TUKIO LA PILI
Baada ya kuwa wameshirikishana mambo kadhaa (washiriki) wawili hawa, hatimaye ilionekana kuna mahali MSH-B aliguswa na hivyo ikampelekea kuwa willing kutoa msaada angalau wa kimawazo, kwa mhusika
- Ni kweli kwamba mhusika alikuwa na hitaji na ambalo alikuwa amemshirikisha MSH-B pamoja na baadhi ya washiriki wengine Kanisani hapo
- Halikuwa hitaji ambalo linaweza kuchukuliwa kuwa linahitaji privacy, hapana
- Provided mtu unafahamiana naye na ni mshiriki ambaye unamwamini kuwa yuko sawa kiakili na kiroho pia, hitaji hilo lilikuwa wazi kwa kila mtu wa aina hiyo
- Hata hivyo pamoja na kumshirkisha MSH-B, mhusika hakuwa amemuomba MSH-B kutoa msaada huo
- Na kutokana na heshima aliyokuwa nayo mhusika kwa MSH-B (ukizingatia mambo kadhaa kama vile tofuti kati ya umri wao, mahusiano yao ya zamani kipindi wanafahamiana kwa mara ya kwanza, na pia mahusiano yao ya sasa kama washiriki wa kanisa la mahali pamoja) mhusika hakuona tatizo lolote kupokea msaada wa kimawazo japo kutoka kwa mtu ambaye hakuwa amemuomba msaada wa aina hiyo
- Vile vile mhusika yeye kwa upande mwingine, alidhani pengine yaweza hata kuwa MSH-B ameshauriwa na uongozi wa kanisa akiwemo KM-B, kwamba aweze kutoa ushauri na msaada huo kwa mhusika
Wakiwa katika kushauriana kwao, ilitokea siku moja baada ya Ibada ya jioni
- MSH-B alimwita mhusika pembeni ili waongee kwa faragaha, ila ndani ya Kanisa
- Wakati huo kuna kikundi cha kwaya kilikuwa kilikuwa kinaendeea kufanya mazoezi ya nyimbo baada ya Ibada kuisha, na drums zilikuwa zinapigwa kwa mlio wa juu sana (ana maana yake kuyawekea bold maneno haya) kiasi kwamba hata kusilkilizana ilikuwa ni shida sana
Kwenye siku hii, hapakuwa na ulazima wa wawili hawa kuongea ndani ya Kanisa wakati tayari Ibada ilikuwa imeisha na ukizingatia kuwa wote walikuwa na mpango wa kuondoka hapo Kanisani kuelekea nyumbani Wangeweza kuongea wakasikilizana vizuri wakiwa nje pembezoni mwa kanisa, kukwepa kelele zilizokuwa zinatokana na vyombo vya muziki ndani ya Kanisa
Baada ya kuwa amemwita pembeni mhusika
- MSH-B alifungua Biblia na kumsomea mhusika fungu kutoka kwenye maandiko matakatifu
- Baada ya kuwa amelisoma fungu hilo, MSH-B alilihusianaisha na hitaji mojawapo la mhusika ambalo MSH-B alikuwa amejitoa mhanga kumsaidia au kulishughulikia
- Mwishoni mwa maongezi hayo, MSH-B alimshauri mhusika kwamba J2 ya wiki inayofuata atoe sadaka ya shukurani kwenye Ibada ile ya asubuhi kabisa (morning glory) na sadaka hiyo aiweke kwenye bahasha
- Sadaka hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya hitaji lake mhusika ambalo MSH-B alikuwa ameamua kulivalia njuga
Ilipofika siku ya J2, mhusika alitekeleza maaelekezo ya
“mentor”wake huyo kwenye Ibada ya asubuhi ya morning glory.
