Now here's is a bulleted "combined post", a combination of the two most recent long posts already appearing above
UPDATE: WEDNESDAY 08 DECEMBER 2021
KUSHINDWA KUMUONA MKUU WA IDARA (MWI) OFISINI KWAKE BAADA YA MHUSIKA KUOGOPA KUFANYA HIVYO
Mhusika alirudi ofisini kutoka likizo, J3 ya tarehe 27 Septemba 2021
- Alipofika ofisini kwa MWI alikuta barua ambayo baada ya kuisoma, aliona kuna haja ya kumuona MWI ili aweze kupata ufafanuzi kutoka kwake, wa mambo kadhaa kuhusiana na barua hiyo
- Mhusika alimuomba Katibu Muhtasi wa MWI (KMMWI) ili ampangie nafasi ya kuonana na MWI, aidha siku hiyo au ndani ya wiki hiyo
- Ombi lake lilikubaliwa
Baada ya hapo, mhusika hakuweza kupewa majibu ya ombi lake isipokuwa, zilianza kutokea coincidences za MWI na mhusika kuwa wanaonana kwenye mazingira ya nje (ndani ya jengo), aidha kwenye korido au kwenye veranda, na katika mazingira ambayo yalionyesha dhahiri kabisa kuwa
- Mhusika na MWI wangeweaza kuongea kuhusu appointent hiyo wakiwa kwenye veranda au kwenye korido
- Baada ya pale, mhusika na MWI wangeweza kuongozana wakiwa wawili kuelekea ofisini kwa MWI, possibly hata bila ya uwepo wa KMMWI
Kwa hiyo kilichokuwa kinakwepwa hapa ni maongezi ya mhusika na MWI kufanyika katika namna ambayo yangeonekana kuwa:
- Mhusika aliomba appointment ya kuonana na MWI.
- KMMWI kumpa appointment ya kuongea na MWI
- KMMWI kumwita mhusika na kumruhusu aingie ndani ofisini kwa MWI ili wafanye maongezi
Picha iliyokuwa inatakiwa kuonekana ni kwamba mhusika alitakiwa aoenekane kuwa ni yeye mwenyewe tu alichukua jukumu la kuimfuata MWI ofisini kwake pasipo ruhusa wala appointment kupitia kwa KMMWI
Baada ya mhusika kuona hali iko hivyo, aliamua kuacha kufuatilia ombi lake hilo, kwa kujua kuwa pengine ipo siku atapewa appointment hiyo.
Baada ya kuwa zimepita takribani wiki tatu hivi, KMMWI pamoja na MWI wakatengeneza mtego mwingine tena mpya wa kumsababisha mhusika ajipeleke mwenyewe ofisini kwa MWI.
SET UP YA MTEGO WENYEWE
Wahusika wa mtego huu walikuwa ni MWI pamoja na KMMWI
Ilikuwa siku moja, asubuhi moja ya J3 ambayo hakumbuki tarehe yake, mhusika aliwasili maeneo ya ofisini
Baada ya kupandisha ghorofa ya kwanza, akiwa anaelekea ofisini kwake, kabla hajakifikia kitasa cha mlango wa ofisi yake akiwa bado yuko kwenye korido alisikia sauti kwa nyuma ikimwita. Alipogeuka alikutana uso kwa uso na KMMWI. Hapo sasa ikabidi asimame asiendelee mbele kuelekea ofisini kwake na kuanza kuongea naye, wakiwa kwenye korido
- KMMWI alimuuliza mhusika kama katika kipindi cha hivi karibuni, amepokea barua yoyote ile ya PROMOTION
- Mbali na kuuliza swali hilo, KMMWI alikuwa ameshika pia barua nyingine mkononi mwake
Na kwa sababu barua aliyokuwa ameipata mhusika baada ya kutoka likizo KMMWI naye pia alikuwa anaijua, lakini kwa wakati huo tena KMMWI alikuwa ameshika barua nyingine mkononi na ambayo alikuwa haelekei kuitoa kwa mhusika wakiwa kwenye korido
