Mkapa awapa neno wanaotaka Magufuli aongoze mihula mitatu

Mkapa awapa neno wanaotaka Magufuli aongoze mihula mitatu

Hofu yangu , atakaeingia awamu ya sita ataendeleza kazi ya JPM ? Japo sio utamaduni wetu tumpe mda zaidi ainyooshe nchi ,matunda yameshaonekana .

Sent using Jamii Forums mobile app

Hayo matunda yaliyoonekana ni
1. kufa kwa private sekta
2. Kudumaza demokrasia nchini na kufanya siasa za kikatili na uonevu
3. Kuumiza wakulima wa korosho
4. Kupotea trilion 1.5
5. Kufanya manunuzi ya ndege bila kupitia bunge na sheria ya procurement
6. Kununua wapinzani
7. Kauli tata na zisizo za kiungwana kwa watoto wa kike wenye ujauzito, wahanga wa tetemeko kagera
8. Kuongezeka kwa deni la taifa kwa kasi ya kutisha
9. Kutoajiri
10. Kutolipa madeni ya watu wanayoidai serikali
11. Hakuna nyongeza za mishahara kwa wafanyakazi
12. Kuchelewesha madeni ya pensheni ya wazee wastaafu na kuwapiga danadana
13. Kuwanyima wananchi haki yao ya kuchagua viongozi wanaowataka kwa kuwasimikia viongozi wa serikali za mitaa
14. Kuwapa watu wanaokosoa na wafanyabiashara kesi za uhujumu uchumi na kuwatoa baada ya kuwakamua pesa
15. Teuzi zinazonuka ubaguzi wa kidini na kikanda
16. Watu kuokotwa kwenye viroba kwenye fukwe za bahari bila kujulikana wametoka wapi

Hayo ndo matunda yanayoonekana?
 
RAIS wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, amesema ana hakika Rais Dk. John Magufuli hatataka kuongeza mhula wa tatu wa uongozi badala yake atafuata nyayo za watangulizi wake kwa kuhudumu mihula miwili.

Alitoa kauli hiyo jijini Mwanza juzi wakati wa hafla ya utambulisho wa kitabu chake cha ‘My Life, My Purpose’ kinachoelezea maisha yake.

Mkapa alisema kazi ya urais ina changamoto nyingi na ina majaribu tofauti kutoka ndani na nje ya nchi, hivyo linapokuja suala la kukaa madarakani kwa zaidi ya mihula miwili haoni sababu ya kufanya hivyo.

Alisema anaamini kuwa hata Dk. Magufuli hawezi kuongeza muda wa kukaa madarakani kwani licha ya ugumu wa kazi hiyo pia umekuwa kama utamaduni wa taifa.

“Kuna maneno nayasikia sikia watu wanasema eti Rais Magufuli anaweza kubadili Katiba na akabakia madarakani kwa zaidi ya mihula tuliyoizoea kwa maana ya mihula miwili ya kipindi cha miaka kumi, binafsi sidhani kama hilo lipo na hata simshauri kufanya hivyo.

“Labda niwakumbushe tu, kipindi nilipokuwa madarakani kuna wakati wazee wa Zanzibar walinifuata mara kadhaa wakiniomba wao kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi wabadilishe Katiba ili wapate fursa ya kumchagua kiongozi kwa mihula mitatu kwa maana ya miaka 15, suala ambalo naweka wazi kuwa lilitaka kutikisa kidogo muungano wetu.

“Pamoja na kuniomba sana sikuwa tayari kuunga mkono suala hilo, walifanya kila liwezekanalo kunishawishi lakini niligoma na mwisho walinielewa na kuendelea na utaratibu wa kawaida wa mihula miwili ya miaka mitano kila mmoja na hadi sasa wameendelea nao.

“Ninachoweza kusema ni kwamba utaratibu huu wa mihula miwili, sasa hata Watanzania weshauzoea na umegeuka kama utamaduni wa taifa.

