Makanyaga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2007
- 11,129
- 7,321
- Thread starter
- #841
UPDATE-2: TUESDAY 14TH DECEMBER 2021 KWA WAUMINI WA KANISA A NA WENGINEO WALIO WAKRISTO:
KUHUSINA NA SEHEMU YA MAFUNDISHO YALIYOTOLEWA MADHABAHUNI J2 YA TAREHE 12/12/2021 WAKATI WA IBADA YA KWANZA KWA KUTAJWA MAFUNGU YALIYOSEMEKANA KUWA NI YA KISHETANI
Mafungu hayo hayajawahi kuwepo na wala hayapo kwenye Biblia. Angalieni hapa
Luka 4: 1-9
Yesu Ajaribiwa Na Shetani
4 Kisha Yesu, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akarudi kutoka Yordani akaongozwa hadi jangwani. Alikaa huko jangwani siku arobaini 2 akijaribiwa na shetani. Siku zote hizo hakula cho chote , kwa hiyo baada ya muda huo aliona njaa.
3 Shetani akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru jiwe hili liwe mkate.”
4 Yesu akamjibu, “Imeandikwa katika maandiko, ‘mtu haishi kwa chakula tu.’ ”
5 Kisha shetani akamchukua hadi juu ya mlima mrefu akamwo nyesha kwa mara moja milki zote za dunia. 6-7 Akamwambia, “Uki piga magoti na kuniabudu, nitakupa uwezo juu ya milki zote hizi na fahari yake; maana ni zangu na ninaweza kumpa ye yote nita kaye.”
8 Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia yeye peke yake.’ ”
9-11 Ndipo shetani akamfikisha Yerusalemu, akampandisha juu ya mnara wa Hekalu, akamwambia: “Kama wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini kwani imeandikwa, ‘Mungu ataamrisha malaika wake wakulinde
12 Yesu akamwambia, “Pia imeandikwa, ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’ ”
Mungu wako.’ ”
13 Basi Shetani alipomaliza majaribu yote, akamwacha Yesu kwa muda.
Yesu Ahubiri Galilaya
14 Kisha Yesu akarudi Galilaya, akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu. Habari zake zikaenea katika sehemu zote za wilaya ile. 15 Alifundisha katika masinagogi yao na wote wakamsifu.
HOJA ZA MHUSIKA KUHUSIANA NA HOJA ZILIZOTOLEWA NA MTUMISHI J2 ILIYOPITA
MOJA: Je kwenye majibu ya Yesu aliyomjibu shetani, hakuna mafundisho? MBILI: Na kama kuna mafundisho, je “hatuwezi kusema kuwa kuna pumzi ya Mungu kwenye maandiko hayo kwamba kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho”?
Hii ni kwa sababu majibu haya ya Yesu yasingepatikana bila ya shetani kuwa amesema kile alichokisema na hatimaye kupelekea kiandikwe ndani ya Maandiko Matakatifu; kwa maana kuwa kama alichoomba shetani kifanywe na Yesu, kisingekuwa kimeandikwa, basi mafundisho yayotokana na majibu ya Yesu yasingekuwepo kwetu sisi waumini leo
TATU: Je, tunaweza kusema kuwa mafungu haya yenye maneno ambayo shetani alimwambia Yesu ni ya kishetani kama ilivyopadaiwa J2 Kanisani na mtumishi aliyesimama madhabahuni wakati wa Ibada ya kwanza?
Ukweli ni kuwa kwa uelewa wake yeye mhusika, kwenye Biblia HAYAPO MAFUNGU YA KISHETANI, ISIPOKUWA YAPO MAFUNGU YANAYOMHUSU SHETANI, baadhi ya mafungu hayo yakiwa ni haya yaliyotajwa hapa
Wenye uelewa zaidi wa Maandiko Matakatifu wanaweza kumsahihisaha mhusika katika hili. Possibkly mtumishi huyu naye amepotoshwa akiwa huko huko kwenye masomo yake
MUBARIKIWE TENA NA BWANA