Mkapa awapa neno wanaotaka Magufuli aongoze mihula mitatu

Hata ungemleta Trump akasimamia Uchaguzi, JPM 2020 atashinda kwa kura nyingi. Mnajidanganya hasa watoto wa mitandao
Mkuu 'Njinjo', kwani kuna sehemu yoyote uliyonisoma na kukuta nikikataa asishinde uchaguzi ulio huru.

Hebu nisome tena vizuri unielewe nilichoandika.

Atapata heshima kubwa sana akiruhusu uchaguzi wa wazi, huru kabisa na ashinde kwa kishindo kama unavyoeleza hapa.

Mimi pia nitampongeza sana kwa ushindi wa aina hiyo.

Lakini akilazimisha kubaki madarakani kwa njia zozote, ziwe za kuiba kura, kunyima watu wasitumie haki yao ya kuwachagua viongozi wao kwa kuwakandamiza akitumia polisi ili abaki madarakani; hebu niambie ukweli kabisa mkuu 'Njinjo' wewe bado utakuwa unaendelea kushangilia maovu hayo?

Naomba unijibu kama umenielewa nilichoandika hapa.
 
Usitumie watanzania kwani wanao piga kura wote wanakad za vyama vyao na wanamapenzi na vyama vyao hamna mtanzania wa kawaida alie wahi kwenda kupiga kura wala kuchagua mtu mfano ni mm kwanza siamin katika siasa na wala siwez poteza muda kwenda kupiga kura eti nachagua fulan

Sent using Jamii Forums mobile app
Kapige tu Kura mkuu, huna cha kupoteza. Piga kura rudi nyumbani ukajitulize.
 
Una hakika unayo akili timamu?

Wewe ndio una akili timamu kutaja marais wa hovyo hivyo kua mifano ya sisi kuiga?

Akili yako ina akili kweli?

Marais takataka kabisa hao mnawataja as if ndio wa kupigia mfano?

Mbuzi wa maziwa nyie!
 
Mkuu 'Njinjo', kwani kuna sehemu yoyote uliyonisoma na kukuta nikikataa asishinde uchaguzi ulio huru.

Hebu nisome tena vizuri unielewe nilichoandika.

Atapata heshima kubwa sana akiruhusu uchaguzi wa wazi, huru kabisa na ashinde kwa kishindo kama unavyoeleza hapa.

Mimi pia nitampongeza sana kwa ushindi wa aina hiyo.

Lakini akilazimisha kubaki madarakani kwa njia zozote, ziwe za kuiba kura, kunyima watu wasitumie haki yao ya kuwachagua viongozi wao kwa kuwakandamiza akitumia polisi ili abaki madarakani; hebu niambie ukweli kabisa mkuu 'Njinjo' wewe bado utakuwa unaendelea kushangilia maovu hayo?

Naomba unijibu kama umenielewa nilichoandika hapa.
Uchaguzi mtakaouita huru na haki ni pale atakaposhindwa tu. Hata aje trump kusikamia, asiposhindwa mtalalama ati si huru na haki. Dawa yenu ni kuweka nta katika masikio na kuvaa Miwani ya mbao. Maisha yanasonga mbele. Angalia watu wqnanyanyaswa CDM wakihama ati wamenunuliwa, nyalandu huyo ni jembe kwa vile katoka kule. Hamna maana nyie wote hapa JF
 
America ina utamaduni wa kuchagua Rais ambaye anatakiwa abaki madarakani kwa term mbili tu, lakini kwenye miaka ya1930/40s Rais Roosevelt alichaguliwa kuwa Rais kwa term nne kutokana na hali ya uchumi pamoja na WW2 - wananchi waliona kwamba Rais Roosevelt ndiye alikuwa na uwezo mkubwa kuongoza Taifa hilo wakati likiwa linakabiliana na WW2 sio kwamba walikosa kumpata Rais mbadala, la hasha, wapiga kura waliona Roosevelt ndiye alikuwa na uwezo mkubwa kulivusha Rubicon Taifa la Amerika.

Binafsi naona uongozi wa awamu zilizopita ndio walihusika kutumbukiza Taifa letu kwenye kuendekeza rushwa, ufisadi ulio pitiliza mipaka, kukosa uwajibikaji, nepotism and all vices you can imagine - hali ilikuwa imefikia kwenye level ya kutisha.

