IFRS
JF-Expert Member
- Dec 19, 2014
- 2,915
- 5,233
Kaka usione tupo kimya tupo na weweHuo ndio ukweli KIONGOZI
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kaka usione tupo kimya tupo na weweHuo ndio ukweli KIONGOZI
Walokole hamtakiwi hapa😆! Maliza mkuu!
Mzee wake gado nasikia alishafarikiMkuu nimeimaliza labda uulize maswali sasa
Naomba nikuulize swali...nimekuwa na marafiki wengi sana wakurya..na nimefika had huko kwenu...swali ni hili..kwanini kila familia moja unakuta baba ana wake wawili?..watoto pia wameoa wake kuanzia wawili...mna shida gan mkuu? Yaani sijji kama nna rafiki hana wake wawili...kha!y?
Khaaa🙌🙌🙌🙌Nimekua jirani wa wakurya kwa miaka mingi ili mwanaume aonekane kidume cha haja anatakiwa awe na wake wengi zaidi
Hao wanaokejeli watakuwa washirikina[emoji16][emoji16][emoji28]Mbona anaandika vizuri tu, kwani humuelewi?
Kwani yeye nimuandishi wa Habari hadi aweze kusimulia na kuandika kiufasaha?
Kwa nini Watanzania hatupendi kupeana moyo? Lengo la mleta Mada ni kutuelimisha ila huoni hilo unaangalia kitu kisicho cha msingi.
TUACHE HII TABIA JAMANI
We ni mgeni humu mkuu? PotezeaHumu watu ni wajuaji kweli yaani kila kitu wao ndio wanajua
Mkuu vip kuhusu yule Bibi kusaga saga 50k?Ndio KIONGOZI alishafariki alikuwa anaitwa mzee NYANDA..nimemzungumzia japo kwa ufupi kwenye andiko
KWELI hapa nilisahau haya ndio madhara ya tungi..Mkuu vip kuhusu yule Bibi kusaga saga 50k?
Ulisema utaelezea hiyo siri?
INAENDELEA:
Huyu Gado akaendelea kuwa tajiri sana mwenye ukwasi wa kufa mtu, nakumbuka mwaka 2015 alimuita ndugu yangu mmoja hotelini pale Musoma mjini baada ya kuja kusalimia kijijini Hawa walikuwa hawajaonana siku nyingi katika maongezi yao aligusia kwamba kwa mda ule alikuwa na akiba bank kama 400m hivi...
Jamaa akawa anaogolea kwenye ukwasi na pale kijijini akawa anaheshimika sana na akawa tayari amepata watoto wawili na yule mkewe traffic... kitu nilichogundua ukiwa na pesa hata watu wakijua ni za madhara bado watakuheshimu na kukunyekea tu yaani huyu jamaa alikuwa ananyenyekewa pale kijijini utafikiri mfalme.
Kuna mwaka, mama mkwe wa Wasosi ambaye Sasa ni shemeji yake na huyu Gado maana Kaka yake ni yule aliyetolewa kafara akafariki pale kijijini na Mimi Kama kijana nikaenda kushiriki ule msiba, Cha kushangaza Gado sijui alipata wapi Ujasiri akafunga safari kuja msibani.
Pale Msibani alikuwepo mama yake Wasosi pia, wakawa wamepata taarifa za ujio wake huyu mwamba msibani jamaa alipofika na mkewe lile gari tu kuingia yule mama yake Wasosi alipiga ukunga ambao sijawahi uona Aisee huku akilalamika kwa uchungu na kutukana..nanukuu baadhi ya maneno ninayayakumbuka..." Uwiiiiiiiiiii mbwa wewe, Shetani mkubwa umemuua mwanangu Sasa wewe unafurahia na maisha, umeuua mwananangu, kweli umeuua mwananangu au hiyo gari ndio mwanangu" huyu mama alikiwa akiongea haya huku akionekana kuishiwa nguvu.
Wabibi wenzake wakawa wanamtuliza na baadhi ya wazeee lakini hali ya pale Msibani ikawa sio nzuri japo jamaa hakuonekana kujali kabisa..na baada ya kuzika yeye akaondoka.
