Part Four B: Maisha ya ujana
1990 - 1993
Tukiacha ubabe wa shule za boarding, tulikuwa wababe kwa wanafunzi wa chuo cha ualimu matogolo , maana shule yenye form 1 - 6 mchanganyiko toka mikoa tofauti, haikuwa rahisi kui handle.
Matogolo ni jirani, kuna wasichana na sisi tunawataka , na ma boy wao hapo chuo wanawataka.
Ni mwendo wa bifu za mapenzi na mambo mengine, kuna wale wanywa ulanzi wakiwashiwa moto, wanaleta taarifa jeshi la box 2 linaenda kumaliza kazi. Nilikuwa doja wa hatari kwenye matukio kama hayo.
Siku moja mbawala aliniambia nimsindikize rizaboni , ilikuwa siku ya jumapili, (kila jumapili tunaruhusiwa kutoka kwenda kanisani mwisho saa 10 jioni)
Tumefika rizaboni , kumbe mwamba amemfata mtoto wa mwanajeshi, wamesimama wanaongea pembeni ya njia, akaibuka mtu migombani mara jamaa ameshikwa. Binti akachanganyikiwa, nikaunganishwa na mimi.
Kumbe ni baba yake na binti, akatupeleka kambi ya jeshi pale Ruhuwiko, wakatupatia machangu matatu ya adhabu.
Ya kwanza, tufanye kama tunaendesha gari, tunashikana mashati, tuzunguke jengo flani pale mara 100 kisha tupotee
(Hapa kuna konda na dereva, unatakiwa usimame uite abiria, uchukie nauli, mpige story, hope unajua watoto wakicheza lazima kila kitendo wakielezee)
Ya Pili wawashe moto, tukae kuota hapo juani kama saa 7 /8 hivi, moto ukizima tupotee.
(moto wenyewe kuni kubwa sio wa mabua na ni kiangazi mko juani).
Ya tatu tuletewe wali ndoo ndogo umejaa, tuhakikishe umeisha kisha tupotee.
(watu wawili wali ndoo ya lita 10, hakuna kudondosha, akishindwa kumaliza mnapiga push up kuita njaa, mnarudi kumalizia.)
Siku hiyo ndio nilichukia kazi ya jeshi, tuliona option ya kwanza ni nafuu, nikawa dereva mwenzangu konda.
Kazi yangu mungurumo wa gari na honi visikike, mwenzangu ahakikishe anapiga debe kuita abiria, adai nauli, awakemee abiria wakorofi nk
(matukio yote common yanayotokea kwenye daladala yasikike loud and clear. )
Baada ya rounds 50 wakatufukuza, na kupewa onyo tusionekane na yule binti tena. Tumetoka yule boya anacheka eti.
Baada ya wiki tatu anasema yule binti amemtumia ujumbe, wakutane mfaranyaki, nikatoka nduki maana nisije ponzwa tena. [emoji125][emoji125]
…….
Mara nyingi kipindi cha likizo nilikuwa nakaa wiki 1 Songea na 3 Arusha kwa mama.
Kuna kipindi niliachiwa chumba na rafiki yake kaka (askari), alienda kusoma, ilikuwa likizo ya pasaka.
Likizo Ilipoisha niliacha funguo kwa kaka, ila ikawa kila nikienda nalala kwenye kile chumba.
Siku moja kulikuwa na michezo ya kishule, tukaenda uwanja wa zimani moto. Michezo ikiwa inaendele pale zimani moto. Nilimpanga mdigo wangu tukatoe 'singo' akakubali nikam 'pack' kwenye kile chumba.
Kilikuwa chumba cha 4 kutoka geti kuu la kuingia uwanja wa maji maji mkono wa.......[emoji119]
Lengo langu lilikuwa akae kwa muda pale ili mchezo ninao shiriki, ukiisha tupongezane kwa mara ya kwanza, nilikuwa nacheza 'volleyball' na nilikuwa kwenye Playlist vinginevyo ninge doji.
Yeye alikuja kama mshangiliaji tu hakuwa na mchezo anaoshiriki, ni wale 'usiniumizie'.
Lengo langu halikutimia, niliponzwaa kijinga, waswahili walisema usilolijua ni usiku wa giza.
Jasmin alinishawishi tunywe pombe kidogo, mwenzangu alikuwa mzoefu, nikajidanganya nikanywa ili mtoto asinione wa kuja hata bia sinywi.
' hivi vile vijumba vya nyasi kwenye ile chupa ya safari vina maana gani?'
Ndio mara ya kwanza na ya mwisho kuonja pombe, nilikunywa chupa 2 za 'safari lager' nikiwa nimekaa, nilipo simama ndio nikajua pombe sio chai.
