Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kweli braza alikua noumaa kuharibu redio tu Ndio kichapo mpaka kutaka vunja mbavu mtu dahhh!!Part Two
1963
Mwaka 1963 Walipata kijana wa kiume wakamuita Edward, furaha iliongezeka maana familia imepata mwanachama mpya.
Mwaka 1965 walipata mtoto wa pili wakamuita Edwin furaha ilizidi mara dufu. Familia ikawa na watu wanne.
Mwaka 1974 walipata mtoto wa tatu wakamuita Edson. Hapa sasa Anthony akaona kuna umuhimu wa kutafuta kazi ili aweze kumuda mahitaji ya familia.
Mwaka 1976 TAZARA walitangaza nafasi za kazi, Anthony alitumia nafasi hiyo kuomba kazi, bahati ikawa yake akapata kazi na kituo chake cha kazi kikawa kijiji cha kitete, wilaya mrimba, mkoa wa Iringa.
***
Hii ni simulizi ya maisha halisi ya Edson kijana wa tatu wa mzee Anthony na mama Antonia.
****
Naitwa Edson Anthony,nina haiba ya upole. Nimezaliwa mwaka 1974 katika kijiji 'X' wilaya 'X' mkoa 'X'. Mimi ni mtoto wa mwisho kati ya watoto watatu wa mzee Anthony na mama Antonia.
Kaka yangu wa kwanza anaitwa Edward (RIP) na mwingine ni Edwin.
Baba yangu ni mwenyeji wa 'X' mama yangu ni mwenyeji wa ''X'' lakini amekulia Arusha. Baba yake alihamia mkoa huo kutoka mkoa wake wa ''X'' .
Baba yangu mzee Anthony alikuwa ni mwajiriwa wa TAZARA (Tanzania and Zambia Railway) Kituo chake cha kazi kilikuwa kijiji cha kitete wilaya ya mrimba mkoa wa Iringa.
Maisha yalikuwa mazuri kiasi na yenye furaha na upendo. Baba alikuwa na ng'ombe wapatao 50 na buzi 70, pale kijijini kwetu. Kutokana na mifugo ikabidi mama abaki pale kijijini kwa ajili ya uangalizi wa mji.
Tulikuwa na mashamba ambayo tulikuwa tunajipatia chakula kama mihogo, viazi, mtama, uwele, ufuta yaani tulikuwa tunafanya kilimo mseto.
Napenda kuchukua nafasi hii kusimulia histori ya maisha yangu, kuanzia malezi, elimu, mapenzi, utafutaji wa pesa na mafanikio yangu maishani.
**********
1974-1989
Maisha ya utoto
Nimezaliwa na kulelewa pale kijiji cha 'X', kabla ya kuanza shule nilikuwa nachunga mifugo yetu.
Kaka zangu walikuwa wanaishi na baba Iringa. Nilibaki mimi kwa kuwa nilikuwa mdogo.
Maisha ya machungani yalikuwa mazuri sana maana tulikuwa tunakamua maziwa ya ng'ombe tunakunywa pindi tukisikia njaa na kiu, nakumbuka moments za kubeba viazi vya kuchoma kwenye mkoba wa ngozi, maziwa kwenye kibuyu n.k
Machunganii ilikuwa ni kawaida kukutana na wachungaji wengine, hapo michezo iliendelea na kufanya nipende kwenda kuchunga.
Mama alinipa malezi naweza sema mazuri sana, mama yangu sio mkali, muda wote sura yake imechanua tabasamu. Baba yangu alikuwa mkimya sana ila aside na masihara.
Safari yangu ya kwanza kwenda Songea
Mwaka 1981 nilipelekwa shule lakini nilishindwa kushika sikio nikarudishwa. Nilianza shule ya msingi mwaka 1982 katika shule ya msingi 'X' nikiwa na miaka 8. Kipindi hicho ilikuwa lazima ushike sikio ndio uandikishwe shule.
Nilikuwa na bidii sana shuleni, pia nilikuwa najua kusoma herufi a, e i o u na kuhesabu mpaka kumi. Ikiwa ni kazi ya mama yangu tukiwa nyumbani nyumbani.
'My mom was my first teacher.'
