TUKIRUDI TENA KWENYE MADA ILIYOPO MEZANI
Baada ya mhusika kuachana na mwandishi wa kitabu, alisogea mbele kidogo, akapaki tena gari pembeni mwa barabara karibu na kituo cha daladala, akaelekea kwenye kantini moja kubwa ya chakula ambapo kwa uhakika alijua kuwa kulikuwa na maji. Hapo napo hakuambulia kitu, walidai kuwa nao pia hawana na wamekuwa wakichota maji nje ya hapo. Walimwelekeza mhusika kwenda kuchota sehemu ambayo ilipelekea aanze kuona kuwa mwishowe ataonekana kama ana pilika pilika za kutafuta kitu kingine ambacho ni tofauti na maji. Baada ya hapo alinyoosha moja kwa hadi nyumbani. Hiyo siku ikawa imepita, hakuopata maji
Siku nyingine mbili zilizofuata za J4 na J5, alichota maji mazingira ya ofisini, ndani ya jengo ilimo ofisi yake, japo huwa hapendelei sana kuchota maji hayo
Alhamis ikapita na hatimaye ikawadia Ijumaa ya tarehe 19/11/2021 na hapa ndipo sasa Mr X anapokuja ku-pop-in. Kwa MR X haya mambo kwake yeye ni natural, ni inborn, yana-flow menyewe tu kutoka kwenye damu
ILIKUWAJE?
Ijumaa hiyo, MR X akawa ana darasa kwenye kile chumba ambacho J3 ya wiki hiyo, mhusika alikiacha kwa mara ya kwanza kikiwa na mtu ndani yake, binti. Darasa lilikuwa likimshirikisha pia Senior Msataafu wa Kiume-II (SMME-II) mwingine
KABLA YA KWENDA MBALI ZAIDI: MACHACHE KUHUSIANA NA HUYU SMME-II
Huyu SMME-II yeye alikuwa hayupo tena mazingira ya ofisini tangu January 2021 na kwa taarifa alizokuwa amewahi kuzipata mhusika baada ya kuwa amemiss mazingira ya ofisini ni kuwa alikuwa ameshaacha tena kufanya kazi kwa mkataba
Ijumaa hiyo mhusika akiwa yupo ofisini kwake mlango wa ofisi yake ukiwa uko wazi anapata hewa ya kutoka nje huku akiwa anafanya kazi, SMME-II alifika maeneo yale akiwa anataka kuingia ofisi ile ya jirani,ambayo walikuwa na darasa kwa pamoja na MR X muda mfupi uliokuwa unafuata.
- Ofisi hiyo ilikuwa imefungwa na hivyo SMME-II ilibidi asimame kwa muda mlangoni akiwa anasubiria funguo alizokuwa ameagiza aletewe
- SMME-II hakuingia ofisini kwa mhusika, ila mhusika alikuwa amemkaribisha akae kwa muda wakati akiwa anasubiria funguo
- Katika maongezi yao wawili hawa, mhusika alimweleza SMME-II kuwa hajamuona kwa kipindi kirefu
- SMME-II yeye akajibu kuwa kila Ijumaa amekuwa akiwepo kwenye darasa hilo anafundisha isipokuwa mhusika ndiyo huwa anakuwa hayupo ofisini kwake na hicho ndicho kinachopelekea wasioanane, na hapa ndipo kosa lilipoanzia
Kwa kawaida mhusika
- Akiingia ofisini huwa hatoki, hata lunch huwa haendi
- Ijumaa pekee aliyowahi kukosa ofisini tangu arudi kutoka likizo ya mwaka 2021, ni moja tu. Ni ijumaa ambayo gari lake lilikuwa na shida na alilazimika kwenda kukaa gereji kwa muda muda mrefu kiasi
- Ijumaa hiyo aliyowahi kukosa kazini, ni kipindi kirefu nyuma kabla wanafunzi hawajarudi kutoka likizo
- Tangu wanafunzi warudi kutoka likizo, hakuna Ijumaa nyingine ambayo mhusika amewahi kutokuwepo ofisini
Baada ya hoja hii kuwa imemchenga mhusika, hakuona haja ya kuiendeleaza kwa majadiliano, walishia pale.
Baada ya muda funguo zililetwa, SMME-II na MR X wakaendekea na darasa lao lilillokuwa chumba cha jirani, mhusika akiwa anaendeklea na kazi zake, mlango wa ofisi yake akiwa ameendele kuuacha wazi sawia kama vile ulivyokuwa wakati mhusika na SMME-II walipokuwan wanaongea
DARASA LA AKINA MR X LIKIWA LINAKARIBIA KUISHA:MTU (MHITIMU MWINGINE WA MWAKA 2021????) MWINGINE AWASILI OFISINI KWA MHUSIKA AKIWA NA BEGI DOGO
Mhusika akiwa yupo ofisini kwake mlango wa ofisi ukiwa bado uko wazi, binti ambaye sura yake siyo ngeni machoni kwa mhusika, alifika ofisini hapo na kuomba aache begi lake pale kwa muda. Mhusika alimkatalia tena kwa lugha ambayo ni ya msisitizo kidogo, na binti yule aliondoka na begi lake.
Baada ya kuondoka ofisini kwa mhusika, binti huyu aliingia chumba jirani walomokuwa na darasa MR X na SMME-II, japo kwenye darasa hilo yeye hakuwemo siku hiyo. Yeye alikuja tu kutoka nje moja kwa moja na kunyoosha hadi ofisini kwa mhusika na kuomba aache begi lake pale na kwa sababu ambazo hakuzitaja
KWA KIFUPI: NAMNA MHUSIKA ALIVYODHANI KUMFAHAMU BINTI HUYU HAPO KABLA
Kwa kumbukumbu zake, mhusika yeye alidhani kuwa binti huyu naye pia ni mhitimu wa Julai 2021. Still, kama hakuwa mhitimu wa Julai 2021, basi kwa vyovyote vile alitakiwa atakuwa yuko mwaka wa mwisho
- Na kwa sababu yuko mwaka wa mwisho, basi alitakiwa kuwemo kwenye darasa lile walilokuwa wanafundssha akina MR X kwa sababu lilikuwa ni la watu wa mwaka huo
- Yeye hakuwemo kwenye darasa hilo
Na kwa sababu hakuwemo kwenye darasa hilo, basi yawezekana mhusika akawa yuko sahaihi kuwa huyu naye pia ni mhitimu wa mwaka 2021, au si ila alitamani kumpa picha mhusika kuwa alikuwemo kwenye darasa hilo, na kwamba alitokea humo na kuingia ofisini kwa mhusika
Baada ya mhusika kumkatalia binti huyu kuacha begi lake. Ndiyo sasa aliingia kwenye darasa la lakina MR X, ambapo hapo kabla hakuwemo kwenye darasa hilo.
Wakati huo darasa hilo lilikuwa tayari limeshafikia na baadhi ya wanafunzi walikuwa wameshaanza kuondoka. MR X naye alikuwa tayari ameshaanza kujitayarisha kuondoka, mlanfgo ukiwa umefunguliwa, MR X akiwa amesimama mlangoni
………………..inaendelea
KWA KIFUPI: NAMNA MHUSIKA ALIVYODHANI KUMFAHAMU BINTI HUYU HAPO KABLA