#COVID19 Mkasa wa kipekee kuhusu pilikapilika za kujikinga na COVID-19

#COVID19 Mkasa wa kipekee kuhusu pilikapilika za kujikinga na COVID-19

EBR. 6:4-6 SUV

Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.
 
UPDATE: TUESDAY 26th JANUARY 2021

NYONGEZA MUHIMU


Hili swala la kukosekana kwa simu za mezani (extension) ofisini ndiyo hilo linalopelekea baadhi ya mambo kama:

  • Mtu anapata promotion halafu mwisho wa mwezi anagundua kuwa mashahara wake haujaongezeka
  • Baada ya hapo, anajaribu kufuatilia kwa baadhi ya wahusika walioko ngazi za chini halafu wahusika hao wanamushauri aende akaonane kwanza na Afisa Rasilimali Watu
  • Na kwa sababu hakuna simu za mezani, inabidi kweli (iwapo kama kweli anahitaji mshahara huo uongezeke), mtu huyo aidha aache kazi zake, anyanyuke kutoka ofisini kwake kuelekea ofisi husika au asiende halafu mshahara uendelee kubaki ule ule pamoja na ukweli kwamba amepewa promotion
Na kwa bahati nzuri au mbaya, mtu huyu anamua kutokufutilia maofisini, na hali hii inapelekea kweli mshahara huo kuendelea kubaki uleule tangia Julai 2012 kupitia Novemba 2017 (muda wa promotion) na hadi leo hii January 2021

EBR. 6:4-6 SUV

Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.


MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
UPDATE: WEDNESDAY 27th JANUARY 2021

MBINU MBADALA NA ILE ILIYOTAJWA HAPO JUU, ZINAZOTUMIKA KUMUWEKEA MITEGO YA KUMNASA MHUSIKA KWA SASA




Wakishamuona kuwa ha-respond kwenye mtego wao mmoja wa kufuatilia jambo moja, wanatengeneza mtego mwingine, ili aanze kufuatilia jambo jingine mbadala. Kwa mfano, mtego mmojawapo ni kwa sasa ni ule unaohuisana na umeme na maji. Na kwa huu mtego mpya wa unaohusiana na umeme, details zake ni kama ifuatavyo:

Wamepunguza umeme nyumbani kwake kwenye baadhi ya phase na kusababisha Micro-Wave isiweze kufanya kazi. You can imagine namna situation ilivyo ngumu kwake kwamnmba anaishi kwa maisha ya micro-wave tangu mwaka 2006

  • Mara zote huwa wanatengeneza mitego yao pindi wanafunzi wanapokkuwa wako–off. Ili anapokuwa anafanya ufutiliaji, pasiwepo na mashahidi wengi kwenye mazingira ya kazi
  • Kwa hali hiyo yeye naye pia alishatengeneza counter strategy, kwamba akipatwa na tatizo wanafunzi wakiwa hawapo, huwa anavumilia kiasi cha kuwasubiria wanafunzi hao mpaka pale watakaporudi tena ndiyo naye anaanza tena kufuatilia tatizo hilo
  • Mara ya kwanza alifanya ufuatiliaji ofisini kwa ajili ya swala hili la umeme mwanzoni mwa Desemba, muda mfupi tu baada ya wanafunzi kuwa wamerudi
  • Alipewa ahadi za kuridhisha sana lakini baada ya hapo, uliwekwa mtego wa kijinga na alipoukwepa, hakupata response nyingine tena mpaka sikukuu za Christmas na mwaka mpya zinaingia
  • Na kwa sababu wakati huo wanafunzi walikuwa wameshaondoka tena kwa ajili ya sikukuu, aliacha kufuatilia swala hilo akisubiri warudi tena
  • Jumanne ya wiki jana ya tarehe 20/01/2020, ndiyo alirudi tena kwa ajili ya ufuatiliaji wa swala hilo pamoja ikiwa ni pamoja na lile la zamani la maji
  • Alikutana na mitego ya kijinga details zake hawezi kuzidisclose humu jukwaani
  • Baada ya hapo, alirudi ofisini kwake na ndiyo akakuta nako kulikuwa tayari kuna mtu alikuwa anamtafuta kwa ajili ya ukarabati ambao ulitakiwa kuanzia ofisini kwake, details zake ameshazitoa kwa kirefu kwenye posts zilizopita hapo juu hivi karibuni
  • Haya matukio yanaonyesha coincidence “if A, then not B. If not A, then B


HITIMISHO


Walipunguza umeme nyumbani kwake kwenye baadhi ya phase tu tangu mwaka jana mwezi wa tisa mara tu baada ya wanafunzi kuwa wameondoka

Kwa hiyo mpaka muda huu, ameshajaribu kufuatilia swala hili la umeme mara mbili kwa wahusika ofisini, na kila akienda anaenda kukutana na mitego ya ajabu ajabu pamoja na response nzuri sana, halafu baada ya hapo inakuwa kimya. Ukimya huu unamaanisha kuwa anatakiwa arudi tena kufuatilia kwa mara nyingine ili akakutane na mtego mwingine tena watakaokuwa wameutengeneza kwa matarajio yao kuwa pengine labda huo unaweza ukafanakiwa

Na haya yote yametokea baada ya kuwa ameacha kufautailia maslahi yake ofisi ya rasilimali watu na kwingineko



MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
UPDATE-2: WEDNESDAY 27th JANUARY 2021

