Mkasa: Wema ni akiba, usiache kutenda wema

Mkasa: Wema ni akiba, usiache kutenda wema

Part Three: Nanusurika kuuwawa.

1983 - 1989

Nikaanza maisha mapya ya kijijini tena, kijiji kilikua kidogo sana. Nilikutana na changamoto nyingine pale kitete, hakukua na mashine ya kusaga, ilitubidi kwenda mgororo kwa gari moshi kusaga, na kununua mahitaji kama vile mafuta ya taa.

Nilipelekwa shule ya msingi kitete kuendelea na darasa la 3, nilisoma hapo mwaka mmoja tu.

Kutokana na kuwa kijiji ni kidogo, nikakosa wenzangu wa kucheza nao, (hapo kambini wototo wa rika langu walikuwa wachache, kijiji kilikuwa mbali na kambi) nilianza kwenda kutembea makambako kila jumamosi.

Ukiwa mgeni pale makambako , ukinunua chai, wanakupozea kabisa, maana kuna baridi kiasi kwamba wewe mgeni huwezi sikia moto wa chai, baadae mdomo utakapo babuka ndio utajua uliungua.

Kule makambako kulikuwa na mjomba, nae ni mfanyakazi wa TAZARA kituo cha makambako.
……..
Kwenda kila jumamosi ilikuwa rahisi kwa sababu familia za wafanyakazi wote wa TAZARA walikuwa na 'free pass' ya kupanda gari moshi kwenda kokote inapofika TAZARA.

Yaani unaweza kwenda Dar mpaka Mbeya bure tu. Nilitumia hiyo nafasi kushinda kwenye gari moshi, nachotakiwa kujua ni ratiba tu za gari moshi.

Nilipendelea sana kupanda schoma (schoema-lokomotiven), hizi hutumiwa na wafanyakazi kukagua reli na kubebea vifaa vya ufundi.

Zinakimbia sana, breki za haraka kama gari. Natoka asubuhi na schoma /gari moshi ya abiria inayoenda Zambia nashukia makambako, jioni narudi na gari moshi ya mizigo 'goods' tukawa tunaita 'gusi' naenda tu kwa station master na mwambia mimi ni mtoto wa mfanyakazi flani, naomba usafiri wa kwenda sehemu flani, basi ananipatia.

Siku moja nilichukuliwa na marafiki zangu kwenda kwenye kijiji cha jirani, wao walikuwa wenyeji. Pale kitete ilikuwa ni kambi ya wafanyakazi na kulikuwa na station ila wenyeji walikuwa wanakaa pembeni kidogo. Tulienda uelekeo wa mrimba kwa miguu.

Njiani tunapita kwenye mahandaki ambayo yana giza sana, mimi kutokana na ugeni wangu nilikuwa nabeba tochi kila tukienda huko. Kunakua na giza kiasi kwamba unaweza kupishana na mtu bila kujua, labda uwe na taa, au mkutane upande mmoja (mgongane).

Uzuri ni kua kila handaki lina vyumba vidogo vidogo vingi, just in case gari moshi likikukuta humo unaingia kwenye chumba, usipoingia linakusaga maana ni njia ni nyembamba.

Hakuna nyoka kwenye handaki na wala hawasubutu kuingia kwa sababu ya mafuta yanayomwagwa 'diesel' au oil.

Kuna handaki moja refu sana linaitwa 'handaki 14', niliwahi kusimuliwa kuwa kipindi Nyerere alipokuwa anazindua hiyo reli, alikataa kupita kwenye hilo handaki ikabidi apitishwe juu ya mlima kwa helicopter. Sababu ni refu sana, kwa wasiojua handaki wanachimba mlima kutengeneza njia ya gari moshi.

Siku hiyo nimeenda na rafiki zangu kutembea uko handaki 14, ilikuwa ni kipindi cha kiangazi. Kutokana na umbali na jua kali, niliamua kurudia njiani baada ya kuchoka, wale wenzangu walikuwa wametumwa huko kijijini, mimi niliunga tu tera.

Nikiwa narudi nilipita kwenye mahandaki madogo madogo, giza likiwa limetanda ingawa nje jua kali.

Nikiwa nimekaribi sehemu ambapo wakati tunapita tuliwakuta mafundi wakiendelea na kazi, nilianza kusikia michakato ya kitu kinakanyaga majani makavu. Nikisimama na kugeuka kuangalia sioni kitu wala kusikia michakato, nikitembea naisikia.

