WAKIWA WAPO KWENYE LODGE, KETUMBEINE WANASUBIRIA CHAKULA………
....................inaendelea
Baada ya chakula kuwa tayari, kililetwa kikiwa pungufu ya Sahani moja. Kililletwa kwa watu wote isipokuwa mmoja aliyeongezeka, yule aliyekuwa anasema “kasikia EXPERT amekuja
Hapakuwa na logic sana ya mtu huyu kukosa chakula kwa sababu aliyekuwa ametoa ofa, alikuwa ametoa kwa ajlili ya watu wote watakaokuwepo pale pasipo kubagua
- Pamoja na kwamba huyu aliyeongezeka alikuta oda tayari imeshatolewa, bado alikuja muda muafaka kwa share yake kuongezwa ili na yeye aweze kupata chakulla
- Mbali na hilo, mtu huyu aliyeongezeka alikuwa anaonyesha kuwa na ukaribu wa kipekee mno na watu waliokuwa wenyeji wa lodge hiyo kiasi kwamba ilikuwa haileti logic yoyote ya yeye kukosa chakula, hata kama angekuwa amawasili pale katika muda ambao chakula hicho kilikuwa kimeshakuwa tayari
Mtu huyu alikosa chakula kwa sababu moja kubwa; kwamba isije ikaonekana huko nbele ya safari kuwa alikuwa amekaribishwa. Ilitakiwa ije ionekane kuwa allikuwa alijileta mwenyewe
BAADA YA CHAKULA HICHO CHA JIONI KUPITA
Ikumbukwe kuwa mhusika alikuwa mgeni kwenye mazingira ya eneo hili, ila hakuwa mgeni kwenye mazingira ya kazi iliyokuwa imempeleka huko. Mpaka muda huo, tayari alikuwa ana uzoefu wa takribani mwaka mmoja na nusu akiifanya kazi, tangu alipoianza kwa maraya kwanza Julai 2007
Mhusika alijiunga rasmi na kitengo hiki cha matetemeko March 2007. Kabla ya hapo hakuwa anafanya kazi kwenye kitengo hicho
Kwa hiyo mpaka muda huo, wengi wa aliokuwa amewahi kufanya nao kazi walikuwa tayari wameshamsoma na kumjua ratiba yake ya jioni baada ya saa za kazi huwa inakuwaje. Kwa hiyo hata wale ambao alikuwa hajwahi kufanya nao kazi za aina hiyo, akiwemo Boss X na Dereva X, nao pia walikuwa tayari wanazo hints za ratiba yake ya jioni kwa sababu ni kawaida watu huwa wanapeana taarifa
Kwa hiyo; baada ya chakula cha jioni siku hiyo
- Walisogea kaunta wakaanza kupata vinywaji
- Dereva X na Boss X nao pia walikuwepo kwenye kikao hicho isipokuwa Boss X hakukaa sana kwa kwa sababu “kinywaji popular” kilichokuwa kinatembea mahali pale huwa hatumii
- Kwa hali hiyo Boss X alikaa muda mfupi tu baada ya chakula halafu akaingia chumbani kwake
- Kwa hiyo waliokuwa walioendelea kuwepo kwenye kikao hicho siku hiyo ni mhusika, Dereva X, mgeni aliyefika mahali pale akidhania kuwa “EXPERT” alikuwa amekuja(tumite MGENI MWENYEJI -X pamoja na vijana wengine wenyeji wa mahali pale
Baadaye mhusika aliona siyo fair kula “
kilaji” peke yake, alianza kumnunulia pia MGENI MWENYEJI -X na wakati huo walikuwa wameshaanza kuzoeana
Baada ya muda Dereva X naye aliamua kwenda kulala
- Mpaka muda huo sasa akawa amebaki mhusika tu na wenyeji wengine wote
- Haukupita muda mrefu sana naye akaamua kwenda chumbani kulala, na hapo ndiyo mambo yalipoanzia
- Ni baada ya wahudumu wa kwenye duka la vinywaji kuamua kufunga ili wakalale
Baada ya mhusika kuwa amemweleza MGENI MWENYEJI –X, (ambaye sasa walikuwa tayari wameshazoeana kwa sababu ya kununuliana vinywaji),kuwa anataka aingie ndani akalale
- MGENI MWENYEJI-X alimshauri mhusika waende mtaani wakazunguke zunguke kidogo na kuongeza zaidi “kilaji”
- Hapo sasa ilikuwa ni mida ya baada ya saa 4:00, na sehemu hiyo na porini kwenye vichaka na giza totoro, na sehemu ambayo haikuwa hata mawasiliano ya simu wakati huo
- Mhusika aliuliza kama kuna chochote huko cha ziada kwa ajili ya “kampani” ya usiku
- MGENI MWENYEJI-X akajibu ndiyo bila kusita sita.