LEO MHUSIKA AMEBAHATIKA KUFIKA TENA KWENYE BANK ZOTE MBILI, BANK A NA BANK B

BANK A


  • Hii ndiyo Benki yake ya zamani, ambayo ameshafunga akaunti zake zote
  • Hata hivyo kuna muamala alikuwa anahitajika kuUfanya kwenye benki hiyo kwa ajili ya mtu mwingine
  • Katika harakati hizo, amefanikiwa pia kuonana na “banker special” aliyekuwa mara zote akimptia salio la akunti yake kwenye Benki hiyo
  • Mara ya mwisho mhusika kufanya muamala kwenye akaunti yake na benki hiyo ilikuwa April 2020
  • Siku hiyo alikuta akaunti yake imezuiliwa kutoa fedha kaunta, ikabidi teller aliyekuwa dirishani siku hiyo, aombe authorization kutoka kwa mtu mwingine
  • Teller alimpa mhusika kikaratasi na kumwelekeza mtu wa kumpelekea kwa ajili ya kutoa hiyo authorization, na mtu huyo alikuwa ndiyo huyu “special banker”
  • Mhusika leo alijaribu kuongea naye kwa ufupi sana kutaka kujua tu ni nini kilikuwa kimetokea kwenye akaunti yake siku hiyo hadi ikapelekea huyu banker aombwe kutoa authorisatin
  • Banker amejibu kwa kusema kuwa hata hakumbuki chochote kile cha siku hiyo


KULE BANK B

  • Hajaonana na yeyote yule kati ya wale wahusika ambao walikuwa special kwa ajili ya kumpatia salio la akaunti yake
  • Zaidi alitaka kuonana na yule aliyetuma mtu kumjulisha mhusika kuwa kulikuwa na barua yake, lakinI inaonyesha mtu huyo alikuwa yuko bize sana
  • Huyu naye ndiyo mmojawapo wa waliokuwa wakimpatia salio mhusika mara kwa mara hapo BB
Zaidi ni kuwa barua ile aliyoitiwa mhusika mwezi jana, hakuikuta, ameambiwa kuwa haipo



HITIMISHO

Huyu mtu kutoka mamlaka ya mapato, aliyebuni mfumo wa wafanyakazi wote kuwa na TIN amefanya ubunifu wa kupongezwa sana. Ameokoa haki za watu wengi muno, bila yeye mwenyewe kujua



MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
NEXT: KITU KINGINE AMBACHO SIYO CHA KAWAIDA, ALICHOFANYA HUYU MFANYAKAZI WA BENKI B WAKATI MHUSIKA AKIWA HAPO BENKI LEO.

Ni yule ambaye aliwahi kumuitia barua ya majibu mhusika, au kutaka kumtumia watu wampelekee barua hiyo ofisini kwake.

Anaonekana kama huwa haishiwi plans, kama alichofanya leo haikuwa coincidence ya kawaida tu!
 
UPDATE: THURSDAY 28th JANUARY 2021

TAREHE 27 JANUARI 2021 MHUSIKA ALIPOKUWA YUKO BANK B (BB)


ALIOMBWA KUKUTANA NA “SPECIAL BANKER” SEHEMU TOFAUTI NA ZILE AMBAZO KWAIDA BANKERS HUWA WANAKUTANA NA WATEJA WAO KWA AMONGEZI MAALUMU, KAMA VILE CUSTOMER SERVICE (CS)

Siku hiyo mhusika alifika kwenye dawati la CS la BB na kuomba salio.

  • Kwa mara ya kwanza alihudumiwa na mtu mwingine tofauti, na hapakuwa na matatizo ya mtandao siku hiyo
  • Mhusika aliulizia pia kuhusu barua yake aliyowahi kuitiwa siku kadhaa nyuma, na alitumwa mtoto kutoka pale na kuingia ndani kusikoonekana kwa ajili kwenda kuichukua na kuileta
Baada ya hapo, zilipita takriban dakika thelathini mtoto hajarudi, na baada ya mhusika kuulizia aliambiwa kuwa barua hiyo haipo

BAADA YA MHUSIKA KUJULISHWA NA WATU WA CS KUWA BARUA HIYO HAIKUWEPO

  • Aliwauliza watu wa CS kama ‘fulani” yaani yule “special banker” alikuwepo kazini siku hiyo
  • CS walimjibu kwa kumwambia kuwa “ndiye tuliyekuwa tunaongea naye kwenye simu sasa hivi”
  • Mhusika aliwaomba wamuombe aje CS ili waongee pale
  • CS walimpigia simu tena na kumweleza ombi la mteja
  • Special Banker (SB) huyo aliwajibu kwa kuwaeleza kuwa inabidi mteja asogee sehemu kule ndani wakongee huko
Hapa ndipo tatizo lilipoanzia kwa sababu:

  • Sehemu aliyoshauri SB waonane na mteja siyo sehemu rasmi kwa maongezi na wateja mahali hapo
  • Benki ni sehemu ambayo ni sensitive, kiasi kwamba SB anajua fika kabisa kuwa mteja kawaida hatakiwi kuonekana sehemu nyingine yoyote tofauti na sehemu zile za kawaida tu ambazo yuko authorized
  • Kawaida mteja yoyote yule kwenye Benki yoyote ile, anatakiwa kuonekana CS au kwenye sehemu ya kusubiria kuelekea kwenye counters za walipa/ wapokea fedha
  • Sehemu nyingine maalumu hapo BB kwa mteja yeyote mwenye jambo muhimu na anayetakiwa kuonana na wahudumu wa Benki, ni kwenye ofisi iliyoko mkabala na dawati la CS, yenye vioo vinavyoonyesha wazi watu wanaokuwa wamekaa humo wakifanya maongezi yao ya faragha,
  • Mara zote mhusika alipokuwa ana jambo muhimu, amekuwa akikutana amekuwa akikutana na baadhi ya wafanyakazi wa Benki hiyo, ndani ya ofisi hii aliyoitaja hapa, baadhi yao akiwa ni meneja wa tawi hilo pamoja na wasaidizi wake wote
  • Mhusika hajawahi kukutana na mtu mwingine yeyote kwenye BB tofauti na sehemu hizi alizozitaja hapa
Kwa hiyo mara zote, mhusika amekuwa akikutana na watu wa BB kwenye sehemu special kwa ajili ya wateja, ikiwemo siku ya kwanza alipofika mahali pale kwa mara ya kwanza kabisa kwa ajili ya kufungua akaunti zake

