UPDATE:WEDNESDAY; 6th JANUARY 2021
“RARE COINCIDENCE” NYINGINE AMBAYO INAWEZA KUWA IMETOKEA “KANISA A”
Msomaji inabidi azingatie kwa umakini kidogo maelezo ya mhusika kwenye taarifa hii kwamba, coincidence hii:
- inaweza kuwa imetokea au haijatokea
- uwepo wake unategemea kile ambacho kinaweza kuwa kimetokea katika uhalisia (if A then B, if not A then not B)
UTANGULIZI
Kuna kipindi kwenye maelezo yake ya nyuma, mhusika aliwahi kugusia swala la kipindi cha Ibada ya maombezi kuvamiwa na watu kutoka nje ya Kanisa A, na ambao walidhihirika kutokuwa na nia njema na kipindi hicho
- Hiki ni kipindi ambacho huwa kinakuwepo kila Jumapili mara baada ya Ibada ya pili
- Kawaida huwa kinaanza kwenye mida ya baada ya saa 7, ila kwa mara nyingi kuanza kwake hutegemea sana muda ambao Ibada ya pili ilimalizika
- Washiriki wake walio wengi, ni waumini ambao huwa wamekuwepo na ambao huwa wameshiriki kwenye Ibada ya pili
Nadhani ilikuwa mwaka 2011 na 2012, ambapo kipindi hiki kilikuwa kinafanyikia kwenye la jengo la ghorofa, na kilikuwa kinafanyikia kwenye ghorofa ya kwanza ya jengio hilo lililo ndani ya uzio wa Kanisa A
- Baadaye kipindi hicho kilihamishwa na kuwa kinafanyikia kwenye banda ambalo ni Kanisa kwa ajili ya Ibada ya watoto wadogo kabisa wale wa rika la mwanzo kanisani hapo
- Banda hili ndiyo lile ambalo mhusika hivi karibuni alililamika kuwa linawekewa makreti ya soda pembezoni kwa ajili ya watoto kukanyaga juu yake, kukwepa kukanyaga maji ya mvua ambayo huwa yanajitenga pembezoni mwa banda hilo
- Baada ya Ibada ya maombezi kuhamishiwa kwenye nyumba hiyo ya Ibada ya watoto wadogo, mamluki wa kuvamia Ibada hii ya maombezi, walianza kuonekana kwenye Ibada hiyo
Ni kwa sababu banda hilo liko karibu na geti la kuingilia Kanisani hapo hivyo ilikuwa ni rahisi zaidi kwa wao kuingia haraka haraka ndani na kujiunga na watu waliokuwa wanakuwa kwenye Ibada hiyo ya maombezi
- Kule ghrorofani ambako Ibada hiyo mwanzoni ilikuwa inafanyikia, haikuwa rahisi sana kwa wavamizi hawa kufika sehemu hiyo. Ingekuwa rahisi sana kwa wao kustukiwa kwa sababu walikuwa wanakuja kutokea nje, wakati maombezi hayo washiriki wake wote huwa ni watu ambao wengi wao ni wale ambao wanakuwa wamehudhuria Ibada ya pili
- Na kwa sababu ghorofa liko umbali wa kutosha kutoka getini, haikuwa rahisi kwa mtu mgeni na mwenye sura ngeni, kutembea kote kutoka getini hadi lilipo ghorofa hilo, na hatimaye kupandisha juu ghorofani kujiunga na maombi hayo
Ni katika wakati huu tu ambapo kipindi hiki kilihamia karibu na getini, ndiyo watu hawa nao walianza kuonekana kwenye Ibada hiyo
Kwenye mojawapo ya pilika pilika zao wavamizi hawa wa Ibada, kuna siku walionekana kuwasili wakiwa wamekodi tax, na mhusika kubahatika kuwaona kwa macho yake wakipokelewa na
binti mmoja mwenyeji wa kanisani hapo, ambaye pia ni mmojawapo wa washiriki mahiri wa Ibada ya Kusifu na Kuabudu Kanisani hapo
MAELEZO YA TUKIO LENYEWE
Binti huyu ambaye ametajwa hapo juu, ni
mshiriki mzuri sana na pia
kiongozi mzuri sana wa Ibada ya kusifu na kuabudu na ni mara chache sana kwake kutokuonekana Kanisani. Hata hivyo kuna kipindi fulani aliwahi kupotea madhabahuni kwa muga mrefuu kiasi, na kwa sababu ambazo ni za msingi sana, na ambazo mhusika asingependa kuziongelea hapa
