Mkandarasi Kings Ltd tengeneza njia mbadala unapojenga barabara

Mkandarasi Kings Ltd tengeneza njia mbadala unapojenga barabara

Mookiesbad98

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2015
Posts
3,574
Reaction score
4,856
Hili ni kumbusho kwamba Kings umeshinda tenda zote za ujenzi hapa dsm onesha uwezo wako kwa ujenzi wa barabara kuwa wa viwango na uishe kwa wakati kwani umezua taharuki kubwa hasa maeneo ya kilongawima mpaka mbezi jangwani beach.

Ni takwa la. Kisheria na kitendaji unapochepusha barabara basi unahitajika hata kuzipitisha greda ili watumiaji wasafari kwa haraka. Lakini.hilo kule kunduchi NDC halijakaa vizuri na kilongawima kwa Mwamunyange halipo kabisa. Michepusho uliyoiweka ni mibovu na inaharibu.sana magari na kusababisha foleni zisizoepukika.

Lingine naona nafasi ipo lakini unajenga barabara nyembamba sana na.kama serikali ina akili hii njia ya kunduchi ilibidi iwe njia nne kama sio tatu maana ni.njia mbadala ya hiyo ya mwendokasi inayojengwa kivietnam nafasi ipo lakini.kwa ubahili na rushwa inajengwa njia nyembamba.

Hatujaona mitaro inayoeleweka ya kupitisha maji sijui mkataba haukugusa njia za maji maana nyakati.za masika kilongawima inajaaga maji haswa

Nawasilisha

Cc. Mbunge Godfrey Timoth
Waziri wa Ujenzi
 
Mmiliki wa hii kampuni sijui ni nani? Anatesa sana madereva na ile michepuko yake ya kilomita 1+
Yaani unaendesha gari kwenye rough road mpaka unakata tamaa!!
 
Kwa kweli magari yetu.yamekufa kabisa halafu.kumbe kunduchi anatengeneza kopande tu.cha barabara mpaka pale bar ya.malanja basi.

Hivi mbogamboga tumewakosea.nini.unatengenezaje.barabara kopande tuu tena main road ya.kwenda bagamoyo
 
Back
Top Bottom