Sasa SB safari hii yeye alitaka akutane na mteja tofauti na sehemu hiyo, tena ndani ya Benki, mahali ambapo ni sensitive, na kwa mteja ambaye hamjui zaidi ya kuwa wanakutana naye pale benki tu. Zaidi ni kuwa mteja alikuwa ameomba kuonana na SB sehemu shahiki kabisa ambayo ni CS kwa sababu hapakuwa na usiri wowote wa maongezi kati ya hawa wawili. Yeye mhusika alitamani waongee wakiwa CS na watu wote waliokuwa pale wasikie maongezi yao. Huyu SB yeye hakutaka hicho kitu kifanyike.

Mhusika anajaribu kujiiuliza mpaka muda huu kwamba huyu mama alikuwa na mpango gani, ukizingatia kuwa hata ile barua aliyowahi kumuitia nayo pia ilikuwa tayari uimeshayeyuka?



HITIMISHO

Mhusika hakuweza kuridhia ushauri huo na hivyo aliamua kuondoka mahali pale pasipo kuonana na SB huyo. Kwa hiyo mpaka muda huu inaonyesha kama hela yake iliyowahi kukaa Benki kwa muda wa zaidi ya miezi minane, aidha haijalipwa kabisa riba, au kama imelipwa basi itakuwa ni kiasi cha TZS 400,000/= tofauti na makubaliano ya kiasi cha riba walichowekeana wakati mteja anafungua akaunti hiyo mwaka 2018

Kawaida alikuwa anadai kiasi kisichopungua million mbili na nusu, kwa riba waliyokubaliana kwenye mkataba wa akaunti hiyo. Vinginevyo kama hela hiyo ingekuwa imewekwa kwenye FDR, basi angestahili kulipwa malipo ya takribani shillingi million sita (TZS 6,000,000/=)



MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
UPDATE-2: THURSDAY 28th JANUARY 2021

MBINU ILIYOTUMIWA NA SB WA BENKI (BB) INAFANANA NA ZILE ZINAZOENDELEA KUTUMIKA OFISINI, NA PIA ZILE ZILIZOWAHI KUTUMIKA KANISANI, KWA MHUISKA


Alichofanya huyu SB wa BB ni sawa na kile ambacho wanafanya kwa sasa, baadhi ya watu wa ofisini kwa mhusika:

  • Waliowahi kumkatia maji tangu Novemba 2018
  • Walioamua kupunguza umeme kwenye baadhi ya phase ndani ya nyumba anayoishi, tangu mwanzoni mwa Septemba 2020,
  • Ambao wamekuwa wakishikilia sehemu ya maslahi yake
Hawa wote wamekuwa wakitumia mbinu noja pindi wanapokuwa “wamem-set” kwenye pilika pilika za kufuatilia msaada anaouhitaji kutoka kwao. Mbinu hizi wanaambukizana kama magonjwa ya kuambukiza, yaani communicable diseases

Hata hivyo, “mastermind” wa mbinu hii wapo Kanisa B, king wao akiwa Mzee wa Kanisa B (MZK-B). Tutarudi kwao tena hivi karibuni, baada ya kuwa tumeachana nao kwa takribani wiki mbili sasa. Wiki ijayo tutarudi kwao tena



MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
UPDATE: MONDAY 1ST FEBRUARY 2021

KWA WAUMINI WOTE WA KANISA A:


KAMA MATUKIO HAYA YALIYOTOKEA KIPINDI CHA HIVI KARIBUNI YATAKUWA SIYO CINCIDENCES, BASI LAZIMA YATAKUWA NI MAIGIZO YALIYOKUWA YAMEPANGILIWA KWA UTAALAMU WA HALI YA JUU SANA

Kama matukio hayo yatakuwa siyo coincidences bali yalipangwa, basi wahusika wakuu watakuwa ni wafuatao

NAMBA MOJA: Kiongozi Mkuu

  • Huyu ndiye alianza kwa kufungua milango wakati anafundisha somo la hivi karibuni lililokuwa linahusu nafsi, roho na mwili pamoja na milango mitano ya fahamu (macho, pua, masikio, ngozi, ulimi)
  • Alikuwa anafundisha kwa kutumia watu aliokuwa anawasimamisha mbele ya madhabahu muda wote akiwa anafundisha somo hilo
Baada ya kufundisha somo hilo, alipotea madhabahuni, kwa maana ya kuwa hakuwahi kusimama tena madhabahuni kwenye siku za Jumapili kwa ajili ya kufundisha maandiko matakatifu.
Hapo sasa akawa tayari ameshamliza kazi moja ya kufungua mashambulizi ya kiroho kwa baadhi ya waumini kupitia viungo hivyo vya waumini (milango mitano ya fahamu), ikiwa ni pamoja na mashambulizi kwa kupitia nafsi (akili, fikra mawazo)

Baada ya hapo tena, ndiyo sasa baadhi ya waumini wakatokea kulalamikia kuona visivyostahili kuonekana.