- Bila kuingia ofisini kwake, mhusika aligeuza njia wakawa wameongozana na KMMWI kuelekea ofisini kwa MWI ili akaione barua hiyo
- Baada ya kufika ofisini kwa MWI, KMMWI alimpa mhusika barua ile ile ya mwanzo ambayo aliikuta baada ya kutoka likizo ya mwaka 2021. Mhusika alishangaa sana
Baada ya hapo mhusika alimjibu KMMWI kuwa barua hiyo anayo ndiyo ile aliyoikuta baada ya kutoka likizo
- Wakati huo MWI alikuwa ndani ofisini kwake na mlango wa ofisi yake alikuwa ameuacha wazi
- KMMWI aliongezea kwa kusema “si ulihitaji kuongea na MWI, basi huyo hapo ingia uongee naye”
Mhusika aliimjibu KMMWI kwa kumwambia kuwa alichokuwa anataka kuongea naye MWI tayari ameshakipatia ufumbuzi kwa sababu ni siku nyingi tayari zilikuwa zimeshapita tokea siku alipoomba kuongea naye
HILI TULIITE TUKIO LA KWANZA
TUKIO LA PILI:
MHUSIKA AANDIKIWA BARUA NA KAIMU MWI YA KUKARIBISHWA KWENYE KIKAO CHA NDANI CHA IDARA
Kwenye wiki ya kuanzia tarehe 21-28, MWI wa siku zote alisafiri na hivyo kukaimisha mamlaka yake kwa ofisa mwingine. Huyu
KAIMU MWI ndiye yule yule aliyewahi kukaimu Januray 2021, katika muda ambao barua za mhusika zilikuwa zikirudishwa kwa madai ya kukosewa anuani
- KAIMU MWI huyu, alikuwa hajawahi kukaimu tena nafasi hiyo tangu alipokaimu January 2021, unless kama alifanya hivyo tena katika kipindi kile ambacho mhusika alikuwa yuko likizo
- Ilipofika siku ya Ijumaa ya tarehe 26/11/2021, KAIMU MWI alifika ofisni kwa mhusika na kumuuliza kama amepata barua yake
- Mhusika alisema hajafahamu kama ana barua na hajaipata
- Baada ya hapo KAIMU MWI alimjulisha mhusika kuwa J4 ya tarehe 30/11/2021 wiki inayofuata kutakuwa na kikao kifupi idarani na yeye mhusika anatakiwa pia kuwepo
- Zaidi KAIMU MWI alisema kuwa amemwandikia barua mhusika kuhusiana na kikao hicho na hivyo ataipata kupitia kwa KMMWI
Maongezi yao yaliishia hapo, na baadaye mhusika alipandisha juu na kukuta barua hiyo ikiwa imewekwa kwenye pigeon hole yake. Barua hiyo haikuwa na minutes za kikao, na wala haikuwa wazi sana ni nini hasa kitafanyiak J4 hiyo
Hatimaye J4 hiyo ilifika na kikao kikafanyika na kuisha salama.
Mambo kadhaa aliyoyaona baada ya kikao hicho kuwa kimefanyika
- Kawaida vikao vya aina hiyo huwa vinafanyika MWI naye akiwepo, lakini yeye hakuwepo, japo alikuwa tayari amesharudi ofisini
- Huyu aliyekuwa anakaimu yeye alikuwepo kwenye kikao. Hata hivyo kukaimu kwake kulikuwa tayari kumeshaisha; kuliishia siku ya Ijumaa tarehe 26/11/2021
- Baada ya kikao, aliyekuwa KAIMU (kwa wakati huo hakuwa anakaimu tena) aliamua kupita pita kwenye baadhi ya maabara, kulikuwa na watu aliamua kuwapitisha humo
- Mhusika yeye hakuwa mmojawapo wa watu hao, japo kulikuwa na dalili zote zilizoonyesha kuwa hata yeye ingependeza aungane nao kwenye zoezi hilo. Kwa hiyo mhusika hakushiriki kwenye zoezi hilo
HITIMISHO:
Hapakuwa na haja ya
KAIMU MWI kumwandikia barua mhusika kwa ajili ya kuhudhuria kikao ambacho mara zote huwa anahudhuria hata kwa kupewa taarifa za mdomoni tu, taarifa za mdomoni tu kutoka kwake
