KWA UFUPI SANA:
CHRONOLOGY YA MATUKIO YA KUPANDISHWA NA KUSHUSHWA VYEO/NGAZI IKIWA PAMOJA NA KUKATWA MSHAHARA KWA MHUSIKA; TANGU AAJIRIWE KWA MARA YA KWANZA MWAKA 2000
KUANZIA FEBRUARI 2000 HADI JUNE 30, 2003: MHUSIKA ALITUMIKA KWENYE NGAZI A
Mhusika aliajiriwa mnamo Februari mwaka 2000 na ilipofika
Julai mosi 2003, mhusika alipanda daraja kwa mara ya kwanza tuseme kutoka ngazi A kwenda ngazi B
- Kwa hiyo, kuanzia Februari 2000 hadi 30 Juni 2003 mhusika alitumika kwenye ngazi A ya ajira yake
- Mhusika hapa hana uhakika sana lakini katika hali ya kawaida, anadhani kuwa pengine alitakiwa apande tena daraja mnamo March mosi 2003 na si Julai 2003 kwa sababu aliajiriwa Februari 2000
- Katika hali ya kawaida, kwenye kada aliyoajiriwa, mtumishi huwa anapanda ngazi kila baada ya miaka mitatu kamili
BAADA YA MHUSIKA KUPANDA DARAJA KWA MARA YA KWANZA JULAI MOSI 2003; HADI KUFIKIA NGAZI YA MWISHO KABISA,NGAZI ZINGINE KADHAA ZILIKUWA BADO ZIKO MBELE YAKE ZIKIMSUBIRI
Baada ya kuwa amepanda daraja Julai mosi 2003, mhusika akawa amebakiza ngazi zingine kadhaa hapa katikati, kufikia ngazi ya mwisho kabisa ambayo ni H
Kwa maana hiyo, kuanzia pale alitakiwa apitie tena kwenye ngazi zingine C, D, E, F, G na hatimaye H ikiwa ndiyo ngazi ya mwisho kwake
Under no merit situation, na katika
minimum performance ambayo iko
recommended na mwajiri, mhusika alitakiwa atumie mafungu ya miaka mingine mitatu mitatu kwenye kila mojawapo ya ngazi zilizokuwa zimebaki mbele yake, yaani kuanzia ngazi C hadi kufikia ngazi ile ya mwisho ambayo ni H
KUANZIA JULAI MOSI 2003 HADI JUNE 30, 2006: MHUSIKA ALITUMIKA KWENYE NGAZI B
Mhusika akiwa bado anatumika kwenye ngazi hii ya B,
alifanikiwa kupata shahada ya pili na hivyo ilipofika tarehe 23 June 2006 (
wiki moja kabla ya tarehe ya kupanda ngazi kutoka ngazi B kwenda ngazi C ambayo ilikuwa ni Julai mosi 2006);
- Mhusika alipandishwa ngazi kwa kurushwa ngazi moja na hivyo kufanikiwa kupanda kutoka ngazi B akivuka ngazi C na kufika ngazi D
- Kwa hiyo kuanzia tarehe 23 June 2003, mhusika alipanda kutoka ngazi B na kuwa ngazi D
- Kufika kwa mhusika ngazi D mnamo tarehe 23 June 2006, kulipelekea sasa mhusika aweze kupandishwa tena ngazi kutoka D kwenda ngazi E, wiki moja baadaye, kutokana na kule kupanda kwa kawaida ambako huwa kunaendana na miaka mitatu mitaatu yautumishi kwenye ngazi husika, yaani ifikapo tarehe mosi Julai 2006
Kwa hiyo kwa kuunganisha barua hizi mbili, ile ya
tarehe 23 Juni 2006 ambayo ilihusiana na mhusika kuhitimu masomo ya uzamili pamoja na nyingine ya
tarehe mosi Julai 2006, ambayo ilitokana na mhusika kupanda ngazi kwa kufuata muda wa utumishi wa miaka mitatu kwenye ngazi husika; ndani ya kipindi cha fungu la miaka hii mitatu ya kuanzia
Julai mosi 2003 hadi 30 June 2006
