Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha Sitasahau cha Radio Free Africa

Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha Sitasahau cha Radio Free Africa

Kama unadhani nimetumia program yoyote kuibadili hii story nakujuza si kweli,nimeandika kwa mkono wangu kipande kwa kipande,sitaki kujisifu ila ninajitahd ktk upande wa kuandika tena natumia simu tu wala si computer,kuna story km 3 nimeshazidownload ila changamoto ni muda tu
Du, Basi umeutoa sadaka muda wako, siyo mchezo. Mungu akubariki
 
MKASA WA KUSISIMUA WA ROJAZ:
katika kipindi cha sitasahau cha radio free Africa



Sehemu ya 4



Kitendo cha kuwa huru kiukweli nilimshukuru Mungu sana na kujisemea peke yangu moyoni kuwa ukimuona mtu anamfanyia hila mwingine na kupelekea huyo mtu kupelekwa jela ujue huyo sio mtu mzuri katika maisha yako,nilishukuru kwa kuwa haki imetendeka na imebainika kuwa kuwa mimi sio mhusika wa lile tukio ingawa haikuwa ndani ya siku moja au mbili lakini ukweli umejulikana,nimerejea sasa uraiani na maisha yanaendelea na nashukuru kwa uhuru nilionao kuweza kujiamulia mambo yangu,ndugu jamaa na marafiki walijitokeza wenye kunipongeza,wenye kunipa pole yote hayo niliyapokea lakini nina ahadi mimi nilimuahidi mtu nikiwa kule gerezani,huyu mtu nimekutana nae gerezani,huyu mtu aliniomba sana niende kuitembelea familia yake alinipa maelekezo tena alizungumza nami mengi kuhusiana na familia yake hasa kuhusu watoto wake kuwa kuna mwanamke ambaye alizaa nae hao watoto lakini kwa wakati huu hawako kwenye mahusiano na pia ana mchumba wake kwahiyo haya maelekezo yote nilikuwa nayakumbuka nyakati hizi wakati nipo uraiani,zilipita kama wiki tatu hivi nikawa nasikia kama mzigo ndani ya moyo wangu kwanini niahidi kitu alafu nishindwe kukitekeleza ni kweli kwamba nimeshindwa kwenda kuwaona hawa watoto?

Nikasema hapana na kwakuwa nilikuwa na vijisenti kidogo kwa sababu nimetoka gerezani familia yangu ipo nashukuru walinishika mkono na nikawa hapa nyumbani,nilitumia kapesa changu kidogo kwa kununua nyama kilo moja nakumbukb na nilinunua sukari nusu kilo nilivibeba nikiwa na dhumuni la kwenda kuitizama familia ya mtu ambaye nimekutana nae gerezani na wala sikuwa namjua kabla ya hapo yaani tumekutana gerezani,nikafata maelekezo hadi nikafika lile eneo ambalo nililoelekezwa,kweli nilifika na kweli ndicho nilichokutana nacho,nilikutana na mwanamke mmoja,mwanamke huyo alikuwa mnene na mweupe sana,alinikaribisha na nikamueleza ujumbe ambao nilikuwa nimepewa na rafiki wa kule gerezani,nakumbuka sentensi ambayo alinambia huyu mama "eeh kwahyo amekuambiaje?" Hii ndio sentensi ya kwanza huyu mama alinambia nami nikamwambia "amenituma nije kuwasalimia watoto" akanambia "eeh ukishawasalimia?" Nikamjibu ndio alivyoniagiza kuja kuwasalimia angalau nizungumze nao na kuwaeleza jinsi baba yao anawapenda sana na siku zote anawaombea baraka,akasema "hayo maneno nimeshayasikia sana je yanasaidia nini kwa watoto wangu,yanasaidia nini?

Kiukweli huyu mama hakunipokea vizuri lakini nilishapewa tahadhari toka kule gerezani kuwa huyu mama ni mkorofi sana,sasa kwa sababu nilishaelezwa hayo ilibidi tu niwe mpole,akaendelea kunichamba "kwahiyo uko gerezani hakuna kitu anachona sisi kinatufaa zaidi ya hiyo nyama na sukari,kwahiyo tunaishi kwa ajili ya nyama na sukari? Hao ndugu zake washenzi wasio na maana kila siku napata ujumbe ntasaidiwa ntasaidiwa je nasaidiwa kitu gani? Ameharibu maisha yangu mbwa yule" akaanza kutamka maneno ya kashfa kumuhusu kaka yule na kiukweli ukiniuliza mimi nafahamu mengi kiasi gani kumuhusu yule kaka kule gerezani kiukweli sijui na hauwezi amini ni machache ambayo yeye amenieleza na upande wa pili wa ubaya wake mimi siuelewi lakini ni mtu aliyenifanyia wema nyakati tukiwa gerezani na alikuwa mtetezi wangu katika mambo mengi sababu gerezani kuna maisha yake uko,kuna watu wababe,wakorofi lakini kama kuna mtu anakukingia kifua unamuona huyu ni kaka,kaka mzuri kwahiyo hajawai kunitendea ubaya wowote na inawezekana kweli ni mtu mbaya kwa sababu alishanieleza kuwa yupo hapo kwa sababu alitakiwa kulipia yale yote aliyoyatenda uraiani,anatumikia kifungo anachoamini alistahili,huyu mama alizungumza mengi nami nikawa nimetulia tu namsikiliza na nikamwambia "tuzungumze tu kwani mimi ni mjumbe tu na mjumbe hauwawi,mimi ni mtu mwema tu ambaye nilifungwa na nikakutana na huyu ndugu baba watoto wako,ni mtu ambaye aliniomba sana nitakapotoka nisiache kuja kuwana watoto wake,sasa ahadi nilimpa na toka nimetoka gerezani ilitakiwa nifanye mapema na nimekuwa nikijisikia hatia kwa sababu nimeshindwa kulitekeleza hilo kwa haraka kwahiyo nimekuja ili kuweza kusikia amani ndani ya moyo wangu" nilimueleza hayo na nikapata nafasi ya kuzungumza na watoto,ana watoto wazuri sana,baba yuko gerezani na kwa mtu mwelevu ukitizama mazingira ulikuwa unapata picha kuwa hawakuwa na maisha mazuri kwahiyo mama anajipigania kwa vile anavyoweza na mama mbabe sana huyu maana hata akiongea tu unajua kama huyu mama ni mbabe,niliwambia watoto bac yao anawasalimia sana na anawapenda na siku moja anaamini atajumuika na nyinyi na nakumbuka mtoto wake mmoja mkubwa alinambia kuwa mama yao aliwaambia hawataweza tena kujumuika na baba yao katika maisha wanayoishi nami nikawaeleza kuwa sio kweli kwani baba siku moja atajumuika nao na wataungana nae na kula nae chakula pamoja na furaha itakuwa katika maisha yao ya kila siku.

