Part Six A :Tasting honey with the tip of a knife[emoji182]
1994-1996
Matokeo ya mtihani yalitoka , nilifaulu kwa maksi nzuri sana nikapangiwa shule ya Tabora boys, kipindi kile walizingatia chaguo lako kati ya yale matatu, 'first option' yangu ilikuwa Tabora boys.
Mama hakupenda niende Tabora,kwa kigezo kuwa nitapata shida maana sina ndugu huko.
Alimuomba baba afanye mapango niende Ilboru. Baba alipata mzee wa mjini pale wizarani nikabadilishiwa shule kwenda Ilboru.
Nilianza kidato cha tano pale nikichukua EGM (Economics, Geography and Mathematics).
Kipindi Mr.Collins amerudi kunitafuta nilikuwa namalizia kidato cha tano.
Kutokana na hurka yangu ya upole, sikuwa na mambo mengi pale Ilboru. Sikuwa na matukio yoyote maana ni kipindi ambacho nilishajitambua. Nikawa ni mimi na kitabu basi.
Maisha yakabadilika sana pale nyumbani. Nilikuwa nimeingia kidato cha tano .Mr. Collins aliemdelea kuwasiliana na mimi kupitia ile email, alinitumia vitabu vingi sana vinavyohusu mchepuo wangu (EGM) vikiwa softcopy, pamoja na pesa kila mwezi.
Wakati nasoma kidato cha tano. Nilitokea kufahamiana na mabinti wawili. Zainabu na Zaituni.
Hawa nilifahamiana nao kupitia duka la nguo la mama, baadae nilikuja kujua wanaishi sakina jirani na Sakina super market.
Walikuwa na mchanganyiko wa mhindi na mwarabu, mama alikuwa mhindi baba mwarabu.
Walikuwa wanaishi Dar na baba yao maana biashara zake zilikuwa huko. Arusha walikuwa wanakuja kwa mama yao aliekuwa anafanya kazi shirika moja binafsi pia alikuwa na bekari mjini kati.
Tulitokea kuelewana sana, nikakaribishwa kwao, Ilikuwa ngumu sana kukubali ule mwaliko mpaka waliponihakikishia kuwa wanaishi na mama yao tu, na walikwisha ongea nae hana noma.
Ilikuwa siku ya jumamosi nilipoitikia ule mwaliko, niliwakuta wananisubiri, wakanipokea vizuri sana.
Mama yao alikuwa mkarimu sana na mwenye tabasamu mda wote, nilitambulishwa kama rafiki yao na mama akakumbushwa siku wamekuja kufanya shopping dukani kwetu, mama alikumbuka na akafurahi sana.
Nililetewa shalubati ya tende na maziwa ya ngamia, kwa mara ya kwanza nikaonja hivyo vitu.
Kisha nikakaribishwa mezani, nikakuta biriani la kuku, tulikula huku tunaongea kama vile ni ndugu wote pale.
Baada ya chakula mama alienda kulala akatuacha tunaagalia filamu za kihindi, niliongea mengi na Zainabu na Zaituni.
Hatimaye muda wa kuondoka ukawadia, nikafungashiwa chakula na vitafunwa mbali mbali nimpelekee mama.
Wakanisindikiza kidogo nikaagama nao.
Nilimfikishia mama zawadi zile na kumweleza kuhusu familia ile, akafurahi sana ila akaniambia niwe makini na watoto wa kihindi!/kiarabu maana hizo jamii hazikuwa zikipenda kuchangamana na waafrika.
Nilimhakishia mama kuwa uhusiano wetu ni wa kirafiki tu na wala sio mapenzi, ndio maana nilikubali kwenda kwao nifahamike.
Mama aliniangalia akacheka, akasema huki ana nyanyukaβ¦
"ndivyo mapenzi yanavyoanza baba"
Mama alikuwa ni zaidi ya rafiki yangu,ukitukuta unaweza hisi ni mtu na cousin yake, tunavyotanianai na kudekeana. Alizoea kuniita baba maana nimepewa jina la pili la baba yake.
**************
Next
Part Six B:Tasting honey with the tip of a knife[emoji182]