Kama kweli vitu hivi walivyovilalamikia vilikuwa ni halisi na si malalamiko ya hewani tu, basi inaonekana kama vilikuwa vimepangwa. Vilianza kufanyiwa kazi siku Kiongozi Mkuu alipoanza kufundisha somo tajwa hapo juu. Somo hilio lilikuwa limekusudiwa kufungua milango ya kuwashambulia watu kwa njia ya milango hiyo mitano ya fahamu, yaani

  • Macho-kuona
  • Pua-kunusa
  • Masikio-Kusikia
  • Ngozi-uzinzi (feeling) ikiwa ni pamoja na joto (ubaridi, umoto) unashambulia kupitia ngozi ya mwanadamu
  • Ulimi-ladha, kuonja kupitia ulimi ikiwa ni ni pamoja na kula chakula
Kwa hiyo mapando yote yalifanyikia kule kweye picha za ajabu, kama kweli zilikuwepo. Na ndiyo sababu Kiongozi Mkuu hakuwa amehudhuria

NAMBA MBILI: Mhubiri wa uzinzi


Inaonekana kama kilichokuwa kinaendelea yalikuwa ni maigizo yaliyokuwa yamelenga kuja kuruhusu baadaye Kiongozi Mkuu kutoa tangazo la uzinzi akiwa amesimama madhabahuni

Inaonyesha kama ni maigizo kama ya wale waliowahi kubadilisha imani halafu KM akaja akawatangaza kama wazinzi, kama na hayo nayo yalikuwa ni maigizo pia

Maelezo ya kina kuhusu huyu mtu Mhubiri wa Uzinzi yatafuata baadaye. Anaonekana kama anawatoa kafara watoto wake kwa kuwa anawadhalilisha Kanisani

Maigizo hayo yamehitimishwa na Kiongozi Mkuu kwa kusimama madhabahuni na kutoa tangazo la uzinzi



NAMBA TATU: “MR X”


Huyu ndiye aliyemhamasisha mhusika kwa ajili ya mchango wa harusi, na alitoa

  • Mr X alikuwa mmojawapo wa wanakamati wa kamati ya harusi hiyo ambayo mshiriki mmojawapo amefukuzwa ushiriki na harusi hiyo kufutwa kabisa kuwa haitakuwepo tena kwa sababu ya uzinzi
  • Inaonyesha kama ili kutekeleza mkakati huu wa kutoa tangazo hilo la uzinzi madhabahuni, sadaka pia ilikuwa inahitajika pia
  • Na kama ni hivyo basi michango iliyotolewa na waumini kwa ajili ya harusi hiyo ndiyo imefanya kazi ya sadaka iliyohitajika kwa KM kusimama madhabahuni na kutoa tangazo hilo la uzinzi


HITIMISHO

Kama matukio haya siyo coincidences za kawaida tu, basi watu hawa wanaelekea kubaya, yaani Kiongozi Mkuu na watu wake

Mwandishi wenu atarudi kwa ajili ya maelezo ya kina zaidi, ila inaonyesha kama ambacho kimekuwa kikiendelea kanisani, ni maigizo matupu

Maelezo ya kina zaidi na yenye ufafanuzi murua yatafuata baadaye, possibly siku nyingine




EBR. 6:4-6 SUV


Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.
 
Li kitu lirefu
Afu anaongelea feni mara switch mara sanitizer.....feni hulipii umeme wewe mikono inakuwashia nini?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] dah..
Endelea endelea mbele mkuu,
Me natafuta hedex hapa
 
Baada ya kusoma full thread asee,
Mkuu uandishi wako changamoto.
Ukijumlisha na codes pamoja na coded message ndo balaa lnakua kubwa.
Nikiri nmeelewa like 25% tu na niseme siulizi swali lolote inatoshaaaa!!!
Pole kwa jamaa mhusika tho hadi sasa tunajua ni wewe mwenywe na pole kwa mods maana thread kama hii hata kuedit hawawezi..
Alamsik!
 
How do you manage to tell someone's story without any nukta? In anyway, whether the story is yours or not the nuktas must be around your entire text.
Unless the story is a fabrication, you are being urged to focus mainly on the content, and not on the story teller
There is a thin line between the story and the story teller, Just like lies and the lier! They all goes together, The nuktas is just there to soldfy (nukta).
 
UPDATE: 16 JULY 2020



MAELEZO YA NYONGEZA KUHUSIANA NA CHEMBA AMBAYO IMEKUWA IKITOA MAJI MACHAFU YALIYOCHANGANYIKANA NA KINYESI KANISANI

Ni mtizamo wa mhusika kwamba hii chamber imekuwa ikitunzwa ikae katika hali ya kuvuja, tangu kipindi kirefu nyuma, kwa makusudi ya kuwa inavujisha kinyesi hicho pindi mvua zinappkuwa zimeanza

Fuatana na maelezo ya mhusika katika tukio hlil hapa chini ili uweze kuthibitisha maneno yake

Takribani mwaka mmoja na nusu au miwili hivi imeshapita, ilitokea siku moja mhusika akadhani kuwa pengine labda viongozi wa Kanisani wamepitiwa tu kutokana na shughuli nyingi na hivyo wameshindwa kuiangalia kwa jicho la umakini chamber inayovuja kinyesi Kanisani hapo. Kutokana na dhana hiyo, mhusika siku moja akiwa Kanisani, aliamua kumshirikisha mmojawapo wa mashemasi Kanisani hapo, na ambaye ni mwalimu wake (yaani Shemasi ambaye aliwahi kuwa mwalimu wa kiroho wa mhusika, kipindi mhusika akiwa bado ni mshirika kwa kupitia dararsa la waongofu wapya). Mhusika alliamua kumshirikisha mwalimu wake mambo makubwa mawili

  • MOJA: Kuhusiana na kinyesi kilichokuwa kinavuja kutoka kwenye chemba
  • PILI: Kuhusiana na wito zinazotolewa na viongozi wa watu kupita mbele ya madhabahu, wakati wa Ibada kuu siku za J2
Mhusika alimshirikisha mwalimu wake mambo haya mawili na kumuomba kiongozi huyo kama anaweza kuyafikisha kwenye ngazi za juu Kanisani hapo.

