Mkasa: Wema ni akiba, usiache kutenda wema

Mkasa: Wema ni akiba, usiache kutenda wema

Kibongo bongo tunavyolazimisha kuyaelewa mapenzi, ni tofauti.
Huku kwetu ukitongoza tu unakuwa mlipa bili, wenzetu unaweza kiwa nae hata mwaka hajakuomba helaa.

Sisi waomba hela ndio tunaona tunependa sana. Kumbe penzi sio pesa
Basi utofauti ni mkubwa mno kati yetu na wao, huku watu wanatanguliza fedha mbele ndio upendo unafuata.
 
Vaa wigi mkuu usokote[emoji1787][emoji1787]
52ungzsqoww81.jpg
 
Aisee mwaka juzi tulienda kumzika bibi. Tukiwa himo na Costa tunasibiri kupambazuke tukawa tunapoga kahawa. Jamaa akaja na kvant tukawa tunachanganya na kahawa ya moto hatuna habari.

Kifupi tulifanya safari asubuhi saa 11 mpaka Rombo. Bibi alikuwa anazikwa mchana. Hakuna mjukuu tuliotoka mjini aliweza mzika bibi wote tulilala usingizi w kifo. Tunakuja amka usiku wake kila mtu kichwa kizito na wameshazika.

Tukawekwa kikao na kuonekana hatuna adabu. Tulilipidhwa hela ikanunuliwa mbuzi wa fine 🙂 Ikaisha hiyo juu juu ila nachotaka kusema nina two years sijagusa kinywaji🤣 Alafu mimi ni type ya watu wanaokunyw wanaongea kingereza hatari unawez dhania nilizaliw states ..
😂😂 mlitaka mgundue nini kvant na kahawa? Au kwa kuwa A.K.A yake ni muwa mkajua ni muwa wa sukari mchanganye na kahawa
🤣🤣😂😂!

Mimi huwa sinywi pombe yoyote ile sinywi kabisa!!
Sasa siku moja wifi Zangu ( kwa kaka yao )ni walevi kufaaa wakanilazimisha niende nao club eti Kwanini weekend napenda kujaa tu nyumbani wanapenda kujiachiaa sijawahi ona!! Sasa kwenye kuagiza wameagiza ma wine makali makali wanayajua wenyewe Mimi nikasema waniletee soda tu wee walinichamba Mtu mzima unakunywaje soda wifi hebu jaribu hii nikaonja ikanishinda basi wakamwambia mhudumu aniletee wine Gani sijui kwamba haileweshi sana kwa ambae sijawahi kunywa pombe ..nikaletewa wakaniwekea kwenye kile kiglass kidogoo inalingana kama kakikombe ka kunywea kahawa hivi mi si nishazoea sodaa kunywa guduuu guduu dakika imeisha nikapiga kiglass chakwanza dakika sifuri kimeisha wakaniwekea chapili kikaisha aloo huto tuglass tuwili tu nikaanza jisikia tofauti kichwaniii mara ghafla nikasimama kucheza nilichezaaa mzikii mimi kama mwehuu wakati hata kucheza ukunikuta nacheza labda nimerogwa wifi wanacheka hawana mbavuuu nachezaaa Huku Nacheka cheka tu! Mbona walinirudisha nyumbani kwanza then wao wakarudi huko club asubuhi niliamka kichwaa Sio changu kizitoo😄😄😄😄!!
🤣😂 pombe sio chai ila ulishawishika kirahisi sana why? Ungewakatalia uendelee kuitisha nyuki
 
Part Six A :Tasting honey with the tip of a knife[emoji182]

1994-1996

Matokeo ya mtihani yalitoka , nilifaulu kwa maksi nzuri sana nikapangiwa shule ya Tabora boys, kipindi kile walizingatia chaguo lako kati ya yale matatu, 'first option' yangu ilikuwa Tabora boys.

Mama hakupenda niende Tabora,kwa kigezo kuwa nitapata shida maana sina ndugu huko.

Alimuomba baba afanye mapango niende Ilboru. Baba alipata mzee wa mjini pale wizarani nikabadilishiwa shule kwenda Ilboru.

Nilianza kidato cha tano pale nikichukua EGM (Economics, Geography and Mathematics).

Kipindi Mr.Collins amerudi kunitafuta nilikuwa namalizia kidato cha tano.

Kutokana na hurka yangu ya upole, sikuwa na mambo mengi pale Ilboru. Sikuwa na matukio yoyote maana ni kipindi ambacho nilishajitambua. Nikawa ni mimi na kitabu basi.

Maisha yakabadilika sana pale nyumbani. Nilikuwa nimeingia kidato cha tano .Mr. Collins aliemdelea kuwasiliana na mimi kupitia ile email, alinitumia vitabu vingi sana vinavyohusu mchepuo wangu (EGM) vikiwa softcopy, pamoja na pesa kila mwezi.

Wakati nasoma kidato cha tano. Nilitokea kufahamiana na mabinti wawili. Zainabu na Zaituni.

Hawa nilifahamiana nao kupitia duka la nguo la mama, baadae nilikuja kujua wanaishi sakina jirani na Sakina super market.

Walikuwa na mchanganyiko wa mhindi na mwarabu, mama alikuwa mhindi baba mwarabu.

Walikuwa wanaishi Dar na baba yao maana biashara zake zilikuwa huko. Arusha walikuwa wanakuja kwa mama yao aliekuwa anafanya kazi shirika moja binafsi pia alikuwa na bekari mjini kati.

Tulitokea kuelewana sana, nikakaribishwa kwao, Ilikuwa ngumu sana kukubali ule mwaliko mpaka waliponihakikishia kuwa wanaishi na mama yao tu, na walikwisha ongea nae hana noma.

Ilikuwa siku ya jumamosi nilipoitikia ule mwaliko, niliwakuta wananisubiri, wakanipokea vizuri sana.

Mama yao alikuwa mkarimu sana na mwenye tabasamu mda wote, nilitambulishwa kama rafiki yao na mama akakumbushwa siku wamekuja kufanya shopping dukani kwetu, mama alikumbuka na akafurahi sana.

Nililetewa shalubati ya tende na maziwa ya ngamia, kwa mara ya kwanza nikaonja hivyo vitu.

Kisha nikakaribishwa mezani, nikakuta biriani la kuku, tulikula huku tunaongea kama vile ni ndugu wote pale.

Baada ya chakula mama alienda kulala akatuacha tunaagalia filamu za kihindi, niliongea mengi na Zainabu na Zaituni.

Hatimaye muda wa kuondoka ukawadia, nikafungashiwa chakula na vitafunwa mbali mbali nimpelekee mama.

Wakanisindikiza kidogo nikaagama nao.

Nilimfikishia mama zawadi zile na kumweleza kuhusu familia ile, akafurahi sana ila akaniambia niwe makini na watoto wa kihindi!/kiarabu maana hizo jamii hazikuwa zikipenda kuchangamana na waafrika.

Nilimhakishia mama kuwa uhusiano wetu ni wa kirafiki tu na wala sio mapenzi, ndio maana nilikubali kwenda kwao nifahamike.

Mama aliniangalia akacheka, akasema huki ana nyanyuka…

"ndivyo mapenzi yanavyoanza baba"

Mama alikuwa ni zaidi ya rafiki yangu,ukitukuta unaweza hisi ni mtu na cousin yake, tunavyotanianai na kudekeana. Alizoea kuniita baba maana nimepewa jina la pili la baba yake.

**************
Next
Part Six B:Tasting honey with the tip of a knife[emoji182]
Table.jpg
Ilboru%20.jpg
 
Back
Top Bottom