Huyu Yapi atakuwa kandarasi wa kazi za kuunga unga pengine na mtaji wake ni mdogo.
Kama yeye miezi saba hajalipa wafanya kazi wake na anatoa tangazo la kulipa nusu mshahara na siku ya malipo kama nimeona vizuri ni ijumaa ambayo ni sikukuu, huo ndio uhuni na utapeli wa hali ya juu.
Siku moja nilisikiliza hotuba ya Mheshimiwa akisema Yapi walipe hao makandarasi ili kazi iishe kwa wakati,
Tuseme government ndo haimlipi Yapi, maana mikataba ya malipo inafahamika, kandarasi hulipwa kila baada ya hatua au baada ya kipande fulani cha kazi.
Yapi tuseme kalipwa kalala mbele na hela za watu?
okay, endapo wafanyakazi wa Yapi watagoma wao kama front line ya kazi, hao wa nyuma yao watafanya kazi gani.
Au tuseme reli ya Mheshimiwa imesimama kujengwa mpaka kandarasi aamue kulipa wafanyakazi wake na alipe kandarasi nyingine ndogo ndogo.
Hapa ni jamvini, Mheshimiwa yuko msibani lakini anao vijana wake huku mitandaoni ambao yote mema hata mabaya yatamfikia.
Poleni wafanyakazi wote na kandarasi zote mnaofanya kazi kwenye reli ya Mheshimiwa.
Hili nalo litapita, ni muda tu.
Sent using
Jamii Forums mobile app