SIKU YA SAFARI FIELD YA KIGAMBONI
Siku hiyo lilipowadia, Boss X aliwajulisha wageni kutoka nje ya nchi kwamba ilikuwa ni siku nzuri pia ya wao kwenda kuliona daraja la Kigamboni. Ikumbukwe kuwa wakati mhusika anakwepa kwenda Kigamboni mwaka 2010 kwa safari binafsi, daraja la Kigamboni lilikuwa bado halijajengwa na hivyo halikuwepo
Siku hii ya safari ya field ya kikazi ilipowadia, mhusika alienda akamuona Kaimu Mkuu wa Idara na kumuomba amruhusu yeye asiende Kigamboni mkuu huyo hakuona tatizo aliridhia, na hivyo mhusika hakwenda Kigamboni siku hiyo
Ikumbukuwe pia kuwa tangu March 2013, mhusika alikuwa ameshauandikia uongozi wa juu wa taasisi akiuomba umruhusu kutokusafiri nje ya Dar es Salaam, na hivyo nje ya nchi pia.
Hata hivyo, safari hii ya Kigamboni ilikuwa ni ya ndani ya Dar es Salaam na hivyo ilihitaji ridhaa ya mkuu wa kazi wa mhusika kuridhia kwa yeye (mhusika) kutokwenda Kigambon siku hiyoi
MENGINE KADHAA YA MUHIMU YALIYOJIRI WAKATI WA MKUTANO HUO WA KIMATAIFA, UKIONDOA LILE LA MSHIRIKI ALIYEKUWA ANAFANYA KAZI KWA KUPIGA PICHA SCREEN ZA COMPUTER
Kuna mambo mengine kadhaa ya muhimu yaliwahi kujiri wakati wa mkutano huo, na ambayo yalihusisha set-up ya Boss X pia kwa maana kwamba yalitokea baada ya yeye kuwa amenuia yatokee kama yalivyotokea
MAELEZO YA UTANGULIZI
MAELEZO MUHIMU KUHUSIANA NA MTOTO (BINTI) RAFIKI YAKE NA MHUSIKA ALIYEKUWA ANAFANYA KAZI KWENYE JENGO ILIMO OFISI YA MHUSIKA KIPINDI HICHO
Huyu binti alikuwa ni mtoto wa miaka inayozidi kidogo 20, kwa kipindi hicho
- Alikuwa ni mfanyakazi wa kampuni ya usafi iliyokuwa inafanya kazi kwenye jengo ilimo ofisi ya mhusika
- Alipofika idarani kwa mara ya kwanza, mojawapo ya ofisi alizokuwa anahudumia ni ile ya mhusika
- Kutokana na hali hiyo, mhusika na binti huyu walitokea kuzoeana sana na hatimaye kuwa marafiki, huku wakiitana babu na mjukuu
Zaidi ni kuwa binti huyu anatokea kanda ile maalumu ambako mhusika aliwahi kuishi kwa mwaka mmoja akiwa JKT, na hatimaye kuondoka huko akiwa ametengeneza marafiki kadhaa ambao huwa anakuwakumbuka hadi leo, hajawasahau. Kwa hiyo naturally, mhusika huwa mara nyingi anapenda kutengenesza urafiki na watu wanaotoka mkoa anaotokea huyu binti
KILICHOTOKEA PINDI MKUTANO HUU WA KIMATATIFA ULIPOKUWA UNAENDELEA. BINTI HUYU AKIWA MMOJAWAPO WA WAHUDUMU WA BITES ZA CHAI YA SAA 4;00 ASUBUHI NA SAA 10:00 JIONI
Asubuhi moja kwenye mojawapo ya siku za mkutano huo, binti huyu na wenzake walifika wakiwa wamebeba bites, asubuhi saa mbili kabla hata ya mkutano kuanza
- Siku hiyo, ilikuwa ni siku ya tatu au ya nne tangu siku ya kwanza ya kuanza kwa mkutano huo
- Bites hizi waliziwahisha na kuzihifadhi sehemu muhimu ya karibu ili wakati wa chai utakapofika, waweze kuzihudumu kutokea pale karibu badala ya kutokea kule ambako zilikuwa zinanaandaliwa,; na mhusika alibahatika kuziona bites hizo (kwenye malaji husika huwa hapitwi na kitu na hilo ndiyo tatizo lake la siku zote)
- Mojawapo ya bites hizo vilikuwa ni VITUMBUA; na mara zote mhusika anapenda vitumbua.