Nikawaambia mimi ni anko wao na nitakuja mara kwa mara kuwatembelea na kama kuna uhitaji wa vifaa vyovyote vya shule wataniagiza na ntakaporejea tena ntawaletea hivyo vitu,wakaniandikia vitu vyao ingawa nilikuwa siko poa kivile na ukizingatia nina muda mfupi toka nitoke gerezani lakini mazingira yao yalinisukuma tu kuweza kufanya hilo jambo,mimi ni mwanaume tena mpambanaji nimeguswa sana na hii familia hasa hawa watoto,niliondoka nikiwa najisikia deni ndani yangu tena nakumbuka yule mtoto mdogo aliniuliza "utarudi kweli? Utakuja tena kuja kutuona? Nikamjibu "ntarudi na ntaleta hivi vitu mlivyoniagiza kwa ajili ya shule" nikaondoka zangu kurejea nyumbani na nakumbuka pia nilishea hili jambo na kaka nilipofika nyumbani,nilimueleza kaka jinsi nilivyoikuta familia ya yule ndugu wa kule gerezani,kaka alisikitika sana na kusema "maskini hakuwaza kama siku moja atakuwa mbali na watoto wake tazama sasa future ya watoto inaweza kuharibika kama mama atakosa misingi mizuri ya malezi kwa ajili ya watoto,akijichanganya tu anaharibu watoto lakini kama atasimama anaweza kuwalea watoto wake vyema" nikamueleza jinsi nilivyomuona ni kama mama ambaye ameshajichanganya sana na tukasikitika pamoja na nikamueleza jinsi watoto walivyonipa mahitaji yao ya vifaa vya shule lakini bro mimi navitoa wapi? Kaka akacheka na kunambia "ndio ukapambane sasa mwenzetu umeshapata familia eeh msamaria mwema umejikuta umekuwa na familia ya watoto wawili,mimi sina la kukusaidia nadhani unajua kuhusu hali yangu ya kipesa,wewe pambana bwana ahadi umetoa ipambanie" maisha yakaendelea na kaka kule gerezani nilimuahidi ntakapoenda kwa watoto wake ningekwenda kumjulisha maendeleo yao,kwakuwa mi niko kitaa nikaona sio vyema kukaa tu na ni vyema kusaka dili za kufanya kwakuwa maisha lazima yaendelee,katika kutafuta japo videiwaka na ukitilia maanani nimetoka gerezani kuaminika nako kukawa ni mtihani kwa walio wengi maana wengine akijua ulienda ndani anajua kama ulitenda kumbe uhusiki chochote,kuaminika kulipunguwa maana wanahisi unaweza kumpa gari yako ana mikosi gari ikapata matatizo yaani nikawa nakataliwa kihivyo,maisha yaliendelea kuwa magumu japo kaka alikuwa ananiambia "hivi ndivyo ilivyo kwa wewe kujenga kuaminika inahitaji muda kidogo,wako watakaoona una nuksi,wapo watakaona ulihusika kwa namna moja au nyingine ukweli unaujua wewe na Mungu wako lakini ni muda mfupi tu lakini uvumilivu unahitajika ili mambo haya yapite na tuyaruhusu yale mazuri yaje kwetu"

Familia yangu ilinitia sana moyo,ilinifariji sana,kila ninachojaribu kufanya kwangu kilikuwa hakifanikiwi pamoja na kuwa ni dereva mzuri tu hata deiwaka sipati,kuna siku nikaona ngoja nikamcheki mshkaji kule gerezani nikikumbuka pia nina ujumbe kutoka kwa watoto wake nimpelekee zile salamu watoto wake walinipa ,sijafanikiwa katika ahadi ambazo niliwaahidi,nikaenda na nikapata nafasi ya kuzungumza na mshkaji,mshkaji alinambia "umekuja?umekuja kuniona mimi?"

Alifurahi sana, Nikamwambia "ndio kaka si nilikuahidi" akanambia "nilihisi hautakuja maana siku niliona zinasogea na nikaona ahadi zako zitakuwa kama ahadi za watu wengine walizokuwa wakiniahidi" nikamwambia "hapana lazima ningekuja kwani sijawahi kumuahidi mtu kitu cha uongo sipendi kufanya hayo ya kuahidi alafu nisitekeleze,lakini nimerudi uraiani mambo yamekuwa si rahisi" akasema "najua hayawezi kuwa rahisi lazima ujipe muda" nikamwambia "ni kweli,kweli kabisa nimerelax najipa muda" akanambia "mambo yatakaa vizuri,amini Rojaz mambo yatakaa vizuri,niambie kuhusu watoto wangu" ndipo nilipomueleza mazingira niliyowakuta watoto wake ila wako na afya njema tu asiwe na wasiwasi akasema "wamesemaje? Wamenikumbuka?" Nikamjibu "ndio wanaonesha kukukumbuka sana na wanaonesha kukupenda sana" akasema "mama yao anawafanyia ukatili watoto hataki kabisa hata watoto wanitembelee,naumia sana" niliona jinsi anavyosononeka akizungumza hayo nikamwambia "mambo yatakaa tu sawa,nimewaahidi watoto wako kuwa wewe utatoka siku moja utajumuika nao" akacheka,akasema "mmh eeh wakasemaje" nikamwambia "inaonekana kama walikuwa hawana matumaini lakini nilipowaambia nyuso zao zimeonekana kuwa zenye furaha" akanambia "umewaambia vyema,asante nakushukuru sana,umerejesha furaha yangu na umenifanyia jambo ambalo sikuwahi kulitegemea,kwa hii sentensi naomba uamini ninachokisema,umetenda kwangu jambo kubwa sana,nimekuwa nikitamani nikutane na mtu mwenye utu kama wewe lakini hauwezi amini sijawahi kukutana nae" mimi nikatabasamu na kujiuliza hivi kitu gani cha thamani nimefanya hapa,haya ni maisha yangu ya kila siku kwani nimekuwa nikiguswa na watu wenye changamoto za hapa na pale na mimi ni huyu,mimi ndio Rojaz ninapomuahidi mtu kitu ninachoweza kwa hakika kukitenda lazima nikitekeleze kwahiyo nimefanya haya ndio maisha yangu ya kila siku hakuna wema ambao natakiwa nionekane nimetenda wema,haya ni maisha yangu ya kila siku,akanambia "aisee Rojaz nakushukuru sana umepanda kwangu kitu kikubwa sana,Rojaz unaweza kunisaidia kitu?"

Nikasema "ndio mimi niko hapa" akasema "sawa Rojaz naomba sasa ukamtembelee msichana wangu,najua amevunjika moyo,watu wamemvunja moyo lakini naomba ukanipelekee salamu" nikamwambia "nikamwambie nini? Akasema "najua wewe ni mtu mwema we nenda kazungumze nae tu,ukamwambie jinsi tulivyoishi vyema tukiwa huku gerezani na jinsi ambavyo nilikuwa nikimzungumzia vizuri na jinsi ambavyo nampenda,kitu ambacho kinaniuma ni kukosa uhuru na kuishi na mwanamke ambaye ninampenda" nakumbuka nilitabasamu tu aliponambia hayo,nikamwambia "brother siku utapata chance na utaishi na mwanamke unayempenda" akasema "haiwezekani,hawezi kuningoja mie majira yote hayo,najua na sitamlaumu,sitamlaumu hata siku moja" nikamwambia "sawa" ila alifurahi sana,yaani unafanya kitu kwa mtu yaani unamuona anafurahi mpaka unashangaa alifurahi nini kwa kiwango iki na alisema "umenipa furaha isiyo ya kawaida,baada ya hapo nakumbuka niliondoka nakurudi zangu nyumbani na harakati zangu za kudonoadonoa kama kawaida ziliendelea kama kawaida kwa sababu mambo yalikuwa bado hayajakaa vizuri,kweli siku nilipanga na kama alivyonielekeza nilienda,mimi niliombwa kwahiyo kama niliombwa na nilimuahidi kutenda ndio nilienda sasa,kweli nilikutana na huyo mwanamke na nikafanya nilivyoelekezwa kikubwa nilimpa salamu zake nyingi sana na nikamueleza jinsi huyu kaka anavyompenda na jinsi anavyojisikia vibaya kuishi gerezani na kukosa kuishi na mwanamke anayempenda,mwanamke wa ndoto yake,kiukweli yule dada nilimuona ni mtu aliyekwisha mkatia tamaa mshkaji lakini mimi nilimwambia mapenzi ya kweli uwa hayafi,mapenzi ni kuvumilia na kama kweli unampenda utamvumilia na siku moja atakuwa huru na mtaungana tena uraiani na kuishi yale maisha mliyokuwa mkiishi awali,lakini mtu akiwa gerezani na hasa ambao wana miaka mingi gerezani watu wao wa karibu wanakuwa na ukaribu siku zile za mwanzo lakini kadri siku zinavyosogea watu huchoka na huyu ndio binadamu alivyo,atakuwa na bidii sana mwaka wa kwanza,mwaka wa pili,ukianza mwaka wa tatu anaanza kuchechemea baadae aah anaanza kuchoka,anachoka kweli kweli anaona kwani nini na jamii nayo watu wako tofauti,mtu ameshaenda gerezani miaka thelathini unamngoja wa nini,huyo mtu amefungwa kifungo cha maisha unamngoja wa nini ushindwe kuendelea na maisha yako,watu wana mapokeo tofauti mwingine anaanza maisha mapya,mwingine anavumilia lakini unamuona hizi ni dalili za mwisho hizi kachoka kabisa lakini ujumbe mimi kama mjumbe nilifikisha na nilimwambia ntakuwa nakuja mara kwa mara kukusalimia na kukujulia hali kwa namna moja au nyingine lakini ni mwanamke ambaye maelezo yangu aliyapokea kikawaida tu "nashukuru,asante" yaani hivyo.