KAIMU MWI zilikuwa zinatosha. Mhusika hana huo u-special unaoweza kumlazimu hadi
KAIMU MWI amwandikie barua kwa ajili ya kuhudhuria kikao na mabcho ni cha ndani tu. Mara zote barua za aina hiyo huwa zinatokea mara chache zikiwa zinahusiana na kazi, inapotokea labda anatakiwa afanye kazi ambayo ni special assignment na ambayo ina deadline fulani
Swala la kumwandikia barua mhusika, inaonyesha kama kulikuwa na kitu kingine cha ziada ambacho barua hiyo ilikusudiwa kuwa tahadhari ambayo ingekuja kutumika kama ushahidi hapo baadaye, just in case of anything
Pia ughafla wa maamuzi wa mhusika kushirikishwa kwenye kikao hicho, ndiko kulikompelekea
KAIMU MWI afike tena ofisini kwa mhusika kumjulisha ana kwa ana juu ya kikao hicho, pamoja na kuwa alikuwa tayari ameshamwandikia barua. Hii ni kutokana na ukweli kuwa ubunifu wa mpango wa mhusika kushiriki kwenye kikao hicho ulikuwa ni wa ghafla na ambao possibly hapo awali, mpango huo haukuwepo
Mhusika anaona mengi sana, japo anaweza kuandika baadhi yake tu; machache; na asingependa kuliongelea sana swala hili kwa sababu kikao kilihusisha pia na watu wengine kadhaa kutoka nje ya taasisi.
MUBARIKIWE TENA NABWANA
MATUKIO MAWILI YA MUHIMU YANAYOMHSU KAIMU MKUU WA IDARA AMBAYE TAARIFA ZAKE ZIMEELEZWA HAPO JUU
TUKIO LA KWANZA: KUITWA OFISINI KWA MWI NA KAIMU MWI NA KUKUTA OFISI IKO WAZI KAMU MWI AKIWA HAYUMO OFISINI
Tukio la kwanza lilitokea January 2021, siku ambayo barua za mhusika zilirudishwa kwa kosa la kutokuwa na anwani sahihi.
Awali, mhusika hakuona haja ya kuliongelea tukio hili kwa sababu alikuwa analiona kuwa halikuwa na maana yoyote isipokuwa kwa sasa, kwa mbali linaonyesha dalili kama lilikuwa na maana fulani na za muhimu
Baada ya barua zake kuwa zimerudishwa, KMMWI alitumwa na KAIMU kwenda kumwita mhusika ofisini kwake ili aende ofisi ya MWI kwa ajili ya maongezi ambayo yalihusiana na barua hizo
- Mhusika aliondoka ofisini kwake muda huo huo, huku wakiwa wameongozana na KMMWI
- Wawili hao wakiwa wameongozana kuelekea ofisini kwa MWI, mhusika hakumbuki vizuri KMMWI alielekea wapi baada ya hapo, lila hadi mhusika anafika ofisini kwa MWI, KMMWI alikuwa hayupo ofisini kwenye kiti chake. Japo walikuwa wameongozana, KMMWI badaaye alipitia sehemu nyingine, akimwacha mhusika akiendelea kuelekea ofisini kwa MWI
- Mhusika alipofika ofisni kwa MWI alimkuta kijana mwingine staff, ambaye yeye si mhusika wa ofisi hiyo, ila ni staff
- Ni kijana ana kama matatizo kidogo ya ki-afya na si mara zote huwa anafika ofisini, ila siku hiyo alikuwa amebahatika kuja ofisini
- Mlango wa ofisi ya MWI ulikuwa umefungwa, na mhusika aliposhika kitasa na kuufungua, hapakuwa na mtu ndani. Hata KAIMU MWI ambaye ndiye alikuwa ameagiza mhusika aitwe, naye pia hakuwamo ofisini kwake
Baada ya kuona ofisi ya MWI haina mtu, hakuingia bali alibaki kibarazani akiongea na yule kijana aliyekuwa amekaa kwenye ofisi ya KMMWI.