Mazingira ya hapo yalikuwa mimi natembea kwenye mataruma ya reli nje tu ya handaki, (kwa vile kutengeneza mahandaki wanachimba mlima) yale mataruma yalikuwa chini kuna kingo za udongo kila upande na juu ya mlima ndio kuna nyasi. Kwa hiyo ile michakato ilikuwa inashuka kutoka mlimani kuja chini niliko,mkono wangu wa kulia.

Wale mafundi walikuwa sehemu tambalale,lakini kuna kona, walikiona kile kilichokuwa kinanifata bila mimi kukiona . Ikawabidi wapande kilimani ili waone kile kitu kinawinda nini pale.

Hilo eneo kitete liko jirani na mbuga ya wanyama ya seluu. Wakiwa hapo mlimani waliniona mimi niko pale chini natembea huku nikigeuka mara kwa mara, umbali wangu na wao ulikuwa kama mita 70 tu.

Wakaanza kupiga kelele huku wakikimbilia huku niliko, kelele zao zikanishtua, ile nageuka nyuma ndio nikakiona kilichokuwa kinaniwinda. Alikuwa ni simba dume, alikuwa ananinyatia nikisimama anatulia , kwa vile majani ni marefu sana na makavu sikuwa nimemuona kabla.

Nilianza kukimbia kuwafata wale mafundi, pembeni yangu mkono wa kulia yule simba nae aliongeza spidi sasa akaacha kunyata maana nimeanza mbio. Akawa anashuka mlima ili aniwahi kwa mbele, tulikuwa sambamba ila mimi niko chini yeye juu ya mlima.

Bahati ilikuwa upande wangu maana wale mafundi walipiga risasi kule mlimani aliko simba ikabidi abadili uelekeo. Nikiwa kama mita 15 kuwafikia wale mafundi nilianguka nikapoteza fahamu kutokana na ile hofu.

Nilikuja kuzinduka mida ya jioni kama saa 10 maana muda ule wa tukio ilikuwa saa 6 mchana . Baada ya kupata chakula wafanyakazi wenzake baba walikuja kunipa pole kwa mkasa ule. Sikuwa na haja ya kueleze kitu chochote kwa kuwa wale mafundi walieleza kuhusu lile tukio zima.

Kumbe ilikuwa ni kawaida kipindi cha kiangazi, wakati wa mavuno kijijini, wanyama mbali mbali walikuwa wanaingia vijijini kutafuta chakula mashambani na maji. Mimi na ugeni wangu sikuwa nafahamu hilo.

Wafanyakazi wa TAZARA walikuwa na magobole kwa ajili ya usalama wao wawapo porini kwenye kazi zao.

Siku moja usiku mzee wangu alinionyesha simba waliokuja pale kijijini. Walikuwa wawili, macho yao yalikuwa yanawaka kama tochi usiku, wale simba walikuwa kwenye kilima wanashuka. Watu pale kambini wakapiga risasi hewani wale simba wakakimbia.
…………..

Ndani ya A city….
Baada ya tukio lile mama alipopata habari alimwambia baba nirudi nyumbani maana kule sio salama kwangu. Mzee wangu hakupinga maana na yeye alipata uhamisho kipindi hicho, kwenda makao mkuu pale TAZARA Dar es Salaam, kule kitete alikuwa station master. Alipanda cheo akahamishwa .

Mzee aliamua mama ahame kule kijiji ''X'' ahamie mjini afanye biahara. Alitaka mama amfate Dar lakini Mama alichagua kuhamia mkoa wa Arusha kwa kuwa alikuwa amekulia huko.Anaoufahamu vizuri kuliko Dar.

Pia ingekuwa rahisi kurudi nyumbani kuangalia maendeleo ya mashamba maana sio mbali kwenda ''X'' kulinganisha na Dar.

Mzee aliuza ng'ombe wote na mbuzi, alinunua nyumba eneo la Sakina Arusha.

Pia Alinunua shamba la migomba lililokuwa jirani na hiyo nyumba, akajenga nyumba za wapangaji.

Mama hakutaka kukaa kwenye nyumba iliyonunuliwa maana ilikuwa ya slope. Mzee akaibomoa na kujenga nyumba nyingine kubwa na nzuri pale pale.