Kuhusiana na swal la chemba iliyokuwa inavuja kinyesi, mhusika hakuongea mengi isipokuwa alimwonyesha tu mwalimu wake sehemu hiyo na kuiona (japo sehemu imekaa mahali ambapo mtu yeyote hahitaji kuonyeshwa ili aweze kuiona) na baada ya kuwa naye amehakikisha kuwa kweli ilikuwa inavuja, alikiri kuwa hali hiyo haikuwa nzuri na aliahidi kulifikisha swala la mhusika kunakostahili.

Kwenye mada hii, mwandishi anaomba ajikite zaidi kwenye swala la pili, kulingana na msisitizo wa mtoa maelezo mwenyewe, ambaye ni mhusika



WITO ZILIZOKUWA NA AMBAZO ZIMEKUWA ZIKITOLEWA NA WAHUBIRI KWA WAUMINI KUPITA MBELE YA MADHABAHU SIKU ZA IBADA ZA J2

Kwenye kipengele hiki, mwandishi anapenda ajikite zaidi katika kutoa maelezo ya kina kuhusiana na wito mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa wakati wa mahubiri, zikiita watu wapite mbele ya madhabahu kwa ajili ya msaada wa kufanyiwa maombi zaidi. Wito hizi zina uhusiano na swala linaloongelewa hapa kwa mantiki mhusika alilitoa maobi mawili kwa wakati mmoja likiwemo lile la chemba ya maji machafu

Tangu mhusika arudi kutoka uhamishoni Kanisa B, mwezi April 2017, rekodi ya kumbukumbu zake mpaka wakati huo (yaani hadi kipindi anafanya maongezi na shemasi mwalimu) ilikuwa inamuonyesha kuwa:

  • Kuna wito mmoja tu POSITIVE ambao ulikuwa umewahi kutolewa na Kiongozi Mkuu ukiita watu wapite mbele madhabahuni kwa ajili ya kuombewa ili waweze kufanya vizuri zaidi
  • Wito POSTIVE hapa mhusika anamaanisha wito ule ambao SI LAZIMA kila anayekaribishwa kupita mbele madhabahuni, awe ni yule ambaye ANA MATATIZO SANA KIROHO, japo pia hata walio na matatizo pia wito wa aina hii huwa hauwawekei mipaka na huwa wako huru kupita mbele pale wanapokuwa wanajisikia kufanya hivyo
  • Kwa hiyo hapa Kiongozi Mkuu siku hito alinamaanisha watu ambao wapo Kanisani na ambao wanaona wanaishi sawa sawa na mapenzi ya Mungu, na wanapenda kuendelea kuishi sawasawa na mapenzi ya Mungu, na hivyo wangependa waombewe ili waendelee kufanya vizuri zaidi
  • Watu wa aina hii huwa wapo Kanisani, na wanaweza kuwa ni wengi tu
Baada ya wito huo, muda mfupi mbele na baada ya maongezi ya mhusika na Shemasi mwalimu, J2 nyingine alisimama tena mwingine, yaani Kiongozi X na kuita watu ambao wao wanapenda KUONGEZEWA ujazo wa Roho Mtakatifu, YAANI WAJAZWE ZAIDI NA ZAIDI. Wito huu nao kwa upande mwingine, ulikuwa POSTIVE, japo pia ulikuwa unagusa pande zote mbili. Huyu alisimama kutoa wito huo muda mfupi BAADA ya mhusika na shemasi mwalimu kuwa wameshafanya maongezi yao

Kwa kumbukumbu za mhusika mpaka leo hii, ukiondoa wito hizi mbili zilizoainishwa hapa juu:

  • Hapajawahi tena kutokea wito wa madhabahuni ambao ni PISITIVE, hadi leo hii July 2020
  • Wito zote zingine zimekuwa ni zile ambazo ni NEGATIVE kama vile kwa ajli ya wazinzi, wanaofanya mapenzi ndotoni, wagonjwa, walio na matatizo ya kiroho, wasiokuwa na Roho Mtakatifu, wanaosumbuliwa na nguvu za giza, n.k.
  • Ni sahihi kabisa kwa wito za aina hii kuwa dorminant kwenye nyumba yoyote ile ya Ibada, lakini hii haimaanishi kuwa wito ambazo ni POSITIVE zisiwepo kabisa kwa sababu bado wapo watu wanaofanya vizuri, na ambao nao wanahitaji kupita madhabahuni na kuongezewa nguvu
  • Tatizo liliopo ni kwamba Kiongozi Mkuu huwa anafarijika zaidi pindi inapotokea umetolewa wito ambao ni NEGATIVE halafu akaona kundi la watu wengi wamepita madhabahuni, kitu ambacho siyo sahihi. Hali hii huwa inaonekana kumpa faraja sana badala ya kumsikitisha
  • Hii ni kutokana na ukweli kwamba kuna siku hadi aliwahi kulalamika kuwa kuna watu hawakupita mbele ya madhabahu, waliamua kujificha wakati wanajua wako kwenye kundi la uhalifu uliokuwa ukihitaji maombezi ya wito uliokuwa umetolewa siku hiyo
  • Nadhani alisema haya akiwa ana uhakika wa watu angalau kadhaa, ambao hawakupita madhabahuni wakati alikuwa anajua kuwa maisha yao hayako sawia kiroho
Tukirudi sasa kwenye mada yetu, kipindi mhusika anamshirikisha mawazo yake haya mwalimu Shemasi, ndiyo kipindi ambacho sasa mahubiri ya uzinzi yalikuwa yako kwenye schedule yamepamba moto, na katika kipindi hicho chote, wito nyingi zilizokuwa zikitolewa za watu kupita madhabahuni zilikuwa zimetawaliwa na wale ambao ni wazinzi na wanaofanya mapenzi usingizini. Kwa hiyo ni katika kipindi hicho hicho ambapo mhusika ilibidi amshirikishe mwalimu wake mambo makubwa mawili ambayo ni

