Mkasa: Wema ni akiba, usiache kutenda wema

Mkasa: Wema ni akiba, usiache kutenda wema

Safi sana chief picha ya train ikitoka kwenye handaki imenikumbusha 2021 nilipanda hiyo chuma toka makambako ifakara.

Reli ya mwendo kasi inayojengwa kipande cha Kilosa uelekeo wa Dodoma pia kuna hizo tunel za kutosha. Sema hizo anazojenga mturuki kipande hiyo zimeboreshwa, kule juu ya handaki kwa ndani kuna taa mwanga wa kuzidi.

So far story iko vyedi ila mwamba unaonekana muhenga [emoji23][emoji23]
Ile ilijengwa na mchina 1975. Hii ya mturuki ni kizazi kipya
Bado sijafikia uhenga, bado ni kijana mdogo kabisa[emoji16]
 
Kweli Kabisa cuzoo akee!
Siku nyingine tena haohao mawifi nilienda nao Pub fulani wakanifundisha kunywaa waliniambia eti nichanganye Serengeti lite na energy zile zakopo kuwa sitalewa Nakumbuka hio Siku nilikunywa Serengeti lite 3 na energy mbili ila kukojoa kojoa sasa mkojo unabana kila dakika pombe[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]!! Gily
Serengeti na energy [emoji298]. Pole sana
 
πŸ˜€πŸ˜€Sipat picha ilikuwaje kunawatu wanazipiga balaa Kuna boss wangu yeye alikuwa anakunywa km kishushio Cha chakula yaaniπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ kuna Watu wasopokunywa siku mbili wanaumwaπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ˜‚πŸ˜‚!
Mi hapana labda naonjaonja wine zisizo na kilevi kuweka akili sawaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ngoja kwanza hivi kipindi unasoma songea boys ile barabara ya songea Njombe ilikuwa na lami?

Anyway songea napafahamu na kuna baadhi ya maeneo uliyotaja nayaelewa mzee. Big up sana chief. Mara ya mwisho kwenda ilikuwa mwaka jana mwezi Oktoba.
Barabara ilikuwa vumbi tu, tena hata ile ya kwenda tunduru mpaka mtwara vumbi mbaya.
 
Sis Kalpana sisi kwenye joint mass tulikua tunacompete na wasichana wa kilakala tunagombania boys wa mzumbe na wengine wanatoka na wanachuo wao( mzumbe) Ila mi nilikua na mwamba wa SUA 2 nd Year πŸ˜„πŸ˜„!
Uweeeee sisyyy...labda unambie ulikua A level hahaahha ila kama ni o level alikua mkubwa sana..hao enzi zetu o level mtu akiwa na mchumba form 5 au 6 tunaita vidato..hahah
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ kuna Watu wasopokunywa siku mbili wanaumwaπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ˜‚πŸ˜‚!
Mi hapana labda naonjaonja wine zisizo na kilevi kuweka akili sawaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Na Walevi wanapenda na kilamtu mtu awe anakunywa ukitaka kuamini muombe elf 20 hawez kukupa ila yukoradh akununulie pombe za elf 50πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
leadermoe
Ulipotaja Lizaboni, nimekumbuka kitongoji kingine kinachoitwa Londoni...
Wangoni majina haya ya miji ya Ulaya waliyapendea nini?

Anyway, zaidi Songea Club na Majimaji hall, kulikuwepo na NBC Club.... club ya kwanza kwanza kupiga boogie hapo Songea.
Hapo londoni ndio kulikuwa na mitambo ya tanesco.
Wangoni ni wa South Africa, wako kiulaya ulaya tu.

Mkuu wewe ni mwenyeji sana kumbe.
 
Uweeeee sisyyy...labda unambie ulikua A level hahaahha ila kama ni o level alikua mkubwa sana..hao enzi zetu o level mtu akiwa na mchumba form 5 au 6 tunaita vidato..hahah
Advance hio sis mi form 5 ye 2nd year !! Outing day ni kwa mwamba tu πŸ˜‚πŸ˜‚! Ananinunulia chips mayai mishikaki na soda nakula tukimaliza Nakumbuka alikua ananikanda na mabarafu mwili mzima ananifuta vizuri kisha anaenda kuniogesha πŸ€­πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ !
Life la boarding na ujana bana!!
 
Advance hio sis mi form 5 ye 2nd year !! Outing day ni kwa mwamba tu [emoji23][emoji23]! Ananinunulia chips nakula tukimaliza Nakumbuka alikua ananikanda na mabarafu mwili mzima ananifuta vizuri kisha anaenda kuniogesha [emoji2960][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] !
Life la boarding bana!!
Tobaaaaa cousin wa mtu anafanyiwa hivyo kweli [emoji23][emoji23]
 
Part Five A: In every life we have some trouble.

1993-1994

Baada ya mtihani wa kidato cha nne, nilirudi kwa mama Arusha. Nilikuta biashara zake zimechanganya hivyo basi akawa bize sana. Pia alikuwa ameshafanya maendeleo pale nyumbani pameboreka sana.

Siku zote nikiwa na mama alikuwa anapenda kunipa usia sana kuhusu maisha, kuheshimu watu wote, kusamehe, kutoa msaada pale ninapoweza , kushiriki vitu na wengine na kikubwa zaidi kumuomba Mungu.

Nilimpenda sana maana na yeye alinipenda sana kuliko watoto wake wote.