- Mhusika alifanikiwa kupanda cheo kwa ngazi tatu; ngazi moja ikiwa inatokana na kupanda daraja kwa muda wa kawaida, na zingine mbili zikiwa zinatokana na kuhitimu masomo ya uzamili
- Kwa hali hiyo hadi kufikia Julai mosi 2006, mhusika akawa amefikia ngazi E
MHUSIKA ASHUSHWA NGAZI KUTOKA E KURUDISHWA D KWA MARA YA KWANZA HUKU MAELEZO YAKIWA YANATOLEWA KWA MDOMO KUWA MOJAWAPO YA BARUA ILIKUWA IMEKOSEWA
Kwenye mchakatio huu wa kupanda ngazi mhusika, kuna kitu
technical ambacho kilifanyika
possibly kikiwa kinatarajiwa kuwa asingeweza kukigundua
BARUA YA TAREHE 23 JUNE ILIYOMPANDISHA KUTOKA NGAZI B KWENDA NGAZI D KUTOKANA NA KUHITIMU MASOMO YA UZAMILI ILICHELEWA KUMFIKIA
Barua hii ilimfikia
Septemba 2006 ikimweleza kuwa kuanzia
tarehe 23 june 2006, alipanda ngazi kutoka B kwenda D. Kwa hiyo taarifa hizi alizipata mwezi wa 9
Ikumbukwe kuwa kabla ya Septemba 2006, tayari mhusika alikuwa amepata barua ya nyingine kupanda ngazi kwa kawaida (promotion) ambayo ilisema kuwa kuanzia
Julai mosi 2006 mhusika alikuwa amepanda ngazi kutoka B kwenda C, kitu ambacho kilikuwa ni contradiction kwa sababu
By 23 June 2006, (
wiki moja kabla ya Julai mosi 2006)
ngazi ya mhusika ilikuwa tayari imeshabadilika na kuwa D isipokuwa tu ni kwamba barua ya mabadiliko hayo ilikuwa bado haijamfikia
- Kwa hiyo by Julai mosi 2006, ngazi ya mhusika ilitakiwa ibadilike kutoka D na kuwa E na si vinginevyo
- Hata hivyo, hli hii haikuwa hivyo kutokana na ukweli kwamba barua iliyotakiwa kuwahi, yaani ile iliyokuwa inampandisha kutoka ngazi B kwenda ngazi D kuanzia tarehe 23 juni 2006, ilichelewa kumfikia; ilimfikia Septemba
- Wakati huo huo, barua ya promotion ya Julai mosi 2006 (ambayo ilitakiwa iiwe ya ifuate baada ya ile ya tarehe 23 June 2006); ndiyo ilikuwa ya kwanza kumfikia na ile iliyotakiwa kumfikia kwanza ndiyo ikawa ya pili kumfikia
BAADA YA KUONA HIVYO, MHUSIKA ALIAMUA KUUFUATILIA MCHAKATO MZIMA WA BARUA HIZI MBILI KWA KUUKUMBUSHA UONGOZI HUSIKA, KUWA KUNA MAHALI WALIKUWA WAMEPITIWA
Baada ya mhusika kugundua makosa kwenye barua hizo mnamo Septemba 2006, mhusika aliamua kuujulisha uongozi husika kwa kuandika.
Baada ya hapo uongozi uliamua kuzibadilisha barua hizo na kuwa hivi
Ile ya kumpandisha kutokana na kuhitimu masomo yake ya uzamili ilirekebishwwa na hivyo badala ya kumpandisha kutoka ngazi B kwenda ngazi D, ikawa inampandisha kutoka ngazi B kwenda C kuanzia 23 Juni 2006
Baada ya hapo, barua ile ya kumpandisha kutokana na muda aliotumika kwenye ngazi husika (
promotion) ikawa sasa inampandisha kutoka ngazi C kwenda D
Kwa hiyo mchakato wa awali uliokuwa umempandisha hadi ngazi E ukawa umefutwa,
akawa amenyang’anywa ngazi E na kurudishwa ngazi D na hivyo kushushwa cheo kwa mara ya kwanza
…………………………..inaendelea