Mimi nilihamia Arusha kwa mama, baada ya baba kuondoka kitete, nilipata shule ya msingi 'Sanawari' nilisoma hapo darasa la 4 mpaka nikamalizia hapo elimu ya msingi mwaka 1989.
……….

Mama alifungua biashara zake akawa anafanya, alikuwa na duka la nguo na restaurant maeneo ya mjini kati.

Matokeo yalipotoka nilipangiwa shule ya Songea boys,(miaka ile Sera ya Nyerere ya kutoa wanafunzi mikoa ya kaskazini kwenda kusoma
mikoa ya kusini, wa kusini anaenda kanda ya ziwa nk ilikuwa bado inafanya kazi) 'narudi tena kwa mjeda',

Mama aliwasiliana na kaka, alimweleza kuhusu mimi kupangiwa shule huko aliko . Mama alimuomba kaka asije kufanya kama yale ya nyuma , kaka yangu Edward alimhakikishia mama kutonifanyia ukatili wowote ule, alisema kipindi kile ni ile hali ya kutoka depo ilisababisha ila kwa sasa amekuwa.

**********

Next Jioni.
View attachment 2553641View attachment 2553642View attachment 2553643View attachment 2553644View attachment 2553645

simba akikukuta humu unatoboa kweli?🤔🤔🤔🤔!

Kwanini nyerere aligoma kuingia handakini au alihisi kategewa kitu au hahaha!! Kiongozi machale bana!
 
simba akikukuta humu unatoboa kweli?[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]!

Kwanini nyerere aligoma kuingia handakini au alihisi kategewa kitu au hahaha!! Kiongozi machale bana!
Sijawahi kusikia kama simba amewahi ingia kwenye handaki.
Nyerere aliogopa kujizika humo. Alihisi linaweza poromoka
 
Part Four: Maisha ya ujana

1990 - 1993

Nilienda Songea kwa mara ya pili tena, kwa ajili ya masomo ya secondary.

Nilipelekwa ku-report pale Songea boys aka box 2, nilianza form one pale, nikikaa bweni la ujamaa.

Maisha ya boarding school ni shida sana. Kule nguvu yako ndio pona yako. Ukiwa mnyonge utaonewa na kila mtu. Harakati za ugali na mchuzi wa maharage, yaani mpaka ukutane na maharage ndani ya bakuri una bahati, hayazidi 10.

Kipindi cha kula wali, tunachanga hela anapewa mpishi wa shule, hapo tuna uhakika wa kupata wali sado nzima (ni mchango) .

Sikuwa mtundu wala mkorofi, nilichofanya ni kujipendekeza kwa mbabe mmoja pale skonga, nikawa kila jumapili lazima nimletee sabuni au mafuta, siku zingine chakula cha nje ya shule. Nikawa ma ulinzi wa uhakika.

Siku moja kuna form 4 watatu walitaka kunipigisha simu chooni. (unainama kwenye tundu la choo cha shimo, unaongea na ndugu zako nyumbani, kuwasimulia maisha ya shule jamaa wanakulinda hapo).

Bahati zuri rafiki yangu aliniona, akamshtua mlinzi wangu kabla hatujafika chooni. Siku ile ilikuwa hatari, zilipigwa hapo, maana wale form 4 walikuwa watatu na jamaa peke yake, ila aliwakalisha. Tangu hapo nikawa naogopwa, maana wameshajua nina mtetezi.

Jamaa alikuwa na tabia ukiingia kwenye kumi na nane zake anakuwinda usiku ukiwa peke yako, anamalizana na wewe.

Nilipofika form 3 nilienda mchepuo wa biashara. Pale shule nilikuwa mkali kiasi wa Book keeping na Commerce darasani kwangu.

Nilikuwa mkimya sana tena sana. Tena nimetoka maisha ya raha kwenda kuishi kama tuko jeshini kulinisumbua sana mwanzoni. Mtu akinikwaza naweza nisimjibu hata kama ni mwalimu, nilikuwa bado sijajua kuwa boss hanuniwi.

Darasa zima nilikuwa mkimya namba 1, baadhi ya wenzangu waliniogopa sio kwa ubabe ila ukimya wangu, sikuwa na socialize nao.

Wengi wakawa wanasema mtu mkimya ukipigana nae anaweza kukuua, lakini sikuwa mgonvi, nilikuwa muepusha shari, hata kama nakuweza na kupotezea tu.
…..

Maisha ya shule yalikuwa mazuri baada ya kuzoea mazingira na kuanza kujichanganya.

