UPDATE MONDAY 1ST AUGUST 2022
SINK LA JIKONI LILIZIBA TENA JANA J2 JIONI NA HAKUNA NAMNA YOYOTE YA MHUSIKA KUWEZA KULIZIBUA.
KWA HALI HIYO INABIDI MHUSIKA AKAJAZE FOMU NYINGINE YA MAOMBI ILI MAFUNDI BOMBA WARUHUSIWE KUJA KUTATUTA TATIZO HILO KWA MARA NYINGINE TENA
Katika hali ya kawaida, mhusika alitakiwa aende akajaze fomu ya kuwaomba tena mafundi bomba kuja kutatua tatizo lake hilo, leo J3 asubuhi alipokuwa anatoka nyumbani akielekea ofisni, lakini kwa makusudi tu aliamua kutokufanya hivyo
Badala yake alinyoosha moja kwa moja hadi ofisini na baada ya kufika huko
alikuta kuna e-mail iliyokuwa imeandikwa na Mkuu wa Idara (MWI) ikimjulisha mhusika kuhudhuria mkutano uliokuwa unaanza saa 2:45 asubuhi na ambao ulikuwa unawahusu si wafanyakazi kwenye idara ya mhusika tu, bali wafanyakazi wote wa taasisi nzima
E-mail hiyo iliandikwa na MWI Ijumaa wiki iliyopita na iliandikwa baada ya saa 11:00 jioni
- Kwa hiyo iwapo kama mhusika angeamua kuanzia ofisi za idara ya miliki ya nyumba
- Uwezekano mkubwa ni kwamba ageweza kukuta hapana mtu husika kule kwa sababu possibly nao pia wangeweza kuwa wameelekea kwenye mkutano
- Zaidi ni kuwa mhusika asingeweza kujua kama kulikuwa na mkutano asubuhi hiyo kwa sababu hakuwa amesoma email kwenye siku za weekened, yaani Jumammosi na Jumapili
RATIBA INAYOAANZA KUJIDHIHIRISHA YA NAMNA SINK HILO LINAVYOZIBA:
LINAZIBA WEEKEND ILI J3 ASUBUHI NA MAPEMA, MHUSIKA AKAJAZE FOMU YA KUOMBA MAFUNDI WAJE WALISHUGHULIKIE
Mpaka muda huu, mhusika ameanza kujiridhisha kuwa sink hilo limekuwa na kawaida ya kuziba siku za weekend na hivyo kupelekea J3 asubuhi ya wiki inayofuata, mhusika alazimike kwenda kutoa ripoti ikiwa ni pamoja na kujaza fomu ili mafundi husika waje walishughulikie
Hii ni kutokana na ukweli kuwa kwenye tukio lililopita la hivi karibuni la kuziba kwa sink hilo,
sink hilo lilikuja kuzibuliwa na fundi Ijumaa asubuhi halafu ilipofika jioni ya siku hiyo hiyo, sink hilo liliziba tena.
Kutokana na hali hiyo, mhusika alilazimika kwenda kutoa ripoti ya tatizo la kuziba tena kwa sink hilo
J3 asubuhi ya wiki iliyofuata; na hatimaye mafundi walikuja kulishughulikia J3 hiyo
Mambo mengi sana yaliendelea J3 ya kuzibuliwa kwa sink hilo, ambayo mhusika hana haja ya kuyarudia tena humu jukwaani
Maelezo kamili ya tukio hili yatafuata baadaye, mhusika akishakamilisha pilika pilika za kiofisi za kuomba mafundi waje walishughulikie tena sink hilo
KUHUSIANA NA JIRANI AMBAYE KWENYE TUKIO LA AWALI, MAJI TAKA TOKA NYUMBANI KWAKE YALIKUWA YAKIVUJA KUPITIA BAFU NA CHOO VYA NYUMBANI KWA MHUSIKA
Katika kipindi chao chote cha ujirani wao katika maisha yao yote, mhusika na jirani huyu
kwa mara ya kwanza walifanikiwa kugongana kwenye parking J2 asubuhi, (mhusika akiwa anatoka kuelekea Kanisani) jirani huyu naye akiwa yupo na familia yake nzima akiwa anarudi kutoka Kanisani
Mojawapo ya watu waliokuwepo kwenye familia jirani huyu J2 hiyo, ni mtoto mjukuu wake na mhusika na ambaye ni rafiki yake wa karibu pia. Katika hali ya kawaida, mhusika asingeweza kumpita mjukuu wake bila kumsalimia, japo alikuwa bado hajashuka kwenye gari
Mhusika alimwita mjukuu akashuka kwenye gari, wakasalimiana na baada ya hapo akawaslimia na wengine wote kwenye familia wakiwemo wazazi wa mjukuu wake
Ilikuwa ni experience ya pekee J2 hiyo kwa sababu
ilikuwa ni mara yake ya kwanza kabisa mhusika kupata nafasi ya kusalimiana na familia nzima kwa mpigo hapo nje kwenye parking
Details zaidi zitafuata baadaye mhusika akishakamilisha kutatua tatizo la sink lililoziba
MUBARIKIWE TENA NA BWANA
UP NEXT:
Clips za mafundisho yote ya siku tatu kuhusiana na unabii, yaliyowahi kutolewa na Mtumishi wa Mungu hapo Kanisa A mwanzoni mwaka 2013