Pamoja na upendo alinifundisha kupika nikiwa mdogo sana, tena tunafanyiana zamu ya kupika na kuosha vyombo bila kujali huyu ni mama.
……..

Nikawa niko mtaani tu nikisikilizia matokeo. Mzee alikuwa anamiliki nyumba za wapangaji mimi nikawa ndio bosi wao wa kufatilia kodi. Maisha nyumbani yalikuwa safi kiaina sio ile saana, ila pesa ya kutesea mtaani ilikuwa haikauki.

Nilikuwa na tabia ya kufanya jogging asubuhi saa 11 kila siku, natoka hapo nyumbani sakina mpaka pale chuo cha habari maalum.

Kama kawaida yangu sikuwa na marafiki wengi walikuwa wa nne tu na kati ya hao mmoja ndie nilikuwa nae karibu sana anaitwa Frank.

Jogging nilikuwa nafanya na huyu Frank wengine walikuwa wavivu nilikuwa nakutana na Frank pale sakina super market tunaliunga mdogo mdogo mpaka ngara mashamba ya serikali karibu na Habari maalum.

Siku moja nimetoka zangu home saa 11:00 nashuka mdogo mdogo, kuna semehu kulikua na shamba kubwa la migomba, huwa kuna giza sana hapo.

Nilipokaribia hilo eneo nikaona gari nyeusi imesimamishwa kwenye shamba la migomba.

Kipindi hicho Arusha ujambazi uko juu sana, sikuwa na hofu maana mida hiyo kuna watu wanaokwenda kufata nyama pale Arusha meat wanakuwa njiani.

Nika punguza mwendo ili nijue lile gari ni la nani na kwa nini liko migombani kama limefichwa, (ni shamba letu) lile shamba la migomba linapakana na nyumba za wapangaji wetu.

Sikufanikiwa kulikaribia gari maana nilihisi kama limeibiwa naweza pata matatizo na vyombo vya dola, au labda kuna mpuuzi kajificha pale ili kufanya ngono kwenye gari.

Ilikuwa kawaida sana kukuta mtu amepaki gari anafanya ngono maana njia yenyewe haikuwa busy sana na migomba ilikuwa mingi kwenye hilo eneo. Ikanibidi niendelee na safari zangu.

Nilikutana na Frank sakina supermarket, ilikuwa meeting point yetu. Tukaunga mpaka kwa idd akasema hajisikii vizuri ikabidi turudie hapo. Ikabidi nimwambie twende nyumbani maana ni karibu sana kuliko kwao.

Frank alikuwa anaishi jirani na 'Arusha Technical college' kama unaelekea mianzini. Wakati napandisha nikiwa na Frank tukalikuta lile gari pale pale, nikamwambia kuwa imekuwa pale toka nashuka.

Tukashauliana tusisogee maana tulihisi tu limeibiwa hatukutaka kujitafutia matatizo. Tukaenda nyumbani.

Ilikuwa 12:30 wakati tunarudi, kulikuwa kume pambazuka, Frank alioga akanywa paracetamol akalala.

Mimi nikatoka ili nikaangalie kama lile gari bado lipo, nikalikuta liko pale pale.kutokana na utundu niliotoka nao Songea boys ukiongeza mazoezi nikawa najiamini sana.

'kama pawa mabula au pawa suzuki vile,' .

Kutokana na tabia ya kufanya mazoezi nikapata ujasiri nikalisogelea maana tayari kulikuwa kume pambazuka na watu wako njiani wengi tu.

Nilipokaribia nikachungulia mbele nikaona mtu amekaa ananiangalia ila amefungwa kitambaa mdomoni. Alipo niona akawa anatikisa kichwa tu mwili umekaza nilitulia pale huku najiuliza nifanyeje.

Nikapata ujasiri wa kusogea karibu, nikamuona vizuri alikuwa ni mzungu ila amekuwa mwekundu kutokana na kamba alizofungwa. Akanipa ishara nikafungua mlango wa mbele, nilimkuta amefungwa kwenye siti ya dereva, miguu imefungwa kamba, amekalishwa kwenye siti na mikono imefungwa nyuma ya siti. Kamba zilipita karibu na mabega hivyo alishindwa hata kujitikisa kwa jinsi manila zilovyokuwa zimebana.

Usoni alifungwa kitambaa ili asipige kelele. Mpaka wakati huo akili ilisimama nisijue la kufanya, ghafla nikapata ujasiri wa kumfungua kitambaa cha mdomoni ndio akaanza kuongea ila kinyonge sana.

Baada ya kumfungua kamba zote, na yeye akajaribu kushuka kwenye gari ila akashindwa kusimama akajimwaga chini. Nilimsaidia kumkalisha akaegemea gari, akawa ananiambia
"Help my wife and my daughter pls. "

"Frankly, I was curious about what was happening there."


Today is Friday, Next later today
Table.jpg
Prado%20.jpg
Sakina%20to%20ngara.jpg
 
Tobaaaaa cousin wa mtu anafanyiwa hivyo kweli [emoji23][emoji23]
πŸƒπŸ»β€β™€οΈπŸƒπŸ»β€β™€οΈπŸƒπŸ»β€β™€οΈπŸƒπŸ»β€β™€οΈπŸƒπŸ»β€β™€οΈπŸƒπŸ»β€β™€οΈπŸ€£πŸ€£πŸ€£Ujana maji ya moto cousin😁😁!
 
Back
Top Bottom