Ilikuwa kila jumapili naenda kwa kaka. Kipindi hicho kaka alikuwa amepata nyumba pale kota za polisi maarufu kama 'line police' jirani na geti la samco(nahisi ni jina hilo) .

Alininunulia baiskeli ya gia kipindi hicho ndio zinaanza kuonekana mtaani. nikawa naitumia kila ninapo enda kwake, nikiondoka inafungiwa.

(Watoto wa kihindi ndio walikuwa nazo sana.)

Nikaanza kuuzoea mji, nikawa nazunguka zunguka mara line police, matarawe, msamala, mahenge 'maji maji memorial museum' bomba mbili, mfaranyaki, misufini, majengo, ruvuma, mateka, rizaboni, kiburang'oma, Ruhuwiko, Ruvuma day, nk

……….

Nikiwa kidato cha tatu nikainginzwa kwenye michakato ya wasichana. Nilikuwa na 'room mate' mwanangu sana anaitwa Mbawala, alikuwa ni mwenyeji wa mbinga. Akawa ndie 'tour guider wangu kunionyesha mahindi yaliyokomaa na yale teketeke '.

(alikuwa sekondari ila ana phd ya kujua wasichana, ananiambia huyu ametumika sana, huyu bado mang'anyu)

Alikuwa anapenda sana mabinti. Huyu jamaa alikuwa hachagui awe mmama, mdada, lishangazi, yeye anapita nao tu. Mimi hata paja sijawahi ona kipindi hicho. Lakini mwamba anajua mpaka chunvini, akirudi story ni hizo tu bwenini.

Nahisi aliesema

.. mngoni mpe hela atakufikishia ila mkeo…,
alikutana na watu kama Mbawala. (wangoni ni shemeji zangu, lazima niwatanie[emoji3])

Tukaanza 'route' za' matogolo teachers college' kufata wasichama ila wana chuo walikuwa wakubwa, chimbo la maana ni 'songea girl', kuna watoto wabichi. Unamlia chunvi na ndimu ili upate radha.

(kama mahindi ya kuchoma ya dar[emoji16])

Katika hiyo michakato nilipata mpenzi sponsored by Mbawala , Jamaa alinitongozea wasichana 3, nikiwa bado nashanga shangaa akawala wawili. Hapendi ujinga yule mwamba. Nikabaki na mdigo mmoja hivi anaitwa Jasmin.

Alikuwa binti wa kidato cha nne, alikuwa na hips na makalio makubwa. Akivaa sketi ya rinda box, tena fupi, lazima ugeuke mkipishana hata kama ndio umetoka kuungama.

(Maumbo wa wasicha yanawaponza sana kwa wanaume wakwale, wengi wao wanaliwa kabla ya kukomaa sababu ya shapes zao)

Mtoto alikuwa mzuri sana , ngozi nyeupe na nyororo.

Waliosoma ' boarding school' wanalijua hili, mabinti wanakuwa na moto sana wa kufanya ngono, muda wote wana genye. Ila na mimba nazo kipindi hicho msipokuwa makini ni kugusa tu imo.

Jasmin alikuwa amechangamka sana, ana aibu kiasi, sauti nyororo. Tulianza rasmi mapenzi ya kutumiana kadi kila jumapili.

Tulikuwa tunakutana pale kanisa la romani karibu na stand kuu kipindi hicho, tunaishia kupiga story pekee, na tukipata nafasi tuna dendeka basi. (nasikia stendi imehamia msamala).

Ukiotea denda unaikumbuka wiki nzima, mimi nilikuwa sina mambo mengi, nikipewa denda na nikashika titi basi, huko baharini sina habari nako.

(kwanza sikuwa najua kuogelea nisije zama bure.)

Alikuwa na counter book limejaa mistari ya nyimbo za mapenzi za kizungu, na picha za wasanii.

Mara kwa mara tuli badilishana barua za mapenzi, mwenzangu alikuwa mkali wa nyimbo za mapenzi.

Tulikuwa tukitoka hapo kanisani tunasindikizana mpaka shuleni kwao, kisha naenda box 2.

Kuna umbali mrefu hapo ila mbele ya binti unaweza toka posta mpaka kimara kwa mguu na huchoki.

Kuna siku nilimpa denda na kiss za hatari uchochoroni, kumbe nimegusa sensitive part yake, kidogo tufumwe. Wiki iliyofata nikapewa barua nikaambiwa nikaisomee shuleni.