Nashukuru baada ya muda nikapata gari lakujishikiza kama deiwaka yaani gari lina dereva wake nami nakuwa kama namsaidia pale anapokuwa amechoka,kaka ndio aliniunganisha kwa huyo jamaa mwenye gari nikawa napigapiga mishe ujue ukitoka jela inakuwa sio rahisi kurudisha uaminifu katika jamii inayokuzunguka,ni watu wenye imani kubwa kwako tu ndio watakaothubutu kuweza kukupata tena nafasi ya kukukabidhi gari wao wanajua ni changamoto tu za kimaisha umekutana nazo tena haukuhusika kiukweli inabidi mtu akujue kwa ukaribu sana kama huyu mtu ananipa gari analerax na naenda na kurudi salama,kweli maisha yakawa yanaenda na Mungu akajaalia nikawa napata vijipesa kidogo nakumbuka nikaenda kununua vifaa kidogo nakumbuka ilikuwa ni peni,rula rula,madaftali na nikaenda kuwacheki wale watoto wa mshkaji,nikaenda kuwatizama wale watoto nakuwapatia yale mahitaji na pia nilibahatika kununua na chakula,nilinunua unga,mchele,mafuta,nilinunua nyama,mafuta kile kidumu kidogo yaani nikaenda safari hii angalau na kifurushi,vifaa vya watoto nilibeba hivyo vichache ingawa waliniandikia vingi,najua mazingira ya pale vyakula ilikuwa ni kitu bora zaidi kukipa kipaumbele katika nilivyochukua,nimefika Mungu mwema nikamkuta na yule mama na akanambia "umekuja tena?" Nikamwambia "ndio bwana nimekuja tena,nimekuja kuwaona hawa ndugu zangu" ilikuwa ni siku nzuri tena ukitilia maanani ilikuwa ni jumamosi wakanambia anko umekuja? Yaani walinikumbuka,nikawaambia "

Si mnakumbuka niliwaambia kuwa ntakuja? Mambo kati hapa hayakuwa rahisi sikupata pesa haraka yakununua vitu ndio maana nikachelewa lakini nimekuja" nikawapatia vitu vyao na chakula,awamu hii yule mama angalau alinipokea vizuri akasema "eeh una ujumbe gani mwenzetu" nikamjibu "sina ujumbe wowote nimekuja tu kwa ajili ya kuwaona hawa ndugu zangu" akasema "haya tunashukuru" nikazungumza na watoto nakuwakabidhi vitu vyao japo sikuwa nimewakamilishia nikawaambia kuwa nitakuja tena na waandike vingine wanavyovihitaji,kwahiyo vile ambavyo sikuvinunua wakaandika na vingine ndio maana kaka anasema mwenzetu umekuwa na familia siku hizi lakini ni mzigo ambao niliubeba ndani yangu kwa kuwaona hawa watoto ambao hawana hatia yoyote,niliondoka hapo nikiwa na furaha kwelikweli na nikiwa na amani sana kwamba leo mimi nimefanikiwa kuwapa chakula watu ambao pengine wangekula mlo mmoja au kesho labda wangekula mlo mmoja au wangeangaika kwenda kuombaomba lakini mimi kwa mchele kidogo,kwa mafuta nimewastili siku mbili tatu watapata chakula kizuri,nilirudi kwa furaha na nikalala usingizi mzuri sana.

Pilikapilika ziliendelea na huku nikiendelea kumuelezea kaka kile kinachoendelea kuhusiana na mimi kwenda kuwatembelea hawa watoto,nilienda tena kuwatembelea hawa watoto,na nikaenda tena,nakumbuka nilienda kama mara tano kwenda kuwatembelea hawa watoto na kila ninapoenda kile nilichobarikiwa naenda kuwapelekea,sasa wameshanizoea na huyu mama alishanizoea hata siku moja alishaniambia "wewe ni rafiki wa baba ...(akitaja jina la mtoto wake) ina maana mmejuliana gerezani,unamjua mtu huyu?" Nikamwambia "sitaki kujua chochote ninachojua ni mtu mwema,tulipokuwa gerezani tumeishi vizuri na hili ni ombi lake kwangu na kwa sababu mimi nipo uraiani hawa wamekuwa kama wadogo zangu"
Muda ukaenda baada ya kuwatembelea hawa watoto na nikaona sasa ni wakati wa kwenda gerezani kumsalimia ndugu yangu,ameshakuwa ndugu yangu angalaunimpashe jinsi mambo yanavyoenda uko uraiani na jinsi watoto wake wanavyoendelea vizuri na maisha yanaendelea,nilipofika gerezani awamu hii na kupata nafasi ya kuzungumza na huyu kaka ambaye mimi nilimkuta gerezani na kumuacha uko viko vitu aliniambia nilishangaa sana!




Itaendelea!
Nashukaaa nayo
 

Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha sitasahau cha radio free africa​


sdhemu ya 5


Katika maisha yangu ya kila siku nimekuwa ni mtu wa kujali sana matatizo ya jamii inayonizunguka na wanajamii kwa kiasi kikubwa walinifahamu hivyo kwahiyo nilivyokutana na huyu mtu gerezani na jinsi alivyokuwa nami kama kaka nimebeba hiyo roho yakuwa sehemu ya kwenda kumtembelea yeye mwenyewe na pia kuwatembelea watoto wake,huyu mtu yupo ndani lakini muda wote akili yake ipo uraiani anawawaza sana watoto wake,anawawaza sana wapo katika mazingira gani kwa sababu anajua mwanamke ambaye amepata nae hawa watoto akili yake kidogo haina utulivu,nakumbuka awamu hii nilipoenda nilienda kumpasha kuhusiana na maendeleo ya watoto wake kuwa wanaendelea vizuri na kumpasha habari nyingine nyingi nilizokuwa nazo kuhusu uraiani na harakati ambazo nimekuwa nazo huku nikimtia moyo huyu ndugu yangu kuwa asikate tamaa mambo yatakaa sawa wala asiwaze sana ajue tu familia yake inaendelea vizuri,katika mengi ambayo nilimueleza ya huku uraiani alinambia "nakuamini,nakuamini sana" nikamwambia "asante" akanambia "unajua niko huku gerezani ni muda sasa na sijawahi kukutana na mtu amenipa matumaini kama wewe,unajua niko huku gerezani toka yule mtoto wangu mdogo akiwa bado ni kichanga" nikamwambia "nakuelewa,nakuelewa" akasema "unajua ndugu zangu wamejua nimepotea huku,nimeishia huku sijawa na mtu wa kumuamini naomba nikuamini" nikamwambia "karibu na uwe na amani" baada ya maneno haya alinishukuru sana.

Shukrani ilikuwa ni sehemu ya utaratibu wake kila tulipokuwa tukiongea na hata siku hii aliponishukuru sikuona kama ni jambo jipya kwakuwa amekuwa akiniambia mara kwa mara,akaendelea kunambia "toka ndani ya moyo wangu nimetokea kukubeba na kukupenda zaidi ya ndugu,naomba nikushirikishe jambo ambalo sijawahi kumshirikisha mtu yoyote katika maisha yangu,naomba nikushirikishe jambo ambalo nilikuwa nilifanye nikiwa uraiani lakini sikubahatika kulifanya" nikamuuliza "ni jambo gani" akanambia "linahitaji uaminifu baina ya mimi na wewe" nikamwambia "haina shida,haina shida" akanambia "basi nenda kajifikirie" nikamwambia "niambie tu wewe niambie lakini naweza kukusaidia kama si jambo baya" akanambia "wala si jambo baya" nikamwambia "sawa nieleze tu" nilimlazimisha anieleze kwa sababu nitakuja tena huku lini,lini ntakuja kwa sababu nami sasa hivi nimekuwa ni mtu ambaye napambana na mishemishe zangu unajua,akanambia "sawa,nataka nikubadilishie maisha yako" nikatabasamu,nikamwambia "mimi? Unibadilishie maisha mimi?" Akasema "ndio,kwani mimi nikiwa gerezani nashindwa kubadilisha maisha ya mtu mmoja uraiani?