  • Kinyesi kilichokuwa kinavuja kutoka kwenye chemba
  • Wito nyingi zaidi za kupita madhabahuni ambazo zilikuwa zimetawaliwa na washiriki ambao walikuwa wanaangukia kwenye kundi la wazinzi zaidi, na kuwashau kabisa wale wengine wasiohusika na makando kando hayo
Ukiachilia mbali hoja ya kwanza (chemba ya maji machafu) ambayo inajieleza yenyewe, kwenye hoja hii ya pili, mhusika alijaribu kutoa utetezi wake kwa mwalimu wake kama ifuatavyo, kuwa:

  • Kwa zaidi ya mwaka mzima, Madhabahu imekuwa ikitawaliwa na wito za kundi la wazinzi, na wito zingine kusahaulika kabisa ambazo zinawahusu waumini wengine ambao hawaangukii katika kundi hilo
  • Ni kweli kundi la wazinzi ni muhimu zaidi kwa sababu maandiko matakatifu yanathibitisha umuhimu wa kondoo mmoja aliyepotea, ukilinganisha na 99 waliomo zizini
  • Bado kundi la wasio wazinzi nalo lilikuwa linahitaji some sort of push mechanisms ya kulisukuma ili liende mbele na liweze kuendelea kufanya vizuri zaidi
  • Ilikuwa ni muhimu kufanya hivyo kwa kundi lisilokuwa la wazinzi, kama tahadhari ya umakini wa kuhakiksha kuwa kundi linalofanya vizuri, linaendelea kufanya vizuri na pengine, pasipo kumegeka na hatimaye kujikuta nalo linaanguka na kujiunga na lile la wazinzi
Kwa hiyo mhusika alishauri kuwe na balance ili angalau wale wasiokuwa wazinzi, wasio wagonjwa, na wengineo wasioangukia kwenye makundi yanayofanana na hayo, nao wawe wanapata nafasi ya kuitwa mbele ya madhabahu. Still hata kama pengine wenye ubora huo hawapo Kanisani, basi wito ziwe zinachanganywa, kwamba kwa mfano wazinzi tuseme mara wakiitwa 10, mfululizo, basi angalau mara moja waitwe nao hao wengine ambao hawaangukii kwenye makundi hayo na kwa wito tuseme, unaofanana kama ule aliowahi kuutumia Kiongozi Mkuu mwaka 2017

Kwa hiyo hoja ya mhusika hapa ilikuwa ni kwamba wito zisiwe ambazo ni NEGATIVE TU, ziwe zinachanganywa, japo katika uhalisia ni kweli wito ambazo ni NEGATIVE inabidi ziwe ni nyingi kuliko zile ambazo ni POSITIVE, lakini isiwe kwamba wito ambazo ni POSITIVE zinakuwa hamna kabisa

Mhusika baada ya kuwa ametoa hoja hizo, mwalimu wake alikubali kuyafikisha mambo haya mawili kwenye meza inayohusika na maongezi yao yaliishia hapo



KILICHOFUATA BAADA YA MAONGEZI YA MHUSIKA NA MWALIMU WAKE:

MHUBIRI ASIMAMA MADHABAHUNI KUKEMEA TABIA YA WATU KULALAMIKA LALAMIKA KANISANI AKIDAI KUWA WAMEKOSA KAZI


  • Siku ya maongezi yao, mhusika na mwalimu wake hawakuwekeana makubaliano ya kurudishiana feedback.
  • Hata hivyo, J2 iliyofuata, alisimama madhabahuni mhubiri na ambaye pia ni Kiongozi Kanisani hapo (tumwite Kiongozi W) akiwa amefura, japo haimaanishi kuwa alikuwa na hasira sana
  • Mahubiri yake yalijikita zaidi katika kulalamika kuwa UKIONA WATU WANAANZA KULALAMIKA LALAMIKA KANISANI, UJUE WAMEKOSA KAZI ZA KUFANYA
Mhusika aliuchukua ujumbe huu kama majibu kwake kwa sababu haikuwa mara yake ya kwanza kujibiwa kwa njia ya mtu kusimama madhabahuni

Mara ya kwanza alijibiwa kwa njia hiyo baada ya kuwa AMETUMA HELA NYUMBANI kwa ajili ya kujenga makaburi ya wazazi. J2 iliyofuata alisimama Kiongozi madhabahuni (si mmojawapo wa wale wote ambao tayari wameshatajwa humu kwenye taarifa hii) , akiwa na ujumbe uliokuwa unasema kuwa Mungu siyo Mungu wa wafu. Kwa bahati mbaya mhubiri huyu aliharibu katika namna ambayo, wiki iliyofuata, ilibidi asimame tena mhubiri mwingine ambaye ni Kiongozi W, kurekebisha hali hiyo. Kiongozi huyu wa pili alisisitiza kuwa kujenga makaburi siyo tatizo, isipokuwa tatizo labda linaweza kutokea tu pale ambapo ujenzi huo unaweza ukaambatana na mambo ya kimila.



Mara ya pili pia alijibiwa kwa njia hiyo baada ya kuwa amefanyiwa kitu ambacho hakikumfurahisha. Kitu hiki kilifanywa na mama ambaye huko nyuma alikuwa amejipambanua kama mtu wa karibu naye, na kama mama yake wa kiroho (hata hivyo, mama huyu yeye naye ana mkanda wake unaojitegemea, mambo yake yanahitaji ufafanuzi wa kipekee, peke yake, isipokuwa)

Kwa kifupi tu ni kwamba mama huyu

  • Naye ni staff mate wa mhusika, Idara tofauti
  • Ndiye alimkaribisha mhusika Kanisani hapo
Kwenye interactions zao huko nyuma baada ya mhusika kuwa ameanza kuabudu Kanisani hapo, ILITOKEA TENA huyu mama akafanya kitu ambacho mhusika HAKIKUMFURAHISHA kwa mara nyingine tena, kwa maana kuwa hakikuwa kizuri kwake na hivyo kupelekea kuandaa mpango wa kumwita mama huyu mbele ya mashemasi, baada ya kuwa mashemasi hao amewapa taarifa kuwa atahitaji kuonana na huyo mama mbele yao

