Mkasa wa kweli: Leo nimetua mzigo mzito wa mahusiano

Mkasa wa kweli: Leo nimetua mzigo mzito wa mahusiano

PART TEN (FINAL)


Baada ya kupata misukosuko sana ya ajali nilikuwa na mawazo sana, kiimani nilishajua wapi nimeharibu kupelekea hali hii, niliwaza niende kwa mganga nikaoshwe mana watu wengi wa karibu yangu walisisitiza hili mpaka ikawa kero.

Lakini mawazo hayo ni kama yaliingia na kupitiliza upande wa pili. Baada ya muda nilisikia kaka yake Recho amepata ajali na kufariki, hapa ni kama nilichochea moto kwa mama yake Recho alitamkia watu waziwazi kuwa mimi nimemroga mtoto wake, niliona hata kwenda msibani kumzika rafiki yangu ingekuwa habari nyingine.

Nilikuwa mtu wa mawazo mno, kiufupi niliisha, nilipungua mno, mama watoto kazi yake ni kunifariji. Sikuwahi fikiria kumwambia ukweli maana nilijua siku nikimwambia hili jambo litamtesa maisha yake yote. Huwa mara nyingi kama ukweli unaumiza kwa mtu na unaweza kuharibu future, is better to keep it.

Hatimae niliamua nimshirikishe mzee kipara swala langu, kwanza alicheka sana, maana alikuwa ananiona mimi ni mtaratibu mno. Nadhani moyoni mwake alijisemea kumbe familia. Alinipa story nyingi sana na mikasa mingi mno kipindi cha ujana wake pia uzee wake.

Nilijisikia faraja sana siku hii, niliwahi pata story siku moja kuwa kaka yake na Recho alikuwa mtu wa mawazo sana kabla ya kifo chake na alianza kutumia vilevi. Nikapata picha kwamba mwamba aliniamini vya kutosha sasa sjui ni alikurupuka kwenye maamuzi, ama alipewa taarifa sio, ama ni hasira zake tu na kutengeneza chuki, hadi leo majibu sina. but RIP familia.

Majanga kwenye biashara hayakuisha, kwa mara ya kwanza nilipata dili la kuhifadhi mzigo wa kemikali hili sitaliongelea sana, mzigo huu haukua na kibali na ubaya wenyewe wanasema ukichanganya na kemikali nyingine unaweza tengeneza mlipuko, me sikufaham lolote, nipe kazi nikufanyie kazi yako.

Mzigo ulikuwa kwenye pipa hizi za blue, kama pipa 20. Nikapata chimbo nikaupigilia, kazi yangu ilikuwa ni kuuhifadhi then wenyewe watakuja kuubeba. Ndani ya siku mbili tu ya kukaa na mzigo nilipata ugeni, nakumbuka ilikuwa usiku kama saa 8 kasoro. Wazee walikwisha tonywa, hii ngoma iliniendesha, bila nguvu ya mzee kipara nilikuwa naisha.

Kwa tetesi za haraka haraka walioleta mzigo ndio wamefikisha taarifa kwa wazee, yaani dereva na wapakuaji. Maana niliupigilia mbali mno.

Nilizikumbuka sana hustle zangu tangu awali na muelekeo ambao naenda nao, nilikumbuka marafiki zangu wengi kwenye boda waliopoteza maisha kwa kupigania ndoto zao. Vijana wanakufa mapema mno tena vifo vichungu. Nilikuja kujifunza mafanikio ni ile hali ya ndani ya kuwa na furaha na amani na kuyamudu mazingira yanayokuzunguka bila kughafirika.

Mafanikio ni kipimo cha kuridhika unachojiwekea, kuridhika huku mara nyingi kunachochewa na PESA. kipimo chako cha mafanikio ndio kitaamua ni kiasi gani cha pesa utafute. Ndio maana ni rahisi kumkuta muuza karanga au mayai anafanya biashara hiyo hiyo miaka nenda miaka rudi, means kwamba akili yake imemwambia hapa ndipo pako unapostahili.

Kipimo chako cha mafanikio ndicho kiamue namna ya kupambana, i had a dream. And i hope one day ningetimiza ndoto hiyo. Na bado ninaamini nitaitimiza.

Nimeamua rasmi kuishi maisha matakatifu, rasmi kuachana na binti ambaye ameiletea matatizo makubwa katika ndoto zangu. Nimejifunza si kila hasara inatokana na kulogwa, au fitna kuna wakati Mungu anaamua kukupitisha katika majaribu ili uujue ukuu wake.

Sikupenda nimuumize binti aliyetokea kunipenda katika maisha yangu, kiukweli amenipenda mno, alikuwa yupo tayari kufanya chochote kile kwaajili yangu. Am so sorry Recho, najua utasahau haya maumivu, naona status zako unazotuma, naziona missed call zako, naziona msg zako. Naona the way unavyoingia kwenye account yangu na ya mke wangu instagram kwa kulike post zetu.

Najua unaumia, najua nimekutesa but nataka niwe na mwanzo mpya. Nipende familia yangu, nirudishe afya yangu, nimpende Mungu wangu. Hadi naandika hii story kuna madhira yalikuwa yanaendelea, kama ajali kwenye miradi yangu, lakini ninaamini ipo siku yatakuwa sawa. Imani yangu ikikaa kwenye mstari mambo yote yatatulia.


Dili zangu na ujanja wa town sijui kama ntaacha mapema, ila kwanza mahusiano yakae pembeni. japo dili haramu nimepiga chini kwasasa.

Am so sorry popote nilipowauzi but nilipenda kushare kisa hiki kidogo ambacho baadhi yetu kinaweza kuwa funzo katika maisha yetu.
 
PXL_20260607_121212115~3.jpg


Endeleeni kupuliza TATEPA kutoka TTB sisi tupo tunachakalika, naona kuna mtu amepost kiwanda cha Mufindi.
 
Hongera kwa story nzuri. Bado funzo ni lile; ukitaka kufanikiwa kwa haraka kama hivi ujue kuna kushikwa mkono, mentored, daraja na hasa hasa crime is involved. Wengine msiotaka halafu mnataka maisha kama ya hawa mtayapata mbinguni labda mambo yabadilike.
 
Back
Top Bottom