Mungu bariki kalipatia Taifa letu Franklin Roosevelt wa Tanzania, yaani ndani ya miaka minne karekebisha uozo ulio kuwa umejengeka kwa zaidi ya miaka thelathini mfululizo, kafikia hatua ya kuleta wawekezaji wa kweli wasio wababaishaji wakajenga viwanda vingi, ujenzi wa miuondo mbinu ya kimataifa, ujenzi wa Gigawatts hydroelectric power Complex, usafiri wa anga majini na nchi kavu,kajenga mashule pamoja na maabara, vyuo vya ufundi, kafuta karo, kajenga vituo vya afya nchi nzima na kununua vifaa tiba vya gharama kubwa vyenye uwezo wa kuifanya Tanzania kuwa Taifa lenye uwezo mkubwa wa kutibu magonjwa yaliyo shindikana, si ajabu Taifa letu likiwa nchi ya utalii wa kitibabu kama ilivyo Apollo ya India, karudisha nidhamu kazini na kudhibiti cancer ya rushwa; katekeleza yote hayo tajwa hapo juu ndani ya miaka minne ya uongozi wake - Mungu atupe nini Watanzania.

Franklin Roosevelt aliendelea kubaki madarakani kwa utashi na mapendekezo ya wapiga kura wa Marekani kutokana na uchapa kazi wake uliyo tukuka, alichaguliwa mara nne kuwa Rais wa Amerika wakati Taifa hilo lilipo kuwa linapitia kwenye wakati mgumu wa kiuchumi na vita. Taifa letu halina tofauti kubwa na changa moto zilizoikumba America kwenye miaka ya 1930s na 1940s - Wamerika walikata shauri kwamba F.D Roosevelt ndie awaongoze bila ya kujali terms za kubaki madarakani, na sisi tunapashwa kuiga mfano mzuri wa wapiga kura wa USA in 1930/40s, tuwe wakweli hapa JPM ana kalama za uongozi na uthubutu kama wa the late F.D Roosevelt ni vema akiendelea kubaki madarakani mpaka Taifa letu litakapo nyooka - tukifanya makosa ya kujidanganya kwamba Rais atakaye kuja ataiga na kuendeleza yote yale yaliyo jengwa na JPM tutakuwa tunajidanganya - wataingia Viongozi wasiojali ambao wataturudisha nyuma yale yote yaliyo simamiwa na Rais Magufuri - tuwe makini sana kabla hatuja haribikiwa, tusitegemee kila Rais atakuwa na uwezo mkubwa wa kiongozi kama wa mzalendo JPM.

Baadhi ya Viongozi wa hivi sasa na wale waliopita wanao jaribu kuweka shinikizo kwamba JPM aongoze kwa term mbili tu, binafsi naona watu hao hawana uchungu wa kweli wa Taifa letu, wanafikiria nafsi zao tu na jamaa zao, kwa kifupi wanataka turudi kule tulipo toka - watu wachache walafi ndio waendelee na ufisadi wao kama kawa na safari hii itakuwa mbaya zaidi - chunguza kwa umakini wale wote wanao fanya kampeini za chini chini za kutaka JPM awe Rais wa term moja tu, na wale wanao jifanya wanatoa ushauri kwa Rais kwamba asizidishe term mbili wanajifanya hawaoni miujiza aliyo fanya JPM katika kipindi chake kifupi cha Uongozi, ukiwangalia washauri hao vizuri usoni wanaonekana wazi wazi wanayo sema hayatoki ndani ya mioyo yao, in other words ni hypocrite - walivyo wa ajabu, hakuna ambaye ana hoji Mwalimu alidumu madarakani kwa miaka mingapi na aliacha Taifa letu likiwa hali gani kiuchumi na kifedha?

Kwa nini tug'ang'anize term mbili kwa mtu ambaye anafanya vizuri karibu kila nyanja ya kuendeleza Taifa letu na hizi si adhithi ni mambo yanayo onekana wazi wazi,kuna haja gani ya kumpangia terms ambazo tunataka abaki madarakani - kwa nini tusipitishe referendum kwa wapiga kura nchini tukawasikiliza wana maoni gani kuhusu muda wa JPM kubaki madarakani, na JPM aheshimu maoni ya wapiga kura.
 
