DOKEZO Mkandarasi wa Reli ya SGR ameishiwa Mafuta ya Diesel, Mradi umesimama, hatufanyi chochote

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Sa100 hii miradi hana nia nayo mpaka anaondoka hakuna utakao kamilika.
 
Siku zote mwenye mradi akiondoka na miradi hufa.
Hakuna aliyepo anaendeleza alichokikuta
 
Haraka ya Nini kuwafungia watu njia zao za asili kwa kuwawekea fence fence ilitakiwa mwishoni kabisa Leo watu wanapata tabu sana kuvuka upande wa pili wa reli kwa sababu ya uzio bila kuacha watu na bodaboda sehemu za kupita kwa kuziba pote sababu wao wanakaa masaki na Osterbay
 
Kumbe watu wenye maarifa bado wapo humu, maan kuna mwingne atakuja kushusha lawama kwa serikali ya Chama tawala
 
Huu mradi umekufa na maghufuli wazee wa malori na mabus sidhani Kama wataukuacha uendelee.
Mradi wa reli SGR na Tazara ,bomba la mafuta tazama ni tishio kwa biashara za GSM,lake oil,oilcom,, Esther
 
Ehhh! Mungu saidia hii ngozi nyeusi walau tutoke hapa tulipo. Kwanini mambo yetu yanakwama kila tukifurukuta? Ni kweli sisi tumelaaniwa?
 
Mimi niseme wazi, huu mradi nilipata utata baada ya kusoma habari fulani kuhusu kampuni ya KORAIL na hawa YAPI MERKEZI wajuzi mtanisaidia kama nipo sahihi. Pia, huwa nayaona magari ya KORAIL kwenye mkoa fulani hivi.

Kwamba, serikali ya Tanzania ilisaini mkataba wa SGR na KORAIL, halafu hao KORAIL wakawapa Yapi Merkez! Hapa tayari kuna halufu ya udalali. Yaani kuna wabongo ndio wanaimiliki YAPI MERKEZ, au kwa namna nyingine kuna watu kati (middlemen) ambao ni wabongo waliunganisha dili kati ya KORAIL,. SERIKALI na YAPI MERKEZ.

Samahanini kama nitakuwa nilipotoka kuhusu KORAIL, basi mtanisahihisha kuhusu uhusika wa KORAIL katika huu mradi wa SGR.

KORAIL ni kampuni kutoka Korea Kusini.
 
Hongera sana mzalendo wa kweli πŸ™πŸ™πŸ™
 
Inasikitisha sana,hii miradi kukamilika utawala wa sa100 sahauni
 
Mm naona huo mradi kuna watu hawataki uishe kabisa,kwa sababu zao wenyewe.
 
Mbona mchina wa lot ya Mwanza hana makelele na anapiga kazi kama kawaida! kwa nini walichukuwa mkandarasi asiekuwa na mtaji? .

Yule CCECC anajenga Kigongo-Busisi na SGR na hana malalamiko.
 
STG ,na bwawa la umeme Ni miradi toka magu anazindua nilikuwa ninawasiwasi nayoo ...haikuwa na Baraka kabisa ya baadhi ya viongozi ,ndio maana wanaipuuza
Hakuna kiongozi mpenda maendeleo aichukie hyo miradi hila njia alizokuwa jpm anatafuta hela kwahyo miradi ndio ngumu mama akisema afuate njia hyo mtalalamika deni la taifa limezidi jpm alikuwa anakopa kwenye mabank ya kibiashara yenye riba kubwa sana mama hawezi kukopa huko lakini ana njia zake kutafuta pesa miradi iendelee na itaendelea
 
Mbona jibu ni simple, mwenye mradi, Serikali, hana hela za mradi!
Utamlaumu mkandarasi bure!!
 
Huyo mkandarasi anataka sisi tumnunulie dizeli? kama aligawa rushwa awafuate hao hao wampe pesa ya dizeli sisi tunahitaji mradi ukamilike kwa wakati.
Haya ni maneno ya mtoto aliybebwa kwenye mbeleko, mama kachoka anakaribia kuzimia, yeye mtoto analilia pipi ya mjini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…