Mtoto alitoa ya moyoni siku ile, nahisi ni moja ya barua iliyosomwa mara nyingi ndani ya wiki moja, kabla ya 'prepo' naanza na barua ya Jasmin.

(mtoto alikuwa na hamu, mwamba sijui lolote.) .

Moja ya dedication iliyoambatana na barua [emoji116]

Song: 'How Sweet It Is
(To Be Loved by You)
Singer: James Taylor
Released: 1975,
Album: Gorilla
Genre: Folk,
Songwriters: Lamont Dozier / Brian Holland /Edward Holland

How sweet it is to be loved by you
How sweet it is to be loved by you
I needed the shelter of someone's arms
And there you were
I needed someone to understand my ups and downs
And there you were
With sweet love and devotion
Deeply touching my emotion

I want to stop and thank you, baby
I wanna stop and thank you baby, yes I do
How sweet it is to be loved by you
Feels so fine
How sweet it is to be loved by you

I close my eyes at night
Wondering where would I be without you in my life
Everything I did was just a bore
Everywhere I went it seems I'd been there before
But you brighten up for me all of my days
With a love so sweet in so many ways

I wanna stop and thank you, baby
I just wanna stop and thank you baby, oh yes
How sweet it is to be loved by you
It's like sugar sometimes
How sweet it is to be loved by you
You were better to me than I was to myself
For me, there's you and there ain't nobody else

I wanna stop and thank you, baby
I just wanna stop and thank you baby, oh now
How sweet it is to be loved by you
How sweet it is to be loved by you
How sweet it is to be loved by you
It's like jelly, baby, oh now
How sweet it is to be loved by you, oh now
How sweet it is to be loved by you
Just like honey to the bee baby, yeah now
Na, na, na, to be loved by you

Wakali wa hizi kazi nazani mnajua hali unayokuwa nayo ukisoma barua yenye ujumbe kama huo. Tena inatoka kwa mtu unaempenda.

Lazima tabasamu likuponyoke bila kupenda, tena unaweza kuongezea na kicheko hafifu kama vile chizi kaona jalala jipya.

'to myself i was like I'm ni paradise already'
……….

**********
Next Tomorrow

Table.jpg
Songea%20boys.jpg
Mwonekano%20wa%20Jasmin%20.jpg
Maji%20maji%20stadium.jpg
Songea%20girls%20.jpg
Gari%20la%20wababe%20wa%20box%202.jpg
 
Attachments

  • Mama%20.jpg
    Mama%20.jpg
    43.3 KB · Views: 80
  • Maji%20maji%20memorial%20museum2.jpg
    Maji%20maji%20memorial%20museum2.jpg
    74.5 KB · Views: 77
  • Mama%20.jpg
    Mama%20.jpg
    43.3 KB · Views: 81

Tukiacha ubabe wa shule za boarding, tulikuwa wababe kwa wanafunzi wa chuo cha ualimu matogolo , maana shule yenye form 1 - 6 mchanganyiko toka mikoa tofauti, haikuwa rahisi kui handle.

Matogolo ni jirani, kuna wasichana na sisi tunawataka , na ma boy wao hapo chuo wanawataka.

Ni mwendo wa bifu za mapenzi na mambo mengine, kuna wale wanywa ulanzi wakiwashiwa moto, wanaleta taarifa jeshi la box 2 linaenda kumaliza kazi. Nilikuwa doja wa hatari kwenye matukio kama hayo.

Siku moja mbawala aliniambia nimsindikize rizaboni , ilikuwa siku ya jumapili, (kila jumapili tunaruhusiwa kutoka kwenda kanisani mwisho saa 10 jioni)

Tumefika rizaboni , kumbe mwamba amemfata mtoto wa mwanajeshi, wamesimama wanaongea pembeni ya njia, akaibuka mtu migombani mara jamaa ameshikwa. Binti akachanganyikiwa, nikaunganishwa na mimi.

Kumbe ni baba yake na binti, akatupeleka kambi ya jeshi pale Ruhuwiko, wakatupatia machangu matatu ya adhabu.

La kwanza, tufanye kama tunaendesha gari, tunashikana mashati, tuzunguke jengo flani pale mara 100 kisha tupotee

(Hapa kuna konda na dereva, unatakiwa usimame uite abiria, uchukie nauli, mpige story, hope unajua watoto wakicheza lazima kila kitendo wakielezee)

La Pili wawashe moto, tukae kuota hapo juani kama saa 7 /8 hivi, moto ukizima tupotee.

