UPDATE: SATURDAY 14TH MAY 2022
KUHUSIANA NA “SPECIALIST”………
TUKIO LA KWANZA KABISA LA MSIBA AMBALO MHUSIKA ALIWAHI KUHUDHURIA MAENEO JIRANI NA OFISINI KWAKE, NA PIA JIRANI NA MAHALI PALE ANAPOISHI YEYE NA KUKUTANA NA WATU WATATU TU ALIOWAFAHAMU; KWENYE MSIBA HUO
Ukiondoa tukio la msiba wa idarani kwake na mhusika ambalo aliwahi kuleta taarifa zake humu na lililotokea mwaka 2020; na ambalo mhusika alijulishwa taarifa zake na Kaimu Mkuu wa Idara (ambaye kwa sasa ndiye Mkuu wa Idara),
kuna tukio jingine la aina hiyo ambalo tayari mhusika alikuwa ameshalishuhudia hapo kabla (nadhani mwishoni mwa mwaka 2016 au mwanzoni mwa mwaka 2017)
Kwa hiyo tukio hili la idarani kwake na mhusika
LILIKUWA NI LA PILI, na lilishahibiana kwa kiasi na lile la kwanza la lililotokea nyumbani kwake na “SPECIALIST”; ila kwa wakati huo mhusika hakutaka kuuongelea mfanano wa matukio haya;
ISIPOKUWA ALILLAZIMKA TU KULIONGELEA LILE LA IDARANI KWAKE (LA PILI) na kuliacha lile la “SPECIALIST” (LA KWANZA) baada ya kuwa ameona kwa mara nyingine tena kuwa hata lile la idarani nalo pia lilikuwa na namna ya mbinu fulani (tricks) hivi ambazo zilikuwa zimekusudiwa maalumu kwa ajili yake mhusika na zilizoshahibiana kwa namna fulani na za tukio lile la kwanza
NAMNA MHUSIKA ALIVYOTOKEA KUPATA TAARIFA ZA KILA MSIBA KWA MISIBA HII
Taarifa za tukio la msiba wa idarani kwake mhusika alizipata
SIKU YA IJUMAA akiwa kwenye korido baada ya saa 6 mchana; maeneo ya ofisini. Ilikuwa ni baada ya kuwa amemaliza darasa alilokuwa nalo siku hiyo. Mhusika alijulishwa kuwa msiba wenyewe ulikuwa maeneo ya karibu kabisa na ofisini, nyumbani kwa mfiwa na ambapo pia ni jirani kabisa na mahali pale anapoishi mhusika.
TUKIO LA KWANZA LINALOFANANA NA HILO AMBALO MHUSIKA ALIKUWA TAYARI AMESHAKUMBANA NALO HAPO KABLA
Tukio la kwanza kabisa la namna hiyo mhusika aliwahi tayari ameshakumbana nalo kwa mara ya kwanza, nyumbani kwa “SPECIALIST”; hili la idarani kwake, lilikuwa la pili
Kwenye tukio la kwanza, mhusika hakupata taarifa kutoka kwa “SPECIALIST’ mwenyewe bali kwa binti msaidizi wake wa ofisini ambaye kwa bahati tu walikutana nje ya Ofisi ya Mkuu wa Idara ofisini kwa mhusika
- Binti huyu alikuwa amefika ofisini pale kwa shida za kiofisi na wakati wanabahatika kukutana na mhusika, binti alikuwa tayari yuko njia moja anarudi ofisini kwake
- Baada ya kusalimiana na mhusika, mhusika alimpa pia binti salaam za swahiba wake “SPECIALIST” ili amfikishie
- Pale ndiyo binti alipomjulisha mhusika kuwa “SPECIALIST” hakuwepo ofisini kwake siku hiyo bali nyumbani kwa sababu alikuwa amepata msiba mkubwa. Siku hiyo ilikuwa ni SIKU YA IJUMAA wakiwa kwenye veranda iliyo mbele ya ofisi ya Mkuu wa Idara
Ilipofika kesho yake Jumamosi, mhusika aliamua kwenda kuhani msiba nyumbani kwake na “SPECIALIST”
Pamoja na kuwa ilikuwa ni Jumamosi, mhusika alikaa pale nyumbani kwa takribani masaa mawili, na katika muda wote wote huo
watu pekee aliowaona na kuwafahamu msibani pale walikuwa ni watatu tu
- “SPECIALIST” mwenyewe
- Injinia mmoja kutoka miliki za nyumba ambaye alikuwa anasimamia ukarabati wa nyumba anayoishi “SPECIALIST”
- Bwana Afya wa taasisi anayofanyia kazi mhusika
Hapakuwa na office-mate yeyote wa “SPECIALIST” kwenye msiba huo; yaani wale ambao anafanya nao kazi idara moja, hawakuwepo hata mmoja
Hawa office-mates wa “SPECIALIST” majority yake mhusika anawafahamu kutokana na interactions nao za kipindi kirefu kiasi cha takribani miezi mitatu; ambazo mhusika aliwahi kuwa nazo na wafanyakazi hao mwaka 2008.
