MHUSIKA ANAOMBA AWAKATIZE KIDOGO WASOMAJI: KABLA HAJAENDELEA TENA NA CODE YA EMBRYOGENESIS
YALE YA MUHIMU YALIYOJRI SIKU MOJA KABLA YA GARI LA MHUSIKA KWENDA GARAGE IUUMAA YA WIKI ILIYOPITA HADI KUFIKIA SIKU YA LEO J5 YA TAREHE 31/07/2024
Siku moja kabla, yaani jioni ya Alhamis ya wiki iliyopita (tarehe 28/07/2024) wakati mhusika anaondoka kurudi nyumbani, pale kwenye gate kuu nje ya jengo, aliwakuta mabinti wawili wakiwa wamesimama pale, na walikuwa pamoja na mkuu wa kitengo cha matetemeko ya ardhi (tumwite MTTMK)
Binti mmoja ni mfanyakazi na mwingine ni intern, na ambao wote wawili walionyesha dalili za kama walikuwa wanahitaji lift kutoka kwa mhusika
Kwa bahati mbaya, kutokana na tahadhari aliyonayo, mhusika alishasitisha huduma hiyo siku nyingi na hivyo hakuonyesha dalilil zozote za kujali hitaji lao
Baada ya mhusika kuelekea kwenye gari lake, huku MTTM akiwa aeona dalili zote kuwa mhusika hakuwa na mpango wa kuwapa mabinti wale lift, MTTM aliamua kutembea kwenda upande wa pili wa jengo ila kwenye uelekeo ule lilipokuwa limepark gari la mhusika; na baada ya kupakaribia, alichepuka na kuingia upande huo wa pili na ubavuni mwa jengo la Idara, uelekeao kama ule wa kuelekea Ubungo
Baada ya kuchepuka MTTM alienda akasimama karibu na ukuta wa
mapana ya jengo la Idara kiasi kwamba akawa haonekani tena na mtu mwingine yeyote yule aliyekuwa
usawa wa mbele wa jengo la Idara, ila alikuwa anaweza kuonekana kutokea kwenye parking kuanzia pale alipokuwa amepaki mhusika na pia parking zingine zilizokuwa upande wa kulia wa pale alipokuwa amepaki mhusika
Kwa hali hiyo, kama mhusika angemkaribisha kwa ajili ya lift kwa sababu siku hiyo hakuwa amekuja na gari, kutokana na configuration za mahali pale alipokuwa amepaki mhusika, hayupo mtu yeyote ambaye angeweza kumuona MTTM akiwa anapanda kwenye gari la mhusika
Hiyo siku ya Alhamis ikapita
Siku ya Ijumaa asubuhi ndiyo pakatokea dharula ya kuharibika kwa ALTERNATOR ya gari la mhusika na muda wote wa siku hiyo aliiutumia garage pamoja na Benki
Siku hiyo akiwa ameenda kuchukua fedha kule Benki kwa ajili ya kuwakabdihi mafundi ili wakanunue vifaa vya matengenezo ya gari, kule benki alikuta
holaaaa kuhusiana na swala la madai yake, ila mshahara aliukuta huku ukiwa umekatwa tena laki mbili taslimu, ambazo zimekuwa zikikatwa tangu Februari 2024
Kesho yake siku ya Jumamosi ikapita
J2 nayo ikapita pia, ila haikupita hivi kwa kule Kanisani; kuna mengi yaliendellea huko ila kwa sasa siyo wakati wake
ILIPOFIKA JUZI J3 YA TAREHE 29/07/2024
Asubuhi akiwa yupo ofisini pamoja na OM-2 huku OM-1 akiwa ametoka, mtu mwenye sura ngeni kabisa kwa mhusika na aliyesemekana kuwa alikuwa ni mwanafunzi aliingia ofisini akiwa ana shida na OM-2
Baada ya majadiliano mafupi kati ya OM-2 na mwanafunzi huyo
walikubaliana kukutana tena muda mfupi baadaye kwa sababu OM-2 alikuwa analazimika kutoka kidogo ofisini na kwenda mahali pengine