Nikacheka na nikamwambia "hata sikuelewi unamaanisha" akasema "namaanisha ninachokisema,unakumbuka nilikwambia umekuja gerezani kwa ajili yangu?" Nikatabasamu na kumwambia "unajua sikuelewi unachosema" akasema "utanielewa" katika harakati zangu nilitamani maisha mazuri,nilitamani maisha mazuri,maisha bora lakini sikuweza kutimiza ndoto zangu najikuta niko katika maisha ambayo sikuwahi kuwaza kama nitaishia uko lakini pengine maisha yangu naweza nikamalizia uko,sijui ni neema gani yaweza ikaja kwangu na nikatoka,nikamwambia "kwanini unasema hivyo,kwanini unasema hivyo na wakati haya mambo tumeshakaa na tukayazungumza unatumikia kifungo chako na kina miaka tajwa" akasema "hauwezi kuelewa,elewa hili ninalosema nataka kukubadilishia maisha yako na ulikuja gerezani kwa ajili yangu" alinambia nirudi nyumbani na niendelee na harakati zangu na nije tena,nikamwambia "unaniweka njia panda sana mshkaji wangu sielewi hata unachomaanisha,hivi mtu aliyeko gerezani anawezaje kumbadilishia maisha mtu niliyeko uraiani? Ambapo mimi napiga mishemishe,napambana na maisha,ujue gerezani mtu unakaa tu,unakaa tu unawezaje kubadilisha maisha yangu mtu namna hiyo?" Alinambia tutangea na kunisisitiza nisiache kwenda kuwatizama watoto wake nami nikamwambia "usiwaze kuhusu hilo na uwe na amani tu ujue umepata mdogo wako ambaye yupo pamoja nawe hata kama uko gerezani uko pamoja na mimi,usiendelee kunung'unika kuhusu ndugu zako ambao wanaona wewe umeishia huku gerezani Mungu ana njia zake za kuinua ndugu basi ujue na mimi Mungu ameniinua niwe ndugu yako,nitafanya hayo kwa moyo wangu wa dhati" nilimwambia hayo na baada ya muda niliondoka zangu lakini niliyawaza maneno aliyonambia,mtu huyu ni mfungwa tu,mfungwa tu wa kawaida na katika nafasi nilipoingia hapa gerezani na nilipokuwa ninaishi hapa nilimuona ni mfungwa tu ambaye ni mtu mbabe mbabe kwa sababu sio mtu wa kuonewaonewa unajua maisha ya uko kuna watu wababe,watu ambao wana nguvu zao yaani yeye hakuwa mtu wa kuonewa na alikuwa mtu wa kutetea wengine kiufupi nilimuona ni mtu mwema kwa muda wote niliopata nafasi yakuwa nae gerezani lakini kwa habari yakunibadilishia maisha kiukweli ni kitu chakuchekesha unajua yaani nilikuwa nikicheka tu.

Nilirudi uraiani na maisha yalikuwa yanaendelea nilikuwa nikiendelea kupiga mishe zangu kwa sababu sasa hivi si haba japo sijapata gari rasmi napiga tu mishe za udeiwaka japo si haba napata chochote,toka nimetoka kule gerezani ulipita kama mwezi na nikapata nafasi ya kwenda kuwatembelea tena wale watoto,nilienda kuwacheki na kuwapelekea vizagazaga kidogo sawa na kipato changu ambacho napata,wakanambia "anko umekuja tena?" Hii sentensi huyu mtoto alikuwa anapenda kuniambia hivi nami nikamuuliza "ulidhani sitakuja tena? Akanambia "nilidhani hautokuja tena" nikamuuliza "kwanini?kwanini unawaza hivyo? Nilishawaeleza mimi ni anko wenu ambaye nitakuwa nakuja mara nyingi sana,mnaendeleaje?" Lakini pia niliwapelekea mahitaji ya hapa na pale kwa ajili ya shule na walifurahi sana na huyu mama sasa kishajua kama nakuja kwa ajili ya kuwatembelea watoto kwa ajili ya rafiki yangu ambaye alikuwa ni mtu wake ambaye hawako tena kwenye mahusiano kwa sababu wao wenyewe wanazijua,nilizungumza na watoto lakini pia nilizungumza na huyu mama na kikubwa nilimwambia "kwanini siku usitenge muda wa kwenda kumuangalia mwenzio gerezani" kwa mara ya kwanza nazungumza na huyu mama sentensi kama hiyo akasema "mimi nikapoteze muda wangu kudili na mtu aliyeniharibia maisha yangu? Nikamwambia "ujue watu ukosea lakini na watu hujirekebisha,unajua watu hujirekebisha sana wakiwa gerezani? Watu wanabadilisha nienendo yao na inawezekana alipokuwa uraiani hakuwa mtu mwema lakini kule ameshabadilika" akasema "hawezi kubadilika yule mtu,hawezi kubadilika yule mpaka mwisho wa dunia,hawezi kubadilika,mbaya yule kuliko unavyodhani na nashangaa unaangaika kumsaidia mtu yuko gerezani na ataozea uko,nakuangalia tu nione hatua zako zitaishia wapi" aliniambia hayo maneno yakunivunja moyo nami nakumbuka nilimwambia "mtu anaweza kuwa mbaya kiasi gani yaani hadi asiweze kuonewa huruma na kwenda kutembelewa" alinambia "mwanaume mbaya sana amenipotezea maisha yangu na kunipotezea muda,ebu tazama wakati mimi niko nae kumbe yuko na mwanamke tena amekwenda hadi kumtambulisha kwao naye ameshakwenda kutambulishwa hadi kwa huyo mwanamke na wako katika hatua flani za uchumba lakini mimi huku kashanipa tena ujauzito,amenifanya nimeishi maisha magumu sana ya ajabu,namchukia sana na siwezi kunyanyua mguu wangu kwenda kumtizama shetani kama yule hata siku moja" yaani mtu huyu anavyotafiriwa unaona si mtu mwema na kuna sentensi ambazo nimekutana nazo nikiwa gerezani "huyu mtu uko nae karibu kivipi? kama hatafsiriwi kwa wema lakini kiundani kwanini mtu huyu si mwema lakini yeye mwenyewe anasema yupo anatumikia kifungo kwa sababu yeye mwenyewe amestahili wala hajaonewa na yoyote,ni malipo ya madhambi yake,nilimsikiliza huyu mama maneno na hasira zake lakini mimi sio yaliyonileta,hata kama baba yao ni mbaya hawa watoto sio wabaya kwahiyo ntazidi kuja kuwaona pale ntakapopata nafasi hata kama navunjwa moyo na mama yao nitajipa moyo kwa sababu nimewapenda hawa watoto nitakuja tena na tena kuwatizama.
Niliaga na kwenda kuendelea na mishe zangu na maisha yangu yakawa yanasonga mbele na siku zikasogea ikapita kama miezi mitatu niko na mishe zangu sikupata nafasi ya kwenda kuwatizama wale watoto wala sikwenda kule gerezani niko na mambo yangu naendelea,nakumbuka siku moja nikasikia kuwiwa sana kwenda kuwatembelea wale watoto,nilienda lakini nilimkosa huyu mama,nilipouliza kwa majirani nikaambiwa yule mtoto mdogo anaumwa,anaumwa sana na amelazwa,kwahiyo nikafatilia hadi kujua wamelazwa wapi,nikaenda kwenye hiyo hospitali na nikamkuta yule mama pamoja na baadhi ya ndugu zake wakiwa katika hali yakumuangaikia mtoto walisema amepata amoeba sijui nini mambo ya watoto basi nami nikawatia moyo nikasema "nilikuja kuwaona na isitoshe mambo yamekuwa ni kukimbizana muda umepita sana sijaja" huyu mama akasema"nilijua hautakuja tena unadhani utakuwa unakuja kutuangalia kila siku kwa maagizo ya huyo mtu ambaye yuko gerezani ambaye atafia uko gerezani" nikamwambia "siji kwa sababu ya rafiki yangu wa kule gerezani,nakuja kwasababu nimeshakuwa na urafiki na hawa watoto" aliniangalia tu huyu mama lakini hali ya mtoto haikuwa mbaya sana basi nami kwakuwa nilipata taarifa ya mtoto kuumwa nikawa nakuja hadi pale aliporuhusiwa na kurudi nyumbani nami nikaendelea na mishe zangu lakini nilitafuta muda siku hiyo nikajisikia tu nikaenda gerezani kwenda kumtizama mshkaji,kweli nilipata nafasi ya kuzungumza nae,nilimpelekea sabuni na vitu vichache vichache na akanambia "mbona umechelewa sana kuja mshkaji wangu?