(moto wenyewe kuni kubwa sio wa mabua na ni kiangazi mko juani).

La tatu tuletewe wali ndoo ndogo umejaa, tuhakikishe umeisha kisha tupotee.

(watu wawili wali ndoo ya lita 10, hakuna kudondosha, akishindwa kumaliza mnapiga push up kuita njaa, mnarudi kumalizia.)

Siku hiyo ndio nilichukia kazi ya jeshi, tuliona option ya kwanza ni nafuu, nikawa dereva mwenzangu konda.

Kazi yangu mungurumo wa gari na honi visikike, mwenzangu ahakikishe anapiga debe kuita abiria, adai nauli, awakemee abiria wakorofi nk

(matukio yote common yanayotokea kwenye daladala yasikike loud and clear. )

Baada ya rounds 50 wakatufukuza, na kupewa onyo tusionekane na yule binti tena. Tumetoka yule boya anacheka eti.

Baada ya wiki tatu anasema yule binti amemtumia ujumbe, wakutane mfaranyaki, nikatoka nduki maana nisije ponzwa tena. [emoji125][emoji125]
…….

Mara nyingi kipindi cha likizo nilikuwa nakaa wiki 1 Songea na 3 Arusha kwa mama.

Kuna kipindi niliachiwa chumba na rafiki yake kaka (askari), alienda kusoma, ilikuwa likizo ya pasaka.

Likizo Ilipoisha niliacha funguo kwa kaka, ila ikawa kila nikienda nalala kwenye kile chumba.

Siku moja kulikuwa na michezo ya kishule, tukaenda uwanja wa zimani moto. Michezo ikiwa inaendele pale zimani moto. Nilimpanga mdigo wangu tukatoe 'singo' akakubali nikam 'pack' kwenye kile chumba.

Kilikuwa chumba cha 4 kutoka geti kuu la kuingia uwanja wa maji maji mkono wa.......[emoji119]

Lengo langu lilikuwa akae kwa muda pale ili mchezo ninao shiriki, ukiisha tupongezane kwa mara ya kwanza, nilikuwa nacheza 'volleyball' na nilikuwa kwenye Playlist vinginevyo ninge doji.

Yeye alikuja kama mshangiliaji tu hakuwa na mchezo anaoshiriki, ni wale 'usiniumizie'.

Lengo langu halikutimia, niliponzwaa kijinga, waswahili walisema usilolijua ni usiku wa giza.

Jasmin alinishawishi tunywe pombe kidogo, mwenzangu alikuwa mzoefu, nikajidanganya nikanywa ili mtoto asinione wa kuja hata bia sinywi.

' hivi vile vijumba vya nyasi kwenye ile chupa ya safari vina maana gani?'

Ndio mara ya kwanza na ya mwisho kuonja pombe, nilikunywa chupa 2 za 'safari lager' nikiwa nimekaa, nilipo simama ndio nikajua pombe sio chai.

Jasmin nae alikunywa chupa 2, ila cha kushangaza alikuwa sawa tu, tena aibu ziliondoka kabisa akachangamka hatari.

Kilichotokea nilitapika sana siku hiyo na kichwa kiliuma sana.

Namuona kabisa Jasmini amevua nguo, mapaja yananiita, chuchu zimesimama ila nguvu ya kusimama sina.[emoji3064]

(alipoingia alivua shati na sketi ili visijikunje, akavaa t-shirt ilikuwepo hapo mdami na taulo).

'kwanza bia chungu sijui wanazipendea nini'

Nililala toka saa 6 mchana mpaka saa 9 jioni mda wa kurudi shule, Jasmin muda wote amenilaza mapajani mwake mimi sijielewi, ilipofika jioni ikabidi aniamshe ili turudi shule na wenzetu.

Waliosema pombe sio chai hawakukosea, sikupata tunda la Jasmin wangu siku hiyo.Nikawa nimefanya harakati za dr. Pimbi wa jarida la sani , nilishindwa hata kumsindikiza nikamfungulia mlango akaondoka.

Nikaoga maji baridi nikalala hapo hata chakula hakipandi, nilimwambia sitaweza kwenda shule nikiwa vile, ilikuwa jumamosi nikapanga niende jumapili.