Nguvu ya kanisa katorik mzee
Ila mzembe alikuwa JK alizidiwa saana nguvu na BEN haiwezekani kipindi kile JK alikuwa amri jeshi mkuu. Rais na Mwenyekiti wa chama anazidiwa nguvu na Mkapa ambaye hakuwa na chochote zaidi ya kuwa na sifa ya kuwa rais wa awamu ya 4. JK alikosea sana kuwa mwepesi. Angepinga na lolote liwe.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ndio una akili timamu kutaja marais wa hovyo hivyo kua mifano ya sisi kuiga?

Akili yako ina akili kweli?

Marais takataka kabisa hao mnawataja as if ndio wa kupigia mfano?

Mbuzi wa maziwa nyie!
Wyatt Matthewson, ya nini tupigiane kelele hapa mkuu wangu.

Nakuomba tafadhari sana, hebu jaribu tena urudi nyuma usome nilichoandika mimi na wewe ukajibu kama ulivyojibu.

Huu utakuwa ni uungwana tu kwa upande wako. Nakuomba sana ufanye hivyo, pamoja na kwamba utapoteza mda wako.

Soma kwa utulivu nilichoandika kwenye bandiko lako na jinsi wewe ulivyojibu. Ukijiridhisha kwamba jibu lako lipo sahihi, nitarudi hapa nikuombe radhi.

Jaribu hasa kuwekea uzito nilipowataja hao marais, "Museveni, Kagame, Nkurunzinza, Mugabe" kuwa ndio niliowataja kuwa mfano wa kuigwa na viongozi wa Tanzania.

Natanguliza shukrani zangu kwa usumbufu huu kwako mkuu wangu.
 
M
Analogia Malenga,
Katika watu waliopelekea watz leo hii wawe wanaishi kama mashetani huyo mzee Mkapa. Halafu leo anataka kujikosha
Na bado anasema jiwe apewe vipindi viwili.
Anasema viwili hata uchaguzi haujafanyika.
Kwa hiyo matokeo nayajua.
Sasa alipokua anasema wapinzani washiriki kuhesabu kura alikua anamaanIsha Nini,na alipokua akisema kuwe na tume inayokubalika na wote alikua anamaanIsha Nini.MUNGU fanya Jambo tafadhari.
 
M
Na bado anasema jiwe apewe vipindi viwili.
Anasema viwili hata uchaguzi haujafanyika.
Kwa hiyo matokeo nayajua.
Sasa alipokua anasema wapinzani washiriki kuhesabu kura alikua anamaanIsha Nini,na alipokua akisema kuwe na time inayokubalika na wore alikua anamaanIsha Nini.MUNGU fanya Jambo tafadhari.
Ccm na unafki ni chanda na pete
 
RAIS wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, amesema ana hakika Rais Dk. John Magufuli hatataka kuongeza mhula wa tatu wa uongozi badala yake atafuata nyayo za watangulizi wake kwa kuhudumu mihula miwili.

Alitoa kauli hiyo jijini Mwanza juzi wakati wa hafla ya utambulisho wa kitabu chake cha ‘My Life, My Purpose’ kinachoelezea maisha yake.

Mkapa alisema kazi ya urais ina changamoto nyingi na ina majaribu tofauti kutoka ndani na nje ya nchi, hivyo linapokuja suala la kukaa madarakani kwa zaidi ya mihula miwili haoni sababu ya kufanya hivyo.

Alisema anaamini kuwa hata Dk. Magufuli hawezi kuongeza muda wa kukaa madarakani kwani licha ya ugumu wa kazi hiyo pia umekuwa kama utamaduni wa taifa.

“Kuna maneno nayasikia sikia watu wanasema eti Rais Magufuli anaweza kubadili Katiba na akabakia madarakani kwa zaidi ya mihula tuliyoizoea kwa maana ya mihula miwili ya kipindi cha miaka kumi, binafsi sidhani kama hilo lipo na hata simshauri kufanya hivyo.

“Labda niwakumbushe tu, kipindi nilipokuwa madarakani kuna wakati wazee wa Zanzibar walinifuata mara kadhaa wakiniomba wao kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi wabadilishe Katiba ili wapate fursa ya kumchagua kiongozi kwa mihula mitatu kwa maana ya miaka 15, suala ambalo naweka wazi kuwa lilitaka kutikisa kidogo muungano wetu.

