BAADA YA MLANGO KUSHINDWA KUFUNGUKA NA HIVYO MHUSIKA KUWA YUKO LOCKED NDANI YA CHOO
Mhusika aliamua kupanda juu ya sink la choo ambapo watu huwa wanakaa na hatimaye kushika juu ya ukuta wa choo, kwenye sehemu iliyokuwa wazi
Hapo aliamua kupaza sauti ili watu wanaopita nje wamsikie, na baada ya takribani dakika mbili hivi, kijana ambaye yuko field; ambaye alikuwa wakati fulani anafanya kazi kwenye mafaili yaliyoko chumba jirani na ofisi yao mhusika, alimsikia mhusika
Kijana aliiona hali hiyo na baada ya hapo alitoka akaenda akarudi na wenzake
MKAKATI WA UOKOAJI
Baada ya majadiliano ya hapa na pale, utaratibu ulikubalika kwamba mhusika apewe stuli mbili kwa ndani ili aziunganizshe halafu apande juu yake, halafu apite juu ya ukuta wa choo kwa sababu kulikuwa na nafasi juu kati ya ukuta na paa
- Stuli zingine mbili zilipangwa pia nje ya sehemu ambapo alitakiwa akanyage miguu yake atakapokuwa anatoka nje
- Utaraibu huo ulifanyika na mhusika akaanza kupanda juu tayari kwa kutoka
- Humo ndani ilibidi akanyage pia kwenye sink la maji ya kufashia choo, ambalo kwa bahati mbaya, lilitoboka na kung’oka kutoka ukutani
Hata hivyo alijitahidi kutumia stuli mbili alizokuwa amepewa na hatimaye kuweza kupanda juu ya ukuta
Pale juu kwenye ceiling, kulikuwa na
tube lights ambazo ilikuwa almanusura azivunje kwa kuzipiga kichwa, lakini vijana waliokuwepo walimtahadharisha baada ya kuwa wameona
reflection ya mwanga iliyokuwa inatokana na mwanga wa taa hizo kuakisiwa kwenye
kichwa cha mhusika
KIMO CHA STULI MBILI ZILIZOKUWA ZIMEPANGWA NJE ILI MHUSIKA AKANYAGE HAPO NA HATIMAYE AWEZE KUSHUKA CHINI NJE YA CHOO
Hapa ndipo zoezi lile la VIMO lilipoingia tena
Stuli hizo zilionekana kuwa ni fupi, KIMO chake kilikuwa hakitoshi kwa KIMO cha mhusika kuweza kufikisha miguu yake pale
- Kutokana na hali hiyo, ilibidi kuongeza stuli nyingine ya TATU
- Baada ya kuongeza stuli ya tatu, KIMO cha stuli kilitosha na hivyo kuendana na KIMO cha mhusika aliyehitaji kutoka nje ya chumba hicho maalumu
Mhusika alitoka salama na bila jeraha lolote, ispokuwa SINK la kuflashia lilitoboka na hilo ndiyo lingeweza kumjeruhi
Wakati mhusika anatoka ofisini kuelekea chooni, ilikuwa ni katika muda ambao wote wawili mhusika na OFFICE MATE-2 (OM-2), walitoka ofisini kumpisha binti ofisini kwa ajili ya usafi
OM-2 naye alikuwepo pia kwenye tukio hilo na ni mmojawapo wa wale waliosaidia kuleta stuli
Zaidi ni kuwa KIMO cha ukuta ambao mhusika aliupita kwa juu, kilikuwa ni KIMO KIGENI kwake, na pia kwa mtu mwingine yeyote kwa sababu tukio la aina hii lilikuwa ni la kwanza tangu jengo lianze kufanya kazi
KWA UCHUNGUZI WAKE WA KINA KWA KUANGALIA MATUKIO KABLA NA BAADA YA TUKIO HILI LA MLANGO WA CHOO KUGOMA KUFUNGUKA AKIWA YUPO NDANI YA CHOO
Aliyehusika na ku-organise tukio hili ni
ADMINISTRATIVE OFFICER (AO) ambaye huwa anapenda kuitwa
HR ila hajaajiriwa kama HR, wakishirikiana na
KATIBU MUHTASI WA MKUU WA IDARA (KMWI)
Wengine ni
MR X pamoja
fundi wa vitasa vya milango ambaye wanamfahamu wao, huwa wanamleta idarani. Mhusika hamfahamu na wala hajawahi kumuona
Uwezekano mkubwa ni kwamba fundi Huyu ndiye ambaye waliwahi kumleta kwenye tukio jingine la mwisho la kitasa cha mlango liliotokea pia siku ya J3 hivi karibuni
Angalau kwa sasa, mhusika ameshabaini kuwa AO ndiye amekuwa aki-plan matukio yote tangu waajiriwa wapya walipoanza, na ameendelea hadi kufikia kuwa anawatumia hata hawa ambao ni wanafunzi wa field
Taarifa zaidi kuhusiana uhusika wa watu hawa zinafuata