Mkasa: Wema ni akiba, usiache kutenda wema

Mkasa: Wema ni akiba, usiache kutenda wema

Kwahio ile ya wafinland inaendelea hapa [emoji848][emoji848][emoji848]???
Ile ilikuwa kipande tu. Niliikatisha ili nimalizie kuiandaa
Hii historia ya familia yangu tangu 1939-2023. Bado niko 1994

Finland inaendele hapa kwa details zaidi, kumbuka mwisho kule nili summarize. (finland, munich,...... )
 
Ile ilikuwa kipande tu. Niliikatisha ili nimalizie kuiandaa
Hii historia ya familia yangu tangu 1939-2023. Bado niko 1994

FFinland inaendele hapa kwa details zaidi, kumbuka mwisho kule nili summarize. (finland, munich,...... )
Sawa mkuu hii nimeweka nukta kwenye shamba la migomba ulipoona gari.

Enjoy your evening guys 🚶🏻‍♀️
Ntarudi
 
Mpendwa msomaji.

Kama ulisoma mkasa[emoji116]
(Nilivyo Okoa Maisha Ya Watalii toka Finland).
Huu ni mkasa kamili wa kisa kile. Nilielezea visa vichache kwa ufupi, maana lengo lilikuwa msaada wa Kuokoa Watalii.

Hapa utapata historia nzima ya maisha yangu na mwendelezo wa ule mkasa na wale watalii in details. Ni mkasa mrefu, ila nitajitahidi kumaliza kwa wakati.

Angalizo: Lengo ni kujifunza, kupitia mapito ya wenzetu, sina maana ya kutaka kuonyesha nilicho nacho.
******'

Maisha na mapito yangu hapa duniani.

Nimeusimulia kwa urefu zaidi tofauti na ile Simulizi Ya kwanza.

Tahadhari:

Picha zilizo tumika katika mkasa huu zimegawanyika katika makundi mawili:-

Kundi la 1:
Hazina uhusiano na mkasa huu, nimeziweka kama Mfano wa yale ninayoyaeleza yanavyofanana na picha husika.
(Mfano: Muonekano wa Rose [emoji257], Zainabu na Zaituni n.k)

Kundi la 2:
Zina uhusiano na mkasa huu, ila sikuzipiga mimi, ziko mtandaoni. (Mfano: majina ya Airport, maduka, hotel n.k)

Majina yote ya watu yaliyotumika sio halisi, yamebuniwa kuleta radha, Wahusika wanayo majina yao halisi.

Maelezo mengine yote ni matukio na majina halisi ya maeneo husika.

Note 'disguised'

'***********************

Utangulizi.

Katika maisha tunakutana na changamoto nyingi, mateso, kukatisha tamaa, umasikini, chuki, hasira, uongo, usariti, na mengine mengi.

Ndio maana kuna maandiko yanasema "ulimwenguni kunayo dhiki nyingi"

Huu ni mkasa unaohusu familia moja ya mzee Anthony na mke wake Antonia. Baada ya changamoto, mateso na manyanyaso mengi, hatimae Anthony anafanikiwa kuandikishwa shule, jambo ambalo baba yake hakuwa ana litaka.

Anthony anapata msaada wa kulelewa na rafiki wa baba yake, malezi ambayo baba yake hakuona umuhimu wa kumpa.

Hatimae Anthony anafanikiwa kuanza maisha mapya, anapata watoto ambao anajitahita kuwapitisha njia salama na malezi bora.

Kijana mdogo anaonekana kipenzi cha wazazi, lakini anapata heka heka kipindi cha masomo yake, yaliyopelekea kuwa mbali na wazazi wake.

Mzee Anthony anawakabidhi vijana wake majukumu, je watayatimiza?

Mama anakata kijana wake asiende kuishi ulaya, je atasikilizwa?

Fuatana nami katika mkasa huu kwani kuna mengi ya kujifunza, kuburusisha na kusikitisha.

