UPDATE: 16 JULY 2020
MAELEZO YA NYONGEZA KUHUSIANA NA CHEMBA AMBAYO IMEKUWA IKITOA MAJI MACHAFU YALIYOCHANGANYIKANA NA KINYESI KANISANI
Ni mtizamo wa mhusika kwamba hii chamber imekuwa ikitunzwa ikae katika hali ya kuvuja, tangu kipindi kirefu nyuma, kwa makusudi ya kuwa inavujisha kinyesi hicho pindi mvua zinappkuwa zimeanza
Fuatana na maelezo ya mhusika katika tukio hlil hapa chini ili uweze kuthibitisha maneno yake
Takribani mwaka mmoja na nusu au miwili hivi imeshapita, ilitokea siku moja mhusika akadhani kuwa pengine labda viongozi wa Kanisani wamepitiwa tu kutokana na shughuli nyingi na hivyo wameshindwa kuiangalia kwa jicho la umakini chamber inayovuja kinyesi Kanisani hapo. Kutokana na dhana hiyo, mhusika siku moja akiwa Kanisani, aliamua kumshirikisha mmojawapo wa mashemasi Kanisani hapo, na ambaye ni mwalimu wake (yaani Shemasi ambaye aliwahi kuwa mwalimu wa kiroho wa mhusika, kipindi mhusika akiwa bado ni mshirika kwa kupitia dararsa la waongofu wapya). Mhusika alliamua kumshirikisha mwalimu wake mambo makubwa mawili
- MOJA: Kuhusiana na kinyesi kilichokuwa kinavuja kutoka kwenye chemba
- PILI: Kuhusiana na wito zinazotolewa na viongozi wa watu kupita mbele ya madhabahu, wakati wa Ibada kuu siku za J2
Mhusika alimshirikisha mwalimu wake mambo haya mawili na kumuomba kiongozi huyo kama anaweza kuyafikisha kwenye ngazi za juu Kanisani hapo.
Kuhusiana na swal la chemba iliyokuwa inavuja kinyesi, mhusika hakuongea mengi isipokuwa alimwonyesha tu mwalimu wake sehemu hiyo na kuiona (japo sehemu imekaa mahali ambapo mtu yeyote hahitaji kuonyeshwa ili aweze kuiona) na baada ya kuwa naye amehakikisha kuwa kweli ilikuwa inavuja, alikiri kuwa hali hiyo haikuwa nzuri na aliahidi kulifikisha swala la mhusika kunakostahili.
Kwenye mada hii, mwandishi anaomba ajikite zaidi kwenye swala la pili, kulingana na msisitizo wa mtoa maelezo mwenyewe, ambaye ni mhusika
WITO ZILIZOKUWA NA AMBAZO ZIMEKUWA ZIKITOLEWA NA WAHUBIRI KWA WAUMINI KUPITA MBELE YA MADHABAHU SIKU ZA IBADA ZA J2
Kwenye kipengele hiki, mwandishi anapenda ajikite zaidi katika kutoa maelezo ya kina kuhusiana na wito mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa wakati wa mahubiri, zikiita watu wapite mbele ya madhabahu kwa ajili ya msaada wa kufanyiwa maombi zaidi. Wito hizi zina uhusiano na swala linaloongelewa hapa kwa mantiki mhusika alilitoa maobi mawili kwa wakati mmoja likiwemo lile la chemba ya maji machafu
Tangu mhusika arudi kutoka uhamishoni Kanisa B, mwezi April 2017, rekodi ya kumbukumbu zake mpaka wakati huo (yaani hadi kipindi anafanya maongezi na shemasi mwalimu) ilikuwa inamuonyesha kuwa:
