Mkanda wa Jeshi(Herpes Zoster au kwa jina lingine Shingles) ni Ugonjwa unaompata mtu ambaye hapo zamani aliwahi kuugua Tetekuwanga(Chicken Pox au kwa jina lingine Varicella Zoster).
Ili mtu apate Mkanda wa jeshi mara nyingi ni wakati Kinga za Mwili zimepungua.
Kinga za Mwili zinaweza kupungua kutokana na:
1/Magonjwa(Kwa mfano Ukimwi, Kansa, Kisukari, TB nk)
2/Umri(Uzee, Utoto nchanga)
3/Lishe Duni.
4/Ujauzito.
5/Matibabu(Mionzi, Madawa makali(Steroid, Broad spectrum Antibiotics, Chemotherapy), Kupandikiza(Transplantation))
*Toka kuja na kuenea kwa Ukimwi duniani idadi ya wanaogua Ugonjwa wa Mkanda wa jeshi imeongezeka sana kwa sababu Ukimwi ni chanzo kikuu cha Kupunguza kinga mwilini. Please nenda kapime ili ujue nini chanzo cha kupata Mkanda wa Jeshi.
NOTE:
Maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi duniani yanatambuliwa rasmi(Diagnosed) kwa kutumia vipimo vya Maabara pekee na sio kwa kukisia kupitia dalili za ugonjwa(Clinical Suspecious).
Please go and test, it is Easy, Simple, Cheap and Rapid to know your HIV sero status.