Mkandarasi aliepewa kazi ya ujenzi wa BRT phase 4 kutoka Mwenge hadi Tegeta, anyang'anywe haraka sana kabla hajatupotezea muda

Niaje waugwana,

Huyu mkandarasi haijulikani alipewa tenda hii ya ujenzi BRT phase 4 kutoka Mwenge hadi Tegeta kwa sifa zipi. Toka tarehe ya ujenzi wa barabara hiyo ilipotangazwa kuanza, hadi leo ni miezi sasa, lakini jamaa utafikiri ndio kwanza wana siku 3 tu. Hakuna hatua yoyote ya maana ya ujenzi iliyopigwa.

Wenzao waliokabidhiwa kile kipande kingine kutoka Ubungo mataa, Mwenge hadi Posta wameshafika mbali na wanaonesha hari ya kumaliza kazi yao mapema kabla hata ya muda waliopewa, lakini hawa wa Mwenge to Tegeta bado wanasua sua tu hata Tangibovu hawajaivuka na miezi inazidi kukatika.

Nina hakika hawa watakuja kukifanya hiki kipande kikawie, kama vilivyokawia vile vya phase 2 na phase 3 ambavyo mpaka leo wakandarasi bado wanasua sua tu kumaliza wanashindwa.

Kama wakiendelea kujenga kwa mwendo huu wa konokono, basi nashauri wanyang'anywe ujenzi huu mapema na kukabidhiwa wale wengine wanaoendelea na ujenzi kwa kasi inayotakiwa.

Asanteni.
Kuna wanaume wapo slow kama misukule
 
Kuna wanaume wapo slow kama misukule
Hii kampuni iliyopewa huo mradi inaongoza kwa uslow mkuu. Inaonekana mwaka utakata bila kumaliza hata kilometer 1.
 
Una hakika anasuasua kwa uzembe wake? Unajua mpaka sasa amepewa fedha kiasi gani? Ukiwa na majibu sahihi ya swali la pili anza kumlaumu mmoja wapo kati ya mtoa fedha au mkandarasi.
 
Team ikifanya uzembe uwanjani, sisi tutawalaumu wachezaji na sio wafadhili wa team. Kisha hao wachezaji ndio watakaotupa sababu zao za kufanya uzembe kuwa zinasababishwa na wao wachezaji, au mwenye team, au mfadhili au kocha.
 
Safi basi nenda mahakamani fungua kesi , kwasababu Kodi yako inatumika vibaya
Nimetanguliza kwanza tahadhari. Hatua isipochukuliwa, nitakwenda mahakamani kuishtaki kampuni kwa uzembe wao.
 
Niaje waugwana,

Huyu mkandarasi haijulikani alipewa tenda hii ya ujenzi BRT phase 4 kutoka Mwenge hadi Tegeta kwa sifa zipi. Toka tarehe ya ujenzi wa barabara hiyo ilipotangazwa kuanza, hadi leo ni miezi sasa, lakini jamaa utafikiri ndio kwanza wana siku 3 tu. Hakuna hatua yoyote ya maana ya ujenzi iliyopigwa.

Wenzao waliokabidhiwa kile kipande kingine kutoka Ubungo mataa, Mwenge hadi Posta wameshafika mbali na wanaonesha hari ya kumaliza kazi yao mapema kabla hata ya muda waliopewa, lakini hawa wa Mwenge to Tegeta bado wanasua sua tu hata Tangibovu hawajaivuka na miezi inazidi kukatika.

Nina hakika hawa watakuja kukifanya hiki kipande kikawie, kama vilivyokawia vile vya phase 2 na phase 3 ambavyo mpaka leo wakandarasi bado wanasua sua tu kumaliza wanashindwa.

Kama wakiendelea kujenga kwa mwendo huu wa konokono, basi nashauri wanyang'anywe ujenzi huu mapema na kukabidhiwa wale wengine wanaoendelea na ujenzi kwa kasi inayotakiwa.

Asanteni.
Jamaa makanjanja sana! Hata wafanyakazi wanaofanya kazi pale wanapigika tu hawapewi mikataba yoyote . Pia wanalipa elfu 12,500 kwa day badala ya 16, 155 kama kima cha chini kinavyo taka . wenzao wa kile kipande cha Mawasiliano -Mwenge -Posta unapoitwa tu siku ya kwanza unapatiwa mkataba siku hiyo hiyo wenye kima cha chini laki 4na20

Nashangaa sana jamaa hawa wanajenga ki local sana
 
Barabara ya Kawawa,Kilwa,Uhuru,Nyerere,Mandela zote kapewa Mchina tena kampuni moja
Hiyo kampuni ya mchina huenda kuna kigogo mmoja ndani ya chama au serikali ana share yake, ndomaana tenda zote zimepewa kampuni moja.
 
Jamaa makanjanja sana! Hata wafanyakazi wanaofanya kazi pale wanapigika tu hawapewi mikataba yoyote . Pia wanalipa elfu 12,500 kwa day badala ya 16, 155 kama kima cha chini kinavyo taka . wenzao wa kile kipande cha Mawasiliano -Mwenge -Posta unapoitwa tu siku ya kwanza unapatiwa mkataba siku hiyo hiyo wenye kima cha chini laki 4na20

Nashangaa sana jamaa hawa wanajenga ki local sana
Inaonekana hii kampuni iliyopewa kipande cha Mwenge to Tegeta ina mkono wa mtu mzito kutoka serikalini au chamani ambae tayari ashachukua pesa na kugawana na mwenye kampuni.

