Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahaha hawa watu wakiharibu huwa hawakosi sababu. Let's wait to see nwisho wake 😂😂😂Wameambiwa wakamilishe kwa haraka kipande cha Mwenge hadi Njia Panda ya Kawe, ndio sababu unaona kama wanachelewa ila clearance wameshafika Makonde 😂😂
Mtag BashungwaNiaje waugwana,
Huyu mkandarasi haijulikani alipewa tenda hii ya ujenzi BRT phase 4 kutoka Mwenge hadi Tegeta kwa sifa zipi. Toka tarehe ya ujenzi wa barabara hiyo ilipotangazwa kuanza, hadi leo ni miezi sasa, lakini jamaa utafikiri ndio kwanza wana siku 3 tu. Hakuna hatua yoyote ya maana ya ujenzi iliyopigwa.
Wenzao waliokabidhiwa kile kipande kingine kutoka Ubungo mataa, Mwenge hadi Posta wameshafika mbali na wanaonesha hari ya kumaliza kazi yao mapema kabla hata ya muda waliopewa, lakini hawa wa Mwenge to Tegeta bado wanasua sua tu hata Tangibovu hawajaivuka na miezi inazidi kukatika.
Nina hakika hawa watakuja kukifanya hiki kipande kikawie, kama vilivyokawia vile vya phase 2 na phase 3 ambavyo mpaka leo wakandarasi bado wanasua sua tu kumaliza wanashindwa.
Kama wakiendelea kujenga kwa mwendo huu wa konokono, basi nashauri wanyang'anywe ujenzi huu mapema na kukabidhiwa wale wengine wanaoendelea na ujenzi kwa kasi inayotakiwa.
Asanteni.
Hiyo ni Amri ya Jeshi siyo Mkandarasi 🐼Hahaha hawa watu wakiharibu huwa hawakosi sababu. Let's wait to see nwisho wake 😂😂😂
Kwa nchi hii siwezi kupinga ulichoandika maana kinawezekana kufanywa na wajanja wachache wanaoweka masilahi ya matumbo yao mbele, kuliko masilahi ya taifa.Huenda pesa zishatolewa na zishaliwa. Sasa pesa ya kuwapa wafanyakazi waendelee na ujenzi tena zitatoka wapi?
That's my thoughts
Kuna watu washalamba asilimia kadhaa hapo mkuu, ndomaana unaona ujenzi haueleweki 😂😂Kwa bahati mbaya au nzuri SHANDONG anayejenga Mwenge - Kawe ndio huyo huyo SICHUAN (SBRG) anayejenga Ubungo to kwenda KIMARA......Sawa na ilivyo SINOHYDRO na STECOL yaaani Tanzania raha tupu! Mdomo koma niko ibadani
Bora kama wameambiwa maana pale ni eneo la jeshi....wafanye haraka wamalize wahamie kwingine, wasijefanya yasiyotakiwaWameambiwa wakamilishe kwa haraka kipande cha Mwenge hadi Njia Panda ya Kawe, ndio sababu unaona kama wanachelewa ila clearance wameshafika Makonde 😂😂
Kuna shida gani? Huu mradi wa BRT ni ufadhili wa 100% serikali haitoi hata shilingi ndururu.Hiii barabara ya Mwenge- Victoria inebomolewa tena wakati imejengwa kwa mambilioni wakati wa Magufuu hata miaka mtano bado?
Alafu isitoshe hawabomoi barabara kama alivyofikiri jamaa, bali wanajenga eneo la katikati ambalo liliachwa wazi makusudi kwa ajili ya ujenzi wa BRT.Kuna shida gani? Huu mradi wa BRT ni ufadhili wa 100% serikali haitoi hata shilingi ndururu.
Fanya mambo yako ,angalia familia yako achana na Contractions za watoto wa mjini
Mimi Nina sikia sikia Tu kuna mikono ya watoto wa kiume wa awamu ya D na F
Kuna mwamba kaorodhesha madai kama ya kwako 👇HELA HAMNA.wachina wale.kuna siku nilienda kuomba kazi pale makao yao kona ya kwenda kawe.nikakutq wafanyakazi wana lalamika.pesa haitoki kwa wakati.TATIZO HILO
Jamaa makanjanja sana! Hata wafanyakazi wanaofanya kazi pale wanapigika tu hawapewi mikataba yoyote . Pia wanalipa elfu 12,500 kwa day badala ya 16, 155 kama kima cha chini kinavyo taka . wenzao wa kile kipande cha Mawasiliano -Mwenge -Posta unapoitwa tu siku ya kwanza unapatiwa mkataba siku hiyo hiyo wenye kima cha chini laki 4na20
Nashangaa sana jamaa hawa wanajenga ki local sana
😀😀😀Kwa nchi hii siwezi kupinga ulichoandika maana kinawezekana kufanywa na wajanja wachache wanaoweka masilahi ya matumbo yao mbele, kuliko masilahi ya taifa.