“Pamoja na kuniomba sana sikuwa tayari kuunga mkono suala hilo, walifanya kila liwezekanalo kunishawishi lakini niligoma na mwisho walinielewa na kuendelea na utaratibu wa kawaida wa mihula miwili ya miaka mitano kila mmoja na hadi sasa wameendelea nao.

“Ninachoweza kusema ni kwamba utaratibu huu wa mihula miwili, sasa hata Watanzania weshauzoea na umegeuka kama utamaduni wa taifa.

“Pia naweza kusema pengine umechangia kwa kiasi kikubwa kulifanya taifa letu kuendelea kuwa na demokrasia ya mfano, hivyo ninaamini hata Rais hatabadilisha Katiba kwenye hilo.

“Ndiye aliyenifuata (Rais Magafuli) akaniambia mzee tukitegemea sana hawa wahisani kasi yetu ya ujenzi wa miundombinu itakuwa ndogo sana. Kwanini sisi wenyewe hatuwezi kuwathibitishia kwamba tuko tayari ‘ku-sacrifies’ kutumia mapato yetu wenyewe kujenga barabara zetu.

“Nikamkubalia tukaenda kwenye Baraza la Mawaziri tukaamua kila mwezi tutatenga kiasi fulani cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara. Ni kazi ya Magufuli.

“Mimi nimeshukuru wananchi wenzangu waliona anafaa huyu, na sasa anaongoza awamu ya tano, Mwenyezi Mungu ampe afya njema aweze kukamilisha na yeye mihula miwili, nina hakika hatataka wa tatu hata kidogo kwa sababu mmeona alivyobadilika katika miaka minne hii,” alisema Mkapa.

SERA YA UBINAFSISHAJI

Akizungumzia sera yake ya ubinafsishaji wakati wa utawala wake, alisema ingawa amekuwa akilaumiwa namna uchumi wa taifa ulivyokuwa umefikia wakati huo, hakukuwa na namna nyingine ya kulijenga taifa tofauti na kufanya ubinafsishaji.

Alisema katika kipindi hicho nchi wahisani na wafadhili walikuwa wameanza kuikimbia Tanzania kutokana na hali ya uchumi isiyoridhisha na kuwa katika hatari ya kupoteza misaada kwa kiwango kikubwa.

Mkapa alisema ili kuwaaminisha wahisani kuwa uchumi wa Tanzania unajengwa kwa kushirikisha Serikali na taasisi binafsi, ilimbidi kufanya ubinafishishaji na jambo lililowezesha taifa kuaminika.

“Jambo lingine ambalo linasemwa ni kwamba ubinafsishwaji Baba wa Taifa hakuupenda, ni kweli lakini nieleze wazi kwamba hakukuwa na ‘altenative’, mashirika haya tuliyaanzisha ili yawe ya kiuchumi kupata faida na faida hiyo iletwe serikalini tuweze kupanua huduma za jamii na miundombinu ya nchi yetu.

“Mengi badala ya kuleta faida walikuwa wanaomba ruzuku kutoka Hazina, tusingaliweza kuvumilia, ilitubidi kutafuta namna ya kuhuisha biashara hizo, viwanda hivyo na hivyo ndivyo tulivyofanya.

“Pointi yangu ni kwamba nilitaka kudhihirisha maendeleo yanaweza kusukumwa na wote sekta binafsi pamoja na Serikali. Kuna mambo ambayo sekta binafsi haiwezi kuchukua gharama zake na hayo yatabebwa na Serikali, miundombinu na kadhalika.

“Lakini kwenye elimu kwa mfano hakuna sababu ya kuzuia sekta binafsi isianzishe shule, kwa hiyo tumemsikia Profesa hapa tulianzisha vyuo vyote hivi kwa sababu tulifikiri kwa ushirikiano huo ndiyo tunaweza kueneza elimu kwa watu wengi zaidi,” alisema Mkapa.

