DOKEZO Mkandarasi ang'oa milango ya kituo cha afya cha Bulige akilalamika kutolipwa pesa zake

DOKEZO Mkandarasi ang'oa milango ya kituo cha afya cha Bulige akilalamika kutolipwa pesa zake

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hasira hasara za hao mafundi..pesa zikiwa tayari itatakiwa kufanyika ukaguzi kabla ya malipo..watakuja kuyaweka tena
Kufanya biashara na taasisi za serikali unaweza kufa kwa presha. Miaka fulani rafiki yangu alipata tenda ya kusupply vipuri kwenye halmashauri fulani akadhani ameula kumbe ameliwa. amepeleka vipuri amedai ile pesa zaidi ya mwaka. mpaka analipwa nako alitoa rushwa yani hakuna faida aliyopata isipokuwa hasara tu.
 
Sheria ndio iko hivyo.

Ndio maana kuchukua kandarasi za ujenzi wa ofisi au miradi ya serikali inataka connection,maana ni kama betting,ukiishajenga tu ofisi tayari sio mali yako tena,ukifanya kama jamaa ni uhalifu unafanya.

Kazi yoyote ya umma inaambatana na wito kwanza.
mpaka mtu anafikia hatua ya kung'oa anakua kishajiridhisha kuna uhuni umetokea, kama hela hela ilikua imetoka na imeliwa kuna mtu lazima ajinyee kama hela haijatoka na mkandaras kaleta wenge lazima mkandaras ajinyee
 
Hapo unakuta ku sign tu cheki ya malipo anajizungusha zungusha
Fedha zinakuwa zimeidhinishwa lakini lile faili la Miradi lenye malipo yako ndani yake (Hundi) halifikishwi kwake n time na likifikishwa linawekwa chini kabisa kule last but one; na yeye kwa uzembe hafuatilii. Vile vibinti kule fedha na Masjala vinatoa majibu mepesi yenye KERO as if umekuja kuvitongoza. Ukiamua kwenda in Person kwa DED, yule PS anakwambia hayupo, au yuko kikaoni au ana wageni.
Hapo Hasira, Kichefuchefu and what have u. Huku una uhakika wanaokudai wako hapo nje kwa matarajio .......
 
Kwani mkataba wao kabla ya kazi unasemaje?
Mahakama hawazijui?
Kama walikabidhi hapo lazima watanyea debe.
Watanzania wajifunze Sheria.
 
Kakosea.Hilo ni kosa na ni hujuma kisheria.Ameenda kuharibu jengo la umma na si kung'oa milango yake.Alipoweka tu hiyo milango(whatever)haikua yake tena.Ni mali ya umma.Akionewa huruma atalipwa na kuitengeneza upya.Akikutana na mimi bush-lawyer,namtupa geto/mung'anda,atatengeneza upya kwa gharama zake na atatoa fidia.Sipendi mtu mjuaji.
Mjuaji kwenye mali yake? Mali inakuwa yako ukishailipia ja kukabidhiwa.
 
Sijui wanataka hawa mafundi waishi vipi?mbona tenda kubwa mnawalipa wageni before kazi kuanza?kwanini isiwe hivyo kwa hawa wakandarasi wazawa.

Kisheria amefanya kosa ila,mnawaonea hawa watu,

Wanaujuzi hawana elimu.

Thread closed!
 
Daah hakika inaumiza sana hii ishu ya kupata zabuni za serikali.

Kuna brother mmoja alikarabati kituo cha afya mpaka akamaliza.

Ishu ya malipo ikawa ni mtihani mithili ya mtu anataka kukopa hela.

Alidai kwa muda mrefu pasi na kupata stahiki zake.

Hitimisho pekee aloamua kufanya ni kunywa sumu.

Endelea kupumzika John.
 

Umeandika yale walopaswa kumfanyia na wakashindwa means wakakosa utu japo ni haki yake.

Pili umeeleza vema namna alivyoshindwa kuzuia hasira zake (hasara juu ya hasara).

Nadhani hii ishu ifike hatua serikali ithamini juhudi na uwajibikaji wa hawa mafundi wazawa.

Wanawatumia kwa bei za hasara sana na bado hawapewi stahiki zao kama inavyotakiwa.

Hata wakipewa hua wanapewa kwa muda usomwafaka.
 
Achananeni na watu wa halmashauri bwana ,muache fundi akauze hata hiyo milango apate hela ya kuishi Ila hakika namueleza angekuwa kwenye halmsahuri yangu angejuta kuzaliwa
 
Back
Top Bottom