Kwa hiyo walio wengi wa wafanyakazi wa idara hiyo mhusika anafahamiana nao na baadhi yake wamekuwa pia ni majirani zake kwenye mazingira ya makazi ya taasisi ambamo mhusika bado anaishi mpaka leo
Mfanano unaotokea hapa ni kwamba, kwenye matukio haya mawili; ni kwamba katika kila tukio
- Mhusika alikuwa anapata taarifa za uwepo wa kila msiba, SIKU ZA IJUMAA aidha akiwa kwenye korido au kwenye veranda
- Matukio yote mawaili yalitokea maeneo jirani kabisa na ofisini kwa mhusika na pia jirani na sehemu ya makazi yake
- Taarifa zilizokuwa zinafikishwa kwa mhusika zilikuwa ni “second hand” kwa maana kuwa waliokuwa wanamjulisha mhusika kuhusiana na uwepo wa msiba walikuwa ni watu wengine na si wahusika wa msiba wenyewe pamoja na kwamba mawasiliano yake ya simu walikuwa wanayo
- Bila kujali ukubwa wa msiba uliokuwa umetokea, kwenye msiba wa kwanza (2016/2017) alikutana na watu watatu aliowafahamu na ambao amewataja hapo juu
- Vile vile, bila kujali ukubwa wa msiba uliokuwa umetokea, kwenye msiba wa PILI (2020) napo alikutana pia na watu watatu tu aliowafahamu. Hawa walikuwa ni jirani yake na mhusika pamoja na mke wake, pamoja na mama mwenye nyumba ambaye mume wake ndiyo alikuwa mfiwa
Staff-mates wengine wote kutoka idarani kwa mhusika hawakuwepo msibani, na mhusika aliondoka ofisini hai hai siku hiyo akiacha ofisi karibia zote zikiwa zimefungwa; huku akidhani kuwa wenzake wote watakuwa walikuwa wametangulia kwenye msiba kwa sababu yeye alikuwa amecchelewa kupata taarifa; alizipata siku hiyo hiyo
Siku hiyo, alipokuwa yupo nje kwenye parking za gari akiwa anajiandaa kuelekea msibani, pale ndiyo alibahatika kumuona SENIOR MSTAAFU WA KIUME (SMME), na akiwa anajiandaa kuwasha gari aondoke, na ndiye mtu pekee aliyekuwa amebaki ndani ya jengo muda huo, ukiondoa mhusika mwenyewe
- Baada ya kumuona SMME, mhusika alidhani kuwa SMME naye alikuwa yuko njia moja kuelekea msibani kwa sababu ndiyo mtu pekee ambaye alikuwa ameabakia idarani siku hiyo
- Baada ya kufika msibani, mhusika hakumkuta SMME
Aidha mhusika hakumkuta mtu mwingine yeyote yule kutoka idarani kwake, na wakati huo huo watu wote ofisini hawakuwepo wakati anaondoka idarani. Ofisi zote zilikuwa zimefungwa
Kabla hajaondoka ofisini siku hiyo, mhusika alikagua kwanza floor zote na alijiridhisha kuwa watu wote hawakuwepo idarani na alipotoka nje ndiyo alimuona SMME tu na hapo ndipo alipogundua kuwa huyo ndiyo alikuwa mtu pekee ambaye naye alikuwa amebakia ndani ya jengo muda huo
HITIMISHO
Tukirudi kwenye tukio hili la “SPECIALIST”, office mates wote kutoka idarani kwa “SPECIALIST”, hawakuwepo kwenye msiba huo, isipokuwa staff-mates hao wawili tu mhusika aliowataja hapo juu ikiwa ni pamoja na “SPECIALIST” mwenyewe ambaye ndiye aliyekuwa mfiwa
MUBARIKIWE TENA NA BWANA