Hata hivyo kabla ya siku ya kuonana kufika, mhusika aliamua kubadilisha mawazo na kusamehe, isipokuwa akaamua kuonana na shemasi mmoja tu kati ya wawili wale aliokuwa amepnaga wawepo kwenye kikao. Shemasi huyo alipokuja alimweleza maneno mafupi tu akamwambia kuwa KAMWAMBIE MAMA KITENDO ALICHOKIFANYA ANAKIJUA, NIMEMSAMEHE ILA NINAOMBA AACHE ASIRUDIE TENA. Hata hivyo mhusika alimpa maelezo ya ziada Shemasi huyo kwa kumwambia kuwa KAMA MAMA ATAONA KUWA SIKO SAHIHI NAMSINGIZIA, BASI NAOMBA UNIJULISHE HALAFU KIKAO KITAKUWEPO BAADAYE KAMA KAWAIDA ILI ALICHOKIFANYA KWANGU NIJE NIKIESEME MBELE YA KIKAO

Baada ya kikao cha mhusika na Shemasi kuisha, mhusika hakupata jibu lolote kutoka kwa shemasi, isipokuwa J2 iliyofuata, Kiongozi Mkuu alisimama madhabahuni na ujumbe uliokuwa unasema UMEHESJHIMIWA, JIHESHIMU, ujumbe ambao aliusimamia kwa wiki mbili ama tatu hivi mfululizo.

Mhusika hapo awali hakujua lakini kumbe ujumbe huu ulitokana na roho ya msamaha mhusika aliiyotoa kwa huyu mama. Analo faili la kutosha tu kuweza kulileta kwenu panapo nafasi, ila kwa sasa acha ashughulike na hili ambalo ndiyo lina kichwa cha habri hii.

Kwa hiyo kipindi Kiongzi Mkuu anatoa ujumbe huo uliosema UMEHESHIMIWA JIHESHIMU, mhusika hakuweza kugundua papo kwa papo kuwa ulimhusu yeye, isipokuwa alikuja kugundua baadaye kadri matukio yalivyokuwa yakijitokeza. Tofauti na ule wa mwanzo uliohusu Mungu siyo Mungu wa wafu, wenyewe ulikuwa direct sana na hivyo huo aliunasa papo kwa papo

Maelezo haya anayaleta kwenu yakiwa ni ya ziada, na kama namna tu ya kuwathibitishia kuwa wakati ujumbe wa watu kulalamika Kanisani kwa sababu hawana kazi ya kufanya unatolewa na Kiongozi W, tayari kule nyuma zilishatolewa jumbe zingine mbili kwa mtindo huo huo wa madhabahuni, na mojwapo ya jumbe hizo ukiwa ni ule uliotolewa na Kiongozi Mkuu.

Kwa hiyo safari hii alichaguliwa tena Kiongozi W ili aulete ujumbe huu kupitia madhabahuni, possibly kwa kuizingatia kuwa yeye ndiye the most learned katika viongozi wote.

Hata hivyo kitu cha kupendeza sana kwa viongozi hawa ni kwamba wanaonekana ni wasomi wazuri na ambao you can even, easily convert them to university dons. Mhusika hana details za elimu zao hao wengine ukiondoa Kiongozi W, (ambaye naye pia ni ex-staff mate wake) lakini wanaonekana hivyo mtu akiwajaribu kuwa-assess kwa jicho la ndani

Baada ya Kiongozi W kuwa ametoa ujumbe wake madhababuni, safari hii mhusika aliamua kuchuka hatua zifuatazo

  • Alimjulisha shemasi mwalimu juu ya kutoridhiswhwa kwake na ujumbe huo uliotolewa na Kionngozi W
  • Zaidi alimusihi shemasi mwalimu ajaribu kuangalia uwezekano wa kuwaomba viongozi wote au baadhi yao, kama wanaweza kupata nafasi ya kukutana kwa ajili ya kikao na mhusika, na alikubali kuwajulisha viongozi hao
Zaidi ya hayo, mhusika aliweka wazi maswala kadhaa kwa mwalimu shemasi, na kumuomba kuyafikisha kwa uongozi wote ikiwa ni pamoja na mhubiri Kiongozi W, kwamba:

  • Mhusika haoni mantiki ya uwepo wa uzinzi Kanisani ambao suluhisho lake ni watu kuitwa mbele ya madhabahu tu kwa siku za J2 tu badala ya kuwepo mkakati kama wa Semina maalum kwa jili ya kushgughulikia tatizo
  • Uongozi wote wa ngazi za juu wa kitaifa unalijua na huwa unalisifu sana sana Kanisa hilo kwa sifa ya utoaji sadaka, na possibly ndiyo linaloongoza kwa utoaji Tanzania nzima
  • Mhusika anaona ni PARADOX kwa Kanisa ambalo uongoiz wa Kanisa ngazi za juu kitaifa, unalijua kama Kanisa la watoaji linaongoza Tanzania nzima, na ndiyo maana linajenga Kanisa zuri na kubwa mno.
  • Kanisa ambalo uzinzi ni dorminant na waumini wake hawana Roho Mtakatifu kiasi kwamba kila J2 ni watu wenye matatizo tu ambao huwa wanaalikwa kupita madhabahuni, lina dalili zote zinazoonyesha kuwa walio wazuri hawapo Kanisani hapo, na hivyo haliwezi kuwa ni zuri kwa utoaji ama kuongoza katika uwanja huowa utoaji kitaifa
  • Hii tayari ni pardox ya ajabu sana kwamba waumini ambao hawana Roho Mtakatifu, ni wazinzi, lakini bado tena waumini hao hao wanaongoza Tanzania nzima kwa utoaji wa sadaka. Ni paradox ya ajabu sana
  • Mhusika aliongea na mwalimu wake mengi, ila kwa humu jukwaani haya yanatosha.


