INAENDELEA:
Huyu Gado akaendelea kuwa tajiri sana mwenye ukwasi wa kufa mtu, nakumbuka mwaka 2015 alimuita ndugu yangu mmoja hotelini pale Musoma mjini baada ya kuja kusalimia kijijini Hawa walikuwa hawajaonana siku nyingi katika maongezi yao aligusia kwamba kwa mda ule alikuwa na akiba bank kama 400m hivi...
Jamaa akawa anaogolea kwenye ukwasi na pale kijijini akawa anaheshimika sana na akawa tayari amepata watoto wawili na yule mkewe traffic... kitu nilichogundua ukiwa na pesa hata watu wakijua ni za madhara bado watakuheshimu na kukunyekea tu yaani huyu jamaa alikuwa ananyenyekewa pale kijijini utafikiri mfalme.
Kuna mwaka, mama mkwe wa Wasosi ambaye Sasa ni shemeji yake na huyu Gado maana Kaka yake ni yule aliyetolewa kafara akafariki pale kijijini na Mimi Kama kijana nikaenda kushiriki ule msiba, Cha kushangaza Gado sijui alipata wapi Ujasiri akafunga safari kuja msibani.
Pale Msibani alikuwepo mama yake Wasosi pia, wakawa wamepata taarifa za ujio wake huyu mwamba msibani jamaa alipofika na mkewe lile gari tu kuingia yule mama yake Wasosi alipiga ukunga ambao sijawahi uona Aisee huku akilalamika kwa uchungu na kutukana..nanukuu baadhi ya maneno ninayayakumbuka..." Uwiiiiiiiiiii mbwa wewe, Shetani mkubwa umemuua mwanangu Sasa wewe unafurahia na maisha, umeuua mwananangu, kweli umeuua mwananangu au hiyo gari ndio mwanangu" huyu mama alikiwa akiongea haya huku akionekana kuishiwa nguvu.
Wabibi wenzake wakawa wanamtuliza na baadhi ya wazeee lakini hali ya pale Msibani ikawa sio nzuri japo jamaa hakuonekana kujali kabisa..na baada ya kuzika yeye akaondoka.
Mimi nilikuja kuondoka pale kijijini nikaendelea na harakati za kutafuta maisha mikoani, mwaka juzi nikapata habari za huyu mwamba kwamba ameanza kufirisika ..kweli mpaka nakuja Arusha huyu Gado amebaki na Ghorofa moja tu zingine zote ameshauza na hata gari Hana..mke alishamkimbia nadhani hata hii ghorofa itauzwa mda si mrefu sijui alikosea wapi kwenye masharti yake huyu mwamba.
Mishe zimemgomea kabisa, Hana pesa tena.
Kibaya zaidi familia imeshaparanganika baba yao alishafariki.., watoto wote na mama hawaamini tena na hata upendo kati yao haupo kabisa yaani wanapitana Kama unavyompita mtu njiani..wanaishi kwa kuviziana sana.
Huyu mkubwa Joseph kwa Sasa ni Dereva Merelani hapo na afadhari amerudi kupatapata vipesa yuko njema kiasi chake kwa Sasa.
Yule mtoto wa Sarah, kwa Sasa ni binti mkubwa yuko vidato kadhaa na anajua kila kitu kuhusu stori ya kifo Cha baba yake...binti ana kisasi sana na Hawa ndugu ndugu zake
kupitia kwa watu na hata Joseph mwenyewe anasema binti amesema hawatambui akiwemo mama yake mzazi Sarah na hajawahi hata kwenda kuwasalimia hata kwenye simu.
Maisha yao yamegeuzwa kuwa Arusha japo kwa Sasa yamekuwa magumu sana wanaona soni kurudi pale kijijini tena na pale Kijijini Kuna miamba mipya iliyofuata nyayo za Gado imeibuka ndio inatawala sasa.
Sarah kachoka sana hadi anatia huruma...
,.........................................................
Hiki kisa ni cha kweli na hakijatokea miaka mingi..Ukiwa unatoka mwanza au Bunda na unaenda Musoma mjini au Tarime shuka hapo sabasaba mbele ya kiabakari na Mazami...hapohapo barabara kuu ya Musoma ulizia kwa mzee Nyanda au uliza mtu yeyote hii stori ukifika sabasaba.
Kwa mlioko mjini unaweza kumuona huyo Kiringo hapo udsm na atakupa huu mkasa uliochukua maisha ya kaka yake.
Poleni kwa uandishi wangu mbovu....
Niko zangu sitimbi now mapumziko naangalia madon wapya walioibuka