Kiitos

***********



1939

Part One
Anthony
Anthony amezaliwa mwaka 1939 katika kijiji cha 'X', wilaya ya 'X' mkoa wa 'X'. Haiba yake ni mpole.

Ni mtoto yatima , mama yake alifariki Anthony akiwa na miaka mitatu tu. Aliugua malaria kutokana na umbali kutoka hapo kijijini ''X'' mpaka hospitali ya wilaya 'X', alipoteza maisha akiwa njiani.

Anthony amelelewa na baba yake kwa msaada wa bibi yake, bibi yake alifariki Anthony alipofikisha miaka 7. Akabaki na bana pekee.

Baba yake Anthony alioa mke mwingine, mke mdogo hakumpenda Anthony, alimtumikisha na kumtuhumu mambo ya uongo.

Siku moja mzee George alitembelewa na rafiki yake mzee John, mzee John alikuwa anaishi kijiji 'X' kiko jirani na kijiji 'X' anakoishi mzee George .

Mzee John alimkuta Anthony akifanya kazi ya kutwanga kisamvu, mama yake mdogo amekaa anakula karanga, Ilikuwa ni majira ya saa 10 jioni.

Kumbe toka asubuhi mtoto wa miaka 8 hakuwa amekula, mama yake wa kambo alipika chakula mchana akala peke yake kikaisha, mtoto aliporudi toka machungani ndio akapewa kazi ya kutwanga kisanvu, kisha kipikwe ndio ale.

Baba yake aliyajua yote hayo ila alipuuza kwa madai kuwa anamfundiasha maisha. Mzee George hakuwa amempeleka shule Anthony japo ana miaka 8.

Mzee John hakupendezwa na mazingira anayoishi Anthony, alijaribu kumshauri rafiki yake, lakini haikusaidia.

Mzee John hakupendezwa na majibu ya rafiki yake, akaomba apewe yule mtoto ili akamsomee kwake, mzee George kwa kuona anapunguziwa mzigo alikubari. Mzee John aliondoka na Anthony huku akiahidi kumpeleka shule.

………


Anthony akiwa kwa mzee John alikuwa mtoto mtiifu, mzee John na mke wake walimpenda sana. Walikuwa na watoto wawili, Paul na Antonia. Paul alikuwa darasa la 1 shule ya mission. Antonia alikuwa ni binti mdogo.

Anthony aliandikishwa shule ile ile ya mission aliyokuwa anasoma Paul, alikuwa mtiifu sana nyumbani na shuleni. Walimu wake walimpenda.

……….

Akiwa darasa la 3, walipokea taarifa ya kifo cha baba yake, nyumba yao ilishika moto akiwa amelala ndani, kutokana na ulevi mzee George alishindwa kujiokoa , akachomwa na ule moto mpaka mauti.

Mke wake alifanikiwa kukimbia, ila hakurudi tena pale nyumbani. (kulikuwa na tetesi ndie aliwasha ule moto , sababu haikujulikana).

Anthony akawa amepoteza wazazi wote wawili, akabaki yatima. Mzee John aliendelea kumlea kama mwanae bila kumbagua, alipomaliza darasa la nne, mzee John alihamia mkoa wa Arusha na familia yote.

Waliishi kijiji cha ngurudoto wilaya Meru. Akiwa arusha aliendelea kuwa kijana mwema. Alipofikisha umri wa kuoa, alimshirikisha mzee John kama baba, mzee alimwambia anapenda amuozeshe binti yake maana iliona atamfaa zaidi. Hakupenda amruhusu kuoa kabila la wenyeji wao.

Kipindi hicho Antonia alikuwa na miaka 16, ilikuwa mwaka 1962, mzee John aliamua kumuozesha kijana wa rafiki yake ili amtunzie baba yake jina, alimpa binti yake Antonia awe mke wake.