Nilimpanga kaka kuwa siko vizuri, kesho yake nikazuga kwenda kupima malaria ili nipate cheti cha hospitali nikaende shule.

……….

Baada ya siku hiyo hatukupata tena nafasi kama ile, tuliendelea na mapenzi ya nadharia tu.

Kumbe Jasmin alikuwa anatembea na mwanajeshi flani wa ruhuwiko kj, ndie alimfundisha kunywa pombe, sijui walikutanaje[emoji35].

Ila akiwa na mimi ananipanga kuwa hakuna zaidi yangu, sijawahi ufanya, kumbe ni kungwi.

Ndio yale yale ya Kelly Rowland kwenye wimbo dilemma anasema
'Boy, you know I'm crazy over you,
No matter what I do.
All I think about is you
Even when I'm with my boo
You know I'm crazy over you'

Just imagine, Wanawake wa hivi watafika mbinguni wamechoka sana, au huenda pia wasifike.

(ila na mimi nilizingua, sasa kama siwezi kuogelea baharini, nilifata nini ufukweni.)

**********
Kilicho sababisha nisimle Jasmin, sikuwa serious na mapenzi kipindi hicho, nilikuwa na 'enjoy' tu 'love story',akili yangu iko kwenye kitabu pekee. Mizagamuano haikuwa fun yangu tofauti na Mbawala.

Ile kitu ingekuwa inaisha, mbawala angebaki na kishungi tu cha sigara, songea girls wanamjua, matogolo wanamjua, bado mitaani.

Hatimaye Jasmin alimaliza kidato cha nne akaondoka kurudi Tanga. Likawa penzi lilio potea 'lost love' niliotea romance pekee .
…….

Adui yangu mkuu pale shule alikuwa mwalimu moja kijana hivi, alizinguana na kaka huko mtaani kisa msichana wa pale matogolo, kumbe kaka anatoka nae tangu 'binti yuko sekondari' kufika chuo akatamani pesa ya mwalimu.

Siku wamekutana mjini 'binti' yuko na mwalimu, binti akakimbia. Kaka na jezi zake akamkamata mwalimu.

Ikabidi akatoa pesa akaachiwa , baadae alikuja kujua ni kaka yangu akawa anamalizia hasira zake kwangu.

[emoji35]Nilikuja kukutana nae ukubwani pale akiba 'DIT'nikiwa na drive nilitamani kufungia break miguu mwake. Nikakumbuka K. Rogers alisema kwenye coward of the country,

"Promise me, son, not to do the things I've done
Walk away from trouble if you can
Now it won't mean you're weak if you turn the other cheek
I hope you're old enough to understand
Son, you don't have to fight to be a man"

Kwanza hakuwa ananikumbuka, nikampa lift mpaka pale utumishi, alikuwa anafatilia mafao yake.

Nikamkumbusha tukio makusudi, akanikumbuka akaishiwa pozi, nikampa elfu 30 ya nauli nikaondoka. [emoji124][emoji124][emoji124]

*******'**
Disco la majimaji hall, Songea club.

Nakumbuka majina maarufu kama maatiko (matiko) mmiliki wa buhemba hotel na Anex
Mfyule , Matunda, Mkwepo, Saadi , Matomondo alikuwa na guest house nyingi, n. K

Baada ya miaka minne kupita, tukafanya mtihani. Nilitoka Songea boy bila Kumjua mwanamke. Nikaenda kunyonya kwa mama Arusha.

Usengwile sana Songea

**********
Next Tomorrow

View attachment 2553963View attachment 2553969View attachment 2553973View attachment 2553974View attachment 2553975View attachment 2553976View attachment 2553977
Pole sana leadermoe kwa kutoka Songea bila kufaidi .

Ila umenirudisha mbali kidogo kipindi cha mwaka 92 nikiwa likizo fulani .

Nilibahatika kumpata binti wa jeshi hapo Chabruma kambini karibu na mitaa ya lilambo ila baadae akahamishiwa Ruhuwiko ila nilienjoy sana kuwa naye huko kwa wangoni .

Ila nilikuja kufulumushwa na kijana mwenzio aliyekuwa anamkaa mimi nikiwa sipo .

Ikawa mara yangu ya kwanza na mwisho kuwa Songea ila hii mitaa naikumbuka kama leo , Matalawe , Bomba mbili na mitaa ya Kotazi hapo Chabruma .
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Sawa mkuu. Watoto wa kingoni noma sana.
 
Back
Top Bottom