Sababu zifuatazo ndiyo zinahusisha serikali na kipigo cha Dr. Ulimboka;-
Maelezo ya Dr. Ulimboka
Katika maelezo yake ya jinsi alivyokamatwa na kuteswa; Dr Ulimboka anasema waliomteka, walihitaji KUJUA tu NANI YUPO BEHIND YA MIGOMO YA MADAKTARI inayoendelea. Kwakua yeye ni kiongozi wa hiyo migomo, hao watekaji walitegemea kwavyovyote vile Ulimboka angewasaidia katika kuwapa hiyo habari.
-Je, ndugu Hans Rogers Dibagula, unadhani kibaka, jambazi au hata ndugu wa aliyempoteza mgojnwa wake fuatia migomo ya madaktari, habari za nani yupo nyuma ya migomo atazihitaji kwa ajili gani na ili azifanyie nini?...ni..PEKEYAKE SERIKALI NDIYO WANGEZIHITAJI habari hizi, au nani wengine?
Maelezo ya Dr . Deo, ambaye walikuwa pamoja na Ulimboka siku ya tukio, anasema; watu hao watano waliomteka Ulimboka walivaa nguo KAMA za kijeshi huku wakiwa wamebeba bunduki. Kwa hapa nchini, wanao vaa nguo zinazofana kama za jeshi, ni askari wetu wa TISS wanao linda mageti yakuingia ofisini, na kwenye hili, watakuwa wanaotoka eneo kati ya Victoria na Mwenge (fuatia maelezo ya Ulimboka).
Mazingira ya kukamatwa na alipoteswa.
Dr. Uliomboka anakumbuka; wakati akiwa kwenye gari, huku akiwa anachukua kipondo, na kabla hajaingia kwenye nyumba fulani nzuri hivi, alikumbuka kupita maeneo ya victoria (yaani walipita maeneo ya Victoria). Na wakati alipokuwa anaenda kutupwa huko mabwepande, alikumbuka pia kupita maeneo ya mwenge. Kwahiyo kwa hesabu nyepesi tu kabisa, sehemu aliyokuwa anakula kichapo ni eneo lolote kati ya victoria na mwenge, lenye nyumba nzuri.......ulimboka anaeleza pia kuwa; kuna wakati ali'attempt kukimbia wakati anakula mkong'oto ghafla, risasi ikapigwa hewani ili kumzuia asile kona..... Hivyo basi, inaonyesha kuwa eneo aliliopelekwa ili kula nakoz, risasi inaweza kupigwa anyhow na polisi wasiweze kuja kufuatilia mlio huo....
-Hans, ni sehemu gani kati ya mwenge na Victoria unayoweza kudhania ....?
Ufuatiliaji na ujihusishaji wa vyombo vya serikali
TBC1, haikutangaza kabisa katika taarifa yake ya habari ya saa mbili usiku tukio la kukamatwa na kupigwa Dr. Ulimboka, tofauti na vyombo vingine vyote vya binafsi vya TV nchini, vilivyotangaza, tena kama habari ya kwanza. ....Kusafirishwa kwa Dr. Ulimboka, hapo napo TV zote zilitangaza isipokuwa TBC1.
Magazeti mengi ya serikali yaliandika "....kinara wa migomo ya madaktari atekwa..." Lakini kifo cha Kanumba.... nadhani uliona TV yetu nzuri ya taifa TBC1 ilivyokava vyema msiba ule wa kusikitisha.
Katika kituo cha polisi cha kawe ambapo Ulimboka alipelekwa baada ya kuokotwa, polisi hawakufanya juhudi yeyote ya kumtafutia usafiri wa haraka ili akimbizwe hospitalini kuokoa maisha yake kutokana na kuvuja kwa damu nyingi. Polisi walipoulizwa kwanini hawakutoa msaada huo walisema; walikuwa wanawangoja ndugu zake.
".....kamanda shupavu HEMED, alikutwa faragha akiongea na Radio za ki'Police akiripoti;....bado hajafa....pale Muhimbili! Swali kwako ndgu Hans, Kwani alitakiwa afe? (fuatia mazungumzo ya hemedi na wenzie)..."
Tangu Jumanne hadi hii leo, hakuna aliyekamatwa kwa kuhusishwa na tukio hilo.
Hitimisho
Kwa kumtocha vile ili kupata information za aina ile tu, ni kuonyesha ukihiyo na ukilaza wa maafisa waliofanya zoezi hili ulivyo mdogo, ukilaza na ukihiyo, ukizingatia uwepo wavyombo vingi vya kisasa vya kunasa mawasiliano ya email,text, voice call na kumfuatilia 24/7 kila atakapoweka mguu. Halikadhalika, kuna private compony nyingi za uchunguzi zipo nchini na zenye vyombo vya kisasa, in one week mngepata kila mlichotaka.
Intelijensia ya sasa hapa Tz, ni ile yakupeana bila kuangalia uwezo wa mtu na ndiyo inatufikisha hapa....! Tumchukue huyu kijana kwakua mzazi wake aliyekufa na alikuwa mfanyakazi mwenzetu hapa tiss ili kuisaidia familia ya marehemu.....aaah, hata kama ni ZUZU, tumchukue tu...?!! huyu kaletwa na mkuu, tumchukue tu. Matokeo yake, intelijensi haiwezi kujisafisha na kadhia hii mbele ya sura za nchi za kimataifa.....kama ilivyo kuwa kwa Owko jirani zetu, Sarowiwa huko NGA....!
Kibanga Msese.