Mkapa awapa neno wanaotaka Magufuli aongoze mihula mitatu

Mkapa awapa neno wanaotaka Magufuli aongoze mihula mitatu

Kama kuongeza muhula ndo kutafanya daraja la busisi lijengwe na kukamilika,basi aongeze tu, Mimi chadema damu ila kwa ujenzi wa daraja la busisi huyu rais kanikosha kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa watu bwana, na heshima zao wanazopewa na wananchi, sijui akili zao wanaziweka wapi.

Mseveni sio rais, na changamoto hizo anazozungumzia Mkapa hazimhusu?

Kagame je, Nkurunziza, Mgabe na wengine wengi.

Wote hawa changamoto za urais hawakuwa nazo?

Yeye Mkapa, anaona dalili zote, na juhudi kubwa anazofanya kijana wake, halafu anaibuka na komedi za aina yake!

Hapo kijana wake atakapokuwa ametimiza matakwa yake ya kubaki madarakani, tena sio kwa kuongeza ngwe ya tatu tu, bali na zaidi na zaidi..., hapo Mkapa mwenyewe atakuja na maelezo mengine ya kuhalalisha hali hiyo, na kuwaona waTanzania kama mazuzu hivi.

Mtu anafanya juhudi zote kuua upinzani. Anataka ushindi wa asili mia 99..., anataka hayo kwa sabau zipi kama sio kutafuta njia za kuhalalisha nia ovu hiyo.

Umetaja marais vichaa watupu

Museveni,Mugabe,Nkurunzinza,Kagame,etc

Madikteta watupu,hao ndio marais wa Tanzania kuiga?

Bure kabisa!
 
Mkuu hupendi kipenzi chako aongoze walau miaka 15 au ishirini hivi
Makubaliano yetu kama Taifa ( Katiba) hayaruhusu hilo. Kama anavyosema Mkapa, huo umeshageuka kama utamaduni wetu. Mimi ninatoka katika kabila ambalo huwa tunaheshimu sana mila/tamaduni, hivyo napenda mno kuona tamaduni zikilindwa, ni muhimu pia kama Taifa tukawa na utamaduni wa kuheshimu tamaduni zetu.

Magufuli ni kiongozi ambaye umaarufu wake umetokana na kupenda kufuata sheria na haja badilika katika hilo mpaka sasa, naamini hatabadilika, na hata kiuka huu utamaduni tuliojiwekea.
 
Huu utetezi wako ungekuwa na maana iwapo tu angekuwa hanajisi box la kura. Ni hivi, Magufuli ana mpango kwa wazi kutaka kujiongezea muda wa kukaa madarakani, na hilo atalifanya kwa wabunge wote kuwa wa viti maalum huko bungeni, kwani watapita bila kupingwa, na hapo ataweza kuwaamrisha wamuongezee muda wa kukaa madarakani kwani hata yeye atawambia kawapa ubunge wa mezani, vinginevyo wakigoma atawatushia kulivunja bunge warudi wakapambana kiukweli kitu ambacho wabunge hao wanajua hawawezi kushindana kwenye uchaguzi huru


Hiyo ndio hali halisi. Mkapa ameshaona muelekeo kuanzia hii kuchezea chaguzi za nchi, na ndio maana alisema anatamani kuwe na tume huru ya uchaguzi, na kwenye tume hiyo wapinzani washirikishwe. Anajua fika aliyempendekeza atakuja kuleta matatizo makubwa huko mbeleni. Ni muda tu utasema yote.
Na wewe ni mpuuzi tu
 
Ya nini kwenda kote huko 2025!

Akubali sasa hivi uchaguzi uwe huru na haki. Akishinda katika hali hiyo, tutaelewa hata hiyo 2025, kama anataka kuendelea katika mazingira yaliyo wazi na huru, hakuna atakayelalamika.
Hata ungemleta Trump akasimamia Uchaguzi, JPM 2020 atashinda kwa kura nyingi. Mnajidanganya hasa watoto wa mitandao
 
Back
Top Bottom