6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 2,819
- 5,996
Niaje waugwana,
Huyu mkandarasi haijulikani alipewa tenda hii ya ujenzi BRT phase 4 kutoka Mwenge hadi Tegeta kwa sifa zipi. Toka tarehe ya ujenzi wa barabara hiyo ilipotangazwa kuanza, hadi leo ni miezi sasa, lakini jamaa utafikiri ndio kwanza wana siku 3 tu. Hakuna hatua yoyote ya maana ya ujenzi iliyopigwa.
Wenzao waliokabidhiwa kile kipande kingine kutoka Ubungo mataa, Mwenge hadi Posta wameshafika mbali na wanaonesha hari ya kumaliza kazi yao mapema kabla hata ya muda waliopewa, lakini hawa wa Mwenge to Tegeta bado wanasua sua tu hata Tangibovu hawajaivuka na miezi inazidi kukatika.
Nina hakika hawa watakuja kukifanya hiki kipande kikawie, kama vilivyokawia vile vya phase 2 na phase 3 ambavyo mpaka leo wakandarasi bado wanasua sua tu kumaliza wanashindwa.
Kama wakiendelea kujenga kwa mwendo huu wa konokono, basi nashauri wanyang'anywe ujenzi huu mapema na kukabidhiwa wale wengine wanaoendelea na ujenzi kwa kasi inayotakiwa.
Asanteni.