Nilipofika darasa la pili nilichukuliwa na kaka yangu mkubwa Edward, ambae alikuwa askari mkoa wa Ruvuma wilaya ya Songea.
Nakumbuka siku moja kabla ya safari, sikupata usingizi, nilikuwa nawaza kupanda gari kwenda nje ya mkoa wetu.Nilishawahi safiri kwenda Iringa kwa baba ila nikiwa mgongoni, sasa naenda kwa miguu yangu.
Kesho yake asubuhi mapema mama alinivalisha kisha akanipatia maziwa fresh na mkate nile, baada ya kula alitusindikiza mpaka barabarani. Tulipanda bus linaitwa 'X' kutoka hapo kijijini ''X'' kwenda Mwanza, nili enjoy sana kwa mara ya kwanza. Niliona miti inarudi nyuma kadri gari linavyo kimbia.
Kutoka ''X'' mpaka Mwanza ni masaa kadhaa tu, hatimaye tuliingi standi ya ''X'. Kaka alibeba mabegi yetu tukaenda kutafuta taksi ili kwenda station ya gari moshi, kipindi hicho mabasi yalikuwa yanapita Kenya yanatokea Arusha kwenda Dar-Es-Salaam,njia ya kati ilikuwa ni gari moshi maana barabara haikuruhusu.
Tulifanikiwa kupata tiketi za gari moshi daraja la tatu, kaka alilipia siti 3 ili nipate sehemu ya kulala. Ilibidi tusubiri safari saa 10 jioni. Ilipofika sa 9 tulianza kupanda kwenye gari moshi, saa 10 kamili ilipiga honi mara tatu likaondoka.
Gari moshi liliendelea na safari huku watu wakipiga soga, lilikuwa limejaza sana mpaka abiria wengine walikosa siti wakasimama.Mimi nililala kwenye ile siti, kaka akaenda behewa la askari wenzake kupiga soga.
Siku ya tatu asubuhi kama saa 3 tuliingia Dar-es-Salaam, tulishuka na kutafuta UDA ya kuelekea magomeni kota, kwa mdogo wake na baba…
Siku ya pili tulipanda basi kwenda mpaka makambako, nakumbuka jina la basi 'kiswele coach' lilikuwa linaenda songea ila sisi tulishukia makambako ili twende kwa baba pale kitete.
Makambako tulipanda gari moshi la TAZARA kwenda kitete kwa baba. Kaka aliniacha kwa baba, baada ya wiki moja, baba alinipeleka Songea. Kutoka makambako tulipanda costa, tulifika Songea usiku sana.
……..
Nilipelekwa shule ya msingi Misufini kuendelea na darasa la pili.Kaka yangu alikuwa amepanga nyumba mfaranyaki, (jirani na ilipokuwa Buhemba hotel sijui kama bado ipo.)
Maisha mapya hayakuwa na ugumu sana katika kuzoea mzingira.Kutokana na uchezaji wa mpira nilipata marafiki wengi sana kwa haraka.
Kipindi kile kaka alikuwa na redio kaseti aina Panasonic double decks,alikuwa anapenda sana nyimbo za kongo kina Franco Makiadi, Pepe kale, wengineo.
Alikuwa anapenda sana suruali za kitambaa raini na mashati ya dog dog Kama alivyokuwa wanavaa wana muziki wa kongo.
Kaka yangu alikuwa ni mtu wa hasira za haraka sana 'short-temper', hali iliyopelekea kuchezea kichapo mara kwa mara toka kwa mjeda yule.
Alikuwa ananifunga na pingu mikono na kunipiga kwa waya, mikanda na mateke, wakati mwingine alinibana korodani. Nilipitia mateso sana kipindi hicho.
Pamoja na kuwa alinifanyia ukatili mara kwa mara, alikuwa na upendo sana usipomuuzi, tatizo nilikuwa mtoto nahitaji kujifunza, hakunipa hiyo nafasi.
Kila nguo ikitoka ilikuwa lazima niivae kwanza kabla ya watoto wengine pale mtaani, hilo simlaumu.
Kipindi hicho tunatoka mfaranyaki kwenda standi kuu kula chips mayai. Hakukuwa na vibanda vya chips mitaani, na ni lazima kutumia uma kwenye sahani ya bati ha ha haaaa.
