Mkasa: Wema ni akiba, usiache kutenda wema

Kweli braza alikua noumaa kuharibu redio tu Ndio kichapo mpaka kutaka vunja mbavu mtu dahhh!!
 
Part Three: Nanusurika kuuwawa.

1983 - 1989

Nikaanza maisha mapya ya kijijini tena, kijiji kilikua kidogo sana. Nilikutana na changamoto nyingine pale kitete, hakukua na mashine ya kusaga, ilitubidi kwenda mgororo kwa gari moshi kusaga, na kununua mahitaji kama vile mafuta ya taa.

Nilipelekwa shule ya msingi kitete kuendelea na darasa la 3, nilisoma hapo mwaka mmoja tu.

Kutokana na kuwa kijiji ni kidogo, nikakosa wenzangu wa kucheza nao, (hapo kambini wototo wa rika langu walikuwa wachache, kijiji kilikuwa mbali na kambi) nilianza kwenda kutembea makambako kila jumamosi.

Ukiwa mgeni pale makambako , ukinunua chai, wanakupozea kabisa, maana kuna baridi kiasi kwamba wewe mgeni huwezi sikia moto wa chai, baadae mdomo utakapo babuka ndio utajua uliungua.

Kule makambako kulikuwa na mjomba, nae ni mfanyakazi wa TAZARA kituo cha makambako.
……..
Kwenda kila jumamosi ilikuwa rahisi kwa sababu familia za wafanyakazi wote wa TAZARA walikuwa na 'free pass' ya kupanda gari moshi kwenda kokote inapofika TAZARA.

Yaani unaweza kwenda Dar mpaka Mbeya bure tu. Nilitumia hiyo nafasi kushinda kwenye gari moshi, nachotakiwa kujua ni ratiba tu za gari moshi.

Nilipendelea sana kupanda schoma (schoema-lokomotiven), hizi hutumiwa na wafanyakazi kukagua reli na kubebea vifaa vya ufundi.

Zinakimbia sana, breki za haraka kama gari. Natoka asubuhi na schoma /gari moshi ya abiria inayoenda Zambia nashukia makambako, jioni narudi na gari moshi ya mizigo 'goods' tukawa tunaita 'gusi' naenda tu kwa station master na mwambia mimi ni mtoto wa mfanyakazi flani, naomba usafiri wa kwenda sehemu flani, basi ananipatia.

Siku moja nilichukuliwa na marafiki zangu kwenda kwenye kijiji cha jirani, wao walikuwa wenyeji. Pale kitete ilikuwa ni kambi ya wafanyakazi na kulikuwa na station ila wenyeji walikuwa wanakaa pembeni kidogo. Tulienda uelekeo wa mrimba kwa miguu.

Njiani tunapita kwenye mahandaki ambayo yana giza sana, mimi kutokana na ugeni wangu nilikuwa nabeba tochi kila tukienda huko. Kunakua na giza kiasi kwamba unaweza kupishana na mtu bila kujua, labda uwe na taa, au mkutane upande mmoja (mgongane).

Uzuri ni kua kila handaki lina vyumba vidogo vidogo vingi, just in case gari moshi likikukuta humo unaingia kwenye chumba, usipoingia linakusaga maana ni njia ni nyembamba.

Hakuna nyoka kwenye handaki na wala hawasubutu kuingia kwa sababu ya mafuta yanayomwagwa 'diesel' au oil.

Kuna handaki moja refu sana linaitwa 'handaki 14', niliwahi kusimuliwa kuwa kipindi Nyerere alipokuwa anazindua hiyo reli, alikataa kupita kwenye hilo handaki ikabidi apitishwe juu ya mlima kwa helicopter. Sababu ni refu sana, kwa wasiojua handaki wanachimba mlima kutengeneza njia ya gari moshi.

Siku hiyo nimeenda na rafiki zangu kutembea uko handaki 14, ilikuwa ni kipindi cha kiangazi. Kutokana na umbali na jua kali, niliamua kurudia njiani baada ya kuchoka, wale wenzangu walikuwa wametumwa huko kijijini, mimi niliunga tu tera.

Nikiwa narudi nilipita kwenye mahandaki madogo madogo, giza likiwa limetanda ingawa nje jua kali.

Nikiwa nimekaribi sehemu ambapo wakati tunapita tuliwakuta mafundi wakiendelea na kazi, nilianza kusikia michakato ya kitu kinakanyaga majani makavu. Nikisimama na kugeuka kuangalia sioni kitu wala kusikia michakato, nikitembea naisikia.

Mazingira ya hapo yalikuwa mimi natembea kwenye mataruma ya reli nje tu ya handaki, (kwa vile kutengeneza mahandaki wanachimba mlima) yale mataruma yalikuwa chini kuna kingo za udongo kila upande na juu ya mlima ndio kuna nyasi. Kwa hiyo ile michakato ilikuwa inashuka kutoka mlimani kuja chini niliko,mkono wangu wa kulia.