VIONGOZI VIJANA

Kuhusu viongozi vijana, alisema ni lazima vijana wanapotaka kuwa viongozi wasikimbilie tu kujiingiza kwenye siasa, bali wajiandae kwa kiwango cha kutosha ili wanapochukua nafasi ya kuwatumikia wananchi wawe na uwezo wa kulisaidia taifa.

“Ninachoweza kuwashauri ni kuwa kabla ya kuchukua maamuzi ya kutaka uongozi, vijana wanatakiwa wajaribu kujiimarisha, kujifunza na kujiandaa vya kutosha na wakati ukifika basi wawashirikishe wazee waliowatangulia. Kwa kufanya hivyo, natarajia kuona viongozi wenye hekima na busara na watakuwa na maamuzi yenye tija kwa taifa,” alisema Mkapa.

Aliwaasa vijana kujenga utamaduni wa kusoma vitabu na kuachana na kutumia muda mwingi kwenye mitandano kwani maarifa ya kweli yanapatikana kwenye vitabu na ndiyo maana viongozi wengi wa zamani si tu walikuwa na weledi, bali utamaduni wa kujisomea uliwaimarisha kiakili na kuwafanya wasiwe watu wa kuyumbishwa.

Mkapa alidai kuwa amekuwa akilaumiwa kuwa yeye ni jeuri na kwamba anajiona, hivyo aliwaasa watu kusoma kitabu chake waamue kama ni kweli yeye ni jeuri.

KUANDALIWA NA NYERERE

Kuhusu kuandaliwa na Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere kuwa rais, alisema jambo hilo si kweli licha ya watu wengi kuamini kuwa alimpigia debe tangu kwenye mchakato wa kupitishwa na chama.

“Nilichokuwa na hakika nacho katika kufanya kampeni baada ya ‘nomination’, aliniunga mkono na wengine mnajua alifanya kampeni hapa Shinyanga mpaka Tabora,” alisema Mkapa.

Pia alieleza jinsi ambavyo Mwalimu alipinga uamuzi wa timu yake ya kampeni wa kutaka wakodi helkopita ili kufanya kampeni.

“Mwalimu alipinga akisema kuwa hata kama Mungu angetuma malaika wake wawatake watumie helkopita angempinga, kwa sababu kampeni zinahitaji watu waonane, hivyo wasingeweza kutumia usafiri huo,” alisema Mkapa.

SERIKALI YA KIZAZI KIPYA

Alisema kuwa wakati anaunda Serikali yake bungeni kulikuwa na mawaziri wakuu wawili ambao walikuwa wamechaguliwa tena kuwa wabunge ambao aliwaita kwa heshima na kuzungumza nao na kuwaeleza kuwa watamsaidia wakiwa ‘back banch’ siyo katika Serikali yake.

Alisema kuwa lengo lake lilikuwa ni kuunda Serikali yenye kizazi kipya katika siasa, mmoja wao akiwa ni Rais wa sasa Dk. Magufuli, ambaye alikiri kuwa alifanya kazi kubwa ikiwamo kutekeleza ujenzi wa daraja la kuunganisha mikoa ya Kusini katika bonde la Mto Rufiji, maarufu Daraja la Mkapa.

Mkapa alisema hata pale ambapo Dk. Magufuli alipomfuata kumtaka daraja hilo lipewe jina lake alikataa, akiamini kuwa lilipaswa kuitwa jina la Magufuli, lakini alishangazwa wakati wa kulizindua alielezwa kuwa imekwishaamriwa litaitwa kwa jina lake.

NYAYO ZA MKAPA

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Balozi Profesa Costa Mahalu, alisema kama taifa lazima viongozi wafuate nyayo za Mkapa kwani ni muwazi, mkweli na msikivu jambo ambalo viongozi wengi wa Afrika wanakosa.

Alisema iwapo wataweza kufuata nyayo hizo, taifa linaweza kuepuka migongano ya mara kwa mara kati ya viongozi wa Serikali, vyama na wananchi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, alisema uamuzi wa Rais Mkapa kuandika kitabu ni jambo la kujivunia kwa kila mwenye maono mazuri na taifa, kwani ameyafanya mawazo yake yaweze kuishi milele na kuweza kutumiwa na watu wanaotaka kuingia kwenye uongozi.

Chanzo: Mtanzania
Daah
 
Ama kweli saut ya mamlaka imetoweka
 
Back
Top Bottom