“Pia naweza kusema pengine umechangia kwa kiasi kikubwa kulifanya taifa letu kuendelea kuwa na demokrasia ya mfano, hivyo ninaamini hata Rais hatabadilisha Katiba kwenye hilo.

“Ndiye aliyenifuata (Rais Magafuli) akaniambia mzee tukitegemea sana hawa wahisani kasi yetu ya ujenzi wa miundombinu itakuwa ndogo sana. Kwanini sisi wenyewe hatuwezi kuwathibitishia kwamba tuko tayari ‘ku-sacrifies’ kutumia mapato yetu wenyewe kujenga barabara zetu.

“Nikamkubalia tukaenda kwenye Baraza la Mawaziri tukaamua kila mwezi tutatenga kiasi fulani cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara. Ni kazi ya Magufuli.

“Mimi nimeshukuru wananchi wenzangu waliona anafaa huyu, na sasa anaongoza awamu ya tano, Mwenyezi Mungu ampe afya njema aweze kukamilisha na yeye mihula miwili, nina hakika hatataka wa tatu hata kidogo kwa sababu mmeona alivyobadilika katika miaka minne hii,” alisema Mkapa.

SERA YA UBINAFSISHAJI

Akizungumzia sera yake ya ubinafsishaji wakati wa utawala wake, alisema ingawa amekuwa akilaumiwa namna uchumi wa taifa ulivyokuwa umefikia wakati huo, hakukuwa na namna nyingine ya kulijenga taifa tofauti na kufanya ubinafsishaji.

Alisema katika kipindi hicho nchi wahisani na wafadhili walikuwa wameanza kuikimbia Tanzania kutokana na hali ya uchumi isiyoridhisha na kuwa katika hatari ya kupoteza misaada kwa kiwango kikubwa.

Mkapa alisema ili kuwaaminisha wahisani kuwa uchumi wa Tanzania unajengwa kwa kushirikisha Serikali na taasisi binafsi, ilimbidi kufanya ubinafishishaji na jambo lililowezesha taifa kuaminika.

“Jambo lingine ambalo linasemwa ni kwamba ubinafsishwaji Baba wa Taifa hakuupenda, ni kweli lakini nieleze wazi kwamba hakukuwa na ‘altenative’, mashirika haya tuliyaanzisha ili yawe ya kiuchumi kupata faida na faida hiyo iletwe serikalini tuweze kupanua huduma za jamii na miundombinu ya nchi yetu.

“Mengi badala ya kuleta faida walikuwa wanaomba ruzuku kutoka Hazina, tusingaliweza kuvumilia, ilitubidi kutafuta namna ya kuhuisha biashara hizo, viwanda hivyo na hivyo ndivyo tulivyofanya.

“Pointi yangu ni kwamba nilitaka kudhihirisha maendeleo yanaweza kusukumwa na wote sekta binafsi pamoja na Serikali. Kuna mambo ambayo sekta binafsi haiwezi kuchukua gharama zake na hayo yatabebwa na Serikali, miundombinu na kadhalika.

“Lakini kwenye elimu kwa mfano hakuna sababu ya kuzuia sekta binafsi isianzishe shule, kwa hiyo tumemsikia Profesa hapa tulianzisha vyuo vyote hivi kwa sababu tulifikiri kwa ushirikiano huo ndiyo tunaweza kueneza elimu kwa watu wengi zaidi,” alisema Mkapa.

VIONGOZI VIJANA

Kuhusu viongozi vijana, alisema ni lazima vijana wanapotaka kuwa viongozi wasikimbilie tu kujiingiza kwenye siasa, bali wajiandae kwa kiwango cha kutosha ili wanapochukua nafasi ya kuwatumikia wananchi wawe na uwezo wa kulisaidia taifa.

