Mkapa awapa neno wanaotaka Magufuli aongoze mihula mitatu

Mkapa awapa neno wanaotaka Magufuli aongoze mihula mitatu

Watanzani hatuwezi kumpa tena uraisi huyo labda Polisi jesh na usalama lakini 20/20 hatobowi kabisa huyu jiwe
Muwe mnaupima upepo wa raia unapopepelea kwa sasa, ndiyo mnacomment kupata mashiko, lakini ukienda kishabiki mradi usikike umesema, watu wanakushangaa!

Au ndiyo comment za kupima upeponini hizi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekusoma mkuu, ni'apo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Poa poa.

Niliwaambia watu Magufuli hawezi kuwa rais baada ya miaka yake kumi kuisha.

Watu wakawa wanaleta speculations zao.

Sasa tunaona Godfather wake mwenyewe aliyempa maisha ya kisiasa beyond the backbench kaweka maneno wazi kumaliza mjadala.

Namshukuru sana Mzee Mkapa kwa kutoa muongozo kwenye hili jambo muhimu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka mitano katika siasa ni mingi sana,lolote linaweza kutokea.
Poa poa.

Niliwaambia watu Magufuli hawezi kuwa rais baada ya miaka yake kumi kuisha.

Watu wakawa wanaleta speculations zao.

Sasa tunaona Godfather wake mwenyewe aliyempa maisha ya kisiasa beyind the backbench kaweka maneno wazi kumaliza mjadala.

Namshukuru sana Mzee Mkapa kwa kutoa muongozo kwenye hili jambo muhimu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka mitano katika siasa ni mingi sana,lolote linaweza kutokea.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli.

Lakini kwa msingi huo, huwezi kujadili chochote cha maana.

Maana chochote utakachojadili, kinyume chake kinaweza kutokea.

Hapi ndipo tunaji limit kwenye facts.

Fact 1. Kuna katazo la kikatiba la rais kuendela kuwa rais baada ya miaka 10.

Fact 2. Magufuli amesema hataki kuvunja katazo hili.

Fact 3. Wazee wa CCM kina Mkapa wanasema hatavunja katazo hili.

Ukitaka kuongea habari za "lolote linaweza kutokea" unaweza hata kuongea kwamba Christopher Mtikila anaweza kufufuka na kuwa rais baada ya kushinda uchaguzi wa 2020.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mliokaribu na ndugu Nkapa mwambieni sisi watanzani tulioko vijijini tunahitaji nakala za kitabu chake kwa lugha ya Kiswahili tuweze kukisoma na kufahamu yaliyomo.

Je nakala zenye lugha ya Kiswahili tutazipata wapi?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nguvu zipi za maamuzi ambazo Mkapa anazo...anashindwa kukemea vitu vidogo...hana ubavu wa kuitisha press na akayaongea mambo ya ajabu ambayo yanaendelea hivi sasa. MKAPA HANA NGUVU NDANI CHAMA SEMA ALIMZUGA TU MZEE WA MSOGA
Unahisi ukisoma ulichoandika unajielewa....baada ya nyerere anayefuata kwa nguvu ya maamuzi ni mkapa

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenena Mh
Huo ndio Ukweli kabisa hakuna sababu ya kuenenda kunyume na Katiba ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Kuhusu swala la Urais,pia umeshauri vema kuwa mihula miwili ya Urais imeisha kuwa kama utamaduni wa Nchi yetu.
Mwisho Urais ni taasisi ambayo naifananisha na mzigo mzito ambapo uzito wake anafahamu alieubeba jinsi gani mzigo aliobeba ni mzito na wakati mwingine safari yake ikiwa bado mbari hofu yakutoufikisha mzigo humuingia ingawa hubaki siri yake na maumivu yake mwenyewe.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
RAIS wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, amesema ana hakika Rais Dk. John Magufuli hatataka kuongeza mhula wa tatu wa uongozi badala yake atafuata nyayo za watangulizi wake kwa kuhudumu mihula miwili.

Alitoa kauli hiyo jijini Mwanza juzi wakati wa hafla ya utambulisho wa kitabu chake cha ‘My Life, My Purpose’ kinachoelezea maisha yake.

Mkapa alisema kazi ya urais ina changamoto nyingi na ina majaribu tofauti kutoka ndani na nje ya nchi, hivyo linapokuja suala la kukaa madarakani kwa zaidi ya mihula miwili haoni sababu ya kufanya hivyo.

Alisema anaamini kuwa hata Dk. Magufuli hawezi kuongeza muda wa kukaa madarakani kwani licha ya ugumu wa kazi hiyo pia umekuwa kama utamaduni wa taifa.

“Kuna maneno nayasikia sikia watu wanasema eti Rais Magufuli anaweza kubadili Katiba na akabakia madarakani kwa zaidi ya mihula tuliyoizoea kwa maana ya mihula miwili ya kipindi cha miaka kumi, binafsi sidhani kama hilo lipo na hata simshauri kufanya hivyo.

“Labda niwakumbushe tu, kipindi nilipokuwa madarakani kuna wakati wazee wa Zanzibar walinifuata mara kadhaa wakiniomba wao kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi wabadilishe Katiba ili wapate fursa ya kumchagua kiongozi kwa mihula mitatu kwa maana ya miaka 15, suala ambalo naweka wazi kuwa lilitaka kutikisa kidogo muungano wetu.

“Pamoja na kuniomba sana sikuwa tayari kuunga mkono suala hilo, walifanya kila liwezekanalo kunishawishi lakini niligoma na mwisho walinielewa na kuendelea na utaratibu wa kawaida wa mihula miwili ya miaka mitano kila mmoja na hadi sasa wameendelea nao.

“Ninachoweza kusema ni kwamba utaratibu huu wa mihula miwili, sasa hata Watanzania weshauzoea na umegeuka kama utamaduni wa taifa.

“Pia naweza kusema pengine umechangia kwa kiasi kikubwa kulifanya taifa letu kuendelea kuwa na demokrasia ya mfano, hivyo ninaamini hata Rais hatabadilisha Katiba kwenye hilo.

“Ndiye aliyenifuata (Rais Magafuli) akaniambia mzee tukitegemea sana hawa wahisani kasi yetu ya ujenzi wa miundombinu itakuwa ndogo sana. Kwanini sisi wenyewe hatuwezi kuwathibitishia kwamba tuko tayari ‘ku-sacrifies’ kutumia mapato yetu wenyewe kujenga barabara zetu.

“Nikamkubalia tukaenda kwenye Baraza la Mawaziri tukaamua kila mwezi tutatenga kiasi fulani cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara. Ni kazi ya Magufuli.

“Mimi nimeshukuru wananchi wenzangu waliona anafaa huyu, na sasa anaongoza awamu ya tano, Mwenyezi Mungu ampe afya njema aweze kukamilisha na yeye mihula miwili, nina hakika hatataka wa tatu hata kidogo kwa sababu mmeona alivyobadilika katika miaka minne hii,” alisema Mkapa.

Chanzo: Mtanzania
 
Back
Top Bottom