PART TWO
Baada ya kuhitimu elimu yangu niliamua kurudi mtaani na kuwa mwalimu kwenye vituo mbali mbali vya kufundishia, kama vile mchikichini, banana, na maeneo mengine. Mnamo 2020 katikati nilikutana na jamaangu ambaye nilisoma naye O.level akiwa na kituo cha kufundisha ambacho kinakaribia kujifia.
Kiukweli nilifurahi mno kwani shule nyingi na vituo vingi kipindi hiko vilifungwa kutokana na janga la corona, na kupelekea vituo vingi vidogo vidogo vya elimu kujifia. nikaona hii ndo fursa ya kumshawishi tuendeshe kituo kwa pamoja kwani nilikuwa na ndoto ya kumiliki shule siku moja hivyo nikaona huu ndo mwanzo.
Tulipanga siku tukutane tuongee kwa kina kuhusu uendeshaji wa kituo, na kweli siku iliwadia na mipango ikapangwa. Jamaa aliniamini mno kwenye mipango yangu kwani nilikuwa na experience ya kutosha. Nilijiamini mno kwani nilikuwa na kundi kubwa la wanafunzi walioniamini.
Mipango ilipangwa kazi ikaanza, kutokana na kutokuwa na imani na vijana wanapoona mafanikio yanakaribia huwa wanasahau mipango yote, hivyo niliamua tufungue account ya pamoja ambayo tutakuwa tunaweka pesa kila mwisho wa mwezi. Na tukitaka kutoa ni hadi signature za watu wote wawili.
Mungu si athumani kwa baraka zake ndani ya mwezi mmoja advance tuna wanafunzi 28, o level kama 18 hivi. Hapo ada ilikuwa 30,000 kwa kila mwanafunzi.
Nilipanga mikakati na kuiba mwalimu mmoja kiraka kutoka kituo furani akawa anapiga form 4 na advance masomo mawili, na alikuwa nondo kweli.
Tulibahatika kuweka pesa mwezi mmoja tu, nikapata dharura ya kusafiri kuelekea manyara ndani ya week. Kurudi nikakuta kila kitu kimesambaratika. Ada za watoto wakilipa haziandikwi, kulikuwa na daftari la mapato na matumizi, lakini nikakuta baadhi ya page zimechanwa, kwengine full editing. Kaongeza walimu anaowajua yeye vijana tu vimemaliza A.level anavinyonya malipo anaandika makubwa.
Mwili ulisisimka mno pale nilipohoji imekuwaje umejiamulia, majibu niliyopewa yalirarua moyo wangu. Mara aseme ye ndo mwenye kituo sitakiwi kumhoji. Mara natembea na wanafunzi, mara watoto wanatakiwa wasome hadi usiku ndio maana malipo yamezidi.
What i know kipindi hiko nilikuwa mtu wa imani sana, nikamuachia Mungu nikabeba maamuzi mazito ya kutochukua hata mia niliyokuta zaidi ya ile tuliyoweka benki ndio tugawane nusu kwa nusu.
Madaraka na wingi wa wanafunzi kwa kipindi hiko vilimpa imani kuwa ataendeleza kituo. Nikachukua mgao wangu nikaongezea na visenti vyangu nikanunua boda.
Rasmi sasa kutoka kuwa mwalimu na kuwa bodaboda. Sikuona kuwa boda ni kama kufeli maisha bali niliona nguvu kubwa ambayo ipo kwenye kujituma na kuhifadhi hata kidogo unachopata.
Tuwe pamoja najaribu kuvuta nyuma kidogo nitengeneze dots.