“Ninachoweza kuwashauri ni kuwa kabla ya kuchukua maamuzi ya kutaka uongozi, vijana wanatakiwa wajaribu kujiimarisha, kujifunza na kujiandaa vya kutosha na wakati ukifika basi wawashirikishe wazee waliowatangulia. Kwa kufanya hivyo, natarajia kuona viongozi wenye hekima na busara na watakuwa na maamuzi yenye tija kwa taifa,” alisema Mkapa.

Aliwaasa vijana kujenga utamaduni wa kusoma vitabu na kuachana na kutumia muda mwingi kwenye mitandano kwani maarifa ya kweli yanapatikana kwenye vitabu na ndiyo maana viongozi wengi wa zamani si tu walikuwa na weledi, bali utamaduni wa kujisomea uliwaimarisha kiakili na kuwafanya wasiwe watu wa kuyumbishwa.

Mkapa alidai kuwa amekuwa akilaumiwa kuwa yeye ni jeuri na kwamba anajiona, hivyo aliwaasa watu kusoma kitabu chake waamue kama ni kweli yeye ni jeuri.

KUANDALIWA NA NYERERE

Kuhusu kuandaliwa na Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere kuwa rais, alisema jambo hilo si kweli licha ya watu wengi kuamini kuwa alimpigia debe tangu kwenye mchakato wa kupitishwa na chama.

“Nilichokuwa na hakika nacho katika kufanya kampeni baada ya ‘nomination’, aliniunga mkono na wengine mnajua alifanya kampeni hapa Shinyanga mpaka Tabora,” alisema Mkapa.

Pia alieleza jinsi ambavyo Mwalimu alipinga uamuzi wa timu yake ya kampeni wa kutaka wakodi helkopita ili kufanya kampeni.

“Mwalimu alipinga akisema kuwa hata kama Mungu angetuma malaika wake wawatake watumie helkopita angempinga, kwa sababu kampeni zinahitaji watu waonane, hivyo wasingeweza kutumia usafiri huo,” alisema Mkapa.

SERIKALI YA KIZAZI KIPYA

Alisema kuwa wakati anaunda Serikali yake bungeni kulikuwa na mawaziri wakuu wawili ambao walikuwa wamechaguliwa tena kuwa wabunge ambao aliwaita kwa heshima na kuzungumza nao na kuwaeleza kuwa watamsaidia wakiwa ‘back banch’ siyo katika Serikali yake.

Alisema kuwa lengo lake lilikuwa ni kuunda Serikali yenye kizazi kipya katika siasa, mmoja wao akiwa ni Rais wa sasa Dk. Magufuli, ambaye alikiri kuwa alifanya kazi kubwa ikiwamo kutekeleza ujenzi wa daraja la kuunganisha mikoa ya Kusini katika bonde la Mto Rufiji, maarufu Daraja la Mkapa.

Mkapa alisema hata pale ambapo Dk. Magufuli alipomfuata kumtaka daraja hilo lipewe jina lake alikataa, akiamini kuwa lilipaswa kuitwa jina la Magufuli, lakini alishangazwa wakati wa kulizindua alielezwa kuwa imekwishaamriwa litaitwa kwa jina lake.

NYAYO ZA MKAPA

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Balozi Profesa Costa Mahalu, alisema kama taifa lazima viongozi wafuate nyayo za Mkapa kwani ni muwazi, mkweli na msikivu jambo ambalo viongozi wengi wa Afrika wanakosa.

Alisema iwapo wataweza kufuata nyayo hizo, taifa linaweza kuepuka migongano ya mara kwa mara kati ya viongozi wa Serikali, vyama na wananchi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, alisema uamuzi wa Rais Mkapa kuandika kitabu ni jambo la kujivunia kwa kila mwenye maono mazuri na taifa, kwani ameyafanya mawazo yake yaweze kuishi milele na kuweza kutumiwa na watu wanaotaka kuingia kwenye uongozi.