Baada ya kuuzoea mji nilikuwa nafurahia kijichanganya na watoto wemzangu katika michezo. Nilikuwa sikosi uwanja wa maji maji kuangalia mpira wa ligi kuu, kila inapokuja timu yoyote kucheza pale. Kilikuwa ni kipindi maji jami iko moto sana, simba na yanga zilikuwa ni kawaida kufungwa pale.
Kwa kuwa wasimamizi pale getini ni asikari, walikuwa wananipitisha bila malipo. Maisha yangu yote niliyoishi Songea sikuwahi kulipa kiingilio kwa tukio linalo lindwa na polisi pale maji maji.
Nilikuwa mtundu wa kimya kimya sana, nilipenda kujifunza vitu hasa ufundi. Nakumbuka kuna siku nilijifanya fundi nikafungua redio ndogo, kaka alikuwa anapenda kusikiliza mpira RTD. Nikashindwa kuifunga baada ya vitu kubaki, ikabidi nivitupe kupoteza ushahidi (i was a kid). Aliporudi kakuta redio haiongei , kesho yake akaipeleka kwa fundi.
Fundi akanisagia 'kunguni', akamwambia kuna vitu havipo, vikipatika itaongea , nikapewa kazi ya kuvitafuta mpaka jioni akirudi avikute.
Sikufanikiwa kuviona, ikabidi nisubiri kipigo akirudi, jioni aliporudi nikamwambia sijaviona. Alikuwa na kawaida akitaka kunipiga kama ameva kombat anavua shati anabaki na suruali na buti.
Siku hiyo nilifungiwa chumbani kipigo kikaanza, nilichezea mikanda na mateke ya mbavuni mpaka askari wenzake walikuja dirishani, wakaanza kumtisha kuwa wata mshitaki kwa mkubwa wao. Ndio ikawa pona pona yangu. Hiyo nyumba kulikuwa na wapangaji askari watatu.
Kesho yake nilipandisha homa kali, kutokana na kile kipigo cha jana yake. kufika jioni nikazidiwa ikabidi nipelekwe 'mzena dispensary'. Kabla ya kwenda nilipigwa biti kuwa ole wangu niseme nimepigwa.
Kaka alishauriwa na wenzake akaombe gari ya polisi anipele hospitali ya peramiho, ni baada ya hali yangu kuzidi kuwa mbaya. Mwanzo alipata ugumu maana aliogopa chanzo cha ugonjwa wangu kujulikana.
Kesho yake nikawa na hali mbaya zaidi, ikabidi wale wenzake wakaombe gari, jioni hiyo nikapelekwa peramiho, nikatundikiwa drip 3 na nili lazwa kwa siku 5.
Baada ya kupata nafuu nikaruhusiwa kurudi nyumbani, kaka alikuwa mnyonge sana baada ya lile tukio, na vipigo vilipungua sana.
Aliambiwa nimeumia mbavu, ilibaki kidogo moja ivunjike, kwa mateke ya my brother (RIP).
Maisha yaliendelea hatimaye nilipofika darasa la 3, yaani baada ya mwaka mmoja. Tulirudi likizo nyumbani, nikiwa likizo nilimwambia mama kuhusu vipigo ninavyopata. Mama alihuzunika sana, alimsema sana kaka kwa ukatili ule alionifanyia, mama aliamua nisirudi na kaka.
Nikahamishiwa shule kutoka misufini Songea, kwenda kitete Iringa kwa baba…
*******
View attachment 2552846View attachment 2552847View attachment 2552848View attachment 2552850View attachment 2552851
Asante sana ccy
Thank you kipenzi ngoja nitulie nisome
Miss you..upo sisyAsante sana ccy
Enjoy the story sis!Thank you kipenzi ngoja nitulie nisome
Nipo ccyMiss you..upo sisy
🤣🤣🤣 hapa umeniua mbavuUkiwa mgeni pale makambako , ukinunua chai, wanakupozea kabisa, maana kuna baridi kiasi kwamba wewe mgeni huwezi sikia moto wa chai, baadae mdomo utakapo babuka ndio utajua uliungua.
🤣🤣🤣🤣Naona tutalala leo jicho moja.