Mkandarasi wa barabara ya Mbeya mjini inayokwenda kwenda Zambia amesusa kutokana na kutolipwa na serikali?

Shida ni malipo
 
Mkandarasi anadai pesa miradi imesimama harafu Kuna Watu wanatumia Bilioni 34 eti kujenga makumbusho ya Marais ambayo sijui hata nani ataenda kuyasoma wakati hakuna Cha maana wamefanya hao Marais ukimtoa Nyerere.

Nchi Haina vipaombele,hovyo kabisa 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DAkUihpNVl5/?igsh=MXFsaWFjcTlkYTR4Yw==
 
Miradi mingi ya barabara inapumulia mashine.Kuna jamaa yangu mmoja ni mkandarasi wa ndani huwa tunapiga stori ana hali mbaya sana ,njaa ikizidi anaweza kula hata godoro.Anadai serikali haitoi hela wanategemea January,2025 labda ndio iwalipe.
 
Huenda ni kweli kabisa.....
 
Miradi mingi ya barabara inapumulia mashine.Kuna jamaa yangu mmoja ni mkandarasi wa ndani huwa tunapiga stori ana hali mbaya sana ,njaa ikizidi anaweza kula hata godoro.Anadai serikali haitoi hela wanategemea January,2025 labda ndio iwalipe.
Na 2025 ni mwaka wa uchaguzi.
 
Hii ni kwa ajili ya makumbusho yake mwenyewe Samia, asitumie kisingizio cha maraisi waliopita. Anataka tu asisahaulike kama raisi mwanamke wa kwanza Tanzania
 
Ndio,lakini tulielewa serikali ilikuwa inafanya makusudi kutopeleka miradi Mbeya kwa sanabu Mbeya hawakuitaka CCM. Sasa Mbeya si waliahidiwa wakiwaondoa upinzani miradi yao itaenda? Kulikoni sasa?
Kinashangaza na hujuma zote bado kimapato iko juu,hili fisiem linawauma sana!
 
Porojo za vijiweni 👇👇
Haya mambo inaonekana huelewi yanavyoenda. Ni kweli kwamba sasa wanaweza kuwa wamepata hela za kuendelea na kazi na kutoa video kama hizi kwa sababu wanajua watu waliona kuwa mradi umesimama. Unafiiri, kwa uwezo wa akili yako, watakuambia kweli tulipata changamoto sasa kuna fedha kidogo imepatikana tunaendelea ila mradi utachukua zaidi ya miaka miwili tofauti na ilivyokuwa imepangwa? Hata kama wamepata fedha ya miezi mitatu tu watasema hakuna tatizo mambo yako sawa mradi utakamilika -ila kukiwa na sababu za msingi za ucheleweshaji mkandarasi atatuandikia. Hebu jaribu kuwa na akili uliyopanuka kuelewa mambo ya serikali yanavyowekwa hadharani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…