama vile prednisolone husaidia kupunguza maumivu na uvimbe kwa badhi ya wagonjwa. Dawa nyingine zinazofaa kutumika ni pamoja na jamii ya antihistamines kwa ajili ya kupunguza muwasho, dawa za maumivu, calamine lotion kwa ajili ya kupunguza muwasho. Aidha mgonjwa anashauriwa kupata mapumziko ya kutosha

Matarajio
Mkanda wa jeshi kwa kawaida huchukua kati ya wiki mbili hadi tatu kupona wenyewe. Aidha ni nadra sana kwa ugonjwa huu kujirudia tena. Iwapo neva zinazothibiti mwendo katika mwili zitakuwa zimeathirika, mgonjwa anaweza kupatwa na kupooza kwa muda au kwa kudumu kwa sehemu ya mwili iliyoathiriwa. Wakati mwingine, maumivu yanayosababishwa na mkanda wa jeshi yanaweza kudumu kwa miezi mpaka mwaka hata baada ya mgonjwa kupona kabisa. Maumivu haya yanayojulikana kama postherpetic neuralgia kwa kawaida huwakumba wagonjwa wenye umri wa zaidi ya miaka 60 na husababishwa na uharibifu katika neva za mwili.

Madhara
Madhara ya mkanda wa jeshi ni pamoja na kupatwa na shambulio jingine la ugonjwa huu, maambukizi ya bakteria, upofu iwapo eneo la jicho litahusika, ukiziwi, maambukizi katika utando wa ubongo (encephalitis), uwepo wa vimelea kwenye damu (sepsis) au ugonjwa unaoitwa Ramsay Hunt Syndrome iwapo utahusisha neva za uso.


Kinga
Epuka kabisa kugusa eneo lenye vipele au michubuko kwa mtu mwenye mkanda wa jeshi au tetekuwanga iwapo hujawahi kuugua au kupata chanjo ya tetekuwanga.
Ni vema kupata chanjo dhidi ya virus wa Varicella zoster kama inapatikana katika nchi au eneo ulilopo . Tafiti zimeonesha kuwa, watu wazima wanaopata chanjo hii wana uwezekano mdogo sana wa kupata madhara ya mkanda wa jeshi kuliko wale wasiochanjwa.


Ukitaka Matibabu ya huo ugonjwa unaweza kunitafuta mimi
Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili Herbalist mzizimkavu. Au boonyeza hapa.Herbalist MziziMkavu
 
Mkuu MziziMkavu hiyo page niliitembelea pia.

Nimekupa link ya kuwasilian an mimi sio kutembelea tu. Ukitaka Matibabu ya huo ugonjwa unaweza kunitafuta mimi
Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili Herbalist mzizimkavu. Au boonyeza hapa.Herbalist MziziMkavu
 
management of herpes zoster antiviral kama acyclovir kwa ajili ya kumuua huyo kirusi dawa za maumivu(antipain) mfano pcm
 
unampa antibiotic kama cap amoxyline 500mg tds for 5/7 kuzuia maambukizi yatokanayo na bacteria kwani vidonda vipo wazi
 
Back
Top Bottom