Mkapa alisema kazi ya urais ina changamoto nyingi na ina majaribu tofauti kutoka ndani na nje ya nchi, hivyo linapokuja suala la kukaa madarakani kwa zaidi ya mihula miwili haoni sababu ya kufanya hivyo.
Alisema anaamini kuwa hata Dk. Magufuli hawezi kuongeza muda wa kukaa madarakani kwani licha ya ugumu wa kazi hiyo pia umekuwa kama utamaduni wa taifa.
Hawa watu bwana, na heshima zao wanazopewa na wananchi, sijui akili zao wanaziweka wapi.
Mseveni sio rais, na changamoto hizo anazozungumzia Mkapa hazimhusu?
Kagame je, Nkurunziza, Mgabe na wengine wengi.
Wote hawa changamoto za urais hawakuwa nazo?
Yeye Mkapa, anaona dalili zote, na juhudi kubwa anazofanya kijana wake, halafu anaibuka na komedi za aina yake!
Hapo kijana wake atakapokuwa ametimiza matakwa yake ya kubaki madarakani, tena sio kwa kuongeza ngwe ya tatu tu, bali na zaidi na zaidi..., hapo Mkapa mwenyewe atakuja na maelezo mengine ya kuhalalisha hali hiyo, na kuwaona waTanzania kama mazuzu hivi.
Mtu anafanya juhudi zote kuua upinzani. Anataka ushindi wa asili mia 99..., anataka hayo kwa sabau zipi kama sio kutafuta njia za kuhalalisha nia ovu hiyo.