Kuna tetesi zimezagaa mtaani kuwa Ishu nzima ya kutekwa na kuteswa kwa Dr.Ulimboka ni mchezo wa kisiasa uliopangwa baina ya Madaktari na Chama Fulani cha siasa(Jina Limehifadiwa).
TUHUMA HIZI ZINAJENGWA NA HOJA ZIFUATAZO: (UPUUZI MTUPU UMECHELEWA SANA NA MAJAMBAZI WENZIO)
1.Dr.Ulimboka anadai watu walimpigia simu akakutana nao maeneo ya Leaders akiwa na rafiki yake na baada ya muda watu hao walimteka na kuondoka nae kwenye gari kisha rafiki yake kwenda kutoa taarifa polisi.
SWALI?
Kwanini huyu rafiki wa Dr. asinge hangaika kuifuatila gari lililomteka Dr. hukuakiendelea kufanya mawsiliano na ndugu na jamaa,badala yake akakimbilia Polisi na kuruhusu watekaji kupotea?
2.Kulingana na Madai ya Dr. Kuna mpita njia alimuokota alfajiri ya saa kumi na moja akiwa hajitambui akampeleka kituo cha polisi Bunju
SWALI?
Kumekuwa na maswali mengi ni wapi alipokuwa anatoka huyu bwana aliyemuokota Dr. muda huo?
3.Kunamadai kuwa baada ya Dr. kuonekana Madaktari waliomba usafiri wa ambulance kutoka hospital ya Muimbili lakini walinyimwa na kulazimika kukodi ambulance.
SWALI?
Kwa nini kitengo cha emergency-Muhimbili kikatae kutoa ambulance kwa ajili yakumchukua dokta mwenzao aliyeuwa hatarini kufa?
4.Kulingana na taarifa za mtu aliuemuokota Dr. nikwamba Dr. alikuwa hajitambui,chakushangaza alipofikishwa Muhimbili Dr. alizinduka na akazungumza na baadhi ya madaktari na waandishi wa habari,lakini muda mfupi baada Dr. alipoteza fahamu na kupelekwa ICU.
Ikumbukwe pia Dr. alisema baada ya watekaji kumpiga sana alizimia,baadae akazinduka na kujikongoja hadi barabarani,kasha akapoteza tena fahamu.Kwa maelezo hayo ni kuwa Dr. alipoteza fahamu na kuzinduka zaidi ya mara tatu.
SWALI?
Inakuaje mtu alikuwa hajitambui alipofikishwa hospitali akaongea na madaktari wenzie alafu ghafla akapoteza fahamu tena?
5.Madaktari walisema Dr.alitolewa kucha na meno
SWALI?
Mashuda waliokwenda airport wanasema Dr.alikuwa na meno na kucha zake,je madaktari waliongopa?
Hoja hizi pamoja na mambo mengine yaliyojitokeza katika kipindi chote cha sakata hili zinatia mashaka na kuzua utata katika tukio hili.
Kunatetesi kuwa kuna chama cha kisiasa kiliandaa mpango huu ili kukwamisha juhudi za serikali katika kushughulikia tatizo la Madaktari.Eidha kumekuwa na baadhi ya tuhuma zikielekweza kwa baadhi ya wabunge wa chama Fulani waliokuwa mstari wa mbele kutaka suala la Dr.lijadiliwe bungeni.
Je kama ni kweli,Siasa ya nchi hii inaelekea wapi?