Kutokana na hali hiyo, OM-2 alimshauri mwanafunzi akae kidogo nje ya ofisi kwenye korido akiwa anamsubiria kwa muda mfupi
Baada ya hapo, wote OM-2 na mwanafunzi walitoka; mwanafunzi akaenda akasimama kwenye korido na OM-2 akatoweka kwenye floor akaenda sehemu nyingine
BAADA YA MUDA MFUPI KUPITA OM-2 AKIWA HAYUPO, MWANAFUNZI AKIWA YUPO KWENYE KORIDO
Mwanafunzi huy alirudi tena ofisini safari hii akiwa ameambatana na mwanafunzi mwingine wa mwaka wa nne (
ambaye huyu kwa sasa ameshahitimu masomo yake na possibly hatakiwi tena kuwepo kwenye mazingira ya taasisi), na ambaye mhusika anamfahamu sana kwa sura
Baada ya kumsalimia mhusika, mwanafunzi huyu wa mwaka wa nne alimweleza mhusika kuwa alikuwa ameagizwa na OM-2 kuja kumsubiria hapo ndani ofisini; huku wakati huo huo akiwa ameambatana pamja na yuke mwingine wa kwanza ambaye OM-2 alikuwa amemuagiza amsubirie kwenye korido
Mhusika hakuwaruhusu wanafunzi hao kukaa pale ofisini, alifuata instructions za awali za mwenyeji wao
Baadaye tena,wakati wa jioni wakati mhusika anatoka ofisini J3 hiyo kurudi nyumbani, pale kwenye parking alimkuta kijana wa usafi akiwa anaosha baadhi ya magari yaliyokuwa yamepaki pale
Baada ya kuwasha gari, engine ikiwa inaunguruma,
kijana wa usafi alimfuata mhusika na kumweleza kuwa aliagizwa na MR X kumweleza mhusika kuwa MR X angehitaji lift kwenye gari la mhusika siku hiyo
Ilionekana MR X hakuwa amekuja na gari siku hiyo kwa sababu halikuwepo kwenye parking
Mhusika aliupokea ujumbe ila hakuufanyika kazi, na iwapo angeufanyika kazi, ingeonekana kuwa ni yeye aliyemhitaji MR X kuja kupanda kwenye gari lake kwa sababu waktai huo MR X hata hakuwa anajulikana alikuwa wapi; possibly alikuwepo ndani ofisini kwake
Mbali na hilo, ingekuwa sikuya kwanza kwa MR X kupanda gari hilo la mhusika
Hiyo siku ya J3 nayo ikapita pia na jana J4 yalikuwepo pia matukio ila ambayo kwa sasa yanaweza kuonekana kuwa si ya muhimu sana, ila kadri muda unavyopita, pengine labda hapo baadaye yatakuja kuonekana tofauti na yanavyoonekana sasa. Ikitokea hivyo mhusika ataleta taarifa zake humu
BAADA YA HAYA YOTE KUWA YAMETIOKEA KUANZIA IJUMAA YA WIKI ILIYOPITA HADI KUFIKIA JANA J4 YA TAREHE 30/07/2024
Leo siku ya J5 ndiyo mhusika akapokea sasa ujumbe kutoka kwa mtu ambaye si mwajiriwa wa kampuni husika ya mtandao wa simu, uliomzawadia jumla ya ushindi wa TZS million 6 na ambao taarifa zake ziko kwenye post hii
#2,138
UPNEXT: CODE YA EMBRYOGENESIS
Embrogenesis is the formation and development of an
embryo.
Embryogenesis is
the key process to establish complex multicellular life by transitioning from a single-celled fertilized egg (= zygote) to a mature multicellular organism (= embryo). As the last common ancestor was most likely unicellular, embryogenesis evolved independently in animal and plant kingdoms.
……..itaendelea
In the war between falsehood and Truth (GOD), falsehood wins the first battles and truth, the last
MUBARIKIWE TENA NA BWANA