Nikamwambia "kwanini? Akanambia "mbona nilikwambia uje tuzungumze" nikamjibu "unajua mambo uko uraiani ni kupambana sana,mambo yamekuwa mengi mshkaji wangu unisamehe bure ila nilipata nafasi nilikwenda kuwatizama watoto nikakuta mtoto wako anaumwa" akasema "nini tena? Ina maana taarifa hana,hana mtu wakumpelekea taarifa,yaani watu walishamkataa yaani yuko tu huku hana taarifa zozote lakini nikamwambia usiwaze kwani anaendelea vizuri kwa sababu alipatiwa matibabu nami nilikuwa naendaenda pale kwakweli anaendelea vizuri mpaka ameruhusiwa amerejea nyumbani,yaani mtoto anaendelea vizuri kabisa wala usiwaze" akanambia "aisee nashukuru sana,nashukuru sana ndugu yangu,nakushukuru mno na asante sana kwa vitu ambavyo umeniletea" nikamwambia "wala usijali,karibu" akasema "najua moyo wako iko siku utachoka kuja kunitembelea,najua utachoka na hautakuja tena" nikamwambia "sijui,lakini ndugu yangu nikuahidi pale nitakapopata nafasi nitakuwa ninakuja" akasema "lakini naomba tuendelee na mazungumzo yetu ya siku ile tulipoishia " nikamwambia "nakusikia" akanambia "tuliishia pale nilipokwambia nataka kubadirisha maisha yako" nikamwambia "nakumbuka" akanambia "hujaiwaza hiyo sentensi? Nikamwambia "sijaiwaza chochote,kwasababu unaweza wewe kunibadilishia maisha wakati wewe mwenyewe umekosa uhuru na upo tu unafanya kazi za humu ndani,unawezaje kunibadilishia maisha mimi ambaye niko uraiani na nina mwanya wakubadilisha maisha yangu mimi mwenyewe" akasema "ni kweli umesema vyema lakini mimi nimekaa hapa ni kwa sababu nimekosa uhuru wakufanya kitu lakini natamani nifanye kitu nikiwa uraiani" nikamwambia "utawezaje sasa? Akanambia "nataka wewe ukafanye" nikacheka,nikamwambia "kufanya nini? Akanambia "ninao utajiri" nikacheka yaani ni mambo yakuchekesha,nikamwambia "yaani wewe unao utajiri wewe? Akasema "hakuma mtu anajua kama mimi nina utajiri mwingi" nikamwambia "eeh niambie kuhusu utajiri wako" akanambia "hii ni siri nazungumza na wewe na sijawahi kuzungumza na mtu yoyote,natamani uwe rafiki yangu,ndugu wangu wa damu,sina mwingine wa kumuamini moyo wangu umesukumwa na wewe na hata nilipokuwa gerezani nilikuwa nikiomba Mungu usiku na mchana anipe mtu ambaye si ndugu moja na mimi lakini akamfanye awe ndugu yangu,akatimize ndoto zangu uraiani,hivi unajua ni kama vitu visivyoeleweka" nikamwambia "haya nambie,nambie kuhusu utajiri wako" akanambia "ninazo pesa nyingi zakuweza kubadilisha maisha yako,nyingi hata zakuweza kubadilisha maisha ya familia yako lakini niahidi hautawaacha watoto wangu,utawabeba nakuwatunza na kuwalea,utawasomesha,utamsaidia na mama yao,utamsaidia na msichana wangu lakini niahidi,niahidi kitu kimoja,hautamgusa yule mwanamke,utamuacha ataolewa na mtu mwingine,mimi sitaweza kumuoa lakini wewe usimuoe,aolewe na mtu mwingine na msaidie akiwa na matatizo"
Mimi ninayasikia haya,unajua ni kama mambo yasiyoeleweka narudia tena kwa sababu mtu anawezaje kunambia maneno hayo,ananipima? Tunazungumzia habari za pesa ambazo niko huku napambania kweli na udeiwaka mtu ananambia nina utajiri,niliyasikia haya maneno kutoka kwa kaka huyu ambaye tulikutana gerezani na kuishi kama familia na leo ninapoelezwa haya mambo ya pesa na utajiri na mfungwa aliyepo gerezani ananiambia nimuahidi kwanza sikuamini,niamini vipi,niamini vipi kirahisi? Kwanza nikabaki nikitabasamu kwa sababu nimekuwa nikitabasamu hivyo na akanambia "mimi sikutanii na siko kwa ajili ya matani na mimi nilisogea na kuzungumza na wewe toka ulipofika na nikakutana na wewe,nilikuja kwa sababu ya kusudi maalum ili unikamilishie ndoto zangu,wafanye watoto wangu kuwa bora,waishi katika nyumba nzuri,wafanye watoto wangu kuwa watu wa thamani,mama yao pia,sikwambii sana kuhusu ndugu zangu endapo ukiguswa waweza fanya hivyo lakini huu utajiri nakupa wewe,nakutunuku wewe" sasa mfungwa aliyeko
gerezani anawezaje kuwa na pesa,"pesa ziko wapi? Nakumbuka nikamwambia "unanambia mambo mazito yaani sijawahi hata kusikia mtu aliyeko gerezani anaweza kumpa utajiri mtu aliyeko uraiani,basi mimi naweza nikawa nimebahatika ila ndugu yangu nashukuru sana ila huo utajiri sidhani kama mimi nafaa kuupata,naogopa sana vitu hatarishi katika maisha yangu,natamani kufanya vitu vya halali tena vya haki,sitaki matatizo katika maisha yangu,umeniona nimetumikia kwa muda gani hapa gerezani ilihali sijatenda lolote,maisha yangu yalirudi nyuma sana,harakati zangu nilizokuwa nazo zikarudishwa nyuma,unataka na mimi niishie gerezani kama wewe?

Inaonekana maisha yako uraiani hayakuwa mema wewe mwenyewe umesoa unatumikia kile ambacho wewe umestahili kutumikia je unataka na mimi niyaishi maisha ambayo wewe umeyaishi yakakufanya hadi uje gerezani? Akasema "hapana,sio kweli,sio kweli na haijalishi kwa sababu mimi nilikuwa mbaya basi na pesa yangu itakuwa mbaya,unajua nini mimi natamani kufanya,natamani pesa yangu ikafanye mambo mazuri mema" nikamwambia "pesa yenyewe iko wapi? Tunazungumza,tunazungumza nini kwani? Yaani pesa iko wapi unayozungumza wewe? Akanambia "pesa ipo na nataka uniahidi katika mambo niliyokwambia kwa sababu ukitoka hapa unaenda kuchukua pesa kwahiyo ahadi yangu inabidi unipe leo na ahadi yangu nataka uape mbele ya Mungu ya kwamba unaniahidi hata kama mimi kesho nitaondoka ahadi yako kwa Mungu isimame na ikuhukumu kama utaenda kinyume na hayo,mimi nataka kukupa utajiri leo,leo nakupa utajiri,niahidi,najua hauwezi niahidi kwa maandishi lakini kwa kinywa chako niahidi ,niahidi utatunza ahadi hiyo mpaka pale mwisho wa safari ya maisha yako" nikamwambia "kaka we usiongee sana we nambie" akasema "siwezi kuzungumza zaidi ya nilichosema niahidi utawatunza watoto wangu" nikamwambia "ndio nakuahidi nitafanya hivyo" niahidi utamtunza mama wa watoto wangu yaani wale watoto mama yao" nikamwambia ndio nakuahidi, "niahidi utamsaidia mwanamke niliyempenda na kutamani kuishi nae nikiwa uraiani,mwanamke wa ndoto zangu" nikamwambia "ndio" "lakini niahidi huyo mwanamke hautamfanya kuwa mwanamke wako,utamuhudumia na kumsaidia na atakwenda kuolewa na mwanaume anayemtaka yeye lakini sio wewe" nikamwambia "ndio" akasema niapie mbele za Mungu,mimi niko gerezani sasa namjua Mungu,najua mtu ukiapa mbele za Mungu hiyo inasimama kweli" nikamwambia "mbona unanipa vifungu vigumu hivyo kwanini tuape Mungu hapa?