- Baada ya kuwa amepotea kwa kipindi kirefu, hatimaye alirudi tena na akaendelea kushiriki kama kawaida
- Hata hivyo, safari hii alirudi akawa mara zote anaimba kama mshiriki tu wa kikundi hicho, yaani mwimbaji wa kawaida na si kama kiongozi mwimbishaji
- Baada ya binti huyu kuwa amerudi tena, kama kuna Ibada ya kusifu na kuabudu ambayo aliwahi kuiongoza kwa kuimbisha, basi atakuwa alifanya hivyo kwa kipande tu huku akishirikiana na mtu mwingine, ila si kwa Ibada nzima
Hata hivyo, hatimaye ilitokea
Jumapili ya tarehe 26 Julai 2020 ambapo alibahatika kuongoza Ibada nzima ya kusifu na kuabdudu, mwenyewe peke yake, huku wenzake wote kwenye kundi hilo wakiwa ni waitikiaji tu
- Tangia aache kuongoza Ibada hiyo, hadi Jumapili ya hiyo ya tarehe 26 Julai 2020, alikuwa amepitisha takribani mwaka mzima
- Hii ni kutokana na ukweli kuwa hapo kabla, alikuwa pia ameacha kuonekana madhabahuni kwa udhuru uliotokana na sababu za msingi
HITIMISHO
Hata hivyo, tangu Jumapili hiyo tajwa, hajawahi tena kuongoza (kuimbisha) Ibada nzima ya kusifu na kuabudu yeye mwenyewe peke yake na kama amewahi, basi itakuwa ni katika mojawapo ya Jumapili zipatazo tatu zilizotokea mbele ya mwezi huo wa Julai 2020 ambazo mhuiska hakubatika kuwepo kwenye Ibada za Jumapili hizo
- Hii inamanisha kuwa hadi leo hii January 2021, mhusika hajawahi kumuona tena binti huyu akiongoza Ibada hiyo kama alivyoongoza kwa mara ya mwisho tarehe 26 Julai 2020
- Kipindi hiki urefu wake unaeleleka miezi sita sasa, au nusu mwaka
- Vile vile, kabla ya tarehe hiyo tajwa, alikuwa pia amepitisha takriban mwaka mzima bila kuongoza Ibada hiyo
- Kwa hiyo rekodi aliyonayo mhuiska kuhusiana na binti huyu hadi siku ya leo, inaonyesha kama tarehe 26 Julai 2020 aliongoza Ibada yote ya kusifu na kuabudu yeye peke yake bila kushirikiana na mtu mwingine, kwa mara ya mwisho
Wasomaji wa siku zote wa uzi huu watakumbuka kuwa tarehe hiyo tajwa ndiyo siku ambayo
usiku wake mdogo wake na mhusika alipoteza maisha kule nyumbani kwao Mwanza
Unless binti huyu amewahi kuongoza Ibada zingine katika mojawapo ya Jumapili hizo tatu alizozitaja hapo juu, ambazo mhusika hakuwahi kuzishirirki; ila kama sivyo, kwamba hata Ibada hizo binti huyu hakubahatika kuwa kiongozi wake, basi tukio la binti huyu kusimama madhabahuni siku pekee ambayo mdogo wake na mhusika alipoteza maisha, ilhali hakuwa amefanya hivyo kabla ya siku hiyo kipindi kirefu nyuma, na hajawahi tena kufanya hivyo baada ya siku hiyo kipindi kirefu mbele, linaweza kumpelekea mtu yeyote yule mwenye akili timamu kuliita kama
RARE COINCIDENCE
Hata hivyo, tukio hili
haliwezi kuwa rare coincidence kama binti huyu amewahi kuongoza Ibada zingine kwenye Jumapili hizi tatu zilizojitokeza
mbele ya Julai 2020 ambazo mhusika hakubatika kuwepo kwenye Ibada hizo
Siku hiyo pia alihudumu mtumishi wa Mungu kutoka nje ya nyumba ya Ibada ya Kanisa A, na mahubiri yake yalijikita zaidi kwenye utoaji, hali ambayo imepelekea mhusika kwa sasa, kulega lega zaidi kwenye swala la utaoji. Ni kwamba alikuwa tayari ameshalegea, ila kuanzia siku hiyo alilegea zaidi
elly obedy
MUBARIKIWE TENA NA BWANA