Mimi nilikuja kuondoka pale kijijini nikaendelea na harakati za kutafuta maisha mikoani, mwaka juzi nikapata habari za huyu mwamba kwamba ameanza kufirisika ..kweli mpaka nakuja Arusha huyu Gado amebaki na Ghorofa moja tu zingine zote ameshauza na hata gari Hana..mke alishamkimbia nadhani hata hii ghorofa itauzwa mda si mrefu sijui alikosea wapi kwenye masharti yake huyu mwamba.
Mishe zimemgomea kabisa, Hana pesa tena.
Kibaya zaidi familia imeshaparanganika baba yao alishafariki.., watoto wote na mama hawaamini tena na hata upendo kati yao haupo kabisa yaani wanapitana Kama unavyompita mtu njiani..wanaishi kwa kuviziana sana.
Huyu mkubwa Joseph kwa Sasa ni Dereva Merelani hapo na afadhari amerudi kupatapata vipesa yuko njema kiasi chake kwa Sasa.
Yule mtoto wa Sarah, kwa Sasa ni binti mkubwa yuko vidato kadhaa na anajua kila kitu kuhusu stori ya kifo Cha baba yake...binti ana kisasi sana na Hawa ndugu ndugu zake
kupitia kwa watu na hata Joseph mwenyewe anasema binti amesema hawatambui akiwemo mama yake mzazi Sarah na hajawahi hata kwenda kuwasalimia hata kwenye simu.
Maisha yao yamegeuzwa kuwa Arusha japo kwa Sasa yamekuwa magumu sana wanaona soni kurudi pale kijijini tena na pale Kijijini Kuna miamba mipya iliyofuata nyayo za Gado imeibuka ndio inatawala sasa.
Sarah kachoka sana hadi anatia huruma...
,.........................................................
Hiki kisa ni cha kweli na hakijatokea miaka mingi..Ukiwa unatoka mwanza au Bunda na unaenda Musoma mjini au Tarime shuka hapo sabasaba mbele ya kiabakari na Mazami...hapohapo barabara kuu ya Musoma ulizia kwa mzee Nyanda au uliza mtu yeyote hii stori ukifika sabasaba.
Kwa mlioko mjini unaweza kumuona huyo Kiringo hapo udsm na atakupa huu mkasa uliochukua maisha ya kaka yake.
Poleni kwa uandishi wangu mbovu....
Niko zangu sitimbi now mapumziko naangalia madon wapya walioibuka
Leo ntauliza niko maeneo haya haya...ila mie sio sijaamini naamini ni kweli..maana watu wa huku ambaye haparticpate kwa waganga nadhan wakuhesabu! Funzo kubwa hiliHii ni Mikasa ya kweli sio hadithi boss
Njoo hapa unitembelee karibu na kwa mkuu wa wilaya nikupikie ugali wa mhogo na kuku😃😃Leo ntauliza niko maeneo haya haya...ila mie sio sijaamini naamini ni kweli..maana watu wa huku ambaye haparticpate kwa waganga nadhan wakuhesabu! Funzo kubwa hili
Duuuuh, kweli hamna siri hapa duniani[emoji16]KWELI hapa nilisahau haya ndio madhara ya tungi..
Huyu mwamba Gado alikuwa mjanja sana na inaonekana alikuwa amejiwekea kinga za kutosha za kiganga kushindana na uchawi uliokuwa ukimuwinda.
Sasa Kuna mjukuu wa huyo bibi mchawi ambae alikuwa anampenda sana na watu wakawa wanahisi kwamba anarithishwa uchawi...alikuwa anamuita Gado mjomba maana ni mtoto wa Dada yake kutoka familia ya baba yake mkubwa.
Sasa Gado akatengeneza urafiki sana na huyu jamaa, Kuna siku kaja pale Kijijini akamchukua kwenye gari lake pamoja na watu wengine wameenda piga pombe huko mjini dogo akalewa chakali ndio akaanza kutoa Siri za Bibi na akamsihi ajichunge na yeye anawindwa.