Akasema "niapie mbele za Mungu" haya yalikuwa ni mazungumzo na huyu mtu ambaye amenambia atanipa pesa na hizo pesa ziko wapi? Ananipa katika mazingira gani? Anasema anataka kunipa utajiri abadilishe maisha yangu!


Itaendelea!
Nashuka
 

Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha sitasahau cha radio free africa​



Sehemu ya 7





Macho yalipoizoea hali ya kile kijumba ndipo nilipoweza kukiona kile kitanda cha kamba na kukisogelea kwani yule ndugu aliniambia hazina ilikuwa imefukiwa chini ya kile kitanda,nikakiweka pembeni na kuanza kutindua pale usawa wa kile kitanda,ardhi haikuwa ngumu kiasi cha kunipa tabu kwani nilitoka nje na kwenda kuchukua kijembe kidogo kwa kunisaidia katika kuchimba,nikachimba kiasi kama cha mita moja nikasikia kitu kama mlio wa bati hivi,nikangea spidi ya kuchimba,nikachimba,nikachimba na nikakutana na kitu kama tranka,matranka yale kama wanayobebea wanafunzi wanaokwenda shule za bweni sasa nikawa nachimba kwa pembeni kuweza kulitoa mule shimoni,nikakumbuka maneno ya yule ndugu kuwa kuna "hazina" na ndipo nilipoamini ukweli wa maneno yake,alichoniambia ni kweli kwa sababu nimeona tranka na lilikuwa tranka kubwa sana.

Nikiwa naendelea kuchimbua ili kulitoa lile tranka kuweza kuipata hiyo hazina niliyoelekezwa na rafiki yangu,nikakumbuka kuwa alinambia kitu cha kweli,nilifanikiwa kulitoa huku jasho likinitoka kwa hofu na moyo ukinidunda ndipo nikagundua kuwa tranka alikuwa moja katika lile shimo,hili tranka lilikuwa na kufuli ambayo ilmeshakuwa na kutu kabisa tena kufuli gumu kabisa,kuna tranka jingine nalo pia ni kubwa na pia lina kufuli kama ya hili la mwanzo,kuna nini ndani? hilo likawa kitendawili kingine na utaratibu wake mwingine wakujua baada ya kuzing'oa hizi kufuli ili kuweza kujua kuna nini ndani na nawezaje kuondoka na mizigo kama hii hapa kijijini na nikatoka salama? Nakumbuka alinambia "tumia akili yako ya ziada,fanya unavyoweza hakikisha unakuja na mzigo hapa alafu njoo tutazungumza" haya ndio maneno aliyoniambia,sijui kuna nini ndani,lazima nijue kwani nitawezaje kubeba mzigo ambao sijui nimebeba nini ndani,vipi nikikamatwa wakati sijajua natoa maelezo yapi kuhusu haya matranka? Wakati naangaika kulitoa tranka la pili mule shimoni ndipo nikaja kugundua kuwepo tena kwa tranka la tatu kwenye lile shimo,kiukweli woga uliniongezeka na nikawa najisemea peke yangu ni nini hiki huyu ndugu alikifukia humu? Nikifikiria mazingira hayo yalivyo na ukubwa wa yale matranka na idadi yake kiukweli hofu ilinivaa sana,nayatoaje haya hadi kuweza kuyafikisha mjini? Inaonekana huu mzigo pengine umewekwa muda mrefu sana,muda ule ule niliona ni vyema kutafuta namna ya kuhakikisha kujua kuna nini ndani yake na kwa sababu nilikuwa nimeshayatoa katika lile shimo na sijapata kujua kuna nini ndani ikanibidi niyarudishe mule shimoni na kujipanga upya kwani nimejua kuna matranka matatu kilichobaki ni kujua kuna nini ndani ndio mtihani unaonikabili,nikayarudisha na kufikiria kama ni suala la usafiri au nini ili nitafute njia ya kutoka na huu mzigo hapa.

Nikatoka pale katika kile kijumba na kurudi katika mazingira yale na ilipofika muda wa jioni nikaamua kwenda pale senta na Kaombwe hakuwa amerejea,niliamua kwenda senta kwakuwa niliamini vitu vingi naweza kuvipata katika mazingira yale,nilipofika pale nikaenda kwenye kijiwe ambacho kuna magari wanafanya kama taxi na nikamkuta kijana mmoja nikaongea nae na kiu yangu ilikuwa aniazime gari lakini sasa nani ananijua? Ataniamini vipi kuweza kunipa gari lakini nikamuomba nikamwambia "kuna mzigo nataka kuuchukua lakini naomba hii gari nataka kuiendesha mimi kana kwamba mimi nina ndugu yangu na rafiki yangu na vitu kama hivyo" akaniuliza "una vitu gani?" Nikamwambia "nina mazao yangu nahitaji kuyafikisha mjini nitakulipa,nitakulipa pesa nzuri iwapo utanikubalia" kwakuwa nilikuwa na vijiakiba vyangu vya pesa na ujue thamani ya pesa inabebwa na mazingira kwani 5,000 kwa matumizi ya mjini ni tofauti na mazingira yale ya kijijini kwani kijijini inakuwa na nguvu sana,kuna kiasi cha pesa nikamtajia na yule ndugu alistua na kuona mbona nimemtajia pesa kubwa hivi lakini kwa mimi nilikuwa naona ni pesa ya kawaida.

Baada ya maongezi na kukubaliana nikatoka nae hadi pale kwa shangazi ambaye alikuwa amesharudi kutoka shambani, nikamtambulisha shangazi kuwa huyu ni ndugu yangu na niliona vyema kwenda kumsalimia na shangazi akaniuliza "ana gari?" Nikamjibu "ndio ana gari na anaitumia kwa mambo yake na atakuwepo around hapa" lakini lengo langu lilikuwa niichukue hii mizigo niipandishe katika hii taxi lakini bado hadi wakati huo sijajua ndani ya yale matranka kuna nini lakini inabidi nichonge mchongo na huyu mtu na nikamwambia "mimi nina mazao yangu,mazao yangu nataka niyasafirishe lakini mfumo nitakaotumia nimeyahifadhi katika matranka" akasema "mazao gani unayahifadhi katika mtranka?" Yaani kama akashtuka hivi na kule kushtuka nami kama akawa amenishtua akili yaani kweli naweza kusema kwenye matranka makubwa kama vile nimebeba nini,nimebeba nini,yaweza kuhatarisha hata usalama kwa sababu hata mimi mwenyewe sijajua umo ndani kuna nini,basi nikamseti na kumuahidi nitamlipa kwa sababu mimi nimebobea kwenye mazao nataka tufanye kazi nachukua kupeleka mjini,naye akasema "yaani mimi wakati wowote niko tayari" kwahiyo siku hii niliyokuja naye na kuona mazingira na kupiga stori na kuyajenga nikamwambia "naomba uje kesho" yaani siku inayofuata aje,aje kesho nafikiri aje tuchukue mzigo na tundoke nao kwa sababu alistuka namna ya njia ya ubebaji wa hayo mazao katika matranka,kiukweli sikutaka kulichangia kwani niliona kabisa linaweza kuniletea matatizo uko mbele ya safari.