Hapo ndipo MGENI MWENYEJI-X alipofanya kosa lake kubwa la kwanza
- Mhusika akamwambia aenda ukanletee, hiyo ziada, yeye atakuwepo chumbani akiwa anasubiria
- MGENI MWENYEJI-X akasisitiza waende lakini mhusika akagoma
- Baadaye MGENI MWENYEJI-X alikubali kwenda kumletea, mhusika akabaki chumbani
Baada ya kuwa imepita kama saa nzima hivi, mhsikia ameshazima kibatatri kilichokuwa chumbani kwake, akasikia mtu anagonga mlangoni
Mhusika alifungua mlango, hakuwasha kibatari, kulikuwa na mbalamwezi ya kutosha
Aliingia binti chumbani, ila akadai kuwa bado yuko huko mtaani alikuwa anauza chakula bado hajafunga, hivyo akamuomba mhusika waende wote akafunge kwanza halafu ndiyo warudi chumbani
Hapa tayari likafanywa kosa jingine la pili. Mhusika alimgomea binti huyo. Akamweleza kuwa inabidi aende akafunge halafu arudi. Walikubaliana hivyo na binti huyu aliondoka ila hakurudi tena
Mhusika hakuweza kumumaki vizuri sura binti huyu, kwa sababu alikuwa anamwangalia kwa kutumia mbalamwezi. Hapo sasa ulikuwa ni usiku wa J4 kuamkia J5
BAADA YA USIKU HUO KUPITA
Ratiba yao ilikuwa inaonyesha kuwa J5 hiyo wataongdoka Ketumbeine kuleleke Engaruka, kwenye kituo cha mwiisho kilichuokuwepo maeneo hayo
Asubuhi wakati wanajiandaa kuondoka, baada ya chai:
- MGENI MWENYEJI-X alifika tena mahali pale
- Muda si muda, binti mwingine tena ambaye alionekana kama ni mgeni maeneo yale, naye alifika mahali pale
- Binti huyu alikuwa amepata taarifa kuwa kuna gari ianelekea Engaruka na hatimaye mto wa mbu, kwa hiyo alikuja kuomba lift ya kwenda Mto wa Mbu ili baadaye akapande magari ya kuelekea Arusha
Binti huyu alikuja moja kwa moja mpaka pale alipokuwa amesimama mhusika, na kueleza shida yake
Mhusika baada ya kumsilkiliza, alimwelekeza kwa Boss X ili akasikilizwe huko,. Boss X alimsikiliza na akamkubalia
SAFARI YA KUELEKEA ENGARUKA YAANZA
Siku hiyo, mhusika hakuwa amepata taarifa za awali kuwa MGENI MWENYEJI-X naye alikuwa pia ana safari ya kuelekea Mto wa Mbu
- Alikuja kujua baada ya safari kuanza pale alipomuona MGENI MWENYEJI-X naye akipnada kwenye gari
- Kabla ya safari, MGENI MWENYEJI-X hakuwahi kuongea chochote na Boss X wala Dereva X, isipokuwa salamu tu
Katikati pale kabla hawajafika Engaruka, watu waliamua kusimama kwa muda ili kujisitiri kwa ajili ya haja ndogo, wanaume wannne na binti mmoja
Binti huyu katika namna ya kujisitiri, hakujali sana na alienda kwenye sehemu ambayo haimsitiri sana kivile, ishara kama alikuwa amenuia kuwa-excite baadhi ya wanaume aliokuwa nao kwenye gari. Mhusika alimuona na possibly hata wengine pia
- Binti huyu hakufanya hivyo kwa bahati mbaya, ilikuwa ni makusudi
- Mpaka hapa mhusika akawa amepata picha kwamba binti huyu hakuwa mwenyeji bali mgeni, kwenye eneo kule alikokuwa antokea, na possibly wakati huo ndiyo sasa alikuwa yuko safarini kurudi nyumbani
Hii ni kutikana na ukweli kuwa umasaini kuna viboko na siyo rahisi kukuta binti ana tabia za aina hiyo au hata ule uwezo tu wa kuigiza tabia za aina hiyo, haiwezekani.
Walisafiri salama hadi wakafika kwenye kituo cha Engaruka, na kwa bahati mbaya mtu aliyekuwa ni mlinzi wa kituo hicho hakuwepo kituoni, alikuwa amepata dharura iliyopelekea asafiri kwenda Mto wacMbu; umbali ambao ulikuwa ni takribani kilomita 60 kutokea pale kituo kilipokuwepo
Kwa hiyo iilikuwa inahitajika kumfuata mtu huyu Mto wa Mbu, hatimaye kurudi naye tena pale kituoni, na baada ya hapo timu ya utafiti irudi tena Mto wa Mbu tayari sasa kwa ajili ya safari ya kuanza kurudi tena Arusha mjini
Mtu huyu aliyekuwa anatunza kituo hicho alikuwa anaitwa Israel
…………………..inaendelea