Baada ya kuoa kimira , Anthony aliamua kuhama pale nyumbani, alihamia kijiji ''X'' mkoa ''X''. Maisha mapya ya ndoa yalianza rasmi.
**********
View attachment 2552603View attachment 2552605
,Nakadori pita na hapa
 
Kijana, kabla hujaenda mbali tafadhali hariri story yako ili kuleta maana.

Mkoa 'Disguised' wilaya 'Disguised' Kijiji 'Disguised'.

Sasa wametoka sehemu moja kwenda nyingine, kunakosa utofauti. Walau weka majina ya sehemu ya kubuni.
Stori ni nzuri sana ila mwandishi lichukulie hili wazo kwa mtazamo chanya,weka majina japo ya kubuni kuliko kuweka neno "X" ni ushauri tu!
 
Part Five A: In every life we have some trouble.

1993-1994

Baada ya mtihani wa kidato cha nne, nilirudi kwa mama Arusha. Nilikuta biashara zake zimechanganya hivyo basi akawa bize sana. Pia alikuwa ameshafanya maendeleo pale nyumbani pameboreka sana.

Siku zote nikiwa na mama alikuwa anapenda kunipa usia sana kuhusu maisha, kuheshimu watu wote, kusamehe, kutoa msaada pale ninapoweza , kushiriki vitu na wengine na kikubwa zaidi kumuomba Mungu.

Nilimpenda sana maana na yeye alinipenda sana kuliko watoto wake wote.

Pamoja na upendo alinifundisha kupika nikiwa mdogo sana, tena tunafanyiana zamu ya kupika na kuosha vyombo bila kujali huyu ni mama.
……..

Nikawa niko mtaani tu nikisikilizia matokeo. Mzee alikuwa anamiliki nyumba za wapangaji mimi nikawa ndio bosi wao wa kufatilia kodi. Maisha nyumbani yalikuwa safi kiaina sio ile saana, ila pesa ya kutesea mtaani ilikuwa haikauki.

Nilikuwa na tabia ya kufanya jogging asubuhi saa 11 kila siku, natoka hapo nyumbani sakina mpaka pale chuo cha habari maalum.

Kama kawaida yangu sikuwa na marafiki wengi walikuwa wa nne tu na kati ya hao mmoja ndie nilikuwa nae karibu sana anaitwa Frank.

Jogging nilikuwa nafanya na huyu Frank wengine walikuwa wavivu nilikuwa nakutana na Frank pale sakina super market tunaliunga mdogo mdogo mpaka ngara mashamba ya serikali karibu na Habari maalum.

Siku moja nimetoka zangu home saa 11:00 nashuka mdogo mdogo, kuna semehu kulikua na shamba kubwa la migomba, huwa kuna giza sana hapo.

Nilipokaribia hilo eneo nikaona gari nyeusi imesimamishwa kwenye shamba la migomba.

Kipindi hicho Arusha ujambazi uko juu sana, sikuwa na hofu maana mida hiyo kuna watu wanaokwenda kufata nyama pale Arusha meat wanakuwa njiani.

Nika punguza mwendo ili nijue lile gari ni la nani na kwa nini liko migombani kama limefichwa, (ni shamba letu) lile shamba la migomba linapakana na nyumba za wapangaji wetu.

Sikufanikiwa kulikaribia gari maana nilihisi kama limeibiwa naweza pata matatizo na vyombo vya dola, au labda kuna mpuuzi kajificha pale ili kufanya ngono kwenye gari.

Ilikuwa kawaida sana kukuta mtu amepaki gari anafanya ngono maana njia yenyewe haikuwa busy sana na migomba ilikuwa mingi kwenye hilo eneo. Ikanibidi niendelee na safari zangu.

Nilikutana na Frank sakina supermarket, ilikuwa meeting point yetu. Tukaunga mpaka kwa idd akasema hajisikii vizuri ikabidi turudie hapo. Ikabidi nimwambie twende nyumbani maana ni karibu sana kuliko kwao.