- Pasipo yeye kuwa anajua, kumbe kuna baadhi ya watu wengine nao ambao nao pia walishajua kuwa mhusika huwa anapenda vitumbua
Muda wa chai ya saa 4:00 ulipofika, washiriki walizikuta bites na chai vikiwa tayari vimeshaandlaiwa mezani, huku wahudumu wa mlo huo wakiwa hawapo, walikuwa tayari wameshaondoka
- Ilikuwa ni kawaida yao siku zote kuandaa mlo huo kwa mtindo huo
- Hata hivyo, haikuwa kawaida yao kuzitanguliza bites hizo asubuhi sehemu ya ukumbi ambapo mkutano ulikuwa unafanyikia
- Siku wanazitanguliza bites, ilikuwa ni mara ya kwanza kwa wao kufanya hivyo na ndiyo maana mhusika aliziona
Washiriki wa mkutano walipoanza kunywa chai, mhusika aligundua kuwa VITUMBUA havikuwepo tena na alishangaa
- Baada ya kuvikosa VITUMBUA, ikabdi mhusika ampigie simu rafiki yake kumuuliza VITUMBUA vilienda wapi
- Binti rafiki alimjibu mhusika kuwa vitumbua vilikuwa ni kwa ajili ya chai ya saa 10:00 na ndiyo maana hawakuviandaa kwa chai ya muda huo
Maongezi ya mhusika na rafiki yake yakaishia hapo; ila kikubwa kilichofanyika hapa ni kwamba
mhusika alimpigia simu binti, kwa mara ya kwanza ndani ya wiki hiyo ya mkutano
MHUSIKA ALAZIMIKA KUMPIGIA TENA SIMU BINTI KWA MARA NYINGIE YA PILI
Mhusika hakumbuki vizuri ila anadhani ilikuwa ni kwenye siku iliyofuata; ambapo kuna mazingira mengine yalijitokeza tena na hivyo kuepelekea
mhusika ampigie tena simu binti, kwa mara ya pili sasa
Hii ilikuwa ni baada ya Boss X kumuomba mhusika amweleze binti huyo apeleke funguo za ukumbi wa mkutano alizokuwa amezichukua; kwa Boss X ili Boss X aweze kufungua ukumbi huo
Binti huyu alizichukua funguo hizi baada ya chai ya saa, baada ya umeme kuktaika wakati wa chai ya saa 4
Wakati binti anakuja kukusanya vifaa vyake vilivyokuwa vimetukika kwa ajili ya chai ya saa 4 ili akavifanyie usafi, washiriki wote wa mkutano walikuwa wametoka nje ya ukumbi na hivyo wakati anatoka hapo ukumbini, ilibidi afunge ukumbi na pia kuondoka na funguo za ukumbi huo. Kitendio hicho cha binti kuondoka na funguo, ndicho baadaye kilipelekea Boss X amuombe mhusika ampe ujumbe binti uliohusiana na funguo za ukumbi huo
KILICHOPELEKEA BOSS X KUMUOMBA MHUSIKA AMPATIE UJUMBE BINTI
Mkutano ukiwa unaendelea siku hiyo,
wakati wa chai ya saa 4:00 umeme ulikatika, na HAPAKUWA NA STANDBY GENERATOR kwenye jengo hilo ambalo ukumbi wake ulikuwa unatumika na mkutano huo
Kwenye harakati za kujaribu ukumbi mwingine ambao ulikuwa una STANDBY GENERATOR, mhusika na Boss X wakashauriana na kuamua waende kwenye kitengo cha mambo ya ICT kilichopo kwenye taasisi hiyo, ambacho muda jengo huwa linakuwa na umeme.
Meanwhile, as a precaution, Boss X naye akaamua aende pia kwenye kitengo kingine kinachhusika na mambo ya walimu, akaangalie ukumbi mwingine huko
Wawili hawa wakatawanyika, mhusika akaenda kule ICT, na huko alienda akapata ukumbi mara moja pasipo tatizo lolote
Baada ya kupata ukumbi, mhusika akampigia simu Boss X kumweleza kuwa ukumbi umepatikana
Baada ya mashauriano dakika kadhaa, huku simu ya Boss X ikipatikana kwa kukatika katika, Boss X alimjulisha mhusika kuwa kuna ukumbi mwingine tena jengo jirani,(directly opposite, upande wa pili wa barabara) ambao ulikuwa umepatikana
Ukumbi huo alioupata Boss X,
ulikuwa ukumbi mwingine wa pili kwenye Idara ile ile ambayo mkutano huo ulikuwa unafanyikia
Baada ya hapo, mhusika alirudi na alipofika kwenye ukumbi wa awali ambapo alikutana tena na Boss X, hapo ndipo set-up nyingine ya pili iliyosababisha mhusika ampigie simu binti, ilipoanzia. Wakati huo umeme ulikuwa bado haujarudi
WALICHOONGEA BOSS X NA MHUSIKA WALIPOKUTANA PALE NJE YA UKUMBI WA AWALI AMBAO HAUKUWA NA STANDBY GENERATOR
………………….inaendelea