Mkanda wa jeshi (Herpes zoster/ shingles) fahamu kuhusu dalili na tiba yake

Mkanda wa jeshi (Herpes zoster/ shingles) fahamu kuhusu dalili na tiba yake

Haujatoa ufafanuzi wa huo mkanda wa jeshi na habari yako Mkuu umeruka tu juu juu
Mkanda wa jeshi maana ake anahisi tayari jamaa na ukimwi kwsbb dalili mojawapo ni kupata huo ugonjwa wa mkanda wa jeshi.
 
Hana maambukizi huyo, yupo mzee flani kijijini kwetu aliwahi kuugua huu ugonjwa akapewa dawa akapona na hakuwa na maambukizi hadi now anadunda mtaani tena mzee mchesh mno nabmwenye heshima kwa vijana na wazee wenzeka.

Uhakika zaidi mshawishi akapime.
 
Nawashauri huo mkanda wa jeshi apeleke jeshini kwa sababu wale wajeda wakimkuta amevaa madhara yake ni makubwa
 
Mkuu mkanda wa jeshi hauna uhusiano na ukimwi, mkanda waa jeshi husababishwa na kushuka kwa kinga mwilini, kwa hiyo kwa wale wanaougua Ukimwi huwatokea sababu kinga za mwili hushuka.

Wengine husababishwa na kuumwa tetekuwanga na kama haikutibika vizuri, virusi vya tetekuwanga huendelea kuwepo mwilini na huja kufumuka badae kama mkanda wa jeshi.

Na mkanda wa jeshi huambukiza, na ugonjwa unaotokea huwa tetekuwanga. Na ndiyo mana dawa za mkanda wa jeshi ni antiviral drugs. Halafu mkanda wa jeshi huitwa Shingles, sasa wengi huwa tunachanganya na Candidiasis
 
Tatizo la JF wengine wanaleta mizaha humu wakati wengine tunapata elimu
 
Unazingua ujue wewe.......mkanda wa jeshi ni jina la kitaalamu au ndo nini?eka hata picha basi?
Habari wakuu,

Miaka mitano nyuma niliwahi kusikia japo nimepata uhakika sasa,ilisemwa alitembea na mama moja huko kijijini .

Ndugu yangu ndo amemaliza masomo yake ya juu,nasikitika sana ,nguvu kazi yake inapotea hivi hivi naona.

Najaribu kutumia akili nyingi sana kumshawishi afanye utaratibu wa kwenda hospitali japo mi najua tayari amekanyaga waya,

Kijana bado mdogo sana,nimejaribu kumwambia tufanye hivi ili twende hospitali ili nimwahishe kuanza dawa lakini amekua hataki,na bado hajajua kabisa hili ugonjwa.

Papuchi tunazipenda ila zinatupa sana shida,

Nimejaribu kumshawishi kiakili lkn bado naona hajaamini ninachomwambia kuhusu hospitali.

Nashindwa kutumia njia gani kumuokoa huyu ndugu yangu na tumekua wote, tumecheza wote, tumesoma wote, hakika inauma sana.

Mungu tu ndo atuepushe na hayo majanga,ulisema uoe ,utajilinda mwenzako tabia yake pia hujui yaani ni shida kweli
 
Usije ukashangaa Wewe una VVU...afu jamaa mwenye Mkanda wa Jeshi hana VVU....apo ndo utajua Dunia inazunguka
 
Sio kila mkanda wa jeshi unatokana na HIV.
Kumbuka mkanda wa jeshi ulikuwepo hata kabla ukimwi haujatia timu bongo.
Masuala ya immunity yako complicated sana, na sio kila mtu unayemwona na huo mkanda basi amekanyaga miwaya. Kwa uhakika, ni madaktari pekee ndio wanaweza kutoa picha halisi.
 
Dah!! Huu ugonjwa usikie tu maana ukikupata huna pakupapasa, hujui wapi panakuuma na huelewi unaumwa nn!! Unajisikia vibaya hata huwezi kumuelezea mtu unaumwaje!! Nashukuru nilipona haraka Sasa sijui Kama sikupata utando wa ubongo maana nilishuka kimasomo😁😁😁😁
 
NgumiJiwe, inaitwa herpeszoster (sina hakika na spellings) . Google.
Mkanda wa jeshi ni shambulio la nerves by virus. Hii inatokana mostly na upungufu wa kinga mwilini either baada ya kuugua muda mrefu au baada ya stress ya muda mrefu. Magonjwa ya virusi hayana tiba zaidi ya kuu-boost mwili ili uweze kupambana zaidi. Hebu google kwa maelezo zaidi
Upo sahihi sana mkuu. Ulichokiandika na nilichokifeel / kukishuhudia wakati naumwa ugonjwa huu ni sawa kabisa. Hata dawa ni hizo hizo.
Ila huu ugonjwa nilihisi kifo kinasogea kitandani mwangu kabisa.
 
Back
Top Bottom