Wakati huo ukarabati ndiyo ulikuwa umeshaanza siku kadhaa nyuma, na viti vilivyokuwa ndani ya ofisi ya MWI, vilikuwa vimevurugwa vurugwa utadhani kuna watu waliwahi kufanyia mazoezi ya mieleka humo. Kwa ujumla ofisi hiyo haikuwa katika mazingira mazuri sana ambayo watu wangeweza kufikiria kufanyia maongezi yao humo
HATIMAYE KAIMU MWI AWSILI OFISINI HAPO SIKU HIYO
Baada ya takribani dakika 3-5 hivi, KAIMU MWI aliingia, huku KMMWI akiwa bado haonekani ofisini hapo
Mhusika na KAIMU MWI waliingia ofisini kwa MWI wakaongea na hatimaye kumaliza maongezi yao, na baada ya hapo mhusika alitoka na kumkuta kijana bado yupo pale ofisini huku KMMWI akiwa bado hajarudi tena ofisini hapo
Kwa hiyo kwenye maongezi haya, KMMWI alienda akamwita mhusika halafu baada ya hapo (KMMWI) akapotea moja kwa moja hakuonekana tena muda wote; hadi maongezi ya mhusika na KAIMU MWI yalimalizika alikuwa bado hayupo kwenye kiti chake
Hili tuliite sasa tukio la kwanza
TUKIO LA PILI: TAARIFA KUHUSIANA NA UWEPO WA MKUTANO WA GHAFLA WA KWENDA KUPIGA KURA; ZILIZOKUWA ZIKISAMBAZWA KWA MDOMO NA MTU ALIYEKUWA ANAPITA KWENYE KORIDO
Mkutano huu ulifanyika baada ya taarifa zake kuwa zimesambazwa na mtu (staff) aliyekuwa anapita kwenye korido akiwajulisha watu kuwa muda wa kupiga kura ulikuwa umefika, na hivyo watu wote walitakiwa wakusanyike kwenye chumba cha mkutano ili wakapige kura
Mhusika alishangaa kidogo kwa sababu hakuwa amebahatika kupata taarifa hizo kabla
- Muda mfupi kabla ya taarifa hizo, UMEME ULIKUWA UMEKATIKA, na ilikuwa ni majira ya baada ya saa tisa alasiri
- Ilikuwa ni mwanzoni mwa March 2021
- Mhusika aliitikia wito huo na kwenda kupiga kura
- Kura zilihusisha idara mbili ambazo zimeungana na kutengeneza MAJOR UNIT ambayo ni mpya kwenye taasisi
- Kwa hiyo wapiga kura walitoka kwenye idara mbili ambazo zimeshaungana na kutengeneza MAJOR UNITN mpya
Mkutano huu ulikuwa chini ya usimamizi wa MKUU WA MAJOR UNIT, ambaye ndiye anayeiongoza hadi muda huul; na aliyekuwa anatafutwa kwa kutumia kura hizo, ni
MKUU MWINGINE AMBAYE ATAIONGOZA MAJOR UNIT YA SASA BAADA YA KUWA IMEUNGANA TENA NA TAASISI ZINGINE MBILI ZILIZOKO NZEGA NA DODOMA
Kura zilipigwa na aliyeongoza kwenye kura hizo ni huyu KAIMU MWI ambaye taarifa zake zinaendelea kuwajieni hapa
BAADA YA ZOEZI LA KUPIGA KURA KUMALIZIKA
Mkuu wa MAJOR UNIT ambaye ndiye alikuwa anaongoza kikao hicho, alimkaribisha
MAMA SENIOR ambaye kwa wakati huo alikuwa bado hajastaafu, (kwa sasa ayari ameshastaafu), kwa ajili ya neno fupi. MAMA SENIOR huyu alikaribishwa atoe neno kidogo hasa kuhusiana na maandalizi ya siku ya wanawake duniani ambayo wiki yake ilikuwa inaadhimishwa kwenye wiki ya kuanzia tarehe 08 March 2021
Baada ya hapo, MAMA SENIOR alichukua nafasi hiyo na kuanza kueleza mambo kadhaa kuhusiana na sikukuu hiyo na hatimaye allisema kuwa J3 ya wiki inayofuata kutakuwa na kusanyiko la wanawake wote wafanyakazi wa Taasisi hiyo litakalofanyikia ndani ya taasis yenyewe. MAMA SENIOR aliendelea mbele zaidi na kusema kuwa baada ya kusanyiko hilo siku hiyo, anapenda kuwakaribisha watu wote wa idara zote mbili zilizoungana na kutengeneza MAJOR UNIT mpya, wakusanyike tena kwenye ukumbi huo huo walimokuwa siku hiyo, kwa ajili ya kufahamiana zaidi, majira kuanzia saa tisa (9:00) alasiri