- Kuna wito mmoja tu POSITIVE ambao ulikuwa umewahi kutolewa na Kiongozi Mkuu ukiita watu wapite mbele madhabahuni kwa ajili ya kuombewa ili waweze kufanya vizuri zaidi
- Wito POSTIVE hapa mhusika anamaanisha wito ule ambao SI LAZIMA kila anayekaribishwa kupita mbele madhabahuni, awe ni yule ambaye ANA MATATIZO SANA KIROHO, japo pia hata walio na matatizo pia wito wa aina hii huwa hauwawekei mipaka na huwa wako huru kupita mbele pale wanapokuwa wanajisikia kufanya hivyo
- Kwa hiyo hapa Kiongozi Mkuu siku hito alinamaanisha watu ambao wapo Kanisani na ambao wanaona wanaishi sawa sawa na mapenzi ya Mungu, na wanapenda kuendelea kuishi sawasawa na mapenzi ya Mungu, na hivyo wangependa waombewe ili waendelee kufanya vizuri zaidi
- Watu wa aina hii huwa wapo Kanisani, na wanaweza kuwa ni wengi tu
Baada ya wito huo, muda mfupi mbele na baada ya maongezi ya mhusika na Shemasi mwalimu, J2 nyingine alisimama tena mwingine, yaani Kiongozi X na kuita watu ambao wao wanapenda KUONGEZEWA ujazo wa Roho Mtakatifu, YAANI WAJAZWE ZAIDI NA ZAIDI. Wito huu nao kwa upande mwingine, ulikuwa POSTIVE, japo pia ulikuwa unagusa pande zote mbili. Huyu alisimama kutoa wito huo muda mfupi BAADA ya mhusika na shemasi mwalimu kuwa wameshafanya maongezi yao
Kwa kumbukumbu za mhusika mpaka leo hii, ukiondoa wito hizi mbili zilizoainishwa hapa juu:
- Hapajawahi tena kutokea wito wa madhabahuni ambao ni PISITIVE, hadi leo hii July 2020
- Wito zote zingine zimekuwa ni zile ambazo ni NEGATIVE kama vile kwa ajli ya wazinzi, wanaofanya mapenzi ndotoni, wagonjwa, walio na matatizo ya kiroho, wasiokuwa na Roho Mtakatifu, wanaosumbuliwa na nguvu za giza, n.k.
- Ni sahihi kabisa kwa wito za aina hii kuwa dorminant kwenye nyumba yoyote ile ya Ibada, lakini hii haimaanishi kuwa wito ambazo ni POSITIVE zisiwepo kabisa kwa sababu bado wapo watu wanaofanya vizuri, na ambao nao wanahitaji kupita madhabahuni na kuongezewa nguvu
- Tatizo liliopo ni kwamba Kiongozi Mkuu huwa anafarijika zaidi pindi inapotokea umetolewa wito ambao ni NEGATIVE halafu akaona kundi la watu wengi wamepita madhabahuni, kitu ambacho siyo sahihi. Hali hii huwa inaonekana kumpa faraja sana badala ya kumsikitisha
- Hii ni kutokana na ukweli kwamba kuna siku hadi aliwahi kulalamika kuwa kuna watu hawakupita mbele ya madhabahu, waliamua kujificha wakati wanajua wako kwenye kundi la uhalifu uliokuwa ukihitaji maombezi ya wito uliokuwa umetolewa siku hiyo
- Nadhani alisema haya akiwa ana uhakika wa watu angalau kadhaa, ambao hawakupita madhabahuni wakati alikuwa anajua kuwa maisha yao hayako sawia kiroho