Chanzo: Mtanzania
DAWA NI KATIBA. KUBADIKISHA KATIBA NA KUWEKA UKOMO WA RAIS. CCM WAKO WENGI NA WAKITAKA MAMBO YAO WATAPATA TU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hofu yangu , atakaeingia awamu ya sita ataendeleza kazi ya JPM ? Japo sio utamaduni wetu tumpe mda zaidi ainyooshe nchi ,matunda yameshaonekana .

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa taarifa yako hapo Magufuli alipo ameshakata pumzi, hata hiyo miradi miwili mikubwa ya SGR & SG Hana uwezo wa kuikamilisha ndani ya miaka yake mitano kama ilivyotarajiwa, na hata akiongezewa miaka mingine kumi bado hataweza. Mkapa hilo ameshaliona, ila anajua fika Magufuli ni mtu mwenye uchu wa madaraka na amezungukwa na wahuni, ambao wanamdanganya aongeze muda ili waendelee kula.

Na Mkapa inaonekana ameshazungumza na Magufuli kuhusu kutokuongeza muda, lakini Magufuli anatumia Hadaa iwapo wananchi watamtaka aongeze muda atawasakiliza, ila Mkapa anajua tabia ya kulisha maneno wananchi kutokana na madaraka makubwa aliyokuwa nayo rais, huku akijua fika wananchi hawahitaji kiongozi yoyote akae madarakani zaidi ya miaka 10. Hapo alipo Mkapa anapambana kuhakikisha kuwa Magufuli haongezi muda kwani yeye ndio anatupiwa lawama nyuma ya pazia na wanaccm wenzie, kwani yeye ndio alishinikiza Magufuli apitishwe kuwa mgombea wa ccm, huku wanaccm wengi wakiwa hawamtaki kwa kuijua tabia yake.
 
Hii message kutoka kwa B.W Mkapa inatumwa kwa John Pombe mwenyewe na wala sio kwa wapambe wa John. Hata Pinda alifikisha message yake kwa style kama hii.
 
Manelezu naomba nikueleze kuwa ni mpumbavu tu anayeweza fikiria kuwa JPM anaweza ongeza muda baada ya 2025.

Huu utetezi wako ungekuwa na maana iwapo tu angekuwa hanajisi box la kura. Ni hivi, Magufuli ana mpango kwa wazi kutaka kujiongezea muda wa kukaa madarakani, na hilo atalifanya kwa wabunge wote kuwa wa viti maalum huko bungeni, kwani watapita bila kupingwa, na hapo ataweza kuwaamrisha wamuongezee muda wa kukaa madarakani kwani hata yeye atawambia kawapa ubunge wa mezani, vinginevyo wakigoma atawatushia kulivunja bunge warudi wakapambana kiukweli kitu ambacho wabunge hao wanajua hawawezi kushindana kwenye uchaguzi huru
Inaonekana unajua story za jikoni , mambo yanavyoenda huko... Sisi yetu macho tu.

Hiyo ndio hali halisi. Mkapa ameshaona muelekeo kuanzia hii kuchezea chaguzi za nchi, na ndio maana alisema anatamani kuwe na tume huru ya uchaguzi, na kwenye tume hiyo wapinzani washirikishwe. Anajua fika aliyempendekeza atakuja kuleta matatizo makubwa huko mbeleni. Ni muda tu utasema yote.
 
DAWA NI KATIBA. KUBADIKISHA KATIBA NA KUWEKA UKOMO WA RAIS. CCM WAKO WENGI NA WAKITAKA MAMBO YAO WATAPATA TU

Sent using Jamii Forums mobile app
mbona hamjadili kipengele alichosema BWM kuwa (mnaona wenyewe jinsi alivyo badilika) hapo maana yake ni kwamba ametoka nje ya mategemeo ya wengi walivyotegemea wakiwemo hao viongozi wastaafu.Kwa maneno ya nyongeza ni kwamba hajatosha kwenye hiyo nafasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom