Mkandarasi aliepewa kazi ya ujenzi wa BRT phase 4 kutoka Mwenge hadi Tegeta, anyang'anywe haraka sana kabla hajatupotezea muda

Mkandarasi aliepewa kazi ya ujenzi wa BRT phase 4 kutoka Mwenge hadi Tegeta, anyang'anywe haraka sana kabla hajatupotezea muda

Wameambiwa wakamilishe kwa haraka kipande cha Mwenge hadi Njia Panda ya Kawe, ndio sababu unaona kama wanachelewa ila clearance wameshafika Makonde 😂😂
Hahaha hawa watu wakiharibu huwa hawakosi sababu. Let's wait to see nwisho wake 😂😂😂
 
Niaje waugwana,

Huyu mkandarasi haijulikani alipewa tenda hii ya ujenzi BRT phase 4 kutoka Mwenge hadi Tegeta kwa sifa zipi. Toka tarehe ya ujenzi wa barabara hiyo ilipotangazwa kuanza, hadi leo ni miezi sasa, lakini jamaa utafikiri ndio kwanza wana siku 3 tu. Hakuna hatua yoyote ya maana ya ujenzi iliyopigwa.

Wenzao waliokabidhiwa kile kipande kingine kutoka Ubungo mataa, Mwenge hadi Posta wameshafika mbali na wanaonesha hari ya kumaliza kazi yao mapema kabla hata ya muda waliopewa, lakini hawa wa Mwenge to Tegeta bado wanasua sua tu hata Tangibovu hawajaivuka na miezi inazidi kukatika.

Nina hakika hawa watakuja kukifanya hiki kipande kikawie, kama vilivyokawia vile vya phase 2 na phase 3 ambavyo mpaka leo wakandarasi bado wanasua sua tu kumaliza wanashindwa.

Kama wakiendelea kujenga kwa mwendo huu wa konokono, basi nashauri wanyang'anywe ujenzi huu mapema na kukabidhiwa wale wengine wanaoendelea na ujenzi kwa kasi inayotakiwa.

Asanteni.
Mtag Bashungwa
 
Mkandarasi wa BRT PHASE 2-MBAGALA,PHASE 3-GONGO LA MBOTO na -PHASE 4-TEGETA ni huyo huyo mmoja.....
Ndomaana hata aina ya ujengaji wao ni ule ule wa kusua sua 😂😂
 
Huenda pesa zishatolewa na zishaliwa. Sasa pesa ya kuwapa wafanyakazi waendelee na ujenzi tena zitatoka wapi?

That's my thoughts
Kwa nchi hii siwezi kupinga ulichoandika maana kinawezekana kufanywa na wajanja wachache wanaoweka masilahi ya matumbo yao mbele, kuliko masilahi ya taifa.
 
Kwa bahati mbaya au nzuri SHANDONG anayejenga Mwenge - Kawe ndio huyo huyo SICHUAN (SBRG) anayejenga Ubungo to kwenda KIMARA......Sawa na ilivyo SINOHYDRO na STECOL yaaani Tanzania raha tupu! Mdomo koma niko ibadani
Kuna watu washalamba asilimia kadhaa hapo mkuu, ndomaana unaona ujenzi haueleweki 😂😂
 
Kuna shida gani? Huu mradi wa BRT ni ufadhili wa 100% serikali haitoi hata shilingi ndururu.
Alafu isitoshe hawabomoi barabara kama alivyofikiri jamaa, bali wanajenga eneo la katikati ambalo liliachwa wazi makusudi kwa ajili ya ujenzi wa BRT.
 
Hivi haiwezekani wakawa wanajenga na usiku pia ili kuachia matumizi ya barabara mchana.
 
HELA HAMNA.wachina wale.kuna siku nilienda kuomba kazi pale makao yao kona ya kwenda kawe.nikakutq wafanyakazi wana lalamika.pesa haitoki kwa wakati.TATIZO HILO
 
HELA HAMNA.wachina wale.kuna siku nilienda kuomba kazi pale makao yao kona ya kwenda kawe.nikakutq wafanyakazi wana lalamika.pesa haitoki kwa wakati.TATIZO HILO
Kuna mwamba kaorodhesha madai kama ya kwako 👇
Jamaa makanjanja sana! Hata wafanyakazi wanaofanya kazi pale wanapigika tu hawapewi mikataba yoyote . Pia wanalipa elfu 12,500 kwa day badala ya 16, 155 kama kima cha chini kinavyo taka . wenzao wa kile kipande cha Mawasiliano -Mwenge -Posta unapoitwa tu siku ya kwanza unapatiwa mkataba siku hiyo hiyo wenye kima cha chini laki 4na20


Nashangaa sana jamaa hawa wanajenga ki local sana
 
Back
Top Bottom