Kisha kiasi kidogo sana kilichobaki, ndo hicho wanachookota okota vijana wenye njaa mtaani na kuwapa vibarua visivyoendana na ukubwa wa kazi yao. Matokeo yake vijana wanashindwa kufanya kazi kwa kujituma kwani wanacholipwa hakiendani na kazi, na wengine wanakimbia hivyo kufanya wanaojenga kuwa wachache ikilinganishwa na wale wa Sam Nujoma road to Bagamoyo road via Ally Hassan Mwinyi.
 
Hiyo barabara ilipokuwa inajengwa, eneo la katikati liliachwa wazi bila kujengwa kitu kwa ajili ya ujenzi wa mradi huu wa BRT. Kinachosikitisha, waliopewa tenda hiyo ya ujenzi kutoka Mwenge to Tegeta wameonekana kusua sua mapema sana kama kwamba hawana uzoefu wa ujenzi wa barabara hizi.
Vipi tukupe wewe tenda????
Maana ndio lengo lako. Ungeuliza hata contract ni muda gani???? Au nenda pale super near lugalo kuna office zao wanaitwa "shandong ".
 
Hiyo barabara ilipokuwa inajengwa, eneo la katikati liliachwa wazi bila kujengwa kitu kwa ajili ya ujenzi wa mradi huu wa BRT. Kinachosikitisha, waliopewa tenda hiyo ya ujenzi kutoka Mwenge to Tegeta wameonekana kusua sua mapema sana kama kwamba hawana uzoefu wa ujenzi wa barabara hizi.
Wameambiwa wakamilishe kwa haraka kipande cha Mwenge hadi Njia Panda ya Kawe, ndio sababu unaona kama wanachelewa ila clearance wameshafika Makonde 😂😂
 
Kwa bahati mbaya au nzuri SHANDONG anayejenga Mwenge - Kawe ndio huyo huyo SICHUAN (SBRG) anayejenga Ubungo to kwenda KIMARA......Sawa na ilivyo SINOHYDRO na STECOL yaaani Tanzania raha tupu! Mdomo koma niko ibadani
 
Niaje waugwana,

Huyu mkandarasi haijulikani alipewa tenda hii ya ujenzi BRT phase 4 kutoka Mwenge hadi Tegeta kwa sifa zipi. Toka tarehe ya ujenzi wa barabara hiyo ilipotangazwa kuanza, hadi leo ni miezi sasa, lakini jamaa utafikiri ndio kwanza wana siku 3 tu. Hakuna hatua yoyote ya maana ya ujenzi iliyopigwa.

Wenzao waliokabidhiwa kile kipande kingine kutoka Ubungo mataa, Mwenge hadi Posta wameshafika mbali na wanaonesha hari ya kumaliza kazi yao mapema kabla hata ya muda waliopewa, lakini hawa wa Mwenge to Tegeta bado wanasua sua tu hata Tangibovu hawajaivuka na miezi inazidi kukatika.

Nina hakika hawa watakuja kukifanya hiki kipande kikawie, kama vilivyokawia vile vya phase 2 na phase 3 ambavyo mpaka leo wakandarasi bado wanasua sua tu kumaliza wanashindwa.

Kama wakiendelea kujenga kwa mwendo huu wa konokono, basi nashauri wanyang'anywe ujenzi huu mapema na kukabidhiwa wale wengine wanaoendelea na ujenzi kwa kasi inayotakiwa.

Asanteni.
Mkandarasi wa BRT PHASE 2-MBAGALA,PHASE 3-GONGO LA MBOTO na -PHASE 4-TEGETA ni huyo huyo mmoja.....
 
Niaje waugwana,

Huyu mkandarasi haijulikani alipewa tenda hii ya ujenzi BRT phase 4 kutoka Mwenge hadi Tegeta kwa sifa zipi. Toka tarehe ya ujenzi wa barabara hiyo ilipotangazwa kuanza, hadi leo ni miezi sasa, lakini jamaa utafikiri ndio kwanza wana siku 3 tu. Hakuna hatua yoyote ya maana ya ujenzi iliyopigwa.

Wenzao waliokabidhiwa kile kipande kingine kutoka Ubungo mataa, Mwenge hadi Posta wameshafika mbali na wanaonesha hari ya kumaliza kazi yao mapema kabla hata ya muda waliopewa, lakini hawa wa Mwenge to Tegeta bado wanasua sua tu hata Tangibovu hawajaivuka na miezi inazidi kukatika.

Nina hakika hawa watakuja kukifanya hiki kipande kikawie, kama vilivyokawia vile vya phase 2 na phase 3 ambavyo mpaka leo wakandarasi bado wanasua sua tu kumaliza wanashindwa.

Kama wakiendelea kujenga kwa mwendo huu wa konokono, basi nashauri wanyang'anywe ujenzi huu mapema na kukabidhiwa wale wengine wanaoendelea na ujenzi kwa kasi inayotakiwa.

Asanteni.
Nani atamfukuza?
Hiyo 10% waliyokula ndio inampa kiburi.
Hawana ujanja hao nakwambia.
 
Back
Top Bottom