Tukirudi sasa kwenye mada yetu, kipindi mhusika anamshirikisha mawazo yake haya mwalimu Shemasi, ndiyo kipindi ambacho sasa mahubiri ya uzinzi yalikuwa yako kwenye schedule yamepamba moto, na katika kipindi hicho chote, wito nyingi zilizokuwa zikitolewa za watu kupita madhabahuni zilikuwa zimetawaliwa na wale ambao ni wazinzi na wanaofanya mapenzi usingizini. Kwa hiyo ni katika kipindi hicho hicho ambapo mhusika ilibidi amshirikishe mwalimu wake mambo makubwa mawili ambayo ni
- Kinyesi kilichokuwa kinavuja kutoka kwenye chemba
- Wito nyingi zaidi za kupita madhabahuni ambazo zilikuwa zimetawaliwa na washiriki ambao walikuwa wanaangukia kwenye kundi la wazinzi zaidi, na kuwashau kabisa wale wengine wasiohusika na makando kando hayo
Ukiachilia mbali hoja ya kwanza (chemba ya maji machafu) ambayo inajieleza yenyewe, kwenye hoja hii ya pili, mhusika alijaribu kutoa utetezi wake kwa mwalimu wake kama ifuatavyo, kuwa:
- Kwa zaidi ya mwaka mzima, Madhabahu imekuwa ikitawaliwa na wito za kundi la wazinzi, na wito zingine kusahaulika kabisa ambazo zinawahusu waumini wengine ambao hawaangukii katika kundi hilo
- Ni kweli kundi la wazinzi ni muhimu zaidi kwa sababu maandiko matakatifu yanathibitisha umuhimu wa kondoo mmoja aliyepotea, ukilinganisha na 99 waliomo zizini
- Bado kundi la wasio wazinzi nalo lilikuwa linahitaji some sort of push mechanisms ya kulisukuma ili liende mbele na liweze kuendelea kufanya vizuri zaidi
- Ilikuwa ni muhimu kufanya hivyo kwa kundi lisilokuwa la wazinzi, kama tahadhari ya umakini wa kuhakiksha kuwa kundi linalofanya vizuri, linaendelea kufanya vizuri na pengine, pasipo kumegeka na hatimaye kujikuta nalo linaanguka na kujiunga na lile la wazinzi
Kwa hiyo mhusika alishauri kuwe na balance ili angalau wale wasiokuwa wazinzi, wasio wagonjwa, na wengineo wasioangukia kwenye makundi yanayofanana na hayo, nao wawe wanapata nafasi ya kuitwa mbele ya madhabahu. Still hata kama pengine wenye ubora huo hawapo Kanisani, basi wito ziwe zinachanganywa, kwamba kwa mfano wazinzi tuseme mara wakiitwa 10, mfululizo, basi angalau mara moja waitwe nao hao wengine ambao hawaangukii kwenye makundi hayo na kwa wito tuseme, unaofanana kama ule aliowahi kuutumia Kiongozi Mkuu mwaka 2017
Kwa hiyo hoja ya mhusika hapa ilikuwa ni kwamba wito zisiwe ambazo ni NEGATIVE TU, ziwe zinachanganywa, japo katika uhalisia ni kweli wito ambazo ni NEGATIVE inabidi ziwe ni nyingi kuliko zile ambazo ni POSITIVE, lakini isiwe kwamba wito ambazo ni POSITIVE zinakuwa hamna kabisa
Mhusika baada ya kuwa ametoa hoja hizo, mwalimu wake alikubali kuyafikisha mambo haya mawili kwenye meza inayohusika na maongezi yao yaliishia hapo
KILICHOFUATA BAADA YA MAONGEZI YA MHUSIKA NA MWALIMU WAKE:
MHUBIRI ASIMAMA MADHABAHUNI KUKEMEA TABIA YA WATU KULALAMIKA LALAMIKA KANISANI AKIDAI KUWA WAMEKOSA KAZI
- Siku ya maongezi yao, mhusika na mwalimu wake hawakuwekeana makubaliano ya kurudishiana feedback.
