SAFARI YA TATU-MARCH 2011
“MAELEZO YA UTANGULIZI”
Watu watatu wageni kutoka nje ya taasisi, walifika kwenye taasisi wakiwa wanahitaji kufanya kazi na taasisi anayofanyia kazi mhusika
Watu hawa walifika na kupokelewa kwenye ‘MAJOR UNIT” nyingine, (tuiite MAJOR UNTI–B (MU-B)) ndani ya taasisi; tofauti na ile ya mhusika (hapa ya mhusika tuiite MAJOR UNIT –A (MU-A)); na kwa hali hiyo walifikia kwenye idara nyingine kabisa tofauti na ile ya mhusika
Walipofika huko MU-B; wageni hao waliwaelekezwa idarani kwa mhusika; na waliambatana na staff mmoja kutoka huko MU-B (tumwite stMU-B) ambaye katika maongezi yao na yeye walipokuwa bado wako huko MU-B (kabla hawajaelekezwa ofisini kwa mhusika) waliweza kum-earmark kujiridhisha kuwa stMU-B alikuwa anaweza kuifanya vizuri kazi yao kwa kushirikiana na mhusika
Sababu pekee iliyopelekea watu hawa kuelekezwa idarani kwa mhusika ni baada ya kifaa walichohitaji kwa ajili ya kazi; kuonekana kuwa hakikuwepo huko walikokuwa wamefikia; huku stMU-B waliyekutana naye huko, naye pia akiwahakikishia kuwa alikuwa nao uwezo wa kuifanya kazi isipokuwa tu alikuwa ana-miss kifaa cha kazi
Kwa hiyo baada ya hapo, stMU-B aliamua kuwaleta wageni hawa hadi idarani kwa mhusika; na baada ya kikao kifupi kati ya wageni hao na Mkuu wa Idara (MWI), stMU-B pamoja na mhusika mwenyewe, kikao hicho kilikubaliana mambo kadhaa kama yalivyoainishwa hapa chini.
Hii ilikuwa ni baada ya wageni hao kujiridhisha kuwa, kifaa walichokuwa wanakihitaji kwa kazi hiyo, ndiyo hasa kile ambacho kilikuwepo idarani kwa mhusika
Baada ya uhakiki wa kifaa hicho cha kazi; kikao kikiwa kinaongozwa na MWI ndani ofisini kwa Mkuu wa Idara wa idara ile ya mhusika; kikao hicho hatimaye kilikubaliana mambo kadhaa kama ifuatavyo hapa chini
- stMU-B na mhusika wataenda wote pamoja wakafanye kazi hiyo wote wawili; na kwa malipo kulingana na CONSULTANCY POLICY ya taasisi
- Kifaa cha kazi watasafiri nacho kwa njia ya ndege kwenda site kwa ajili ya kazi hiyo
- Mhusika na stMU-B watalipiwa usafiri wa kwenda na kurudi ikiwa ni pamoja na malazi na chakula; huku wakiwa wanaishi kwenye hostel ambayo ni ghorofa
- Ghorofa hilo lilishakodiwa na taasisi hiyo (yenye kuhitaji huduma) na huwa wanishi humo wafanyakazi wake ambao tayari wako huko wakiendelea na kazi
Zaidi ya hayo ni kuwa stMU-B na mhusika walikuwa wanafahamiana tangu kipindi kirefu nyuma, ila tu hawakuwa wamewahi kufanya kazi pamoja.
Mbali na hilo, stMU-B na mhusika wanaongea lugha moja ya kuzaliwa
Wageni waliohitaji huduma ya kazi walikuwa watatu,
na mmojawapo wa watu hao na ambaye ndiye alikuwa anaonekana kuwa ni boss wa wale wengine wawili; alikuwa na jina la ubini linalofanana na la mmojawapo wa viongozi wa Taasisi ya mhusika
Kwa wakati huo kiongozi huyu ambaye jina lake la ubini lilifanana jina la mgeni huyu alikuwa anafanya kazi kwenye MAJOR UNIT nyingine (tuiite MAJOR UNIT C; MU-C), lakini wakati anateuliwa kwenda kufanya kazi huko MU-C, alitokea MU-B, unit ile ambayo stMU-B alikiwa anafanyia kazi na ambako ndiko wageni hawa walikuwa wamefikia na kupokelewa
Hata hivyo, kiongozi huyu aliyekuwa kwa wakati huo anafanya kazi MU-C, bado alikuwa anahesabika kuwa sehemu yake ya kazi ni MU-B, na hadi leo hii bado anahesabika kuwa ni wa MU-B
Ilipofika Desemba 2015, kiongozi huyu alitoka huko MU-C na kuhamia Centra Administarion (CA) baada ya kuwa amepanda ngazi na kuwa miongoni mwa viongozi wanaoshikilia nafasi zile tatu za mwanzo kabisa katika taasisi, yeye akiwa ni wa tatu kutoka kwenye ngazi ya kiongozi wa taasisi nzima; na hadi leo yuko huko akiwa kwenye nafasi hiyo
Kwa hiyo stMU-B na kiongozi huyu
; (aliyetajwa hapa kuwa jina lake la ubini lilifanana na lile la mgeni aliyekuwa ameleta kazi kwenye taasisi); wawili hawa wote walikuwa wanafanya kazi kwenye MAJOR UNIT moja, yaani MU-B; isipokuwa tu kwa wakati huo kiongozi huyu yeye alikuwa yuko MU-C kama mtawala kule
“PLOT”
Mambo yote haya yalitokea mwishoni mwa mwezi wa pili mwaka 2011, na kazi husika ilianza kufanyika mwezi uliofuata, yaani March 2011
Baada ya wageni hawa kuondoka siku hiyo huku nyuma wakiwa makubaliano ya model ya namna kazi yao itakavyofanyika; baada ya siku kadhaa kupita; mgeni yule mwenye kufanana jina na kiongozi wa MU-C; (tumwite MG-MF), alirudi tena idarani, na safari akiwa tena ameambatana na watu wengine wawili
- Mmojawapo kati ya watu hao aliokuwa ameambatana nao alikuwa ni yule waliyekuja naye mara ya kwanza
- Mwingine wa pili alikuwa ni mpya; hakuwa yule ambaye alikuja mara ya pili
- Huyu mpya aliyekuwa amekuja wkati wa safari hii ya pili, naye alionekana kuwa ndiye boss wa MG-MF; na hivyo boss wao wote waliokuwa wamewahi kuja mara ya kwanza
Kwa hiyo mara ya kwanza MG-MF aliwahi kuja akiwa ameambatana na s
urbordinates wake wawili, ila kwa safari ya pili naye alikuja akiwa ameambatana na boss wake mmoja
WALIPOFIKA IDARANI: SAFARI HII MAZUNGUMZO YAFANYIKIA CHUMBA CHA CHAI NA SI OFISINI KWA MKUU WA IDARA KAMA ILIVYOKUWA KWENYE MAZUNGUMZO YALE YA AWALI
……………………..inaendelea