Siku iliyofata nikajiwahi kabla yule mwenye gari hajafika nikajipa kazi mimi binafsi ya kuyafungua nijue je kuna nini ndani ya yale matranka,nilitumia akili ya ziada nikapata muda ndipo nilipofanikiwa kufungua tranka moja,nilipofungua lile tranka nilisisimkwa mwili mzima na kuanza kutetemeka,nilipatwa na hali ambayo sikuwahi kuipata toka kuzaliwa kwangu na nikawa najiuliza ni nini hiki,ni nini hiki? Mikono inanicheza,moyo inanienda mbio,miguu inapoteza uimara wake wa asili! Nilikuta pesa,nlikuta pesa,nilikuta pesa! Hili tranka ni kubwa na ninaposema ni kubwa elewa ni kubwa sio yale matranka madogo na lilijaa pesa alafu pesa zimepangwa,pesa zimepangwa umo alafu hilo ni tranka moja kati ya yale matranka matatu na hili tranka ni kubwa sasa nikawa najiuliza "hivi hizi pesa ziko mpaka chini? Mpaka chini kuna pesa?" Nilipatwa na mshangao pesa zimehifadhiwa mashambani huku,unajua watu wanahifadhi pesa benki maana uko ndio kuna usalama zaidi kwanini pesa zihifadhiwe chini ya ardhi,zichimbiwe uko na ziweke kwenye matranka,nilifunika,nilifunika haraka na nikasema kweli hii ni hazina,kweli na imekuwaje mtu huyu aniamini mimi na sio ndugu zake na ndugu zake wana shida kama nilivyokwambia maisha ya huku kijijini,yaani wana shida sana na kwanini aniamini mimi kwa kiwango hiki,sikuweza hata kupumzika,sikuweza hata kutulia nilijisikia roho yangu inaangaika,moyo unapaparika,pesa ni kitu cha ajabu sana na ukiwa haujawahi kukutana na pesa nyingi kama mimi hizi nilizokutana nazo,ukikutana nazo unastuka alafu kama unajua hizi pesa zinakuwa mikononi mwako,unaweza kupata wehu! Pesa sijajua zina nini ndani yake hadi kuweza kumuwehua mtu,yaani nilikuwa najiona naelekea kupata wehu kwa hilo tranka moja tu,nilitumia akili zangu zote na kuchanganua kujua nitafanyaje kuweza kutoka na hizi pesa mahala hapa salama ndipo nilipoamua kuchukua hivi visalfeti vikubwa na hizi pesa jinsi zilivyopangwa pembeni kulikuwa na nailoni imezungushiwa na mpaka chini kwanza lilitandikwa nailoni.

Nilichukua kisalfeti na kuanza kudumbukiza hizi pesa,kiukweli zilikuwa pesa nyingi sana,peke yangu yaani peke yangu nikawa naifanya hiyo kazi ya kudumbukiza hizo pesa na sikutaka kumshirikisha mtu yoyote yule hata kwenye yale matranka mengine,nikaingiza,nikaingiza huku nikijiwazia kuwa pengine watu uwa wanakuja humu kufanya mambo yao (wazinzi) na hawajui kama kuna utajiri umefukiwa chini yake,watu wanakiona tu kama kijumba,kiasi cha pesa nilichoweka katika kile kisalfeti ukiniuliza hata kukadilia kiukweli sijui,yaani hizi pesa niliwaza naenda kuziweka wapi? Naenda kufanyia nini? Maana zilikuwa ni nyingi mno,nikayakumbuka maneno ambayo niliambiwa "nina hazina ya utajiri,utajiri mkubwa,niahidi katika haya uliyoniambia"

Muda si muda alikuja yule bwana wa gari ambaye nilimpanga kuwa nina nafaka na nataka kuzisafirisha nikawa najiuliza tunaubebaje huu mfurushi? Lakini hauwezi kuamini nguvu ya pesa ni nguvu ya ajabu sana kwanza nilipata nguvu ya kuongea yaani nguvu ya mamlaka nikawa naongea kwa kujiamini nikajiona nina nguvu ya kujiamini kusiko kwa kawaida,nikanyanyua lile loba na kulitia kwenye boneti la gari yule kijana akiniuliza "ni nini hiki umebeba?" Unajua kama ni nafaka muonekano wake unajionesha tu na loba langu likawa linaonekana kama limebeba makaratasi,nikamwambia "naomba nifikishe mahali nataka kwenda ndugu yangu na nafaka zangu hii ni biashara ninayofanya na nitakulipa pesa yako nyuzi na nasema ntakulipa dabo!" Kwenye hela kuna mtu anashindwa kufanya kitu? Na kama anaona hakina shida yoyote? Nikatoka bila ya kuaga wenyeji wangu na tukaianza safari na hata njiani nikawa naona kama dereva anapata mashaka na akanambia "mimi nabebaga mizigo ya mazao lakini sijawahi kuona mazao kama hivi,ni nini umebeba?" nikaona huyu ataniletea shida nikamwambia "uwe na amani,tulichokibeba ni kile kile nilichokwambia ni nafaka,sasa wewe unajua nafaka za iana ngapi?akaanza kunitajia nami nikamwambia "kweli unaweza kujua nafaka lakini sio zote unazozijua,tukifika ntakuonesha wala usiwe na wasiwasi,amani tu imetawala hapa,uwe na amani" na kule tulipotoka yale matranka niliyarudishia mule katika lile shimo na kufukia kama awali,safari awali haikuwa na mikwamo na tulienda mwendo mrefu hadi nikawa najijutia kwanini nisingeacha zile pesa katika yale matranka na pesa ndio kila kitu kwani kama kutatokea kikwazo chochote nguvu ya pesa ingechukua mkondo wake mpaka nifike nyumbani,kuna baadhi ya maeneo maaskari walijaribu kuweka vikwazo ingawa havikuwa vya kivile sikutaka kuweka ugumu maana hata kama ni kosa la gari nilipatana nao mimi na kumaliza mchezo hadi nikafanikiwa kufika na mzigo mjini,nilifika mjini na pesa,yaani ninazo pesa[emoji23]

Nilipofika nyumbani nikiwa natweta nikawa naisikia sauti mawazoni ikinambia "Rojaz kwa purukushani za kupambana mpaka pesa hii umeishika mkononi mwako je unataka kurudi kwa yule mtu aliyekwambia kama kuna pesa? Nani anajua kama kuna pesa kule? Kwasababu hakuna anayejua" na sauti inanambia mtu huyu yuko gerezani na atafia gerezani sasa kuna haja gani ya kwenda kumwambia eti nimefanikiwa kuja na mzigo,nasikia sauti inanambia na pesa tayari niko nazo hapana sijui nafanyaje kwani toka nimeziona hizi pesa nimekutwa na hali isiyo ya kawaida yaani nimekuwa na ujasiri na kujiona hizi ni za kwangu nimezipambania mwenyewe,nimezipambania mpaka zimefika mjini yaani nahisi kupambana kwangu mpaka kupata hizi pesa kuzitoa kijijini na kuzifikisha mjini yaani ndio kama nimezipambania mimi lakini hizi pesa ni za mtu,hizi pesa mwenyewe yuko gerezani na hajamuamini mtu yoyote ameniamini mimi.

Kuna kitu nilikiona kimeingia moyoni mwangu na nilikaa na hizi pesa kwa siri kubwa sikumwambia mtu yoyote yule na sikufanya chochote niko na hizi pesa,unajua katika maisha ambayo tunaishi kila siku,maisha ya kupambana kwa ajili ya msosi ni maisha ambayo watanzania wengi tunaishi kwa mfano kama mimi ninafanya deiwaka kuna siku unakosa gari yaani,unakosa gari unakuwa uko idol idol,ukikosa ina maana mambo hayaendi ina maana unatumia kile ambacho ulikihifadhi kwa ajili ya kula na mahitaji ya hapa na pale sasa hivi nimepata pesa nyingi kwa ghafla na yaani kuna watu wananidaidai hela zile nilikopa kutatua changamoto ndogo ndogo nimepanga siku nawalipa wote[emoji23],nilitulia kwanza na ukiniuliza kwanini nilitulia makubaliano na yule ndugu kule jela ilikuwa mimi nikifika na mzigo na hizo hazina niende kule gerezani niende nikamwambie mshkaji nimeenda nini kinachofata,kwanini mimi nasitasita kwenda na ahadi nilishamuahidi na hata kwa watoto siendi tena nimekaa tu na hizi pesa na mipango mingi inanijia kichwani mwangu,nina mipango mingi najisemea hizi pesa zinanitoa kwenye umaskini mazima,hizi pesa zinaenda kunitajirisha mimi,mimi niliyekuwa naitwa Rojaz mtu wa kuomba deiwaka naenda kuwa na magari yangu,kichwa changu hivi sasa kimekuwa na mambo mengi nayafikiria ninunue magari yangu,nitafute vijana wawe wanaendesha taxi za kwangu,niziite kwa majina yangu,nina mawazo nina mawazo kwa sababu hizi pesa zimekuja kwa ghafla unajua kuna zile pesa zinakuwa unazikusanya unazikusanya unajipangia nikifikisha kiasi flani nitafanya moja mbili tatu kwahiyo unakuwa na malengo yako tayari unayo hivyo zikija tu ni moja kwa moja ni kutupia katika vile vitu ambavyo umevipanga sasa mimi hizi zimekuja kama upepo yaani paap! Hizi hapa,mzigo huu hapa,mzigo umenona huu hapa nahisi kuchanganyikiwa nifanye nini,nikapata muda nikaanza kuzihesabu kwa sababu hizi pesa hauwezi kwenda nazo nyumbani kwa sababu ya mazingira ya pale nyumbani,nlitafuta sehemu,sehemu yaani nitulie hapo,nilihesabu,nilihesabu,nilihesabu hadi nikahisi kuchanganyikiwa,ushawahi kuhesabu pesa hadi ukahisi kuchanganyikiwa? Kwa mfano mtu haujazoea kushika pesa ukapata milioni kumi hapa usilale usingizi,haupati usingizi, mimi leo nina pesa na pesa unahesabu hadi unahisi kuchanganyikiwa,hizi pesa zinahitaji mashine kabisa yaani iwepo hapa kwa ajili ya kufanya kazi ya kuhesabia maana ni kwenye masalfeti pesa zimejazwa umo,sijui kama unaona hiyo hali,uelewi unafanya nini kwahiyo nikakaa nimetulia,nikapitisha wiki mbili nimekaa na hizi pesa na ajabu ya hela niliposhika hela na sijaanza kutumia matumizi lakini kila mtu anayeniona ananambia "Rojaz mbona unatakata,mbona hivyo unashine mwenzetu,tunaona mambo mazuri" ulishawahi kusikia wanasema pesa tunda la roho?