Baada ya hapo, muda kitambo kabla ya Ibada ya kwanza kuanza, mhusika aliamua kutoka nje ya Kanisa, na
hapa ndipo kosa la kwanza lilipofanyikia
Akiwa mlangoni huku akiandaa miguu ikanyage ngazi za kutokea nje kabla hajashuka ngazi, alistukia mtu anamshika begani kwa nyuma, mtu huyo akiwa ndani ya Kanisa. Alivyotupa jicho nyuma akagundua kuwa mtu huyo alikuwa MSH-B. Hawakuongea mengi isipokuwa MSH-B alikuwa anataka kujua kama mhusika alitekeleza kama walivyokubaliana ndani ya wiki kuhusu sadaka. Mhusika alijibu neno moja tu la ndiyo na maongezi yao yakaishia pale. Mpaka hapa mtu yeyote mwenye akili timamu anaweza akaainisha mambo kadhaa kama iifuatavyo:
- MSH-B alikuwa na uwezo wa kumuuliza mhusika kuhusu sadaka hiyo wakiwa ndani ya Kanisa
- MSH-B alisubiria mhusika akiwa anatoka nje, akiwa mlangoni ambapo si ndani wala nje, na kumuuliza swali alilotaka kumuuliza
- Hapakuwa na ulazima wowote wa MSH-B kuhitaji kujua kama mhusika alitoa sadaka hiyo, kwa uharaka wa namna hiyo, yaani mara tu baada ya Ibada husika kuisha ambayo mhusika alitoa sadaka
- Kama MSH-B alihitaji kujua hilo kwa nia njema kabisa, angeweza kulifuatilia hata mara baada ya muda wa Ibada, au hata kwenye wiki zingine zilizokuwa zinafuata mbele ya J2 hiyo
- Moangezi hayo yalichukua muda mfupi sana, kiasi kwamba MSH-B hakutaka kuonekana na watu akiwa anaongea na mhusika
Maongezi hayo:
- Yalifanyikia sehemu ile ile ambayo yaliwahi kufanyikia maongezi ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa A na mhusika siku kiongozi huyo (KM-A) alipofika Kanisani hapo kwa ajili ya huduma ya Ibada
- Ni siku ambayo walipishana KM-A na mhusika, KM-A akiwa anaingia Kanisani na mhusika akiwa anatoka nje
Ikumbukwe pia kuwa,, siku hiyo,
KM-A alikuwa amaambatana na kionngozi mwingine mwenyeji wa kanisani hapo ambaye hakuwa KM-B. Kwa hiyo kiongozi wa Kanisa B aliyewahi kuongelewa humu hapo awali hakuwa huyu ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Kanisa B (KM-B)
HITIMISHO: TUKIO LA PILI
Yaliyotokea baada ya mhusika kuwa ametoa sadaka na hatimaye MSH-B kufuatilia na kujua kuwa mhusika alitoa sadaka hiyo, hatimaye kuna siku mambo haya yaliwahi kumfikia KM-B kwa sababu katika kipindi chake cha miaka mitatu alichowahi kuwepo Kanisa B, mhusika aliwahi kuwa na kesi mara mbili na MSH-B wakiwa wameshitakiana kwa kiongozi huyo
Kwa upande mwingine, Kanisa B lina watu wachache lakini ni wakorofi sana. Wananamfuata mtu na kuanza kumchokoza, wakiwa na mitego ya kumfanya ateleze halafu wapeleke mashtaka kwa Kionngozi Mkuu. Mhusika alipokaa nao na akawafahamu vizuri, aka-device mechanism ya kuwa anawawahi yeye kabla hawajamwahi
Kwa hiyo details za yaliyoendelea baada ya sadaka hiyo tayari anazo KM-B. Izingatiwe pia kuwa huyu KM-B si yule aliyeambatana na KM-A ambaye aliwahi kutamka maneno akimwambia KM-A kuwa
“kumbe huyu mtu aliondka bila kukuaga’. Aliyewahi kutamka maneno haya ni msaidizi wa KM-B na si KM-B. Details zake huyu naye zitafuata baadaye kwenye mada hii hii ya Kabisa B
………………………….inaendelea