- Hata hivyo, J2 iliyofuata, alisimama madhabahuni mhubiri na ambaye pia ni Kiongozi Kanisani hapo (tumwite Kiongozi W) akiwa amefura, japo haimaanishi kuwa alikuwa na hasira sana
- Mahubiri yake yalijikita zaidi katika kulalamika kuwa UKIONA WATU WANAANZA KULALAMIKA LALAMIKA KANISANI, UJUE WAMEKOSA KAZI ZA KUFANYA
Mhusika aliuchukua ujumbe huu kama majibu kwake kwa sababu haikuwa mara yake ya kwanza kujibiwa kwa njia ya mtu kusimama madhabahuni
Mara ya kwanza alijibiwa kwa njia hiyo baada ya kuwa AMETUMA HELA NYUMBANI kwa ajili ya kujenga makaburi ya wazazi. J2 iliyofuata alisimama Kiongozi madhabahuni (si mmojawapo wa wale wote ambao tayari wameshatajwa humu kwenye taarifa hii) , akiwa na ujumbe uliokuwa unasema kuwa Mungu siyo Mungu wa wafu. Kwa bahati mbaya mhubiri huyu aliharibu katika namna ambayo, wiki iliyofuata, ilibidi asimame tena mhubiri mwingine ambaye ni Kiongozi W, kurekebisha hali hiyo. Kiongozi huyu wa pili alisisitiza kuwa kujenga makaburi siyo tatizo, isipokuwa tatizo labda linaweza kutokea tu pale ambapo ujenzi huo unaweza ukaambatana na mambo ya kimila.
Mara ya pili pia alijibiwa kwa njia hiyo baada ya kuwa amefanyiwa kitu ambacho hakikumfurahisha. Kitu hiki kilifanywa na mama ambaye huko nyuma alikuwa amejipambanua kama mtu wa karibu naye, na kama mama yake wa kiroho (hata hivyo, mama huyu yeye naye ana mkanda wake unaojitegemea, mambo yake yanahitaji ufafanuzi wa kipekee, peke yake, isipokuwa)
Kwa kifupi tu ni kwamba mama huyu
- Naye ni staff mate wa mhusika, Idara tofauti
- Ndiye alimkaribisha mhusika Kanisani hapo
Kwenye interactions zao huko nyuma baada ya mhusika kuwa ameanza kuabudu Kanisani hapo, ILITOKEA TENA huyu mama akafanya kitu ambacho mhusika HAKIKUMFURAHISHA kwa mara nyingine tena, kwa maana kuwa hakikuwa kizuri kwake na hivyo kupelekea kuandaa mpango wa kumwita mama huyu mbele ya mashemasi, baada ya kuwa mashemasi hao amewapa taarifa kuwa atahitaji kuonana na huyo mama mbele yao
Hata hivyo kabla ya siku ya kuonana kufika, mhusika aliamua kubadilisha mawazo na kusamehe, isipokuwa akaamua kuonana na shemasi mmoja tu kati ya wawili wale aliokuwa amepnaga wawepo kwenye kikao. Shemasi huyo alipokuja alimweleza maneno mafupi tu akamwambia kuwa KAMWAMBIE MAMA KITENDO ALICHOKIFANYA ANAKIJUA, NIMEMSAMEHE ILA NINAOMBA AACHE ASIRUDIE TENA. Hata hivyo mhusika alimpa maelezo ya ziada Shemasi huyo kwa kumwambia kuwa KAMA MAMA ATAONA KUWA SIKO SAHIHI NAMSINGIZIA, BASI NAOMBA UNIJULISHE HALAFU KIKAO KITAKUWEPO BAADAYE KAMA KAWAIDA ILI ALICHOKIFANYA KWANGU NIJE NIKIESEME MBELE YA KIKAO
Baada ya kikao cha mhusika na Shemasi kuisha, mhusika hakupata jibu lolote kutoka kwa shemasi, isipokuwa J2 iliyofuata, Kiongozi Mkuu alisimama madhabahuni na ujumbe uliokuwa unasema UMEHESJHIMIWA, JIHESHIMU, ujumbe ambao aliusimamia kwa wiki mbili ama tatu hivi mfululizo.