Wale mafundi walikuwa sehemu tambalale,lakini kuna kona, walikiona kile kilichokuwa kinanifata bila mimi kukiona . Ikawabidi wapande kilimani ili waone kile kitu kinawinda nini pale.

Hilo eneo kitete liko jirani na mbuga ya wanyama ya seluu. Wakiwa hapo mlimani waliniona mimi niko pale chini natembea huku nikigeuka mara kwa mara, umbali wangu na wao ulikuwa kama mita 70 tu.

Wakaanza kupiga kelele huku wakikimbilia huku niliko, kelele zao zikanishtua, ile nageuka nyuma ndio nikakiona kilichokuwa kinaniwinda. Alikuwa ni simba dume, alikuwa ananinyatia nikisimama anatulia , kwa vile majani ni marefu sana na makavu sikuwa nimemuona kabla.

Nilianza kukimbia kuwafata wale mafundi, pembeni yangu mkono wa kulia yule simba nae aliongeza spidi sasa akaacha kunyata maana nimeanza mbio. Akawa anashuka mlima ili aniwahi kwa mbele, tulikuwa sambamba ila mimi niko chini yeye juu ya mlima.

Bahati ilikuwa upande wangu maana wale mafundi walipiga risasi kule mlimani aliko simba ikabidi abadili uelekeo. Nikiwa kama mita 15 kuwafikia wale mafundi nilianguka nikapoteza fahamu kutokana na ile hofu.

Nilikuja kuzinduka mida ya jioni kama saa 10 maana muda ule wa tukio ilikuwa saa 6 mchana . Baada ya kupata chakula wafanyakazi wenzake baba walikuja kunipa pole kwa mkasa ule. Sikuwa na haja ya kueleze kitu chochote kwa kuwa wale mafundi walieleza kuhusu lile tukio zima.

Kumbe ilikuwa ni kawaida kipindi cha kiangazi, wakati wa mavuno kijijini, wanyama mbali mbali walikuwa wanaingia vijijini kutafuta chakula mashambani na maji. Mimi na ugeni wangu sikuwa nafahamu hilo.

Wafanyakazi wa TAZARA walikuwa na magobole kwa ajili ya usalama wao wawapo porini kwenye kazi zao.

Siku moja usiku mzee wangu alinionyesha simba waliokuja pale kijijini. Walikuwa wawili, macho yao yalikuwa yanawaka kama tochi usiku, wale simba walikuwa kwenye kilima wanashuka. Watu pale kambini wakapiga risasi hewani wale simba wakakimbia.
…………..

Ndani ya A city….
Baada ya tukio lile mama alipopata habari alimwambia baba nirudi nyumbani maana kule sio salama kwangu. Mzee wangu hakupinga maana na yeye alipata uhamisho kipindi hicho, kwenda makao mkuu pale TAZARA Dar es Salaam, kule kitete alikuwa station master. Alipanda cheo akahamishwa .

Mzee aliamua mama ahame kule kijiji ''X'' ahamie mjini afanye biahara. Alitaka mama amfate Dar lakini Mama alichagua kuhamia mkoa wa Arusha kwa kuwa alikuwa amekulia huko.Anaoufahamu vizuri kuliko Dar.

Pia ingekuwa rahisi kurudi nyumbani kuangalia maendeleo ya mashamba maana sio mbali kwenda ''X'' kulinganisha na Dar.

Mzee aliuza ng'ombe wote na mbuzi, alinunua nyumba eneo la Sakina Arusha.

Pia Alinunua shamba la migomba lililokuwa jirani na hiyo nyumba, akajenga nyumba za wapangaji.

Mama hakutaka kukaa kwenye nyumba iliyonunuliwa maana ilikuwa ya slope. Mzee akaibomoa na kujenga nyumba nyingine kubwa na nzuri pale pale.

Mimi nilihamia Arusha kwa mama, baada ya baba kuondoka kitete, nilipata shule ya msingi 'Sanawari' nilisoma hapo darasa la 4 mpaka nikamalizia hapo elimu ya msingi mwaka 1989.
……….

Mama alifungua biashara zake akawa anafanya, alikuwa na duka la nguo na restaurant maeneo ya mjini kati.

Matokeo yalipotoka nilipangiwa shule ya Songea boys,(miaka ile Sera ya Nyerere ya kutoa wanafunzi mikoa ya kaskazini kwenda kusoma
mikoa ya kusini, wa kusini anaenda kanda ya ziwa nk ilikuwa bado inafanya kazi) 'narudi tena kwa mjeda',

Mama aliwasiliana na kaka, alimweleza kuhusu mimi kupangiwa shule huko aliko . Mama alimuomba kaka asije kufanya kama yale ya nyuma , kaka yangu Edward alimhakikishia mama kutonifanyia ukatili wowote ule, alisema kipindi kile ni ile hali ya kutoka depo ilisababisha ila kwa sasa amekuwa.

**********

Next Jioni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…