LABDA NYONGEZA NYINGINE NDOGO TU KATIKA HAYA NI KAMA IFUATAVYO:

  • Ni kawaida kabisa kwa nyumba hiyo ya Ibada, kuwa na wiki nzima ya maombi yanayoambatana pamoja na Semina, kwa sababu J2 inayofuata kuna utoaji wa ahadi za ujenzi wa Kanisa au Sadaka kwa ajili ya mikutano ya Injili, na si Semina kwa ajili ya kukomesha uzinzi. Hii moja kwa moja inaonyesha kuwa tatizo la uzinzi halipewi uzito wowote wa kulishughulika ukilinganisha na vitu kama Sadaka za ujenzi au Injili
  • Ni rahisi zaidi kuombewa Bahasha iliyotolewa kwa ajili ya Sadaka fulani, kuliko kuombewa Sadaka yenyewe. Unaweza ukapewa bahasha kwa ajili ya Sadaka fulani, halafu bahasha hiyo inaweza ikaombewa, lakini ikitokea ukatoa Sadaka hiyo pale pale na kuirudisha ikiwa kwenye bahasha, Sadaka hiyo uliyotoa papo kwa papo haitaombewa. Wanaombea Bahasha zaidi kuliko sadaka yenyewe
  • Sadaka zinazotolewa kwenye darasa la Uanafunzi na maandiko SIKU ZOTE huwa haziombewi, na kuna makusudi yake ya kufanya hivyo
  • Sadaka zinazotolewa kwenye Ibada za shukurani zinazofanyika kila J2 ya mwisho wa mwezi, nazo pia SIKU ZOTE huwa haziombewi na hii pia nayo inna makusudi yake ykufanyika hivyo
Haya mambo ya kutoa sadaka isiyoombew yameshamghariimusana mhusika na anapolalamikia haya, analalamika akiwa na CONCRETE EVIDENCE, vyote kimwili na kiroho



HITIMISHO

Baada ya Kiongozi W kusimama na kutoa ujumbe wa mahubiri yake madhabahuni

  • Chemba ya kinyesi iliendelea kutoa kinyesi pamoja na kwamba mwalimu shemasi alipeleka taarifa za chemba hiyo. Kiongozi W kusimama madhabahuni na kutoa ujumbe wake kulionyesha kuwa mwalimu Shemasi alifikisha ujumbe
  • Ilionyesha KAMA Kiongozi W alisimama madhabahuni akiwa amefura kwa sababu alihofia kuwa asipofanya hivyo, mhuisika ataendelea kulalalamika kuhusiana na chemba ya maji machafu, kiasi kwamba itabidi yashughulikiwe ili yaache kuendelea kutiririka
  • Ilionyesha KAMA ilikuwa ni plan ya uongozi kuhakikisha kuwa maji hayo hayashughulikiwii ili yaendelee kutiririka
  • Ilionyesha KAMA ilikuwa ni plan ya uongozi kuhakikisha kuwa wanaoendelea kuitwa kupita mbele ya madhabahu ni wazinzi na wale wengine ambao wanafanana na hao, na si wale ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika mahusiaano yao ya kiroho na Mungu wao
Zaidi ni kuwa Mwalimu Shemasi aliwahi kumjulisha mhusika siku nyingi zimepita kwamba kuna baadhi ya viongozi walikuwa wameridhia kufanya kikao na mhusika, lakini kikao ahicho hakijaweza kufanyika hadi leo
Naendelea kusoma, inaonyesha Mhusika ni mtu mkorofi sana, yaani mtu mmoja tu anataka apange kanisa liendeshwe vipi

Hata kama amegundua kuna ushirikina kanisani sasa kwahiyo yeye alijua makanisa yana utakatifu? Mbona ni kawaida tu makanisa na waendeshaji kuwa washirikina?

Mhusika ni mtu wa kupenda sana haki, asiyeweza kukaa kimya jambo ambalo sio baya lakini kwa bahati mbaya hapa duniani watu wa namna hii hupata tabu sana

Ndio sababu kuna watu hukaa kimya, sio lazima useme kila unachokiona, maamuzi sahihi ni kuachana na jambo hilo kama linakukera sana

Najua Mhusika hawezi kuachana na dini basi ataendelea kupata tabu maana kote atakoenda salama yake ni kukaa kimya, ama sivyo ni kibano kila kona na hivyo asitulilie
 
Naendelea kusoma, inaonyesha Mhusika ni mtu mkorofi sana, yaani mtu mmoja tu anataka apange kanisa liendeshwe vipi

Hata kama amegundua kuna ushirikina kanisani sasa kwahiyo yeye alijua makanisa yana utakatifu? Mbona ni kawaida tu makanisa na waendeshaji kuwa washirikina?

Mhusika ni mtu wa kupenda sana haki, asiyeweza kukaa kimya jambo ambalo sio baya lakini kwa bahati mbaya hapa duniani watu wa namna hii hupata tabu sana

Ndio sababu kuna watu hukaa kimya, sio lazima useme kila unachokiona, maamuzi sahihi ni kuachana na jambo hilo kama linakukera sana

Najua Mhusika hawezi kuachana na dini basi ataendelea kupata tabu maana kote atakoenda salama yake ni kukaa kimya, ama sivyo ni kibano kila kona na hivyo asitulilie
Halii. Watu wakafanyie ushirikina kwingine, siyo Kanisani. Na ninavyomuona, kwa hili ana uwezo wa kulisimamia kwenye ulimwengu wa roho
 
Back
Top Bottom