Pesa tunda la roho unatakata bila ya kutumia mafuta,moyo wako unatawaliwa na amani tu yaani wewe una raha tu "Rojaz mwenzetu mbona wiki hii tunaona si haba?" Nina hela nyumbani,nina hela lakini huwezi kumwambia mtu hata kuna kauli zangu zimebadilika kuna namna ya kuongea mimi nimebadilika ukiniuliza imekuwaje automatic nimejikuta nazungumza kimabadiliko,pesa ni kitu cha ajabu sana.



ITAENDELEA!
Nasongaaaa
 
Mkuu,,Me ninavyojua hakuna Rojaz wawili ambao walipitia pale RAF,,,ninamjua Rojaz mmoja tuu,,,na ndiyo huyo alimpeleka Zabron Mzee wa Gamboshi pale RAF,,pia Zabron ndiye alisema Alikutana na Rojaz mtaani anauza mitumba na wakati huo yeye mwenyewe Zabron alikua anauza mitumba ndipo walipoenda mgawahani Rojaz akaanza kumwambia Zabron,,kwamba nimemaliza kipindi ktk kipindi cha sintosahau week iliyopita na nashukuru watu wamenichangia changia ndipo nikaona nianzishe biashara ya kuuza mitumba,,,zabron akamwambi me mwenyewe ninamkasa,,Rojaz akamwambia hebu nisimulie,,Zabron kwa kifupi akamwambia,,ashaishi na jini pia aliwahi kupelekwa ktk Kijiji cha wachawi kimazingara,,,Rojaz akamwabia zabron,,,aisee!!!una bonge la Story hebu twende RAF tukaweke Booking,,ndipo wakaenda na Zabron hadi pale RFA na zabron akaanza kuruka kwa hewa na simulizi yake ya Sitoisahau Gamboshi....

So nimejaribu kukufahamisha Namna gani jamaa alipomaliza Simulizi yake pale RAF na maisha mengine yalivyoendelea,,,Me ni miongoni mwa watu ambao sikubahatika kusikiliza simulizi ya Rojaz Radioni ingawa nilikuwa mpenzi mkubwa sana wa hicho kipindi,,,,na nimeanza kufuatilia kile kipindi baada ya Fredrick Bundala kushika usukani,,ingawa inasemekana creator wa hicho kipindi ni Roy Maganga....
Nakubaliana na Ww hii Story iliruka EFM na Sio RFA,,Hata ukiingia Youtube unaikuta
 
SHUKRANI SANA:

Ndugu zangu nawashukuru nyote kwa kutumia muda wenu kusoma mkasa huu wa Rojas na hapa ndio hitimisho lake,tukutane tena katika mkasa mwingine siku nyingine kwani haikuwa jambo rahisi ukizingatia kutoa maneno katika mfumo wa sauti kuleta katika mfumo wa maandishi kulileta changamoto kidogo ili kuweza kuifanya hadithi ibaki na mvuto wake ule ule,kuna baadhi ya maeneo ilinilazimu kuongeza nyama ili kuweza kuleta muunganiko kwani upande wa audio kulikuwa ama kukatikakatika,kukosekana kipande kirefu au episode kutosikika kwa zaidi ya dakika 10 hapo ikanibidi nijiongeze.
Mkasa huu umenipa mzuka wa kufanya kazi nyingine na nyingine na kama kuna mtu kati yetu anakifahamu kisa chochote kilicho katika mfumo wa sauti na akapendezwa tukilete jukwaani asiwe mchoyo aniPM nami ntatimiza wajibu wangu kama mwana jukwaa,mbarikiwe sana!
Ubarikiwe kwa muda wako
 
Kule ambapo Rojas alichimba pesa, ilionekana kuna pesa zingine aliziacha, vipi?

Mbona kipindi cha kumzika yule mfungwa, hatukusikia hata nduguzake wamesemaje? Hatukusikia watoto wa mfungwa na wanawake wote wawili wa mfungwa walisemaje?

Pia, yule mfungwa alipata wapi hizo pesa?
 
Kule ambapo Rojas alichimba pesa, ilionekana kuna pesa zingine aliziacha, vipi?

Mbona kipindi cha kumzika yule mfungwa, hatukusikia hata nduguzake wamesemaje? Hatukusikia watoto wa mfungwa na wanawake wote wawili wa mfungwa walisemaje?

Pia, yule mfungwa alipata wapi hizo pesa?
Mkono mmoja nisaidie kujibu haya maswali.
 
Kule ambapo Rojas alichimba pesa, ilionekana kuna pesa zingine aliziacha, vipi?

Mbona kipindi cha kumzika yule mfungwa, hatukusikia hata nduguzake wamesemaje? Hatukusikia watoto wa mfungwa na wanawake wote wawili wa mfungwa walisemaje?

Pia, yule mfungwa alipata wapi hizo pesa?
Kwa maelezo ya mhusika hakufafanua moja kwa moja ila kule kijijini hakuacha pesa kwani matranka yote yaliyokuwepo aliyabeba,kuzikwa kwa mfungwa inaonekana hakutaka kuwajuza watoto kwani alihofia kuwaumiza kisaikolojia,wale wanawake na hasa yule mama wa watoto hakujua kuwa chanzo cha misaada yote ni mzazi mwenzake na Rojas hakutaka kuianika siri hyo na hakumjuza kuhusu kifo chake kwani huyu mwanamke kwanza hakujali nafasi ya yule mzazi mwenzake na pia rojas nahisi alikataa kumjuza nadhani alijua akijua anaweza waambia watoto,kuhusu yule mwanamke mwingine kumbuka Rojas alitembea nae na nafsi yake ikajutia sana na kujiona ni kama mwenye hatia kwa rafiki yake na mahusiano yao kati ya Roja na yule mdada yaliharibika nadhani ndio chanzo cha kutomjuza kuhusu kifo cha yule jamaa.
Kuhusu ndugu zake kutohudhuria mazishi kwa upeo wangu nadhani Rojas kama unakumbuka uondokaji wake baada ya kupata pesa hvyo hakutaka tena ukaribu na jamii ya kule
 
Kule ambapo Rojas alichimba pesa, ilionekana kuna pesa zingine aliziacha, vipi?

Mbona kipindi cha kumzika yule mfungwa, hatukusikia hata nduguzake wamesemaje? Hatukusikia watoto wa mfungwa na wanawake wote wawili wa mfungwa walisemaje?

Pia, yule mfungwa alipata wapi hizo pesa?
Kuhusu alipozipata pesa ni siri aliyokufa nayo mwenyewe kwani hata Rojas hakufanikiwa kulijua hilo
 
Back
Top Bottom