Mhusika hapo awali hakujua lakini kumbe ujumbe huu ulitokana na roho ya msamaha mhusika aliiyotoa kwa huyu mama. Analo faili la kutosha tu kuweza kulileta kwenu panapo nafasi, ila kwa sasa acha ashughulike na hili ambalo ndiyo lina kichwa cha habri hii.
Kwa hiyo kipindi Kiongzi Mkuu anatoa ujumbe huo uliosema UMEHESHIMIWA JIHESHIMU, mhusika hakuweza kugundua papo kwa papo kuwa ulimhusu yeye, isipokuwa alikuja kugundua baadaye kadri matukio yalivyokuwa yakijitokeza. Tofauti na ule wa mwanzo uliohusu Mungu siyo Mungu wa wafu, wenyewe ulikuwa direct sana na hivyo huo aliunasa papo kwa papo
Maelezo haya anayaleta kwenu yakiwa ni ya ziada, na kama namna tu ya kuwathibitishia kuwa wakati ujumbe wa watu kulalamika Kanisani kwa sababu hawana kazi ya kufanya unatolewa na Kiongozi W, tayari kule nyuma zilishatolewa jumbe zingine mbili kwa mtindo huo huo wa madhabahuni, na mojwapo ya jumbe hizo ukiwa ni ule uliotolewa na Kiongozi Mkuu.
Kwa hiyo safari hii alichaguliwa tena Kiongozi W ili aulete ujumbe huu kupitia madhabahuni, possibly kwa kuizingatia kuwa yeye ndiye the most learned katika viongozi wote.
Hata hivyo kitu cha kupendeza sana kwa viongozi hawa ni kwamba wanaonekana ni wasomi wazuri na ambao you can even, easily convert them to university dons. Mhusika hana details za elimu zao hao wengine ukiondoa Kiongozi W, (ambaye naye pia ni ex-staff mate wake) lakini wanaonekana hivyo mtu akiwajaribu kuwa-assess kwa jicho la ndani
Baada ya Kiongozi W kuwa ametoa ujumbe wake madhababuni, safari hii mhusika aliamua kuchuka hatua zifuatazo
- Alimjulisha shemasi mwalimu juu ya kutoridhiswhwa kwake na ujumbe huo uliotolewa na Kionngozi W
- Zaidi alimusihi shemasi mwalimu ajaribu kuangalia uwezekano wa kuwaomba viongozi wote au baadhi yao, kama wanaweza kupata nafasi ya kukutana kwa ajili ya kikao na mhusika, na alikubali kuwajulisha viongozi hao
Zaidi ya hayo, mhusika aliweka wazi maswala kadhaa kwa mwalimu shemasi, na kumuomba kuyafikisha kwa uongozi wote ikiwa ni pamoja na mhubiri Kiongozi W, kwamba:
- Mhusika haoni mantiki ya uwepo wa uzinzi Kanisani ambao suluhisho lake ni watu kuitwa mbele ya madhabahu tu kwa siku za J2 tu badala ya kuwepo mkakati kama wa Semina maalum kwa jili ya kushgughulikia tatizo
- Uongozi wote wa ngazi za juu wa kitaifa unalijua na huwa unalisifu sana sana Kanisa hilo kwa sifa ya utoaji sadaka, na possibly ndiyo linaloongoza kwa utoaji Tanzania nzima
- Mhusika anaona ni PARADOX kwa Kanisa ambalo uongoiz wa Kanisa ngazi za juu kitaifa, unalijua kama Kanisa la watoaji linaongoza Tanzania nzima, na ndiyo maana linajenga Kanisa zuri na kubwa mno.
