UPDATE: 03 MARCH 2021
TUKIO LA NNE NDANI YA JENGO SEPTEMBA 2016 LILOMHUSISHA SENIOR MSTAAFU
WA KIUME NA MTU MWINGINE MGENI MWENYE UHUSIANO NAYE NA AMBAYE ALIKUWA AMETOKA NJE YA IDARA.
Tukio hili lilitokea ndani ya wiki ya kuanzia tarehe 12/09/2016 (
J3) hadi 16/09/2016 (
IJUMAA)
- Jumamosi ya wiki kabla ya J3 tajwa hapo juu, ndiyo siku ambayo lilikuwa limetokea tetemeko la Kagera
- J3 tajwa mhusika alifika ofisini asubuhi na kukuta kuna gari moja au mbili (za ma-office mates wake ndani ya jengo hilo), zimepaki kwenye parking
- Gate la kuingilia ndani ya jengo lilikuwa wazi, kuonyesha kuwa kulikuwa na angalau watu ndani ya jengo hilo
- Mhusika aliingia ofisini na kukuta hakuna mtu hata mmoja, kwenye ghorofa ilimo ofisi yake. Ofisi zote zilikuwa zimefungwa na hapakuwa na mtu hata mmoja anayemiliki ofisi kwenye floor hiyo aliyekuwa tayari ameshafika ofisini muda huo
Mpaka hapa, mhusika akakumbuka pia kuwa kwenye siku za Alhamis na Ijumaa wiki iliyopita nyuma yake, hapakuwa na mtu yeyote kwenye floor hiyo. Siku hizo mbili alikuwa mwenyewe peke yake kwenye floor nzima.
Kwa siku hizo mbili za wiki iliyokuwa imepita, kwenye floor inayofuata, walikuwa wamebaki Katibu Mhutasi (KMH) wa MWI pamoja na mtu mmoja mwingine,
tumwite XX_2. Sehemu zingine zote za jengo hapakuwa na mtu na kuna baadhi ya wenye ofisi hizo ambao walikuwa wamesafiri. Kwa mfano,
Mr X pampja na MAMA SENIOR
AMBAYE HAJASTAAFU (MSH), walikuwa wamesafiri kikazi kwenda Kyerwa, Kagera
Kwa hiyo kuanzia Alhamis ya tarehe 08/09/2016 na kuendelea, jengo zima lilikuwa limebaki na watu watatu tu ambao ni XX_2, KMH pamoja na mhusika. Taarifa hizi za uwepo wa watu wachache hivi ndani ya jengo, mhusika alizipata siku hiyo ya J3 ya tarehe 12/09/2016. Hapo kabla hakujua hilo
Baada ya mhusika kufika ofisini na kukuta floor nzima haina watu kwa siku ya tatu mfululizo, aliamua kupandisha juu ofisini kwa MWI. Huko alimkuta Katibu Mhutasi (KMH) wa MWI akiwa peke yake. Hapakuwa hapakuwa na mtu mwingine tena zaidi ya huyo ndani ya jengo kwa muda huo, japo kwenye parking palionyesha kuwa kuna mtu mwingine wa tatu ameshawasili maeneo ya ofixsini ambaye ni
XX_2 kwa sababu gari yake ilikuwepo kwenye parking.
Hata hivyo, kwa wakati huo, XX_2 hakuwemo ndani ya jengo, ila alikuwa bado yupo amekaa ndani ya gari lake lililokuwa kwenye parking
Mhusika katika kujaribu kuongea na KMH, mama huyu alisema kuwa amekuta geti kuu la jengo la ofisi hizo likiwa wazi, na amekuta gari ya
XX_2 ikiwa imepaki. Kwa hiyo mpaka hapa ikaonekana kuwa XX_2 ndiye aliyefungua geti, lakini kumbe hapana, hata XX_2 naye pia hakuwa amefungua geti hilo kwa sababu alivyofika na kupaki na akaendelea kubaki ndani ya gari, hakuwa ameshuka kwenye gari.
Hata hivyo, mpaka hapa, mambo kadhaa yakawa yamejidhihirsha hapa kwamba:
- XX_2 alifika ofisini akakuta geti la lango kuu liko wazi
- Kwa wakati huo, XX_2 alikuwa ameachiwa kukaimu Ukuu wa Idara, na alijua kuwa amebaki na watu wengine wawili tu ndani ya jengo hilo ambao ni KMH na mhusika, na wengine wote hawakuwepo
Kwa hiyo, kitendo cha
XX_2 kufika ofisini na kubaki ndani ya gari kwenye parking kilimuwezesha kuweza kufahamu yafuatayo
- Geti la lango kuu lilikuwa wazi
- Alifika ofisini kabla ya wenzake wawili ambao ni KMH na mhusika
Na kwa sababu watu aliokuwa amebaki nao walikuwa wawili tu na hapo hapo yeye alikuwa amefika akiwa ni wa kwanza na kukuta geti liko wazi, ilhali wale wenzake wawili kwa wakati huo walikuwa bado hawajafika, kuanzia hapa sasa yeye
XX_2 kama KAIMU MWI kwa wakti huo, alitakiwa apate swali kichwani kwamba:
SIYO MIMI (YAANI XX_2) NILIYEFUNGUA GETI LA LANGO KUU NA WALA SI KMH AU MHUSIKA, JE NANI ATAKUWA AMEFUNGUA GETI HILI?
Hii ni kutokana na ukweli kuwa:
- Hata XX_2 naye hakuwa amefungua geti hilo, na wala hakuwa ameingia ndani ya jengo hilo asubuhi hiyo bali alikuwa yupo amebaki kwenye gari yake iliyokuwa ipo kwenye parking,
- Wote wawili KMH pamoja na mhusika waliikuta gari ya XX_2 ikiwa ipo kwenye parking, na wakati huo geti likiwa wazi
- Kwa hiyo, KMH wakati anafika ofisini na kukuta geti la lango kuu liko wazi, alijua kuwa XX_2 ndiyo alifungua geti hilo
- Vile vile, mhusika naye pia alipofika ofisini na kukuta hali hiyo, akajua kuwa mmoja wao kati ya KMH na XX_2 ndio walifungua geti hilo
Kumbe hapana, haikuwa hivyo. Wote hawa watatu hawakuwa wamefungua geti hilo siku hiyo, japo wote walikuwa mazingira ya ofisini. Ni kwa sababu
XX_2 alifika ofisini na kubaki ndani ya gari lake , hakuingia ndani ya jengo, wakati KMH yeye alifika na kuingia ndani ya jengo geti likiwa wazi
Ilionyesha kuwa
XX_2 alifika ofisini wa kwanza na kukuta geti liko wazi, ila hakustuka kuona hivyo
- Baadaye tena ndiyo akaja KMH na kukuta geti liko wazi, akaingia ndani ya jengo, huku XX_2 akiwa yupo ndani ya gari lake na akimuona KMH
- Baadaye tena mhusika naye alifika na kuingia ndani ya jengo, XX_2 akiwa yupo ndani ya gari lake na akimuona mhuiska vilevile
MAELEZO KWA UFUPI SANA KUHUSIANA NA XX_2
Ni mfanyakazi ambaye ana wajina wake ndani ya idara,
YAANI NI MMOJAWAPO WA WATU WAWILI TU NDANI YA IDARA AMBAO MAJINA YAO YA UBINI YAMEFANANA, yaani SURNAME zao zinafanana. Kwa hiyo kuna mwingine tuseme anaitwa XX_1 ambayo jina lake la ubini limefanana na la
XX_2
…………………..inaendelea