Habari wakuu,
Miaka mitano nyuma niliwahi kusikia japo nimepata uhakika sasa,ilisemwa alitembea na mama moja huko kijijini .
Ndugu yangu ndo amemaliza masomo yake ya juu,nasikitika sana ,nguvu kazi yake inapotea hivi hivi naona.
Najaribu kutumia akili nyingi sana kumshawishi afanye utaratibu wa kwenda hospitali japo mi najua tayari amekanyaga waya,
Kijana bado mdogo sana,nimejaribu kumwambia tufanye hivi ili twende hospitali ili nimwahishe kuanza dawa lakini amekua hataki,na bado hajajua kabisa hili ugonjwa.
Papuchi tunazipenda ila zinatupa sana shida,
Nimejaribu kumshawishi kiakili lkn bado naona hajaamini ninachomwambia kuhusu hospitali.
Nashindwa kutumia njia gani kumuokoa huyu ndugu yangu na tumekua wote, tumecheza wote, tumesoma wote, hakika inauma sana.
Mungu tu ndo atuepushe na hayo majanga,ulisema uoe ,utajilinda mwenzako tabia yake pia hujui yaani ni shida kweli