Jasmin nae alikunywa chupa 2, ila cha kushangaza alikuwa sawa tu, tena aibu ziliondoka kabisa akachangamka hatari.
Kilichotokea nilitapika sana siku hiyo na kichwa kiliuma sana.
Namuona kabisa Jasmini amevua nguo, mapaja yananiita, chuchu zimesimama ila nguvu ya kusimama sina.[emoji3064]
(alipoingia alivua shati na sketi ili visijikunje, akavaa t-shirt ilikuwepo hapo mdami na taulo).
'kwanza bia chungu sijui wanazipendea nini'
Nililala toka saa 6 mchana mpaka saa 9 jioni mda wa kurudi shule, Jasmin muda wote amenilaza mapajani mwake mimi sijielewi, ilipofika jioni ikabidi aniamshe ili turudi shule na wenzetu.
Waliosema pombe sio chai hawakukosea, sikupata tunda la Jasmin wangu siku hiyo.Nikawa nimefanya harakati za dr. Pimbi wa jarida la sani , nilishindwa hata kumsindikiza nikamfungulia mlango akaondoka.
Nikaoga maji baridi nikalala hapo hata chakula hakipandi, nilimwambia sitaweza kwenda shule nikiwa vile, ilikuwa jumamosi nikapanga niende jumapili.
Nilimpanga kaka kuwa siko vizuri, kesho yake nikazuga kwenda kupima malaria ili nipate cheti cha hospitali nikaende shule.
……….
Baada ya siku hiyo hatukupata tena nafasi kama ile, tuliendelea na mapenzi ya nadharia tu.
Kumbe Jasmin alikuwa anatembea na mwanajeshi flani wa ruhuwiko kj, ndie alimfundisha kunywa pombe, sijui walikutanaje[emoji35]. Ila akiwa na mimi ananipanga kuwa hakuna zaidi yangu, sijawahi ufanya, kumbe ni kungwi.
Ndio yale yale ya Kelly Rowland kwenye wimbo dilemma anasema
'Boy, you know I'm crazy over you,
No matter what I do.
All I think about is you
Even when I'm with my boo
You know I'm crazy over you'
Just imagine, Wanawake wa hivi watafika mbinguni wamechoka sana, au huenda pia wasifike.
(ila na mimi nilizingua, sasa kama siwezi kuogelea baharini, nilifata nini ufukweni.)
**********
Kilicho sababisha nisimle Jasmin, sikuwa serious na mapenzi kipindi hicho, nilikuwa na 'enjoy' tu 'love story',akili yangu iko kwenye kitabu pekee. Mizagamuano haikuwa fun yangu tofauti na Mbawala.
Ile kitu ingekuwa inaisha, mbawala angebaki na kishungi tu cha sigara, songea girls wanamjua, matogolo wanamjua, bado mitaani.
Hatimaye Jasmin alimaliza kidato cha nne akaondoka kurudi Tanga. Likawa penzi lilio potea 'lost love' niliotea romance pekee .
…….
Adui yangu mkuu pale shule alikuwa mwalimu moja kijana hivi, alizinguana na kaka huko mtaani kisa msichana wa pale matogolo, kumbe kaka anatoka nae tangu 'binti yuko sekondari' kufika chuo akatamani pesa ya mwalimu.
Siku wamekutana mjini 'binti' yuko na mwalimu, binti akakimbia. Kaka na jezi zake akamkamata mwalimu.
Ikabidi akatoa pesa akaachiwa , baadae alikuja kujua ni kaka yangu akawa anamalizia hasira zake kwangu.
[emoji35]Nilikuja kukutana nae ukubwani pale akiba 'DIT'nikiwa na drive nilitamani kufungia break miguu mwake. Nikakumbuka K. Rogers alisema kwenye coward of the country,
"Promise me, son, not to do the things I've done
Walk away from trouble if you can
Now it won't mean you're weak if you turn the other cheek
I hope you're old enough to understand
Son, you don't have to fight to be a man"
Kwanza hakuwa ananikumbuka, nikampa lift mpaka pale utumishi, alikuwa anafatikia mafao yake.
Nikamkumbusha tukio makusudi, akanikumbuka akaishiwa pozi, nikampa elfu 30 ya nauli nikaondoka. [emoji124][emoji124][emoji124]
*******'**
Disco la majimaji hall, Songea club.
Nakumbuka majina maarufu kama maatiko (matiko) mmiliki wa buhemba hotel na Anex
Mfyule , Matunda, Mkwepo, Saadi , Matomondo alikuwa na guest house nyingi, n. K
Baada ya miaka minne kupita, tukafanya mtihani. Nilitoka Songea boys bila Kumjua mwanamke(Clean sheet). Nikaenda kunyonya kwa mama Arusha.
Usengwile sana Songea
**********
Next Jioni
View attachment 2555337