Frank alikuwa anaishi jirani na 'Arusha Technical college' kama unaelekea mianzini. Wakati napandisha nikiwa na Frank tukalikuta lile gari pale pale, nikamwambia kuwa imekuwa pale toka nashuka.

Tukashauliana tusisogee maana tulihisi tu limeibiwa hatukutaka kujitafutia matatizo. Tukaenda nyumbani.

Ilikuwa 12:30 wakati tunarudi, kulikuwa kume pambazuka, Frank alioga akanywa paracetamol akalala.

Mimi nikatoka ili nikaangalie kama lile gari bado lipo, nikalikuta liko pale pale.kutokana na utundu niliotoka nao Songea boys ukiongeza mazoezi nikawa najiamini sana.

'kama pawa mabula au pawa suzuki vile,' .

Kutokana na tabia ya kufanya mazoezi nikapata ujasiri nikalisogelea maana tayari kulikuwa kume pambazuka na watu wako njiani wengi tu.

Nilipokaribia nikachungulia mbele nikaona mtu amekaa ananiangalia ila amefungwa kitambaa mdomoni. Alipo niona akawa anatikisa kichwa tu mwili umekaza nilitulia pale huku najiuliza nifanyeje.

Nikapata ujasiri wa kusogea karibu, nikamuona vizuri alikuwa ni mzungu ila amekuwa mwekundu kutokana na kamba alizofungwa. Akanipa ishara nikafungua mlango wa mbele, nilimkuta amefungwa kwenye siti ya dereva, miguu imefungwa kamba, amekalishwa kwenye siti na mikono imefungwa nyuma ya siti. Kamba zilipita karibu na mabega hivyo alishindwa hata kujitikisa kwa jinsi manila zilovyokuwa zimebana.

Usoni alifungwa kitambaa ili asipige kelele. Mpaka wakati huo akili ilisimama nisijue la kufanya, ghafla nikapata ujasiri wa kumfungua kitambaa cha mdomoni ndio akaanza kuongea ila kinyonge sana.

Baada ya kumfungua kamba zote, na yeye akajaribu kushuka kwenye gari ila akashindwa kusimama akajimwaga chini. Nilimsaidia kumkalisha akaegemea gari, akawa ananiambia
"Help my wife and my daughter pls. "

"Frankly, I was curious about what was happening there."


Today is Friday, Next later todayView attachment 2555443View attachment 2555445View attachment 2555446
Slow down.
 
Advance hio sis mi form 5 ye 2nd year !! Outing day ni kwa mwamba tu 😂😂! Ananinunulia chips mayai mishikaki na soda nakula tukimaliza Nakumbuka alikua ananikanda na mabarafu mwili mzima ananifuta vizuri kisha anaenda kuniogesha 🤭😂😂😂😂 !
Life la boarding na ujana bana!!
Wee nimecheka mnooo...hatari sana sisy hiyo haijirudii..unatakiwa upitie vipindi vyote vya mpito halafu age hii unatuliaaa unaangalia tuu kwa mbalii 😆 😆 😆 😆
Ulienjoy sana sisy nimewaza tuu chips mayai kwa boarding ilikua ni dhahabu hahahah...hayo mabarafu sasa haha
 
Wee nimecheka mnooo...hatari sana sisy hiyo haijirudii..unatakiwa upitie vipindi vyote vya mpito halafu age hii unatuliaaa unaangalia tuu kwa mbalii 😆 😆 😆 😆
Ulienjoy sana sisy nimewaza tuu chips mayai kwa boarding ilikua ni dhahabu hahahah...hayo mabarafu sasa haha

Kweli Kabisa sis kweli siku hazigandi hatimae nasie leo tunawapiga biti mabinti olee wao niwakute na wanaume mtanitambua yanii nitawapasua ivo vichwa😁😁😂!!
 
Back
Top Bottom