- Kanisa ambalo uzinzi ni dorminant na waumini wake hawana Roho Mtakatifu kiasi kwamba kila J2 ni watu wenye matatizo tu ambao huwa wanaalikwa kupita madhabahuni, lina dalili zote zinazoonyesha kuwa walio wazuri hawapo Kanisani hapo, na hivyo haliwezi kuwa ni zuri kwa utoaji ama kuongoza katika uwanja huowa utoaji kitaifa
- Hii tayari ni pardox ya ajabu sana kwamba waumini ambao hawana Roho Mtakatifu, ni wazinzi, lakini bado tena waumini hao hao wanaongoza Tanzania nzima kwa utoaji wa sadaka. Ni paradox ya ajabu sana
- Mhusika aliongea na mwalimu wake mengi, ila kwa humu jukwaani haya yanatosha.
LABDA NYONGEZA NYINGINE NDOGO TU KATIKA HAYA NI KAMA IFUATAVYO:
- Ni kawaida kabisa kwa nyumba hiyo ya Ibada, kuwa na wiki nzima ya maombi yanayoambatana pamoja na Semina, kwa sababu J2 inayofuata kuna utoaji wa ahadi za ujenzi wa Kanisa au Sadaka kwa ajili ya mikutano ya Injili, na si Semina kwa ajili ya kukomesha uzinzi. Hii moja kwa moja inaonyesha kuwa tatizo la uzinzi halipewi uzito wowote wa kulishughulika ukilinganisha na vitu kama Sadaka za ujenzi au Injili
- Ni rahisi zaidi kuombewa Bahasha iliyotolewa kwa ajili ya Sadaka fulani, kuliko kuombewa Sadaka yenyewe. Unaweza ukapewa bahasha kwa ajili ya Sadaka fulani, halafu bahasha hiyo inaweza ikaombewa, lakini ikitokea ukatoa Sadaka hiyo pale pale na kuirudisha ikiwa kwenye bahasha, Sadaka hiyo uliyotoa papo kwa papo haitaombewa. Wanaombea Bahasha zaidi kuliko sadaka yenyewe
- Sadaka zinazotolewa kwenye darasa la Uanafunzi na maandiko SIKU ZOTE huwa haziombewi, na kuna makusudi yake ya kufanya hivyo
- Sadaka zinazotolewa kwenye Ibada za shukurani zinazofanyika kila J2 ya mwisho wa mwezi, nazo pia SIKU ZOTE huwa haziombewi na hii pia nayo inna makusudi yake ykufanyika hivyo
Haya mambo ya kutoa sadaka isiyoombew yameshamghariimusana mhusika na anapolalamikia haya, analalamika akiwa na CONCRETE EVIDENCE, vyote kimwili na kiroho
HITIMISHO
Baada ya Kiongozi W kusimama na kutoa ujumbe wa mahubiri yake madhabahuni
- Chemba ya kinyesi iliendelea kutoa kinyesi pamoja na kwamba mwalimu shemasi alipeleka taarifa za chemba hiyo. Kiongozi W kusimama madhabahuni na kutoa ujumbe wake kulionyesha kuwa mwalimu Shemasi alifikisha ujumbe
- Ilionyesha KAMA Kiongozi W alisimama madhabahuni akiwa amefura kwa sababu alihofia kuwa asipofanya hivyo, mhuisika ataendelea kulalalamika kuhusiana na chemba ya maji machafu, kiasi kwamba itabidi yashughulikiwe ili yaache kuendelea kutiririka
- Ilionyesha KAMA ilikuwa ni plan ya uongozi kuhakikisha kuwa maji hayo hayashughulikiwii ili yaendelee kutiririka
- Ilionyesha KAMA ilikuwa ni plan ya uongozi kuhakikisha kuwa wanaoendelea kuitwa kupita mbele ya madhabahu ni wazinzi na wale wengine ambao wanafanana na hao, na si wale ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika mahusiaano yao ya kiroho na Mungu wao
Zaidi ni kuwa Mwalimu Shemasi aliwahi kumjulisha mhusika siku nyingi zimepita kwamba kuna baadhi ya viongozi walikuwa wameridhia kufanya kikao na mhusika, lakini kikao ahicho hakijaweza kufanyika hadi leo