- Kwa hiyo kusudi la kusanyiko hilo jingine ilikuwa ni wana idara mbili zilizoungana kujitambulisha kwa wenzao ili kuanza kufahamiana zaidi
- Zaidi alisema kuwa kutakuwa na bites (hapa sasa ndipo alipompatia mhusika; angeweza asihudhurie kikao kama bites zisingetajwa. Tatizo la huyu mtu mimi huwa namweleza siku zote, anapenda mno kula, nadhani hata huwa anakula vyote. Huwa hawez kukosekana kwenye malaji)
Haya ndiyo mambo ya msingi aliyoongea MAMA SENIOR kwenye kusanyiko hilo, siku hiyo
Hatimaye kweli siku hiyo iliwadia, na ilikuwa ni siku ya kazi. Hata hivyo badala ya kusanyiko hilo kuanzia saa tisa kana ilivyokuwa imetajwa hapo awali, lilichelewa kidogo na kuanza kwenye ida ya karibia saa kumi (10:00), baada ya idadi ya wahudhuriaji kuwa imeridhisha
- Watu walianza kwa kujitambulisha majina yao na nyadhifa huku vinywaji baridi, soda na maji vikiendelea kusambazwa
- Mkuu wa MAJOR UNIT naye pia alikuwepo
- Vinywaji vilivyoanza kupita zilikuwa soda, na hatimaye ilifuata supu ya nyama ambayo ilikuwa ni SELF SERVICE
- Supu hiyo ilikuwa ni aina ile ambayo inajulikana siku zote kuwa ni FAVOURITE kwa mhusika (mtu anayependa malaji lazima watu wajue ni chakula gani huwa anapendelea; kula kula nako wakati mwingine kuna shida sana)
HITIMISHO
Baada ya kuwa ameona supu jioni hiyo, mhusika alishangaa kidogo kwa nini chakula kile kinaseviwa katika muda ambao siyo sahihuin sana kwake na kwa mazingira ya ofisini. Supu hiyo ilikuwa ni SELF SERVICE; unanyanyuka kwenye kiti chako, unaacha soda yako, unaenda unasevu halafu unarudi unaendelea na chakula na soda yako ambayo tayari ulikuwa umeshaifungua na kuanza kuinywa. Actually soda zilikuwa zinafunguliwa kwa opener na wale waliokuwa wanazisambaza. Unles iwe ni mtu ambaye hakuwa ame-opt kunywa soda siku hiyo; lakini kwa yule ambaye alikuwa na soda, tayari soda hiyo ilikuwa imeshafunguliwa
Baada ya mhusika kuona kuwa zoezi la supu ni self service
- Alikagua kulia na kushoto watu aliokuwa amekaa nao karibu na kukuta mmojawapo ni swahiba wake wa karibu sana na ambaye alimwita na kumkaribisha pale ili wakakae wote kwenye meza moja, na mhusika alienda akakaa hapo baada ikiwa ni ishara yake ya kuitkia ukaribisho huo
- Upande wa pili kulikuwa na mtu mwingine tena ambaye ni siri yake mwenyewe mhusika, asingependelea sana kumtaja hapa
Baada ya ukaguzi huo,
alibugia fundo moja kubwa la soda yake, akaiweka halafu akanyanyuka kuelekea kwenye supu
kama anataka kwenda kusave supu (
hakuwa anakwenda kusevu supu) na kwa bahati nzuri bakuli za kusevia supu alikuta zimeisha, japo watu hawakuwa wengi sana, na zilikuwa zimefuatwa zingine. Baada ya hapo mhusika alitoka nje na kurudi moja kwa moja ofisini kwake na kuanza kuendelea na kazi zake. Dakika kama tano, baada ya mhusika kurudi ofisini,
UMEME ULIKATIKA TENA.
Baada ya kuona hivyo, mhusika alitoka ofisini na kuelekea kwenye gari lake, akawasha gari na kunyoosha moja kwa moja nyumbani. Siku yake kwa siku hiyo ikawa imeisha kwa namna hiyo
MUBARIKIWE TENA NA BWANA